Bajeti Wizara ya Nishati na Madini yapita

Hebu wataalamu wa mambo ya budget tusaidieni, mkopo kuwepo ndani ya budget vipi?
Maana tumezoea kuambiwa budget ni mapato na matumizi, sasa huu mkopo nao ni pato au?
.

Hii ndiyo hofuu kuu aliyokuwa nayo mbowe na mnyika leo wakati wakimuuliza waziri maswali.lakini ameshindwa kujibu vizuri.
 
Swali langu wana JF, Niliwahi kupost thread yangu humu lkn kwa bahati mbaya haikupata pop ya kutosha, lkn kupitia mada hii niulize swali, HIVI KILA MTU HUMU HUWA ANARIDHIKA NA MAJIBU YA MAWAZIRI? kwa masikio yangu leo tena c mara tano pekee, as long as mtu anapata muda wa maswali mawili na jibu utegemea utashi wa Waziri bac ikiwa swali la mwisho la nyongeza likiulizwa kwani budget ya umeme haikuangalia hata kiac kidogo toka vyanzo vya ndani? Jibu ni hakuna tumeangalia na kutathmini mkopo kwa ujumla wake, na hapo swali linakua limejibiwa, hv nyie mnaona sw? Huo ni mfano m1 tu, majibu aliyotoa pinda kuhusu kauli yake ya awali alipozungumzia kuhusu kugusa posho, akapewa swali na Mnyika amejibu mazingaombwe, posho zinamahusiano gani na ghalama za utekelezaji wa sera kwa ujumla? Ina maana kuna wkt watendaji ufikia wkt wakatoa fedha mifukoni? Wana Jf amlioni hili? Hakuna Waziri aliye wahi kushindwa swali.

Kanuni za bunge letu ni utani! Kwa namna yeyote ile kanuni hizi haziwezi kusimamia utendaji wa serikali. Kwa mfano mbunge anauliza swali, waziri anajibu sivyo kabisa, then muuliza swali anarudia tena, waziri again anapiga chenga. hapo ni mwisho.

Kitu ambacho nimeona ni upungufu mkubwa sana wa muongoza vikao iwe Spika, Naibu wake au wenyeviti wa vikao vya bunge. Ukiangalia mabunge mengine hasa yanayofuata mfumo wa madola Spika au muongoza kikao anaingilia kati kama waziri/serikali inajibu kisanii au kupindisha swali. Hapa kwetu Spika anakuwa kama mtazamaji! Hata kwa akili ya kawaida tu, spika anatakiwa aongoze mhimili mmoja wa dola yaani wawakilishi wa wananchi katika kuhoji mmiliki mwingine kwa maana ya serikali. Hivyo ni wajibu wake kuhakikisha kila kinachoulizwa na wabunge kinapata majibu ya kuridhidha na sio vinginevyoo.

Kuna ulazima kabisa wa kuangilia upya hizi kanunu vinginevyo wananchi ni kama wameingizwa mjini. Hakuna kitu bungeni kwa kanuni za sasa.
 
haya mambo yanashangaza sana , hii mipango yote mwisho wake ni 2013 -2014 ,inamaanisha baada ya hapo tunarudi huku huku tena mgao mkali zaidi sababu matumizi yatakuwa yameongezeka , mipango ya muda mrefu imekaa kisiasa zaidi kutokana na ukweli kupata fedha zote hizi ndani ya muda mfupi tena kwa kukopa ni vigumu , ukizingatia TANESCO haikopesheki plus u-jairo , shida tupu !:angry:
 
Maumivu zaidi ni kuambiwa bei zitapanda pindi tu umeme wa uhakika utakapopatikana, bila shaka tutakua tunaanza kuilipa hii mikopo, mbona sasa tunalipa uzembe wa watu , kwa nini wao bado wako maofisini aisee
 
Hebu wataalamu wa mambo ya budget tusaidieni, mkopo kuwepo ndani ya budget vipi? <br />
Maana tumezoea kuambiwa budget ni mapato na matumizi, sasa huu mkopo nao ni pato au?<br />
.
<br />
<br />

Ni sawa kabisa, that is a DEFICIT BUDGET, Na inakuwa financed through borrowing!
Ila budget mama ya wizara ya fedha itakuwa haijaonesha hili!
 
Back
Top Bottom