Bajeti ya elimu 2012/13 itamaliza changamoto hizi?

armanisankara

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
283
49

Shule hii ipo wilayani Muleba mkoani Kagera.

Ndani ya shule hii licha kuwa ni shule yenye kuta na kuezekwa kwa nyasi, bali pia wanafunzi wanakaa chini.

Wanafunzi wa shule ya msingi Misunkumilo ya wilayani Nkasi wakisoma kwenye darasa lililoezakwa kwa turubai, shule hiyo ina madarsa mawili ya namna hiyo ambayo yanatumiwa na wanafunzi wa darasa la tatu, la nne na awali.


BAJETI ya elimu ilisomwa bungeni siku ya Jumatatu, 13 Agosti. Wakati bajeti ya Elimu ilisubiriwa kwa hamu na wadau na hasa wapenda maendeleo ya Elimu, Baadhi ya maeneo nchini bado yanakabiliwa na changamoto kubwa sana hasa hali mbaya ya miundombinu, ukosefu wa vyumba vya madarasa na majengo ya shule ambayo yamesababisha baadhi ya shule kuweka madarasa ya nyasi kama shule ya msingi Selous na Mkapa zilizopo wilayani Namtumbo, Shule ya msingi Silabu iliyoko wilayani Korogwe, Shule ya msingi Misunkumilo ya wilayani Nkasi, na baadhi ya shule wilayani Muleba.


Hali ya elimu imezidi kuwa mbaya kila kukicha, kiasi kwamba hata watu hudiriki kuuliza kama shule hizo zipo nchini, hasa wakiangalia juhudi na kelele nyingi zilizopigwa juu ya mchango mkubwa wa MMEM na MMES kuwa zimefanya kazi kubwa sana kuboresha mazingira ya kujifunzia hasa miundombinu ya shule. Swali Je, shule hizi ziliachwa wapi na mipango hii? Je bajeti ya elimu ya 2012/2013 itatatua baadhi ya changamoto za elimu nchini?na kuondokana na majengo haya yasiyo rafiki kwa mwanafunzi na mwalimu?

Hebu angalia jinsi ambavyo wanafunzi huko Tanga, Rukwa, Kagera na Ruvuma wanavyojifunza kwenye sehemu zinazokatisha tamaa: Watatoka?
 
Wimbo ni ule ule, ... Utasikia taifa letu changa, ...kero hizi serikali imeziona, ... bajeti finyu! ..tunajipanga!... Miaka inaenda hakuna kinachofanyika.
 
Back
Top Bottom