Bajeti ya 2009/2010 Tanzania

Sasa sare za kijani za nini? mi nadhani kuna umuhimu wa kuliangalia upya hili swala la kofia mbili. Ndo maana mambo mengi yanakwenda ndivyo sivyo kwani chama huyo huyo, nchi huyo huyo hakuna wa kumsaidia mwenzie.. linalotoka ni hilo hilo, liwe zuri ama baya..

Anyway wacha tusubilie hizo pumba/mchele ...
Sare za kijani ni nguo kama zilivyo nguo nyingine! Sawa na kanzu mtu yeyote yule anaweza kuvaa mkuu! Isikupe shida saana we sikiliza hotuba ya muheshimiwa!
 
Rais Kikwete ameingia, amefuatana na MR Dr Shein na WM Pinda. Pia Spika Sitta, EL na Mzee John Malecela wameandamana nae
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Eng. James Nsekela amemkaribisha rais.

Rais Kikwete ameanza kuzungumza na kuhiti straight kwenye point Kuanguka kwa Uchumi wa Dunia.
Ameanzia historia ya kuanguka kwa uchumi na athari zitokanazo ambazo anakiri Tanzania haiwezi kukwepa kuathirika, hali iliyopelekea kuiweka pembeni market economy na serikali kuingilia na sasa ndivyo na serikali ya Tanzania itakavyofanya.
 
Muungwana anachomekea kidogo kidogo terminology za kiingereza kama vile 'uchumi wa dunia umedecline kwa 3.8%' etc, sasa sijui hawa wazee wote wanamuelewa au vipi!!
 
Angeongea na waandishi wa habari ili baadaye ajibu maswali, anawaonea tu hawa wazee wa watu...
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MPANGO WA KUUNUSURU UCHUMI WA TANZANIA NA ATHARI ZA MSUKOSUKO WA FEDHA NA UCHUMI DUNIANI



Juni 2009


Yaliyomo
1.
UTANGULIZI. 2
2. ATHARI ZA MSUKOSUKO.. 4
2.1. Athari kwa uchumi wa dunia. 4
2.2. Athari kwa Uchumi wa Tanzania. 5
2.2.1. Ukuaji wa Uchumi kwa Ujumla. 5
2.2.2. Athari kwa utulivu wa uchumi5
2.2.3 Athari Kwa Ajira. 7
2.2.4 Athari kwa Mapato na Matumizi ya Serikali9
2.2.5 Athari Kwenye Uwekezaji Kutoka Nje. 12
2.3. Athari Kisekta. 13
2.3.1. Athari kwenye Utalii14
2.3.2 Athari kwenye Kilimo. 15
2.3.3 Athari Kwenye Madini21
2.3.4. Athari Kwenye Viwanda. 22
2.3.5. Athari kwenye Sekta ya Fedha. 23
3. MAPENDEKEZO YA MKAKATI WA KUKABILI ATHARI HIZI. 26
3.1.
Msingi wa Mkakati Huu. 26
3.2. Hatua Mbalimbali za Kutekeleza Mkakati27
3.2.1.
Kupunguza makali au kuhimili shinikizo la msukosuko – hususan kuwalinda wananchi walio katika hatari kubwa zaidi kimaisha. 27
Kuboresha Mifuko ya Dhamana. 29
3.2.2. Kuinusuru nchi kutokana na athari za uadimu wa chakula duniani zilizochochewa na msukosuko31
3.2.3. Kulinda programu muhimu za kijamii32
3.2.4.
Kulinda uwekezaji muhimu hasa katika miundombinu ili kuendeleza ukuaji wa uchumi na malengo ya milenia33
4. NAMNA YA KUGHARIMIA MPANGO HUU.. 35
4.1.
Serikali kukopa ndani ili kutekeleza bajeti yake. 35
4.2.
Kuharakisha uanzishwaji wa benki za rasilimali na kilimo zitakazotoa mikopo ya muda mrefu na kwa riba nafuu.36
4.3.
Benki Kuu kulegeza hali ya Ukwasi36
4.4.
Misaada Kutoka kwa Wahisani36
5.
FURSA ZINAZOTOKANA NA MSUKOSUKO.. 38

1. UTANGULIZI


Uchumi wa dunia unakabiliwa na msukosuko mkubwa wa fedha na uchumi ambao haujatokea kwa karibu miaka 60 iliyopita. Msukosuko huu ulianzia kwenye mfumo wa fedha wa Marekani kutokana na usimamizi dhaifu wa mfumo huo na baadaye kuenea kwa kasi kwenye nchi zilizoendelea. Kuanzia nusu ya pili ya mwaka 2008, dunia ilishuhudia kuanguka kabisa kwa mfumo wa fedha na uliosababisha kudorora kwa uchumi wa dunia. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2008, masoko ya mitaji ya dunia yalianguka na bei ya bidhaa kuanguka kwa kiwango kikubwa.

Athari za msukosuko huu zilianza kujitokeza kwenye nchi zinazoendelea kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupungua kwa mikopo, kushuka kwa mahitaji na bei za bidhaa na kupungua kwa uwekezaji na misaada kutoka nje. Kutokana na hali hiyo, nchi zinazoendelea zinakabiliwa na hatari ya uchumi wao kuporomoka hasa kuanzia mwaka 2009.

Kutokana na hali hii nchi nyingi, ikiwemo Tanzania, zinakabiliwa na hatari ya kushindwa kufikia malengo waliyojiwekea ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini. Ili kukabiliana na hatari hii nchi nyingi zimekuwa zinachukua hatua mbalimbali ili kunusuru uchumi.

Kutokana na sababu hii, Serikali ya Tanzania imeunda Kikosi kazi cha kuangalia njia na namna ya kukabiliana na athari zinazotokana na msukosuko wa masoko ya fedha pamoja na kuporomoka kwa uchumi duniani kwa uchumi wa Tanzania. Serikali imefanya uamuzi huu kutokana na Tanzania kuwa imeungana na mfumo wa fedha wa dunia kwa kupitia biashara ya bidhaa na huduma kati yake na nchi nyingine duniani, mitaji ya kimataifa inayoingia na kutoka Tanzania pamoja na bei za bidhaa na huduma katika soko la kimataifa. Kwa hiyo, msukosuko huu wa masoko ya fedha duniani unaweza kuathiri uchumi wa Tanzania kutokana na muungano huo kati ya Tanzania na dunia. Madhara yatakayotokana na msukosuko huu utaongeza kiwango cha umasikini nchini kama hatua za kupambana na athari hizo hazitachukuliwa.

Serikali imekipa Kikosi Kazi jukumu la kupitia na kuchambua kwa umakini na undani madhara yanayotokana na msukosuko huo kwa sekta mbalimbali na kupendekeza hatua ambazo Serikali inaweza kuchukua ili kukabiliana na hali hiyo kwa kipindi cha muda mfupi na wa kati; na hata ikiwezekana kuzitumia fursa zinazojitokeza ili kuzuia kutetereka na ikiwezekana kukuza zaidi uchumi wetu.

Ili kutekeleza kazi yake serikali imekipa kikosi kazi majukumu yafuatayo:
(i) Kufanya uchambuzi kuhusu hali halisi ya madhara yatakayotokana na msukosuko wa masoko ya fedha pamoja na kuporomoka kwa uchumi wa dunia kwa uchumi wa Tanzania
(ii) Kushauri,kwa kuzingatia uchambuzi wa hali ya uchumi, hatua ambazo Serikali inaweza kuchukua ili kupunguza athari za msukosuko wa masoko ya fedha ya kimataifa na
(iii) Kuchunguza fursa zinazotokana na msukosuko wa masoko ya fedha ya kimataifa na jinsi ambavyo Tanzania inaweza kufaidika na fursa hizo ili uchumi ubaki imara na kukua zaidi.

Ripoti hii inajumuisha uchambuzi wa athari za msukosuko kwenye sekta mbalimbali, mapendekezo ya hatua ambazo Serikali inaweza kuchukua ili kupunguza athari hizo na inabainisha fursa mbalimbali zinazotokana na msukosuko huo.

2. ATHARI ZA MSUKOSUKO

2.1. Athari kwa uchumi wa dunia


Kulingana na makadirio ya mtazamo wa uchumi wa dunia (World Economic Outlook) katika miaka ya usoni uliotolewa na IMF Aprili 2009, uchumi wa dunia unakisiwa kushuka kwa asilimia 1.3 mwaka 2009 kutoka ongezeko la asilimia 3.2 mwaka 2008, ambapo ule wa nchi zilizoendelea utashuka kwa asilimia 3.8 mwaka 2009 kutoka ongezeko la asilimia 0.8 mwaka 2008. Kwa nchi zinazoendelea ukuaji wa uchumi unatabiriwa kushuka kufikia asilimia 1.6 mwaka 2009 kutoka asilimia 6.1 mwaka 2008.

Ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika unakadiriwa kushuka hadi asilimia 2.0 mwaka 2009 kutoka asilimia 5.2 mwaka 2008 (nchi zinazozalisha mafuta zitaathiriwa zaidi ya nchi zisizozalisha mafuta). Kushuka huku kunasababishwa na kupungua kwa utashi wa bidhaa na huduma, na kupungua kwa rasilimali za uwekezaji na hivyo kupunguza uzalishaji...


Itaendelea...
 
Last edited by a moderator:
Namwona cag, mkulo, kabwe, cheyo, wazee wamekaa mbele kabisa mstari wa kwanza lakini wengi ni mawaziri na wabunge
 
Hahahahaha!
Wa moja hapati mbili kaka.
Kuna kicheko na kicheko kikubwa
Rais kuwa nafasi kubwa kwenye chama kwa Afrika ni mwanya kwa wanachama wenzie kufanya watakayo kaka
Hutuba hizi si ngeni tena
Naamini hakuna jipya
ngoja tumalizie kazi kaka
 
Baba mdogo wa Taifa Dr. Slaa yupo?

Sijaweza kumuona ila watu ni wengi sana na wabunge wote wapo, inamaana yupo, hata Zitto Yupo.
Ameshazungumzia sekta ya kilimo, serikali itaingilia kati.
Pia sekta ya madini ya vito, ikiwepo Tanzanite bei ni nusu bei ya soko. Gold imesimama.

Naomba mlioko kwenye access ya TV, muendeleze briefing ya anachosema ili mimi niwapatie mengineyo sio hutuba.
Mtandao wa Voda ni bure kabisa uko too slow, hivyo anayeona live anaweza post faster kuliko mimi niliyeko
Humu ukumbini.
 
sijaweza kumuona ila watu ni wengi sana na wabunge wote wapo, inamaana yupo, hata zitto yupo.
Ameshazungumzia sekta ya kilimo, serikali itaingilia kati.
Pia sekta ya madini ya vito, ikiwepo tanzanite bei ni nusu bei ya soko. Gold imesimama.

Naomba mlioko kwenye access ya tv, muendeleze briefing ya anachosema ili mimi niwapatie mengineyo sio hutuba.
Mtandao wa voda ni bure kabisa uko too slow, hivyo anayeona live anaweza post faster kuliko mimi niliyeko
humu ukumbini.
sawa pasco ngoja niendeleze
 
Hivi anachosema Mheshimiwa ndicho kilichoandikwa kwenye MADESA yake? Maana huko kuchanganya Kiswanglish sidhani kama ndiyo aliandaliwa hivyo.
 
Mradi wa dola bl 7 wa arthumas umegoma, kabanga 165ml wameahirisha mradi, mtwara kiwanda cha saruji na mbolea pesa hakuna zote on hold
 
Hali ya ajira nchini 2009 soko litakuwa finyu ajira nyingi kutengekeza itakuwa ngumu, 48,000 wameshapoteza ajira mpaka sasa
 
Si hata kama financial crisis isingalikuwepo kwani hao Barick wanatusaidia nini, aache unafiki na kujikosha huyu ni m..mba tu
 
Sasa dhahabu ambayo ndiyo anasema haijayumba ndiyo ina mikataba inayonuka, Anasingizia ng'ombe wa maskini Hazai.... Wizi Mtupu hii nchi
 
Back
Top Bottom