Bainisha na ainisha

Yusuph Salehe

Member
Nov 12, 2010
58
1
Habari zenu wakuu? Leo nimekuja na hili ninashida ya kutofautisha maneno haya BAINISHA na AINISHA.
Mfano: Bainisha na ainisha maneno yafuatayo
1. Anakikimbia
2.Anakula
Naombeni msaada wenu jamani.
 
Habari zenu wakuu? Leo nimekuja na hili ninashida ya kutofautisha maneno haya BAINISHA na AINISHA.
Mfano: Bainisha na ainisha maneno yafuatayo
1. Anakikimbia
2.Anakula
Naombeni msaada wenu jamani.

Hapa unazungumzia sarufi na matumizi ya lugha.

A-na- ki-kimbia
Hapa kuna nafsi mbili tofauti..A mtenda na -ki- mtendwa..-na- ni wakati wa sasa--kimbia ni tendo analofanya mtenda.

A-na-kula
Hapa kuna mtenda tu -A- inayofuata -na- ni wakati wa sasa, -kula- ni tendo analofanya mtenda.

Nililofanya hapo juu ni kuainisha mofimu zilizounda tungo..sasa kubainisha sijui umekusudia nini kwani nijuavyo kubainisha inaongelea matumizi tofauti ya mofimu au neno katika tungo na hapo hukuliweka wazi.

Pia ni jumla jumla tu uchambuzi nilioufanya mimi, kwa sababu hata kitendo unaweza kukichambua viishio vyake.
 
Habari zenu wakuu? Leo nimekuja na hili ninashida ya kutofautisha maneno haya BAINISHA na AINISHA.
Mfano: Bainisha na ainisha maneno yafuatayo
1. Anakikimbia
2.Anakula
Naombeni msaada wenu jamani.
Mkuu.
Baada ya kusoma tena mada yako nimekuelewa sasa. Mfano wako uliotumia ulinibabaisha.
Shida yako ni uelewa wa tofauti kati ya Bainisha na ainisha.
Bainisha ni kuonesha matumisi ya lugha kwa mfano:-
………………………………………………………………………………………………………………...
Bainisha matumizi ya ‘ni' katika sentensi zifuatazo:
i) Amkeni …………………………………………………………………………………………………
ii) Ni mchezo mzuri sana

Wakati ainisha inatumika katika kukutaka uoneshe tungo imejengekaje kama nilivyochambua katika mchango wangu wa mwanzo. Uchanganuzi wa tungo. vijenga tungo wakati kubainisha ni kuonesha matumizi tofauti ya neno au kijineno katika tungo.

Natumai nimechangia lakini weledi watakuelewesha zaidi.
 
Mi navyoelewa kwanza samahani katika kukujibu sitatumia maneno uliyotoa, nianze na neno ainisha, hapa maana yake ni kueleza ama kutoa aina ikiwa ni aina za maneno tungo, virai, vishazi nk mf. Ainisha vishazi katika sentensi hii; Ng'ombe aliyevunjika mguu amekufa. Hapa tungo -aliyevunjika mguu ni kishazi tegemezi na Ng'ombe amekufa ni kishazi huru hapo nimeainisha. Tukija sasa kubainisha navyoelewa mimi ni kuweka kitu bayana, kufichua mf. Bainisha aina ya maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa, BABA YANGU alinunua BAISKELI nzuri, kwahiyo BABA-jina au nomino, YANGU-kivumishi,BAISKELI-nomino, nadhani utanielewa nakaribisha changamoto au maboresho
 
Mmh! Kidogo nimeelewa ila sana nimechanganyikiwa
Bainisha (show.state clearly)....weka bayana matumizi ya neno au kineno,kishazi.
Ainisha...(classify) onesha aina ya mofimu zinazounda neno,tungo au setensi.
Mkuu..bado huoni ndani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom