Bajaj, pikipiki ruksa kuwa teksi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Je, wakodishaji wa pikipiki kama taxi watavaa helmets ili kukinga vichwa vyao kama itatokea ajali?

Bajaj, pikipiki ruksa kuwa teksi
Mwandishi Wetu, Dodoma
Daily News; Thursday,January 29, 2009 @21:15​

Bunge limepitisha muswada wa Sheria ya Marekebisho katika Sheria mbalimbali wa mwaka 2008 ambao umegusa marekebisho ya sheria 11, ikiwamo ya leseni za usafirishaji ambayo sasa itatoa leseni za usafiri kwa pikipiki za bajaj na pikipiki za kawaida na hivyo kutambulika kisheria.

Akiwasilisha muswada huo ili usomwe kwa mara ya pili na ya tatu, jana bungeni Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, alisema pia sheria hiyo inakataza matumizi ya baiskeli katika maeneo ya mijini na kuruhusu zitumike vijijini chini ya usimamizi wa halmashauri za wilaya.

Hata hivyo, baadaye wakati akijibu hoja za wabunge, Mwanasheria Mkuu alikiri kuwa bado hakuna sheria katika halmashauri hizo, ambayo itasimamia baiskeli hizo na kuahidi kuwa katika marekebisho ya muswada huo, kifungu cha sheria hiyo nacho kitaongezwa.

Pamoja na sheria hiyo, pia alisema katika sheria ya vizazi na vifo, sasa itakuwa ni lazima kwa kila Mtanzania kujiandikisha tangu anapozaliwa hadi kufa. Mwanyika pia alisema katika sheria ya Mfuko wa Bima ya Afya, sheria hiyo sasa imewaingiza madiwani wote wa kata ambao si wabunge kutibiwa kupitia Mfuko huo, pamoja na watumishi wa umma wastaafu kuendelea kutibiwa nao.

Kwa upande wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu muswada huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, George Lubeleje, alishauri katika sheria ya leseni na usafirishaji ni muhimu kuzingatia uwezekano wa baiskeli kutumika kama chombo cha usafirishaji wa kibiashara, kwa kuwa hutumiwa na wananchi wengi hasa vijijini.

Katika michango yao juu ya sheria hiyo, wabunge wengi walitaka katika marekebisho ya muswada huo uzingatie umuhimu wa kuruhusu baiskeli, nazo zitambulike kisheria kwa kuwa ndizo zinazotumiwa na wananchi wengi wanamudu kuzinunua kuliko pikipiki na bajaj.

Mjadala huo ambao ulichukua muda mrefu kutokana na malumbano hasa katika kipindi cha kupitisha vifungu, ulitokana na ukweli kuwa wabunge wengi walionyesha kutaka baiskeli nayo itambuliwe kisheria. Akiwasilisha hoja zake, Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), alisema itakuwa ni vyema iwapo baiskeli nazo zitatambuliwa kisheria, kwa kuwa watu wa kawaida kama wakulima, wafanyabiashara wadogo na wafugaji ndio wanaozitumia sana.

“Nitashangaa kama Bunge hili litakataa kuunga mkono utolewaji wa leseni za baiskeli, kwani ukweli ni kwamba wabunge wote hapa tumepanda baiskeli, isitoshe itadhihirisha kuwa Bunge hili pia ni la watu wa kawaida,” alisema Cheyo.

Aidha Cheyo, alisema katika Sheria ya Marekebisho ya Bima ya Afya, aliomba kifungu cha 27, kifanyiwe marekebisho ili madiwani watakaopewa huduma ya tiba kupitia Mfuko huo, wapate huduma hiyo hata pale watakapostaafu.

Naye Mbunge wa Magu, Festus Limbu (CCM), alisema waendesha baiskeli ni wajasiriamali ambao wanatafuta kipato chao kwa uhalali, hivyo kutopewa leseni ni uonevu na pia italeta matatizo makubwa hasa kwa vijana ambao wengi wanatumia baiskeli.

“Nadhani baiskeli zitamkwe waziwazi kwenye sheria hii, kwani Bangladesh wanatumia baiskeli tena za miguu mitatu na ndizo zinatumika sana, iweje sisi tushindwe?” Alihoji. Alitoa rai kuwa wenye baiskeli wasibughudhiwe na vyombo vya Dola kwani wanajitafutia malipo halali kwa kazi halali, hivyo wasajiliwe na halmashauri ziwatambue.

Naye Mbunge wa Nkasi, Ponsiano Nyami (CCM), alipongeza marekebisho ya sheria ya Mfuko wa Bima ya Afya, lakini pia alipendekeza uangaliwe na uwezekano wa kuwaingiza wabunge katika matibabu hayo. Pia alizungumzia suala la sheria ya uchawi, ambako alitaka Serikali ichukue hatua za haraka kuhusu imani hizi za ushirikina, ambazo sasa zinazidi kwani tayari kuna tetesi kuwa pamoja na albino, pia watu wenye vipara, viganja vyenye alama ya M na akinamama wenye ndevu nao ni ‘mali’.
 
. Pia alizungumzia suala la sheria ya uchawi, ambako alitaka Serikali ichukue hatua za haraka kuhusu imani hizi za ushirikina, ambazo sasa zinazidi kwani tayari kuna tetesi kuwa pamoja na albino, pia watu wenye vipara, viganja vyenye alama ya M na akinamama wenye ndevu nao ni ‘mali’.
[/COLOR][/SIZE]

Chonde chonde chonde....nina alama ya M nanunua bastola......
 
Je, wakodishaji wa pikipiki kama taxi watavaa helmets ili kukinga vichwa vyao kama itatokea ajali?

Bajaj, pikipiki ruksa kuwa teksi
]

BABU,
Uamuzi huu kuhusu BAJAJI, na PIKIPIKI umefanyiwa upembuzi yakinifu?
Vinginevyo utazua matatizo badala ya kupunguza matatizo.
 
Je, wakodishaji wa pikipiki kama taxi watavaa helmets ili kukinga vichwa vyao kama itatokea ajali?

Bajaj, pikipiki ruksa kuwa teksi
Mwandishi Wetu, Dodoma
Daily News; Thursday,January 29, 2009 @21:15​

Bunge limepitisha muswada wa Sheria ya Marekebisho katika Sheria mbalimbali wa mwaka 2008 ambao umegusa marekebisho ya sheria 11, ikiwamo ya leseni za usafirishaji ambayo sasa itatoa leseni za usafiri kwa pikipiki za bajaj na pikipiki za kawaida na hivyo kutambulika kisheria.

BAK, hizi helmet ni nzuri kukinga kwa ajali, lakini huoni kutakuwa kuna kuambukizanamagonjwa ya ngozi kichwani?.

Akiwasilisha muswada huo ili usomwe kwa mara ya pili na ya tatu, jana bungeni Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, alisema pia sheria hiyo inakataza matumizi ya baiskeli katika maeneo ya mijini na kuruhusu zitumike vijijini chini ya usimamizi wa halmashauri za wilaya.

Mwanyika pia alisema katika sheria ya Mfuko wa Bima ya Afya, sheria hiyo sasa imewaingiza madiwani wote wa kata ambao si wabunge kutibiwa kupitia Mfuko huo, pamoja na watumishi wa umma wastaafu kuendelea kutibiwa nao.

Aidha Cheyo, alisema katika Sheria ya Marekebisho ya Bima ya Afya, aliomba kifungu cha 27, kifanyiwe marekebisho ili madiwani watakaopewa huduma ya tiba kupitia Mfuko huo, wapate huduma hiyo hata pale watakapostaafu.

Naye Mbunge wa Nkasi, Ponsiano Nyami (CCM), alipongeza marekebisho ya sheria ya Mfuko wa Bima ya Afya, lakini pia alipendekeza uangaliwe na uwezekano wa kuwaingiza wabunge katika matibabu hayo. Pia alizungumzia suala la sheria ya uchawi, ambako alitaka Serikali ichukue hatua za haraka kuhusu imani hizi za ushirikina, ambazo sasa zinazidi kwani tayari kuna tetesi kuwa pamoja na albino, pia watu wenye vipara, viganja vyenye alama ya M na akinamama wenye ndevu nao ni ‘mali'.

Kwa hili, watu wa Bukoba mjini kwenye pikipiki kibao, ambao walikuwa hawaishi kukamatwa na polisi ni furaha kwao. Na wale wasio na uwezo wa kuwekeza ktk magari, basi watajaribu kwa pikipiki. Lakini kuondoa baiskeli maeneo ya mijini hilo ni kosa kubwa sana, sasa wanataka watu watembee kwa miguu, baiskeli ni usafiri rahisi, pia hutumika kukwepa foleni kwa walio nazo. Kwa watu walio wengi wa mji wa Tanga (Mwanzange upo?) hili litapata upinzani mkubwa mno. Nakumbuka mambo ya kuzisajili enzi hizo (vipande).

Kama madiwani wanaombewa kutibiwa na mfuko wa Bima ya afya hata pale wanapostaafu. Diwani akiingia na umri wa miaka 18, akastaafu baada ya miaka 5, atakuwa na miaka 23, ina maana aanze kulipiwa kuanzia miaka 23, jee wafanyakazi wengine vipi?, na mkulima jee?. Na wabunge nao wanaomba waangaliwe!!!.

Kuhusu hili la ushirikina, kama sasa na wenye upara, wenye alama M kiganjani na wasichana wenye ndevu wanatafutwa, Taifa linaelekea kubaya. Na kama tunafikia huko, tutaelekea kubaya zaidi kwa wanaowindwa kuongezeka siku hadi siku. Eeh Mola tusaidie...
 
Je, wakodishaji wa pikipiki kama taxi watavaa helmets ili kukinga vichwa vyao kama itatokea ajali?
[/COLOR][/SIZE]

BAK, nachelea kusema kuwa yawezekana hizi helmet japo ni muhimu kwa kujikinga wakati wa ajali, lakini yawezekana zikasambaza magonjwa ya ngozi.
 
Hii ruksa ya bajaj na pikipiki imesaidia sana kwani vijana walikuwa wanaruhusiwa wakati wa kampeni za uchaguzi na ukiisha polisi wanawaonea hata hao wanasiasa walikuwa hawatetei.
 
Nina wasiwasi na matumizi ya pikipiki kwenye miji yenye msongamano mkubwa wa magari kama Dar es Salaaam....matumizi ya pikipiki yataongeza ajali katika miji hiyo...lkn pia yataharibu madhali ya mji.....ngoja tusuburi na tuone...
 
Nakubaliana nawe kabisa kuhusu Dar. Zikisha kuwa nyingi kupita kiasi na ajali za pikipiki kuongezeka kwa 200% basi watataka kuzipiga marufuku ili zisiwe taxi tena. Tusubiri tuone.
 
Nakubaliana nawe kabisa kuhusu Dar. Zikisha kuwa nyingi kupita kiasi na ajali za pikipiki kuongezeka kwa 200% basi watataka kuzipiga marufuku ili zisiwe taxi tena. Tusubiri tuone.

Binafsi sina tatizo na kuweka mazingira ya kupunguza kero na matatizo ya wananchi. Hata hivyo nakerwa na tabia ya serikali kuziba pengo moja kwa kutoboa mengine mawili. Nadhani sheria ingetamka kabisa kuwa baiskeli na pikipiki zitatumika pale tu ambapo njia maalum zimewekwa kwa ajili ya vyombo hivyo. Kama si hivyo itakuwa hatari sana. Kwa miji kama Tanga, baiskeli na pikipiki zinaongoza kwa kusababisha ajali za barabarani. Na mwenye gari hana haki barabarani. Naogopa sana,.. baada ya kupewa leseni hali itakuwa mbaya sana kama ilivyo Delhi. Katika jiji hilo ni bahati sana kupanda bajaji ukafika unakoenda bila kugonga kitu (ama bajaji nyingine au gari). Kwa hiyo bila kuongelea suala la njia za baiskeli, pikipiki na waenda kwa mguu mijini tutakuwa tunamwaga petrol kwenye moto! Hata hivyo 2010 iko karibu na watu lazima sasa wajionyeshe kuwa wanawajali wapiga kura!!
 
jamani yaani kabisa kabisa mkewangu ndevu atapeleeka wapi kwa style hii mtaua kila mmoja mpaka wenye viungo virefu vya uzazi sasa!!!!
 
Bajaji ni uchafu katika mji na baada ya muda mtakuja kuviona wenyewe,maana msongamano wake treni ni fupi,na njia zetu hizi za ulimi wa nyoka ndio kabisa,mtaani kutakuwa hapatoshi,na vibaka nao itawawia rahisi kukwapua vizigo vilivyolemaa.
 
Back
Top Bottom