Bajeti imewajali watoto katika afya na elimu: Mchumi aliyebobea Dr. Dk. Daniel Ngowi

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,896
1,862
Wadau,
Huku baadhi ya watu, hasa wanasiasa ambao kitaaluma wengi sio wachumi wakionyesha kutoridhishwa na bajeti ya 2012/2013. Mchumi aliyebobea amesema bajeti inawajali sana watoto lkatika afya na elimu.



Na Ninaeli Masaki,

Imeelezwa kuwa bajeti mpya ya mwaka 2012/13 ina mwelekeo mzuri katika kuwajali watoto kwa kuwa imetoa kipaumbele katika sekta za elimu na afya.

Akizungumza katika warsha ya waandishi wa habari iliyohusu bajeti ya watoto, mchumi wa kujitegemea Dk. Daniel Ngowi, alisema nchi inatakiwa kupanga bajeti ambayo ni rafiki kwa mtoto kwasababu zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania ni watoto.

"Serikali inatakiwa kupanga bajeti inayokidhi mahitaji ya kundi kubwa la wananchi na zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania ni watoto…naona ni vyema kwamba bajeti haijawasahau watoto katika sekta ya elimu na afya," alisema Dk. Ngowi.

sosi: :: IPPMEDIA
 
Bw ngowi, sidhan km umezaliwa jana, bajeti ya serikali cku zote nitamu kuisikia masikioni. Lakini je, wanaitekeleza?. Hilo ndio swali. Tumesha choka kusifiana. Bajet ya mwaka jana mliisifia sana nyinyi mnaojiita wachumi, je imetelezekeka?. Uchumi unashuka nyie wachumi mnasema unapanda.
 
Wachumi wanaoangalia kwanza ukubwa wa vitambi vyao, kisha wanafanya utafiti wa matumbo yao,hasa wanapochuku Ph.D zao. Mwigulu anaheshimika sana na ccm kuwa mchumi wao wa drj la 1, kumbe utaalam hasa na wa kweli ni mchumi nambari wani wa kuchukua wake za makada wenzake wakati wa kampeni za chaguzi ndogo. Shame on him!
 
huyo kilaza , vip afya, alafu angeongea dk.prosper ngowi tungemuamini.. Alafu prof lipumba ndo mtasha.zaidi. Kuliko huyo daniel ngowi.. Prof. Anaipinga h!yo bajeti
 
We Tume ya katiba ubongo wako unauhalo kuna shule zina choo kimoja dar achilia madawati watoto wanakaa chini
 
Last edited by a moderator:
We Tume ya katiba ubongo wako unauhalo kuna shule zina choo kimoja dar achilia madawati watoto wanakaa chini
 
Last edited by a moderator:
Tusiwe wakali sana jamani, nimemsikia huyu Dr. Ngowi mara nyingi tu akisema kuhusu udhaifu na mapungufu ya bajeti. Huyu mleta mada kama kawaida ya wale wanaochukua neno moja na kulikuza kuwa kubwaaa, hajasifia bajeti nzima. Wasomi wanaosifia hii bajeti ni vipofu wa CCM.
 
Back
Top Bottom