Bagamoyo Airport or Extension of JKN Intl. Airport?

uko serious ati dar vindege tuchache?

Yes, inategemea uncompare na wapi na unaangalia nini?

kwangu mimi ni vindege vichache na ndio tunakarabati lanes za kutua; priorities and prioritization is key here
 
Dar ndege unahesabu, ndio wanasema think big watakuwa wanarusha ndege kutoka Dar hadi Bwagamoyo. Returm flight itakuwa dola 100. Nyingine itakuwa Chalinze Bwagamoyo abiria watakuwa watumwa wanaofanya kazi Ikulu ya Bwagamoyo.
 
kwa kifupi ninacho maanisha ni kwamba ukitaka kuleta maendeleo sehemu yoyote ile, basi ni vizuri ukaanza na kujiwekea hali ya kuleta hayo maendeleo, sasa tukirudi kwenye suala la Bagamoyo iwe mlingotini nk , tuanze na barabara ambazo zitaunganisha na sehemu zingine za nchi , kwani suala la kiuchumi ni la kutegemeana, jingine ni kuwa na usafiri wa reli mzuri, ambao baadae uta support hiyo processing zone hapo bagamoyo, maana usitegeme pamba itakuja kwa ndege/tumbaku nk nk, na jingine ni la umeme ambao litachoche elimu bora, uzalisha, na mazingira yote kwa ujumla, maana hata hiyo airport inategemeana na uwepo wa nyenzo kama umeme na watu wenye elimu bora.
kwa hiyo wote tuwekeze akili zetu na nguvu zetu kwenye vitu kama hivyo basi maendeleo mengine yatakuja kwa urahisi na speed inayotakikana bila kuathiri nguzo za kiuchumi ama sivyo tutajiwekea dhana ya kwamba mimi kwetu kumesahaulika nataka hichi nataka kile halafu kikiwekwa hakikusaidi kwa sababu umeacha vitu vya msingi.
kwa hiyo kwenye nia yako au plan naomba uanze na vitu vya msingi, na kama unaukaribu na viongozi/mbunge wako naomba uwaeleze kuwa usafiri bora (barabara, Reli) ambao utatuwezesha sisi wafanyakazi kutoka sehemu mbali mbali za tanzania kuja bagamoyo kufanya kazi au kuleta mali ghafi zetu kwa ajili ya epz na Nguvu za Umeme ndio utachochea maendeleo mengine, iwe bandari, airport nk na vitu hivi sio vinakuja overnight vinahitaji mipango ya muda mfupi , kati na muda mrefu
maelezo mengine naona Mkandara nae kaelezea vizuri suala hili.

Mkulu,

Sitaki ionekane kama tunabishana,nataka kukuambia kwamba mimi nakubariana na sababu zako,hasa zile za msingi ambazo wewe na wachangiaji wengine mmezitoa.
Ila kwako inaonyesha wazi kwamba sababu zako nyingine si za msingi kwani hata jogulafia ya maeneo husika huiju na mipango ya serikali inayoendelea kwa maana ya projects either za barabara na hata za mpango mzima wa EPZA ambao umeshaanza pia hujui au hujaona.
Kwa benefit yako na wengine amabao hawalijui hili inawezekana wako nnje ya inchi,Serikali ilishaanza kujenga miundombinu ya hiyo zone ya EP kwa kushirikiana na nchi wanachama wa EA toka hatua za mwanzao mwazo wa kuunda upya wa umoja wao,awamu ya 3 ya uongozi hapa kwetu.mfano barabara ambayo ilianza kujengwa kwenye mpango huu ni ile iliyokua ikiunganisha mkoa wa Tanga na Mombasa,kuanzia maeneo ya Mabokweni mapaka Horohoro kupitia Duga Mafoloni,hii ilishaanza hata Kikwete hajapendekezwa na NEC kugombea na fasasi ya Urais,let alone Kawambwa
Lengo likiwa kuonganisha Mombasa Tanga na hii EPZ kwa kutumia barabara,kwani reli ya kuonganisha maeneo hayo ipo ila ilihitaji kukarabatiwa tu na kuonganisha vipande vichache vichache ambapo kwa bagamoyo kwenye hiyo zone yenyewe kipande kisicho zidi km 30 kinahitajika kuonganisha.kwa sasa ile reli ya kati iliyo kua ikionganisha Dar na Tanga inapita maeneo ya wilaya ya Bagamoyo sehemu za Kidomole,si zaidi ya km nilizo zitaja hapo juu kutoka maeneo ya EPZ.
Kwa kuongezea pia barabara imeshaanza kujengwa na ipo kwenye hatua za mwisho kutoka Chalinze(ikionganisha mikoa ya kati) kwenda Segera zikiwekwa njia nne(watu walimkosoa kawambwa kwenye hili),na Msata (maungio yanayo uganisha wilaya ya bagamoyo na njia hii kubwa kwenda Tanga) kurudi Bong"wa wilaya ya Bagamoyo ambapo pia imesekana barabara nne zitajengwa mpaka either Mbuyuni njia ya kwenda kunduchi au Mwenge(hii itarahisisha sana usafiri kwenda na kutoka maeneo hayo,na hata wale wenye nyumba ambao wanalalamika kodi kushuka watakua na nafasi tena ya kupandisha) .

Swala la umeme,ingawa Mlingotini kunaweza kua hakuna umeme,lakini ukipita barabarani kwenda bagamoyo utaona Tanesco walivyo fanya kazi nzuri kupeleka umeme maeneo husika ya Mradi huu,maguzo makubwa ya umeme w a viwanda yamepita kwenda huko(umeme huu hauingii kokote zaidi ya sehemu husika,kiasi cha kwamba watu wenye nyumba zo zenyekuhitaji umeme maeneo ya Bunju B hawapati umeme huo inawa umepita maeneo hayo tena juu ya mapaa yao)

Nadhani kwa kiasi furani nitakua nimesaidia kuelewehana kwenye hili la ujengwaji wa mji wa bagamoyo,sio sababu ya kuwepo Kikwete madarakani na Shukuru kama waziri wa miundombino ila ni mpango wa serikali zaidi ya tano sasa,mwanzoni ilikua ni inchi 3.na mpano ni wamuda mrefu hata kikwete hajawa MFALME
 
ngoja niende jukwaa la jokes kidogo nikapumzishe akili. nilishawaambia mkapa mtamkumbuka sana huyu jk ndo mtakae mpeleka mahakamani pindi akitoka madarakani
 
Bandugu, nimesoma hii habari kwa mshangao mkubwa, pengine ni 'ignorance' yangu kuhusu umuhimu wa viwanja vya ndege. Lakini mshangao wangu ni hapa ambapo tunalipa watu wa Kipawa kupisha upanuzi wa JKN Intl. Airport wakati kumbe maandalizi ya ujenzi wa Bagamoyo Airport yanatafuna pesa!!! Someone mwenye ufahamu zaidi na haya masuala anielimishe tafadhali...!!!!!!!

Mi nafikiri hii heading ingekuwa Bagamoyo airport or expansion of JKN Intl. Airport
 
To be honest if you set aside politics and who brought what and where....

Tunakokwenda we need serious and efficient airports more than JNIA, na kwa jinsi ya jiji la Dar linavyopanuka bila mpangilio na planners wetu wamekaa kimya, binafsi singeshauri kujenga a Big International Airport Mkuranga, kwasababu ya:

- Jinsi ya jiografia yetu ilivyokaa, babaraba kubwa zote za kwenda mkoa mingi ya Tanzania ziko upande wa north, hivyo italazimika kuingia gharama kubwa ili ku-bypass makazi na miundo mbinu mibovu ya Dar.

- Maana tukiruhusi hiyo Airport ya mkuranga ije kufeed barabara hizo za Dar Hatutatatua kabisa tatizo la trafik jam, so inabidi airport mpya planning yake iangalie hilo, na kwa sasa kwa vile bagamoyo inasemwa sema haitokuwa mbaya sana,

- Else iende nje ya kibaha ambayo bado ni Mkoa wa pwani kama nia ni mkoa huo ( maamuzi ya kisiasa zaid kuliko ya kiuchumi), but there should some tantalising economic objectivity, ili kucatalyse maendeleo na kuencourage new development areas. Wasipeleke tu mahali pori ambapo hakuna mtazamo wala mwelekeo kw baadaye.

Tusikubali kuviringishwa na cobweb ya mawazo binafsi na ya kichoyo ya viongozi. Kama wanania nzuri washirikishe wananchi hasa wataalamu kupanga miundo mbinu kikubwa kama hiyo isije ikawa story za kenya za kujeng Eldoret Airpot ambayo sioproductive ukilinganisha na investment iliyowekwa, kisa tu, Baba Moi alitakport igwe kwake.

Sasa hivi ukienda pale Kenya Revenue Authority wanakadiria ushuru wa mizigo kwa mafungu, ili kuencourage cargo planes kuland pale. Walipojaribu kubadilisha utaratibu ndege muhimu zote ziligoma kwenda kule!

Maslahi ya Taifa kwanza.
 
Acheni majungu na kujenga hoja za kinazi zinazotia watu jazba, kuponda feasibility study za wataalamu ni kutusi taaluma za watu na kumtukuza JK bila sababu za msingi. Bagamoyo ipo na ilikuwepo kabla ya JK na swala la bandari ni la kijiografia na kibiashara zaidi na ilitakiwa kuendelezwa kabla ya uhuru ni Ubinafsi tu na uchoyo hata JK akiondoka haja ya kutengeneza bandari ipo pale pale.

Bagamoyo ndio mji wa kwanza wa biashara miaka kibao iliyopita na sababu ni bandari kama ilivyo mombasa. Wafanyabiashara wa mwanzo walipita huko kutambua bandari ya asili huko, Bandari ya Dar ni ya Kuchimba kwa sababu za kiutawala na upanuzi wake unaukomo.

Kumbukeni pia route rahisi ya kufikisha mizigo rwanda, burundi na congo ni reli ya kati na barabara inayopita kati mkimaliza kupanua bandari. Punguzeni siasa msongembele
 
YOU CANT FIGHT IGNORANCE WITHOUGHT KNOWLEDGE-Songambele
 
Ukiachilia mbali asili yangu ya kua mzaliwa wa Mlingoti,wilaya ya Bagamoyo ambapo swala lako la uvaaji wa tie kwetu ni kitendawili mimi pia ni muathilika a mambo yote hayo matatu hapo juu.
Mipango au tuseme projects zote hizo za serikali zimeniacha njia panda kwani kote inanihusu kutoa plots zangu ili kupisha projects hizo na malipo yake nikiduchu kulinganisha na investment nilikwisha weka.
kwa upande mwengine nimefarijika kwamba,mwishoe mambo yanaweza kuwa mazuri kwa vizazi vijavyo vinavyo toka mazingira ninayotoka mimi,Bagamoyo sio mbali ni mwendo wa 45 dk tu unaweza kwenda hata leo uliza Mlingotini ni wapi hapo ilipokuwa proposed Bandari mpya kujengwa mpaka leo hii umeme hamna kwa wakazi wa maeneo hayo ukiondoa chuo cha uvuvi kilichopo hapo.Asante kwa shule za kata vinginevyo watoto na wajuukuu zetu wangeendelea kuwa wavuvi wasio kua na elimu pamoja ya kua na chuo cha uvuvi maeneo hayo.
Naona tu humu mnapiga Blah blah... kwamba sijui wafalme wa maeneo fulani......sijui vyama vya ushirika....bado hatutaki kukubari ukweli kwamaba kuan baadhi ya maeneo ya inchi yetu yalinyimwa maendeleo na sasa (either muda ulikua bado au ukilitimba wa wafalme....)na sasa ndio high time kupeleka maendeleo katika maeneo hayo,chukua mfano wa Lindi na Mtwala kabla ya ujenzi wa barabara hali ilivyo kua na sasa.........
Mtu aliweza kununua Beach plot heka mojaNchinga mkoa wa lindi kabla ya barabara kujengwa kwa shs.300,000 nenda kaulize sasa kama kujakuta bei ni zaidi ya mara 100.
Hali ni hiyo hiyo kwa Bagamoyo kwa sehemu zile ambazo miradi hii haifiki kwa sasa.
Majumuisho yangu ni kwamba,nilazima upeleke vitu kama hivyo barabara,bandari,na hata hiyo airport kama itajengwa kwenye sehemu hizi ili ulete maendeleo ya haraka ili ziweze kulingana na hata kidogo na maeneo mengine ya inchi yaliyo barkiwa kuwa na (wafalme)

Mkuu kama kweli wewe ni wa Bagamoyo, wala usiombee hayo maendeleo kwa sasa hivi kwa sababu bado wenyeji wengi hawajawa tayari kuyapokea badala yake wanayakimbia. Mara tu mpango huu kutangazwa, mashamba karibu yote yameshauzwa na wenyeji kwenye maeneo ya njiani na vijiji vya Bagamoyo, wenyewe wanazidi kukimbilia porini.

Kama wazo ni shughuli tu za kiuchumi it is fine, lakini kama JK na wewe mnafikiri anawapelea ndugu zake wa Bagamoyo basi ameumia kwa sababu wajanja wameshawasogeza nje. Jitahidini kuwabadili kifikra kwanza na kuwapelekea shughuli/miradi midogomidogo wanazoweza kushiriki.:D
 
Ukiachilia mbali asili yangu ya kua mzaliwa wa Mlingoti,wilaya ya Bagamoyo ambapo swala lako la uvaaji wa tie kwetu ni kitendawili mimi pia ni muathilika a mambo yote hayo matatu hapo juu.
Mipango au tuseme projects zote hizo za serikali zimeniacha njia panda kwani kote inanihusu kutoa plots zangu ili kupisha projects hizo na malipo yake nikiduchu kulinganisha na investment nilikwisha weka.
kwa upande mwengine nimefarijika kwamba,mwishoe mambo yanaweza kuwa mazuri kwa vizazi vijavyo vinavyo toka mazingira ninayotoka mimi,Bagamoyo sio mbali ni mwendo wa 45 dk tu unaweza kwenda hata leo uliza Mlingotini ni wapi hapo ilipokuwa proposed Bandari mpya kujengwa mpaka leo hii umeme hamna kwa wakazi wa maeneo hayo ukiondoa chuo cha uvuvi kilichopo hapo.Asante kwa shule za kata vinginevyo watoto na wajuukuu zetu wangeendelea kuwa wavuvi wasio kua na elimu pamoja ya kua na chuo cha uvuvi maeneo hayo.
Naona tu humu mnapiga Blah blah... kwamba sijui wafalme wa maeneo fulani......sijui vyama vya ushirika....bado hatutaki kukubari ukweli kwamaba kuan baadhi ya maeneo ya inchi yetu yalinyimwa maendeleo na sasa (either muda ulikua bado au ukilitimba wa wafalme....)na sasa ndio high time kupeleka maendeleo katika maeneo hayo,chukua mfano wa Lindi na Mtwala kabla ya ujenzi wa barabara hali ilivyo kua na sasa.........
Mtu aliweza kununua Beach plot heka mojaNchinga mkoa wa lindi kabla ya barabara kujengwa kwa shs.300,000 nenda kaulize sasa kama kujakuta bei ni zaidi ya mara 100.
Hali ni hiyo hiyo kwa Bagamoyo kwa sehemu zile ambazo miradi hii haifiki kwa sasa.
Majumuisho yangu ni kwamba,nilazima upeleke vitu kama hivyo barabara,bandari,na hata hiyo airport kama itajengwa kwenye sehemu hizi ili ulete maendeleo ya haraka ili ziweze kulingana na hata kidogo na maeneo mengine ya inchi yaliyo barkiwa kuwa na (wafalme)

Mkuu kama kweli wewe ni wa Bagamoyo, wala usiombee hayo maendeleo kwa sasa hivi kwa sababu bado wenyeji wengi hawajawa tayari kuyapokea badala yake wanayakimbia. Mara tu mpango huu kutangazwa, mashamba karibu yote yameshauzwa na wenyeji kwenye maeneo ya njiani na vijiji vya Bagamoyo, wenyewe wanazidi kukimbilia porini.

Kama wazo ni shughuli tu za kiuchumi it is fine, lakini kama JK na wewe mnafikiri anawapelekea ndugu zake wa Bagamoyo basi ameumia kwa sababu wajanja wameshawasogeza nje. Jitahidini kuwabadili kifikra kwanza na kuwapelekea shughuli/miradi midogomidogo wanazoweza kushiriki.:D
 
Back
Top Bottom