Bajeti Tegemezi Na Matumizi Yetu Kwenye Misafara: Hivi kweli tunachapa kazi?

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
My thousand words....!

steved-albums-mh_pinda-picture168-msafara-pinda-morogoro-mjngw3b.jpg


steved-albums-mh_pinda-picture167-msafara-pinda-morogoro-mjngw1-jpg2b.jpg


steved-albums-mh_pinda-picture166-msafara-pinda-morogoro-mjngw1.jpg


"Leo mchana [15-10-08] nikiwa njiani kurudi Iringa nilikutana na msafara wa Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kilomita kadhaa kuvuka daraja la Mto Ruaha Mkuu, mpakani mwa Iringa na Morogoro. Ulikuwa ukielekea Morogoro..."

Picha na maelezo kwa hisani ya: mjengwa.blogspot.com
 
Kwa waliosoma kitabu cha Animal Farm cha George Orwen (kama sijakosea jina la mtunzi) wataona wazi nchi yetu inavyolandana na kinachohadithiwa. Nguruwe wale jamani wakapewa/wakajipa uongozi...Ndiyo tunayoona mishahara, posho magari ya kifahari na ufisadi. Vitabu vingine bwana!!
 
Hamna uwanja wa ndge huko anakopenda ili kupunguza gharama za mafuta?Watu kibao na magari yote hayo ya nini?Hii pomposity ni ya kipuuzi sana!
 
Let Think BIG.

Msafara wa Waziri Mkuu utakuwa na haya yafuatayo:-

1. Gari ya Mheshimiwa Waziri Mkuu
2. Gari ya Wanausalama
3. Gari lingine la wanausalama
4. Gari la RPC
5. Gari la RC
6. Gari la DC
7. Gari la OCD
8. Gari la Mkugurugenzi wa Halimashauri
9. Gari/Magari ya Wabunge wa Mkoa/Jimbo husika
10. Gari la Polisi
11. Ambulance
12.
13,

Sasa ukisoma hapo utaona kwamba tunaongea upuuzi tu na sisi kwa maana wa could do better kwa kuongelea mambo mengine ya maana!
 
Naona wameamua wawe na ambulance kabisa manake kurushiwa mawe dakika yoyote

Issue ya ambulance ni complex kidogo. Ambulance inatumiwa na daktari wa mkoa kama official car. Sabau ya kuiona hapo ni kwa vile daktari wa mkoa naye inabidi awe kwenye entourage. Vile vile kuna uwezekano kuwa imeazimwa na uongozi wa mkoa kubeba maafisa wa mkoa ambao wanatakiwa kuwa kwenye msafara. Cha kujiuliza je wagonjwa wanabebwa na nini? its a shame!
 
Let Think BIG.

Msafara wa Waziri Mkuu utakuwa na haya yafuatayo:-

1. Gari ya Mheshimiwa Waziri Mkuu
2. Gari ya Wanausalama
3. Gari lingine la wanausalama
4. Gari la RPC
5. Gari la RC
6. Gari la DC
7. Gari la OCD
8. Gari la Mkugurugenzi wa Halimashauri
9. Gari/Magari ya Wabunge wa Mkoa/Jimbo husika
10. Gari la Polisi
11. Ambulance
12.
13,

Sasa ukisoma hapo utaona kwamba tunaongea upuuzi tu na sisi kwa maana wa could do better kwa kuongelea mambo mengine ya maana!

Kasheshe, sidhani kama ni upuuzi Watanzania kujiuliza maswali kuhusiana na msafara huo.

Naamini Mh. Waziri alikuwa katika harakati za kawaida katika kazi alizopangiwa na majukumu aliyonayo kama Waziri Mkuu. Basi katika kutambua kazi yake, watu wanaweza kujiuliza maswali kwa nia ya kujua na kutathmini matumizi yetu... naamini wengi wanajiuliza maswali kwa kulinganisha majukumu na matumizi ya Waziri wetu na mawaziri wakuu wengineo katika nchi mbalimbali na gharama za matumizi za mawaziri hao nchini mwao.

Hata hivyo kwa hoja yako, kimoja ninachoweza kukuuliza ni kuwa:

--iwapo msafara wa Mh. Waziri Mkuu unatakiwa uongozane na viongozi wote hao, je ni kwa utajiri upi Tanzania tunatumia magari aghali kama hayo?

--swali la nyongeza ndugu: kama wafahamu, waweza kutuwekea pia orodha ya wanaoongozana na Mh. Rais au Makamu wake? Ahsante.
 
kama kuna ulazima wa kuongozana na wakuu hawa katika ziara, kwa nini yasinunuliwe mabasi kila mkoa ukapewa basi moja?
 
My thousand words....!

steved-albums-mh_pinda-picture168-msafara-pinda-morogoro-mjngw3b.jpg


steved-albums-mh_pinda-picture167-msafara-pinda-morogoro-mjngw1-jpg2b.jpg


steved-albums-mh_pinda-picture166-msafara-pinda-morogoro-mjngw1.jpg


"Leo mchana [15-10-08] nikiwa njiani kurudi Iringa nilikutana na msafara wa Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kilomita kadhaa kuvuka daraja la Mto Ruaha Mkuu, mpakani mwa Iringa na Morogoro. Ulikuwa ukielekea Morogoro..."

Picha na maelezo kwa hisani ya: mjengwa.blogspot.com

Tanzania inasikitisha na kutia huzuni sana. Kama msafara wa waziri mkuu unatumia magari yote hayo tunategemea nini?. Kwa hesabu zangu mbovu na za haraka haraka katika msafara huo kuna watu si chini ya 30, na kama kawaida ni lazima walipwe imprest ya kumtoa Mh. waziri mkuu toka point A kwenda point B. Magari na pikipiki zinatumia mafuta na wala si maji. Ni kwa utajiri gani tuliokuwa nao watanzania kuishi maisha kama hayo?.

Waziri mkuu wetu anapata ulinzi wote huo nani anamtafuta kumwua?. Osama hana mpango na wala hamjui Kikwete itakuwa Pinda?.

Enough is enough, upuuzi kama huu ni lazima ukomeshwe mara moja bila ya kuona haya. Tunahitaji pesa kwa ajili ya mambo muhimu, kama viongozi wetu wana maadui na wanahitaji ulinzi zaidi basi tuambiwe maadui hao ni nani na kwanini wana maadui.

Serikali baada ya kuwapa ulinzi wa kutosha maalbino ili wasichinjwe wanawapa ulinzi viongozi ambao ukweli ni kwamba hawaitaji na pia hawastaili kupata ulinzi huo. I am sick about this.

Jamani kwa wale wenzetu mlio Ulaya na America misafara ya viongozi inakuwaje huko?
 
Let Think BIG.

Msafara wa Waziri Mkuu utakuwa na haya yafuatayo:-

1. Gari ya Mheshimiwa Waziri Mkuu
2. Gari ya Wanausalama
3. Gari lingine la wanausalama
4. Gari la RPC
5. Gari la RC
6. Gari la DC
7. Gari la OCD
8. Gari la Mkugurugenzi wa Halimashauri
9. Gari/Magari ya Wabunge wa Mkoa/Jimbo husika
10. Gari la Polisi
11. Ambulance
12.
13,

Sasa ukisoma hapo utaona kwamba tunaongea upuuzi tu na sisi kwa maana wa could do better kwa kuongelea mambo mengine ya maana!

Let's think SMALL.


Gari la Wasaidizi wa Waziri Mkuu limesahaulika kwenye orodha au wanajumulishwa kwenye magari ya wana usalama?

Msafara huu wa:

Gari 4: 2 za Wanausalama, moja ya polisi, 1 Ambulance.
Gari 2 zingetosha.
Ni vigumu kuelewa ni kazi gani inahitaji kufanywa na wanausalama walio kwenye magari mawili. Kama kuna tishio ama wasiwasi wa majangili kujaribu kuuteka nyara msafara wa kiongozi ni bora viongozi wetu wakifanya ziara mikoani wapande helikopta. Chopper itaweza kubeba kiongozi mwenyewe, walinzi wawili, msaidizi mmoja. Kwa maana hiyo kutakuwa hakuna ulazima wowote wa kusindikizwa na hao akina RC, DC, RPC, OCD etc wa mkoa anaotoka. Viongozi wa Mkoa anakokwenda, watampokea atakakotua.

Kama kuna ulazima wa kwenda na magari na kuandamana na hao wote.
Je, RC na DC hawawezi kupanda gari moja, kwa nini?

Kuna mwiko gani RPC na OCD kutumia gari moja?

Mkurugenzi wa Halmashauri naye apande gari la Gari na Mbunge/Wabunge.

Kinacholalamikiwa ni matumizi yasiyo ya lazima ya magari, gharama za mafuta n.k. kutokana na wingi wa magari katika msafara wa Waziri Mkuu. Kwa nini kila msindikizaji awe na gari lake? Twataka ufahari katika nchi maskini?
 
Let Think BIG.

Msafara wa Waziri Mkuu utakuwa na haya yafuatayo:-

1. Gari ya Mheshimiwa Waziri Mkuu
2. Gari ya Wanausalama
3. Gari lingine la wanausalama
4. Gari la RPC
5. Gari la RC
6. Gari la DC
7. Gari la OCD
8. Gari la Mkugurugenzi wa Halimashauri
9. Gari/Magari ya Wabunge wa Mkoa/Jimbo husika
10. Gari la Polisi
11. Ambulance
12.
13,

Sasa ukisoma hapo utaona kwamba tunaongea upuuzi tu na sisi kwa maana wa could do better kwa kuongelea mambo mengine ya maana!

I agree, usisahau afisa elimu...
 
Naona sasa watu tunakuwa wajinga... u mean to tell me that of all the misappropriation that happens in Tanzania hili ndio mmeona kubwa..lol
mngekuwa na akili mngegundua kuwa huu ni msafara wa PM akiwa kwenye ziara including, as stated above. RC, PRC, DC au ma DC wote wa mkoa husika, usalama, na maafisa wengine wengi.. Mimi nimkazi wa Oysterbay na mara nyingi nakutana na msafara wa waziri mkuu... ukweli ni kwamba akiwa dar-es-salaam akienda kazini anakuwa na gari yake, mbili za walinzi na piki piki... sasa muache kuwa mnatoa hoja zisizo na kichwa wala mkia... This is the loss of objectivity in exchange for jazba... mnakuwa kama Michael Moore..lol..
 
Kwanza nilidhani ni msafara wa JK..Then nikashtushwa kidogo kuja kuambiwa ni wa PM.
Ama kweli ulinzi huo si wa kawaida...Hivi mkoloni naye alilindwa hivi?
Kuna wenye picha za wakoloni walipotutawala?
This kwa kweli ni too much...Duh!
Inawezekana mambo si mazuri?....Sasa huo ulinzi wote huo ni wa kukulinda dhidi ya wananchi wanaokupigia kura? Ulinzi kwa viongozi wetu ni muhimu lakini this one is just too much tena ukizingatia na mambo ya gharama!
Nakubaliana na mama...Hao wengine watafutiwe basi zuri tu....At least during ziara jamani...Hivi hao wananchi hamuwaonei huruma?
Inasikitisha sana.
 
Naona sasa watu tunakuwa wajinga...

Wewe wasema.

u mean to tell me that of all the misappropriation that happens in Tanzania hili ndio mmeona kubwa..lol
Lawezekana kuwa dogo sana machoni pako na kwa baadhi ya wachache uwajuao. Lakini miongoni mwa Watanzania wengi masikini hilo naamini kuwa ni kubwa kwa kipimo cha maisha yao.

By the way, waweza kututajia misappropriation kubwa zozote zile ulizo na uhakika nazo ili kutuhabarisha siye "tusiojua?"

mngekuwa na akili mngegundua kuwa huu ni msafara wa PM akiwa kwenye ziara including,
Usijali, hatuna akili siye. Tulifikiri huo ni msafara wa Michael Jackson akielekea Serengeti ku-shoot kideo kipya cha thriller version 4, the master copy.

as stated above. RC, PRC, DC au ma DC wote wa mkoa husika, usalama, na maafisa wengine wengi.. Mimi nimkazi wa Oysterbay na mara nyingi nakutana na msafara wa waziri mkuu... ukweli ni kwamba akiwa dar-es-salaam akienda kazini anakuwa na gari yake, mbili za walinzi na piki piki...
Akiwa anaenda Morogoro siyo kwamba anakuwa anakwenda kazini pia ndani ya nchi yake?! Au anakuwa kama anasafiri kwenda Pluto hivyo anahitaji kujilinda na vimondo njiani?!
Waliopendekeza makao makuu ya serikali kuwa Dodoma labda walikuwa na lao jambo...either way, something is not right and we feel we have the right to question and be told. Out right dismissal of our thoughts and queries won't absolve anyone from their irresponsibilities.

sasa muache kuwa mnatoa hoja zisizo na kichwa wala mkia...
Hata zile zenye manyoya tu, nazo za paswa kusikilizwa kwanza.

This is the loss of objectivity in exchange for jazba... mnakuwa kama Michael Moore..lol..
Our objective is to see the economy of our Nation forge ahead, and we know that can be enhanced by curbing unnecessary expenditures within the government and its many institutions.... we certainly won't be doing so while - LoL! :(
 
JF kwenye ni burudani....magari yanayoingia kwenye bajeti ya matumizi ya waziri mkuu hayazidi matano inafurahisha kuona eti kuna mtu analiingiza gari ya RPC kwenye bajeti ya waziri mkuu.. hii fweza ya matumizi haya inapitishwa na bunge hapo inaonekana wakati wa bunge watu mlikua mnasoma fugures tu hamjui zinatumika kwa matumizi gani.. sidhani kama tutafika huko tunakokwenda labda tu nimuulize Mh. Zitto au Dr. Slaa kama kwenye kikao kijacho cha bunge waziri mkuu akawaambia kuwa aliona hela mliyompa kwa matumizi ya ofisi yake ilikuwa nyingi hivyo akaamua kuitumia kwenye shughuli nyingine ya maendeleo ya kujenga barabara huko Rukwa. Kwa kweli kama mtakubaliana na yeye itabidi nijiulize ni kwa mimi tusilivyunje bunge..

But that is not the funny part ambayo ilinibidi nichangie hapa.. hebu mtu mmoja aniambie kwamba kama waziri mkuu asingekuwepo huko hayo magari yangekuwa yanafanya nini.. RC, RPC, DC, OCD etc unaweza kushangaa yanatumia mafuta kidogo yakiwa kwenye msafara wa waziri mkuu ..kwa kuwa yako pamoja basi watu mnaanza kuweweseka.. mara mwisho wa dunia, hela zetu zinafujwa..mafisadi.. kila mtu anasema lake.... kama kila moja lingekuwa linatembea kivyake kila mtu angekaa kimya. Ila siwashangai, watu wakiambiwa kuwa wakinamama kumi wanafariki kila mwezi kwa matatizo ya uzazi sidhani kama itakuwa big deal. Kwa sababu kila mtu anafariki kivyake na anazikwa kivyake ila let say unachukua maiti 120 za akina mama waliofariki kwa matatizo ya uzazi na kuwaweka pamoja uchelewi kumsikia mwanakijiji anamuomba rais ajiuzuru.

Lakini hii ndiyo new generation hapa JF ambayo imejaa "Copy & Paste Politics" hakuna hoja ya nguvu inayotolewa kabla haijatoka kwenye chombo fulani cha habari. Wakati mwingine Rev. na Mwanakijiji wanajitahidi kuanzisha hoja lakini tatizo linakuja hoja zao nyingi naweza nikaziita ni "Burger King Politics"... at Burger King you order you want it what and how you want it. It should be what and how WE want.
 
Mbona hayo machache? Yapo yaliyotangulia kabla hajaondoka. Na yanayomsubiri huko aendako
 
sam karibu tena,

....michango yako inahitajika hapa JF.......usipotee sana
 
Back
Top Bottom