Bajeti Tanzania

muchetz

JF-Expert Member
Aug 16, 2010
943
732
Kwa yeyote ambaye anaufahamu wa mambo ya bajeti/uchumi naomba kuuliza.

Kwa mujibu wa bajeti yetu ya mwaka huu (na miaka iliyopita zinafanana), tunatumia 70% kufanaya maendeleo ya 30%(kwa mkopo). Percent zinatofautiana kidogo kutoka mwaka hadi mwaka.
Maswali

1. Kwa staili ya bajeti hii sio kwamba tuko kwenye mzunguko "cycle" usioisha wa kukopa ili kufanikisha matumizi kwajili ya maendeleo ambayo hatufanyi sababu kila bajeti tunalipia madeni kwajili ya matumizi ya bajeti iliyoisha?

2. Kwanini bajeti zetu zisiwe mfano 40% matumizi ya kufanyia maendeleo 60%? kwanini uwiano unakuwa kinyume? Ni lazima (requirement) ya kiuchumi au?

3. Kwenye hizo bajeti za matumizi ya serikali wanalipia nini (hiyo 70%) iwapo maendeleo wanayotarajia kufanya ni 30% pekee? Mfano nataka kuzalisha shs 20 logic ya kutumia shs 60 kutengeneza shs 20 inakuwa justified vipi?

Kwa machache hayo mwenye kujua mambo hayo ya bajeti naomba anipe ufafanuzi kidogo.
 
Back
Top Bottom