Bajaji za Wajawazito, Uhalisia na Vipaumbele vya Taifa

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Jana tarehe 9/3/2011 Waziri wa Afya alizindua Pikipiki za tairi tatu kwa ajili ya kusafirisha wanawake wajawazito kupata huduma katika maeneo mengi ya Tanzania (Kwa mujibu wa Tanzania Daima la leo)

Tunashukuru, kwani hii ilikuwa ni mojawapo ya ahadi alizotoa JK wakati anaomba kura. Ahadi hii aliitoa tarehe31/08/2010 Wilayani Chunya.

Sambamba na uzinduzi huu wa serikali, gazeti la Habari Leo lina taarifa kwamba shirika lisilo la kiserikali la Care International limetoa msaada wa pikipiki za tairi tatu kwa vijiji 11 wilayani Kigoma. Tarehe 10/05/2010 Waziri mkuu Pinda aliagiza halmashauri za mkoa wa Rukwa kununua pikipiki za tairi tatu kwa ajili ya Wajawazito.

Wakati huo huo, iliripotiwa Bungeni tarehe 15/02/2010 kuwa Wabunge watapewa mikopo ya shilingi 90bil kujinunulia magari (Jumla kuu takribani 3.2 bil). Ikumbukwe pia kwamba takribani theluthi moja wa wabunge wote ni wanawake, 102 kati yao wakiwa ni wabunge wa viti maalum (kutetea haki za wanawake)

Waziri wa afya alitangaza kwamba pikipiki hizi kila moja inagharimu dola za kimarekani 5,900 (sijui swala la value for money). Hii ina maana kwamba kwa pikipiki 400 alizoahidi JK zinagarimu takribani shilingi 4 bil.

Uhalisia
Wachambuzi wa mambo wamekosoa mpango huu wa kununulia wajawazito pikipiki za tairi tatu badala ya gari. Sababu zinazotolewa ni pamoja na kwamba katika hali halisi mwanamke mjamzito aliye kwenye uchungu atapata karaa na mateso kusafirishwa kwa hiyo bajaji. Naomba angalia picha ya hiyo bajaji kisha ujiulize yafuatayo;

Mjamzito amefungiwa peke yake kitandani na msaidizi amekaa nyuma ya dereva, mjamzito atapataje usaidizi akiwa safarini? Mvua ikinyesha? Jua kali? Vumbi? Mtoto akitoka wakati bajaji ikiwa mwendo kasi? Mjamzito anatokwa na damu au majimaji, nani atamhifadhi njiani? Bajaji hii inaweza kumsafirisha mjamzito umbali gani (wale mnaotoka vijijini mnapata picha hapa)? Kule milima ya Uluguru itafika? Barabara za vijijini mbovu itamudu?

Vipaumbele
1. Wabunge wakae bungeni kwa garama kubwa wakipiga porojo na vijembe wakati wajawazito hawana huduma?
2. Wabunge wajinunulie magari mazuri wajawazito usafiri wa karaa na mateso?
3. Dowans walipwe haraka wajawazito wasubiri au wapewe bajaji?
4. JK na msururu wake watalii dunia wajawazito wataabike?
5. Kilimo kwanza ya wakubwa wanunuliwe power tillers wajawazito wanunuliwe bajaji? Kwani mkulima mkuu nchi hii ni mwanaume au mwanamke?
6. Halmashauri zinadekezwa kufuja mabilioni wakati hatuna pesa za kujali wanawake waliotuzaa?
7. Je, huu mpango wa kusafirisha wajawazito kutumia pikipiki ni sera iliyopitishwa na wajawazito wenyewe? Tunaona mashirika ya kimataifa nayo yanaanza kutoa msaada wa bajaji kusafirisha wajawazito ingawa wanaweza kuwa na pesa za kununua magari!
8. Halmashauri sasa zianze kupanga bajeti kununua bajaji kusafirisha wajawazito?
etc, etc.
 

Attachments

  • Bajaji Wajawazito 2.jpg
    Bajaji Wajawazito 2.jpg
    54.8 KB · Views: 49
  • Bajaji Wajawazito.jpg
    Bajaji Wajawazito.jpg
    48.4 KB · Views: 45
Back
Top Bottom