Bagamoyo kuuzwa haikubaliki-wenyewe tupo.

Nina kishamba changu huko Mapinga, naomba mnijulishe ili niamue kusuka au kunyoa!!! Je na chenyewe kitakuwa kimemezwa na EPZ???
 
Katika moja ya mada zilizopita kulikuwa na Mada moja ilikuwa inaongelea Waziri Muhongo akataa mwekezaji mwenye dollar 20 mill. mdao bila kujali uwekezaji huo ulikuwa na masharti gani alilaumu kuwa hiyo ni hujuma. Mwingine leo analalamika kuwa bagamoyo imeuzwa kwa kuwa kuna mwekezaji mkubwa anapewa hilo eneo kwa njia ya EPZ.

Hawa wote wenye maoni kama haya ni watanzania. Siku zote na shindwa kuelewa ni lipi jema kwetu wtz? do we real know what we want? au tunaongea tu pale tunajisikia kuongea na kupinga kila kitu na kuingiza siasa zisizokuwa na maana. Mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini pia siamini kuwa kama ccm ikiondoka madarakani chama kitakachotawala kitafukuza wawekezaji na waachia wazawa kuendesha miradi yote mikubwa. Kama ndiyo huo utakuwa mwanzo wa kuianganiza kabisa Tanzania na itakuwa muhimu kwa wtz kuwa makini na wanasiasa wanaohubiri siasa zenye malengo ya kupinga uwekezaji wa nje. Hakuna nchi hapa duniani ambayo inakataa wawekezaji kutoka nje. Hata China ambao ni communist country hivi sasa wanakaribisha makampuni makubwa kwenda kuwekeza kwao. Sisi wtz tunahubiri kukataa uwekezaji. Nadhani imefika mahali sasa tuwe makini, vinginevyo tunaandika vitu ambavyo hatumaanishi katika uhalisia.

Kaka itikadi zinatumaliza watu humu ndani wameacha kujadili hoja wanajadili vyama,suala la uwekezaji ni kero,kwa vyovyote vile sera hii inayoendelea itasababisha vizazi vijavyo kuishi km wakimbizi kwani wawekezaji wanapewa maeneo ambayo yanatumiwa na watu wa hali ya chini badala ya kupewa maeneo yasiyotumiwa. Tunaona namna wananchi wanavyoondolewa mijini na kutupwa maporini kwa kigezo cha kuendeleza miji. Pia wananchi wananyang'anywa viwanja wanauziana wakubwa,ukweli inauma na awamu ya nne ndio inaongoza kwa unynyasaji, wananchi wakichachamaa utasikia wanasema chama fulani cha upinzani kinahusika ni folish minds
 
Nakubaliana nawe Mkuu ila tatizo kubwa tulinalo ni kwamba ndai ya Serikali hii kumejaa mataahira (I am very sorry to say so) ambao hawaoni athari kubwa siku za usoni za hizi sera za za kifisadi za kuiuza nchi huku na kule bila hata woga.

Imefika wakati kuiangalia upya hii sera ya uwekezaji, kumekuwa na malalamiko ya utekelezaji wake karibu nchi nzima. Kama nakumbuka vizuri hii sera iliibuka sana kipindi cha awamu ya tatu ya uongozi wa nchi, naomba kujuzwa hii sera haina mwisho??
Nionavyo hii nchi itaingia kwenye ukombozi mwingine,huko nyuma tulijikomboa kisaisa kutoka kwenye mikono dhalimu ya wakoloni na huko tuendako hali itakuwa ngumu sana wakati watoto na wajukuu zetu watakapokuwa wanatafuta ukombozi wa kiuchumi katika nchi yao wenyewe. Nasema haya kwa nia njema tu na sio uchochezi kama baadhi yetu mtakavyotafsiri.
 
Nakubaliana nawe Mkuu ila tatizo kubwa tulinalo ni kwamba ndai ya Serikali hii kumejaa mataahira (I am very sorry to say so) ambao hawaoni athari kubwa siku za usoni za hizi sera za za kifisadi za kuiuza nchi huku na kule bila hata woga.

Taahira sio tusi, maana yake " ni mtu mwenye akili iliyochelewa kupevuka kulingana na unri wake" . Kamusi ya Kiswahili fasaha, Oxford, Baraza la Kiswahili Zanzibar, 2010.

Wanachofanya ni kiashiria cha utaahira
 
Katika moja ya mada zilizopita kulikuwa na Mada moja ilikuwa inaongelea Waziri Muhongo akataa mwekezaji mwenye dollar 20 mill. mdao bila kujali uwekezaji huo ulikuwa na masharti gani alilaumu kuwa hiyo ni hujuma. Mwingine leo analalamika kuwa bagamoyo imeuzwa kwa kuwa kuna mwekezaji mkubwa anapewa hilo eneo kwa njia ya EPZ.

Hawa wote wenye maoni kama haya ni watanzania. Siku zote na shindwa kuelewa ni lipi jema kwetu wtz? do we real know what we want? au tunaongea tu pale tunajisikia kuongea na kupinga kila kitu na kuingiza siasa zisizokuwa na maana. Mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini pia siamini kuwa kama ccm ikiondoka madarakani chama kitakachotawala kitafukuza wawekezaji na waachia wazawa kuendesha miradi yote mikubwa. Kama ndiyo huo utakuwa mwanzo wa kuianganiza kabisa Tanzania na itakuwa muhimu kwa wtz kuwa makini na wanasiasa wanaohubiri siasa zenye malengo ya kupinga uwekezaji wa nje. Hakuna nchi hapa duniani ambayo inakataa wawekezaji kutoka nje. Hata China ambao ni communist country hivi sasa wanakaribisha makampuni makubwa kwenda kuwekeza kwao. Sisi wtz tunahubiri kukataa uwekezaji. Nadhani imefika mahali sasa tuwe makini, vinginevyo tunaandika vitu ambavyo hatumaanishi katika uhalisia.

suala ni wanawekeza wapi na mikataba inasema nini. ni wazi wawekezaji hawekezi hapa kwa kuwa wanatupenda bali kwa ajili ya faida yao. hivyo ni wajibu wa serikali kuwa makini na kuhakikisha kwamba pamoja na wawekezaji kupata faida nchi nayo inafaidika. hapo ndipo penye busara.
 
Mwaka 2007 niliweka mada hapa iliyohusu uuzaji huu. Iko hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/137815-public-debate-on-land-grabbing-in-tanzania-2.html

Nilitaja vile vile kwamba mie kwa sasa ni wa Bagamoyo, pamoja na kwamba nilizaliwa kwingine. Nilitabiri kwamba hata huko Kilimanjaro nilikotoka watauza, na nikalalama kuhusu uuzaji wa sehemu mbali mbali za Tanzania kama ifutayo (July 14, 2007).

The Bones of My Ancestors

I am concerned, very concerned, about the bones of my ancestors. It so happens that my ancestors are buried on the slopes of Mount Kilimanjaro, and there is every possibility that the government will one day either rent out or sell the whole area, to an investor. It would appear that they are already in the process of renting out most of the Lake Eyasi area to some hunting company from the UAE. I have attached below an article that alludes to just that.

At one level, I am mightily amused. Why lease out that land to a hunting firm while it is already inhabited by the Hadzabe, who are great hunters? The Lake Eyas area is already full of hunters, namely the Hadzabe people. Why lease it out to a foreign hunting firm?

Now, once Lake Eyas is leased off (or sold off, whichever comes first), what will they sell next? I am afraid that it will be Mt. Kilimanjaro. That would be awfully attractive to any investor. But then, what would such an investor do to the bones of our many ancestors who are buried there?

Augustine Moshi
 
Watanzania wengi wamewekeza kwa uwezo wao wote eneo la karibu na barabara toka Dar hadi Bagamoyo. Ni kujidharau sisi wenyewe kusema ondokeni amepatikana mwekezaji. Sisi tumeshawekeza kwenye vijiekari vyetu vidogo vidogo.

Kidogo chako ni bora kuliko kikubwa cha mwenzio.

Hatukatai wawekezaji. Wawekeze sehemu zilizo wazi. Ni ukoloni mambo leo kutufukuza nyumbani kwetu ili tumpishe mwekezaji. Kama mnataka tutafute kwingine maporini, kwanini wasifanye hivyo hao wawekezaji wenu?
 
Tatizo sio sera ya uwekezaji, tatizo ni aina ya viongozi tulionao. Wakiona watapata vijisent hata kama wanachofanya kinamadhara makubwa na kuhatarisha mustakabal wa taifa hawajali. Ethiopia inpokea wawekezaj lakin wapo strict, hawakubali upuuzi huu tunao uona na wapo mbali kimaendeleo. Tz tumebaki na viongoz wezi, mafedhuli na wehu. Ni wehu kwasababu wanajiibia na kuibia ndugu zao.
 
Najiuliza swali la msingi. Usalama wa taifa wapo wapi kudhibiti upuuzi huu na mwingine.. Hawa si ndio wamefunzwa kuitumikia nchi na kupewa dhamana kubwa ya usalama wa taifa hili. Hawana uwezo au wamelewa hela na madaraka. Faida tunayoipata kwenye mikataba ya madini kama nchi ni chini ya asilimia 5 ukilinganisha na faida wanayopata waweklezaj kwenye soko la dunia! Haitosh bado tunaibiwa kwenye nishat ya umeme mikataba yaajabu kwa faida ya wachache! Maziwa mangapi wawekezaj wanafanya wanavyotaka ardhi ndio usiseme. Tunakwenda wapi? Nani wakusitisha haya kama sio usalama wa taifa? Au hayatishii usalama? Naamin walioasisi aman na mshikamano wa hii nchi walitumia hichi kitengo vizuri kisipo amka kitaendelea kupoteza heshima yake hadi. Mnaishije na jamii inayonyanyaswa kila siku?
 
Katika moja ya mada zilizopita kulikuwa na Mada moja ilikuwa inaongelea Waziri Muhongo akataa mwekezaji mwenye dollar 20 mill. mdao bila kujali uwekezaji huo ulikuwa na masharti gani alilaumu kuwa hiyo ni hujuma. Mwingine leo analalamika kuwa bagamoyo imeuzwa kwa kuwa kuna mwekezaji mkubwa anapewa hilo eneo kwa njia ya EPZ.

Hawa wote wenye maoni kama haya ni watanzania. Siku zote na shindwa kuelewa ni lipi jema kwetu wtz? do we real know what we want? au tunaongea tu pale tunajisikia kuongea na kupinga kila kitu na kuingiza siasa zisizokuwa na maana. Mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini pia siamini kuwa kama ccm ikiondoka madarakani chama kitakachotawala kitafukuza wawekezaji na waachia wazawa kuendesha miradi yote mikubwa. Kama ndiyo huo utakuwa mwanzo wa kuianganiza kabisa Tanzania na itakuwa muhimu kwa wtz kuwa makini na wanasia sa wanaohubiri siasa zenye malengo ya kupinga uwekezaji wa nje. Hakuna nchi h apa duniani ambayo inakataa wawekezaji kutoka nje. Hata China ambao ni communist country hivi sasa wanakaribisha makampuni makubwa kwenda kuwekeza kwao. Sisi wtz tunahubiri kukataa uwekezaji. Nadhani imefika mahali sasa tuwe makini, vinginevyo tunaandika vitu ambavyo hatumaanishi katika uhalisia.
Wacha Uoga kwahiyo Tanzania kabla ya Wawekezaji ilikuwa imeangamia? oi Tulikuwa na aina nyingi za Viwanda tulivyoviongoza wenyewe uongozi mbovu ndio ulitumaliza sasa hivi kuna wawekezaji waliopo kwa ajili ya nchi wanazotoka so ni bora waondoke tu kwani hakuna tunalofaidika na wao Zaidi ya kuona Bidhaa zikipanda bei kila kukicha... au wewe unafidika nao?

Wakiondoka hawa tutawepa kujiendesha kwa Sheria Kali tu Tutaweza Tusomeshe Wataalamu wa Sayansi tuwe na viwanda vya kila zao tunaozalisha hapo ndio utajua kuwa hawa unaowaita wawekezaji si laolote bali ni Wakoloni tu p/zao

Wacheni uoga Watanganyika Zindukeni Mmelala usingizi wa Pono Nadhani Tutafute Kauli Mbiu ya Kuwafukuza Wakoloni kama ule wa MAUMAU(Mzungu arudi Ulaya Mwafrika Apate Uhuru)
 
Katika moja ya mada zilizopita kulikuwa na Mada moja ilikuwa inaongelea Waziri Muhongo akataa mwekezaji mwenye dollar 20 mill. mdao bila kujali uwekezaji huo ulikuwa na masharti gani alilaumu kuwa hiyo ni hujuma. Mwingine leo analalamika kuwa bagamoyo imeuzwa kwa kuwa kuna mwekezaji mkubwa anapewa hilo eneo kwa njia ya EPZ.

Hawa wote wenye maoni kama haya ni watanzania. Siku zote na shindwa kuelewa ni lipi jema kwetu wtz? do we real know what we want? au tunaongea tu pale tunajisikia kuongea na kupinga kila kitu na kuingiza siasa zisizokuwa na maana. Mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini pia siamini kuwa kama ccm ikiondoka madarakani chama kitakachotawala kitafukuza wawekezaji na waachia wazawa kuendesha miradi yote mikubwa. Kama ndiyo huo utakuwa mwanzo wa kuianganiza kabisa Tanzania na itakuwa muhimu kwa wtz kuwa makini na wanasiasa wanaohubiri siasa zenye malengo ya kupinga uwekezaji wa nje. Hakuna nchi hapa duniani ambayo inakataa wawekezaji kutoka nje. Hata China ambao ni communist country hivi sasa wanakaribisha makampuni makubwa kwenda kuwekeza kwao. Sisi wtz tunahubiri kukataa uwekezaji. Nadhani imefika mahali sasa tuwe makini, vinginevyo tunaandika vitu ambavyo hatumaanishi katika uhalisia.
Uwekazaji sawa, lakini uwe kwa vitu tulivyokubaliana kuwekeza sio kwa style hii ya mlipuko. msije wekeza hata familia zetu.
 
Back
Top Bottom