Bagamoyo Airport or Extension of JKN Intl. Airport?

Nafikiri ni wazo zuri sana kujenga airport Bagamoyo. Statistics zinaonyesha Dar airport inaelemewa sana na traffic ya midege inayotua kila dakika. Hata ikipanuliwa hivi inavyotakiwa kupanuliwa bado haitaweza kuhimili. Tunahitaji specifically airport mpya bagamoyo kwa sababu ya urahisi wa bagamoyo road kuingia dar. Barabara ni pana sana, haina magari mengi hasa kutokea Tegeta-Mbezi Beach-Ali H Mwinyi hadi city centre; barabara iko idle kabisa, pana ya kutosha magari yanaenda full speed. Bandari pia itajengwa Bagamoyo kwa sababu hiyo hiyo ya urahisi wa barabara kuingia Dar. Mizigo mingi zaidi itashukia kule italetwa na magari fasta jijini. Yaani serikali hii ina mawazo endelevu mazuri sana.

umepokea rushwa nini?
 
Inasikitisha Nchi inaendeshwa kama Genge la Mzee Jongo au Kiduka cha Mangushi, Kiongozi akiamka na ndoto yake basi inaundiwa mradi!! Kwa mwendo huu na Mtaji huu tutufikishana kweliiiiiiiiiiiiiiiiiiiii????
 
mbona hamsemi kuhusu kupeleka maendeleo PEMBA au Pemba hawa deserve haya madaraja, miji eapoti na mijibandari yenu
 
Nyie mbona hamtaki kueleze ukweli

hivi vyote vingejengwa Moshi au Arusha ingeonekana its normal

wacha wajenge Bagamoyo wakimaliza wakajenge na ule mradi mkubwa zaidi kule Pemba

sioni tatizo liko wapi

Acha kasumba na wivu Moshi imejengwa na wachagga wenyewe hata kabla ya Uhuru na hufulia na kuneemeka kutokana na zao la kahawa na maua na utalii kwa sasa ambayo yote yanafanywa na watu binafsi! Huoni hata aibu! Na Arusha huwezi fananisha na Bagamoyo hata siku moja kwa sababu ukifanya Cost Benefit Analysis (CBA) Hizo investments za Bagamoyo hazitaweza lipa hata miaka 50 ijayo na Arusha kuna germstones na idadi kubwa ya watu, viwanda na kilimo cha kufa mtu! Tuwe wakweli Bagamoyo haistahili International Airport au Harbour kwa vile ya proximity to Dar es salaam if Strategic Environmental Assessment (SEA) itafanywa! Huu ni umimi au ukabila nashangaa Watanzania huwika kila siku ati Wachagga ni Wakabila lakini leo hii ukienda huko kila kitu kasoro barabara vimejengwa na wao wenyewe kuanzia kabla ya uhuru mpk sasa tukianza na vyuo vyote mpk KCMC ni wenyewe wame-fight kupitia KNCU na Lutheran church na taasisi za dini serikali ilijua kutaifisha tu! hata KIA ilijengwa kutokana na serikali kutaka kurahisisha utalii in Nn Circuit na ndo maana uko mpakani kwa vile watalii wote walikuwa wakishukia Nairobi. Na hotel zote zilizo Moshi ni za Wachagga wenyewe! Acheni ubabaishaji na wivu uliza si tulioishi huko!

Hii serikali iache ubinafsi Mwanza ndo sehemu inayohitaji international Airport kwa sasa kama watatumia ushauri wa kitaalamu kwenye ku-recover costs invested! Na hatuhitaji new harbour sasa Tanga na Mtwara ziboreshwe ili zisaidie migodi ya coal na chuma na pia kwa land locked countriea kama malawi, DRC na Zambia Kusini kwa Mtwara na migodi ya Kaskazini kwa kwa Tanga Victoria basin kuna zaidi ya watu million 10 na pia kuna nchi za uganda, Rwanda na Burundi zitatumia hiyo bandari

bagamoyo inahitaji airstrip na jetty tu kwa ajili ya kushukia cruise ships
 
niliongea na mtaalamu wa masuala ya ndege akasema kwa sheria ( as he told me) uwanja wa ndege wa kimataifa unatakiwa uwe na "alternative landing ground, in case of any thing" akanipa mfano wa KIA na Arusha, na Jomo kinyata na Wiliams sasa sijui ndio maana wanajenga bagamoyo au vipi, ila kwangu mimi bandari na reli ndo priority ila ndo hivyo viongozi wetu n i mabigwa wa rivasi (reverse) kwenye kufikiri

Nani kakudanganya Kenyatta na Wilson, ni kwa vile Wilson ilikuwepo tangu awali na pia Embakasi! Na Arusha kilikuwepo kabla ya KIA. Ndo mana nasema kama watu wana-think big Arusha hakuitajiki another Airport KIA can serve both Kilimanjaro na Arusha na vivyo vivyo bagamoyo hakuhitajili International Airport wajenge Mwanza kwa vile ya idadi ya watu wengi wape jamani lake region needs International Airport now!!!!
 
Game Theory,
Mkuu unaweza sema non sense mara 100 lakini haiwezi badilisha ukweli kwa sababu huelewi umuhimu wa viwanja vya ndege na bandari kwa taifa, zaidi ya kudhania italeta maendeleo sehemu hizo..Wala sikulaumu kwani wajali zaidi mkono unakulisha, hujui mapishi ya chakula..
 
- Mkulu PM, with all due respect hebu na wengine waendelezwe pia, I mean sasa akitoka bila kufanya kitu yatakuwa makubwa kuliko haya, kutesa kwa zamu jamani, kwa hili mnyonge mnyongeni tuwaachieni na wengine nao wasogee kidogo!

- Kweli mnataka akitoka Ikulu aende wapi?, Lushoto kama yule mwingine aliyekimbia kwao kwa sababu hakufanya kitu mambo ya utandawazi tu! akhaa kuweni na huruma kidogo!

- Infact, mkulu yupo mjini ngoja nimuwahi kula dataz kidogo, kabla hajaanua!

Respect.

FMEs!

jamani mkapa hajakimbia kwao...ile nyumba ya lushoto its his holiday farm house ...na anayo nyumba nzuri Lupaso,masasi ambayo its a native home...hata juzi alimkaribisha pinda...

jamani si mmekaa nje mmeona ......mtu ukiwa na uwezo si unakazana kujenga vijumba ..ovyo sinza..magomeni ..etc ..ukitaka kufurahia pesa yako lazima uwe na RESIDENCE home, na holiday home..[hii ustaarabu wake inajengwa porini kwenye kimya kingi na ...kila nyumba inakuwa na eneo la heka 10...ambako unaweka farasi ,mbwa,...na wanyama wengine watakaofanya maisha yako yawe safi....ikifika ijumaa unaenda unakaa hadi jumatatu....matajiri wa kibongo hawana life stlyle hii zaidi ya kupenda kuimbwa na bendi]

kwenye hili la bagamoyo tuweke maslahi ya Taifa mbele...mtwara,tanga na mwanza pia wanahitaji maendeleo......kama tulivokmkatalia Sumaye kujenga airport arusha ....pamoja na taratibu za tenda na kuweka uzio kufanyika ...pia tunamkatalia kikwete kujenga GBOLITE bagamoyo.....tunatambua utajiri wa kihistoria wa bagamoyo tusiuharibu...bagamoyo uwe mji wa kitaliii....wa kimataifa....mombasa wanafaidika sana na crusie ships ...maaskari wote wa marekani wakiwa releaved hufika na meli za kitalii pale na kutumia pesa.........hapa kwetu hawaji kwa kuwa we dont have facilities..that deal is just very economical viable kwa bagamoyo...naongea kama strategist hapo....
 
Acha kasumba na wivu Moshi imejengwa na wachagga wenyewe hata kabla ya Uhuru na hufulia na kuneemeka kutokana na zao la kahawa na maua na utalii kwa sasa ambayo yote yanafanywa na watu binafsi! Huoni hata aibu!

kaka you spoke it all....kabla ya uhuru ufalme wa kilimanjaro tayari ulikuwa na serikali ,baraza la ushauri[mawaziri],ikulu,bunge ....yote ya kisasa ...na hadi sasa rais akiwa kilimanjaro hufikia kwenye ikulu iliyojengwa na wachagga hao...na bunge lao ndio makao makuu ya wilaya..moshi vijijini...

kabla ya uhuru tayari ufalme wao ulikuwa umejenga chuo cha ushirika,chuo cha kahawa,lyamungo,etc..

upande wa afya kwa kushirikiana na mashirika ya dini walishajenga hospitali kila tarafa...hospityali ya kibosho,marangu,na machame....

upande wa elimu ya msingi walikuwa wakisambaza vitabu na madaftari yenye nemmbo yao ya chui....kwa watoto wote ...na walikuwa wakisomesha watoto [scholarships]

upande wa fedha na biashara ..tayari kwa kupitia chama cha ushirika moja ya vya mwanzo afrika KNCU ...WALIkuwa wakiuza kahawa nje....na walikuwa na akaunti za fedha za kigeni nje ya nchi.....

upande wa umwagiliaji ...hata kabla ya uhuru tawala yao ilikuwa imeshajenga mfumo wa umwagiliaji wa mashamba ya mogomba na kahawa kwenye viijiji vyote na ikisimamiwa kimila....

barabara baadhi hasa za vijijini zilishajengwa kwa kujitolea..

Upande wa utalii tayari wakikuwa na hoteli ya mwanzo kabisa tanganyika kuwa na lift .na kuwa ya kitalii...KNCU hotel....

MALI ZOTE HIZI PAMOJA NA AKAUNTI ZA FEDHA ZA KIGENI ZILITAIFISHWA NA SERIKALI NA WATU WA MKOA HUO WALA HAWAJAWAHI KUONGELEA KUDAI PESA ZAO ZA KODI WALIZOKUWA WAKILIPA KWA MANGI ZILIZOJENGA VITEGA UCHUMI HIVYO KWA SERIKALI!!

ndio maana huwa haingii akilini na ni kama tusi kusema wananchi wa kilimanjaro kuwa wameshapata upendeleo na serikali ......kwa kuwa ni kweli HATA AKIFUFUKA MTU ALIYEKUFA MWAKA 1967....HATAKUTA MKOA UMEBADILIKA SANA zaidi ya idadi ya watu na ukame kuongezeka ..NA HASA DHELUJI YA MLIMA KUENDELEA KUPOTEA KUTOKANA NA SHUGHULI ZA KIBINADAMU......ni wazi kuwa kama upendeleo wowote ungefanyika kilimanjaro basi...leo hii labda ingeweza kuwa mbele zaidi na tofauti ingeonekana dhahiri.....leo hii majengo mengi mazuri yanajengwa na vijana wanaoamua kuwekeza kwao...kwani kwa watu wa kule hona aibu sana ....familia kukosa maendeleo....na sasa utashangaa baadhi ya vijiji tayari wanaona ni kila familia inatakiwa kuwa na ghorofa.....!!..

nadhani watanzania tushindane kwa maendeleo.....ni vema wakazi wa maeneo mengine nchini wakatembelea maeneo ya vijijini kilimanjaro na kuona wakazi wa huko wamewezaje kujiletea maendeleo kuanzia ngazi ya familia bila kungoja serikali......badala ya kufikiria vinginevyo!!
 
Heshima kwako PM.

Unataka niongeze nini tena hapa yaani umemaliza kila kitu.

mradi wa airport bagamoyo umekaa kiubinafsi...mpango wa awali tangu enzi mwandosya yupo mawasiliano ni kujenga airport mkuranga na eneo limeshatengwa ....mtu haoni hata aibu airport bagamoyo....,bandari mpya bagamoyo[wakati mtwara na tanga hazijaendelezwa na dar ...ipo karibu just 40 km apart]......na hivi anajenga kempski wami bagamoyo[for your infromation].....
nyumba zake msoga-makao makuu ya mkoa ,chalinze...just in five years ......he is so hurry........
nadhani ni vema mji wa bagamoyo uendelezwe uwe wa kitalii...pengine hata kama ni bandari ijengwe ya tourist cruise ships ambazo hatunufaiki nazo......lakini kupeleka kila kitu pale si sawa....aiport irudi mkuranga....na pesa ya kujenga bandari ...wajenge ndogo ya kitalii pale pesa inayobaki waboreshe natural harbour yetu ya mtwara ...kwa kuunganisha na reli ya tazara na barabara...na kuilink bandari ya tanga na musoma...

I disagree with you... ni kazi ngumu kutoka mkuranga kwenda dodoma, tabora, mbeya, tanga nk. kulinganisha na bagamoyo, strategically bagamoyo iko better placed hasa ukizingatia productivity na tunapoelekea EAF

Lets ake some positives out of a few issues kupunguza stress
 
niliongea na mtaalamu wa masuala ya ndege akasema kwa sheria ( as he told me) uwanja wa ndege wa kimataifa unatakiwa uwe na "alternative landing ground, in case of any thing" akanipa mfano wa KIA na Arusha, na Jomo kinyata na Wiliams sasa sijui ndio maana wanajenga bagamoyo au vipi, ila kwangu mimi bandari na reli ndo priority ila ndo hivyo viongozi wetu n i mabigwa wa rivasi (reverse) kwenye kufikiri

Mkuu,

Hilo siyo tatizo kabisa. Mkoa wa Pwani kuna uwanja wa Jeshi na si mbali sana na Msata alikozaliwa Muungwana. Unaweza kuangalia hii ramani na ukaona umbali wake ni kama km 130 tu kutoka JKNIA hadi hapo Ngerengere. Na nafikiri viwanja vya jeshi vitakuwa bomba sana.

Kwa dharula kwa nini kisitumike kuokowa watu? Hata nchi za West huwa inatokea wanapokea ndege za abiria kwenye kambi/uwanja wa jeshi.
 
Attachments

  • Uwanja wa Jeshi.JPG
    Uwanja wa Jeshi.JPG
    171.7 KB · Views: 58
I disagree with you... ni kazi ngumu kutoka mkuranga kwenda dodoma, tabora, mbeya, tanga nk. kulinganisha na bagamoyo, strategically bagamoyo iko better placed hasa ukizingatia productivity na tunapoelekea EAF

Lets ake some positives out of a few issues kupunguza stress

Mkuu,

Umenikumbusha hii chemsha bongo:

"Ndege inasafiri kutoka Dar kwenda Mwanza inatumia saa moja na nusu na ikitoka Mwanza kuja Dar inatumia dakika 90. Swali ni kwa nini kuna tofauti ya muda?"
 
Miafrika kwa matumizi tu hatujambo, yaani ubishi wote huu ni matumizi hakuna fikra za kuelewa sababu, dhumuni na nia ya ujenzi wa chanzo chochote isipokuwa maonyesho tu..I mean, mtu anambie sababu ya kujenga International Airport mbili (130 Km apart) kutoka uwanja mwingine wa International ktk population wa watu wasiozidi millioni 5, ndege kubwa zinazotua kwa siku hupishana zaidi ya saa nzima..
 
1.EPZA
2.SATALLITE CITIES(mfano wa kibamba Luguluni na zinginezo ambazo ziko njiani) kwa sababu Dar haipangiki tena.
3.KIGAMBONI NEW CITY
 
1.EPZA
2.SATALLITE CITIES(mfano wa kibamba Luguluni na zinginezo ambazo ziko njiani) kwa sababu Dar haipangiki tena.
3.KIGAMBONI NEW CITY
Tanzania kwa sasa hahitaji uwanja wa Kimataifa Bagamoyo, ila barabara pana na zilizo pangwa vizuri ilikuondokana na Kero ya foleni, Reli kwa ajili ya mizigo mikubwa na pia kusaidia kupunguza msongamano kwenye bara bara kwa kuweka Trums na Umeme wa Hukakika, hiki vingine naomba ndugu yangu uhifadhi hiyo Plot kwenye miaka 20 ijayo hicho kiwanja kitakuja tu kutokana na msukumo wa kiuchumi, kwa sasa hali sivyo, bali tupo katika hali ya kujinusuru, na kuanguka kwa uchumi wetu na huduma zingine.
kwa mfano wewe mwenyewe umekuwa ni mfano mzuri kwamba unaweza kuvaa tie/ mjusi au umetuwekea picha ya mtu wa kufanana na hivyo kwenye avatar yako lakini ni kwa sababu unatoka kwenye nyumba nzuri hivyo watu watakuelewa au huyo mtu anatoka katika hali kama hiyo , lakini jiweke unatoka kwenye nyumba ambayo haiendani na kuweza kuhihifadhi hiyo tie/mjusi katika hali nzuri watu watashindwa kukuelewa.
hivyo basi tujiweke hayo mazingira ya kuweka hiyo int airport bagamoyo, na si kwamba airport ianze ndipo vitu vingine vifuate. bali kunyume chake.
 
Sidhani kama hata nina kuelewa kwa maelezo hayo hapo juu.ila nitakujibu vile nionavyo mimi.
Ukiachilia mbali asili yangu ya kua mzaliwa wa Mlingoti,wilaya ya Bagamoyo ambapo swala lako la uvaaji wa tie kwetu ni kitendawili mimi pia ni muathilika a mambo yote hayo matatu hapo juu.
Mipango au tuseme projects zote hizo za serikali zimeniacha njia panda kwani kote inanihusu kutoa plots zangu ili kupisha projects hizo na malipo yake nikiduchu kulinganisha na investment nilikwisha weka.
kwa upande mwengine nimefarijika kwamba,mwishoe mambo yanaweza kuwa mazuri kwa vizazi vijavyo vinavyo toka mazingira ninayotoka mimi,Bagamoyo sio mbali ni mwendo wa 45 dk tu unaweza kwenda hata leo uliza Mlingotini ni wapi hapo ilipokuwa proposed Bandari mpya kujengwa mpaka leo hii umeme hamna kwa wakazi wa maeneo hayo ukiondoa chuo cha uvuvi kilichopo hapo.Asante kwa shule za kata vinginevyo watoto na wajuukuu zetu wangeendelea kuwa wavuvi wasio kua na elimu pamoja ya kua na chuo cha uvuvi maeneo hayo.
Naona tu humu mnapiga Blah blah... kwamba sijui wafalme wa maeneo fulani......sijui vyama vya ushirika....bado hatutaki kukubari ukweli kwamaba kuan baadhi ya maeneo ya inchi yetu yalinyimwa maendeleo na sasa (either muda ulikua bado au ukilitimba wa wafalme....)na sasa ndio high time kupeleka maendeleo katika maeneo hayo,chukua mfano wa Lindi na Mtwala kabla ya ujenzi wa barabara hali ilivyo kua na sasa.........
Mtu aliweza kununua Beach plot heka mojaNchinga mkoa wa lindi kabla ya barabara kujengwa kwa shs.300,000 nenda kaulize sasa kama kujakuta bei ni zaidi ya mara 100.
Hali ni hiyo hiyo kwa Bagamoyo kwa sehemu zile ambazo miradi hii haifiki kwa sasa.
Majumuisho yangu ni kwamba,nilazima upeleke vitu kama hivyo barabara,bandari,na hata hiyo airport kama itajengwa kwenye sehemu hizi ili ulete maendeleo ya haraka ili ziweze kulingana na hata kidogo na maeneo mengine ya inchi yaliyo barkiwa kuwa na (wafalme)
 
Sikonge,
Mkuu kupelekea maendeleo Bagamoyo hilo ni swala ambalo hakuna mtu anayepinga hata kidogo isipokuwa ni muhimu sana kuzingatia hali halisi ya uwezekano wa maendeleo hayo..
Ujenzi wa makao makuu Dodoma ulikuwa na nia safi sana ya kupeleka maendelo huko badala yake tunaona jinsi serikali inavyotumia mabillioni ya fedha kuhifadhi majengo ambayo leo hii ni kama makumbusho.

Mtwara na Tanga zimejengwa bandari miaka na zinatugharimu zaidi ya pato linalotokana na bandari hizo. hakuna maendeleo ktk sehemu hizo kwa sababu bandari hizo hazina barabara wala reli zinazorahisisha usafiri wa mizigo...Mtwara na Tanga ni ile ile aloacha Mkoloni huwezi potea hata mtaa mmoja, na serikali kwa miaka yote imeshindwa kuziboresha kwa sababu aidha hatuna fedha ama ndio tabia yetu ktk matumizi pasipo kuona mbele.

Ni sawa na kujenga jumba kubwa mlimani usiweke barabara za magari ukitegemea ukubwa wa jengo utawavuta Wapangaji..Leo hii Mbezi beach nyumba zimeshuka bei ajabu hata kupangisha tu ni shida kwa sababu ya Usafiri mbovu kwa wananchi kwenda makazini..

Katika lugha ya Kiuchumi serikali inatakiwa kutazama soko na sii kufikiria vyanzo kwa mahitaji ya kufurahisha watu..Ni dunia ya Biahsara hii mkuu wangu kila tunapo invest ni lazima tuangalie wateja wetu waptapendelea kitu gani na lugha ni ile ile..Principal ni zile zile kwamba Location matters in all aspect ya biashara na uwekezaji.

Hivyo naweza kubaliana na hoja ya Bandari kuhamishwa toka Dar kwenda Bagamoyo kutokana na uwezo mdogo wa bandari yetu ya Dar lakini itahitajika ujenzi mwingine wa reli kuunganisha na ile ya kati na sii mizigo kurudi tena Dar kabla haijasafirishwa kwenda mikoani na nchi jirani iwe kwa TRC au Tazara..Hili halitawezekana na pengine tutakata miaka 50 mingine kabla ya haya kutimia wakati Bandari imeshajengwa..

Kumbuka tena nilivyosema kwamba wafanyabiashara wote wa ndege na Meli wanategemea zaidi pato lao toka usafirishaji wa mizigo kuliko Abiria..Hivyo inahitajika reli na barabara mpya kutoka Bagamoyo kwenda Dar na mikoani na ikiwa hatyutaweza kufanya hivyo hakuna Meli itakayo tinga Bagamoyo, Mombasa wataendelea kutupiga magoli..Another mult billion protect failed..

Na nikitazama uwanja wa ndege ndio kabisaaaaaa! sioni sababu ya kujenga uwanja wa Kimataifa bagamoyo ikiwa tunashindwa kuuboresha uwanja wa Dar toka mwalimu..Kimeongezeka kitu gani labda yale maduka ya duty free kwa mali fake toka India na China...Tumeshindwa kuongeza jengo la mapokezi na kuondoka liwe na sehemu kubwa mbili za wasafiri na wapokelaji wakati nafasi kubwa ipo. Tumeshindwa kujenga runaway zaidi kwa miaka zaidi ya miaka 37.. mkuu miaka 37 uwanja wetu haupanuki ila ni malisho ya ng'ombe na hata wananchi wamejenga nyumba zao ktk baadhi ya meneno ya kiwanja hicho. Leo sababu ya kushindwa upanuzi imekuwa ati wakazi wa Kipawa kuandamana. Uzembe gani huu leo mtake kujenga kiwanja kipya hali tumeshindwa kabisa kuhudumia vilivyopo ktk maeneo hayo hayo.

Mkuu wangu hapa Canada, mji wa Montreal walijenga uwanja mkubwa sana wa ndege kuhudumia sehemu za east ya Canada. Lakini kutokana na jiografia ya mkoa wenyewe na kuwepo kwa viwanja baina yake na miji ya Ottawa na Toronto, pia biahsara chache upande ule wa east wakitegemea zaidi bandari, Uwanja ule umeshindwa kushindana kibiashara kwa sababu ya Population ndogo, incovenience ktk muda wa usafiri kuelekea west coast ambako ndiko kwenye biashara kubwa za mizigo ya ndege..mahesabu yalikataa kabisa na imekuwa hasara kubwa kwa province hiyo.
Hivyo, wamevua na kunawa mikono, uwanja ule wa Kimataifa unatakiwa kufungwa na kijengwe kitu kingine kabisa kwa sababu hakuna biashara..Ni aibu ya pili kwa Qebec baada ya ile ya ujenzi wa uwanja wa Olimpic ambao walitegema pia utaweza kuleta maendeleo Quebec badala yake umekula mifuko ya wananchi kwa ushuru..

Kwa hiuyo binafsi natazama picha nzima kibishara na kiuchumi.. Ni makosa makubwa kujenga Kiwnaja cha ndege Bagamoyo ikiwa tunaweza kabisa kukiendeleza kiwanja cha Dar kufikia hadhi ya kimataifa kwani hatuna ndege nyingi kiasi cha kufikiria tunahitaji jiwanja kama JFK..Tena basi nilipokuwa Mwanza niliona ndege nyingi zikishuka kuruka huko kuliko hata Dar.

Kwa hiyo bado tuna safari ndefu sana. Tukiweza kujifunza ukarabati na matunzo ya vitu vyetu (ndipo ajira zinapotokana) pengine tunaweza fikiria miradi mipya ili kuboresha huduma toka ile ya zamani, lakini maadam hiyo ya zamani bado tunashindwa kuiwezesha kufanya kazi nusu ya kiwango chake.. basi sioni sababu kabisa ya kuweka mikono mfukoni na kupoteza mabillioni mengine..
 
Sidhani kama hata nina kuelewa kwa maelezo hayo hapo juu.ila nitakujibu vile nionavyo mimi.
Ukiachilia mbali asili yangu ya kua mzaliwa wa Mlingoti,wilaya ya Bagamoyo ambapo swala lako la uvaaji wa tie kwetu ni kitendawili mimi pia ni muathilika a mambo yote hayo matatu hapo juu.
Mipango au tuseme projects zote hizo za serikali zimeniacha njia panda kwani kote inanihusu kutoa plots zangu ili kupisha projects hizo na malipo yake nikiduchu kulinganisha na investment nilikwisha weka.
kwa upande mwengine nimefarijika kwamba,mwishoe mambo yanaweza kuwa mazuri kwa vizazi vijavyo vinavyo toka mazingira ninayotoka mimi,Bagamoyo sio mbali ni mwendo wa 45 dk tu unaweza kwenda hata leo uliza Mlingotini ni wapi hapo ilipokuwa proposed Bandari mpya kujengwa mpaka leo hii umeme hamna kwa wakazi wa maeneo hayo ukiondoa chuo cha uvuvi kilichopo hapo.Asante kwa shule za kata vinginevyo watoto na wajuukuu zetu wangeendelea kuwa wavuvi wasio kua na elimu pamoja ya kua na chuo cha uvuvi maeneo hayo.
Naona tu humu mnapiga Blah blah... kwamba sijui wafalme wa maeneo fulani......sijui vyama vya ushirika....bado hatutaki kukubari ukweli kwamaba kuan baadhi ya maeneo ya inchi yetu yalinyimwa maendeleo na sasa (either muda ulikua bado au ukilitimba wa wafalme....)na sasa ndio high time kupeleka maendeleo katika maeneo hayo,chukua mfano wa Lindi na Mtwala kabla ya ujenzi wa barabara hali ilivyo kua na sasa.........
Mtu aliweza kununua Beach plot heka mojaNchinga mkoa wa lindi kabla ya barabara kujengwa kwa shs.300,000 nenda kaulize sasa kama kujakuta bei ni zaidi ya mara 100.
Hali ni hiyo hiyo kwa Bagamoyo kwa sehemu zile ambazo miradi hii haifiki kwa sasa.
Majumuisho yangu ni kwamba,nilazima upeleke vitu kama hivyo barabara,bandari,na hata hiyo airport kama itajengwa kwenye sehemu hizi ili ulete maendeleo ya haraka ili ziweze kulingana na hata kidogo na maeneo mengine ya inchi yaliyo barkiwa kuwa na (wafalme)
kwa kifupi ninacho maanisha ni kwamba ukitaka kuleta maendeleo sehemu yoyote ile, basi ni vizuri ukaanza na kujiwekea hali ya kuleta hayo maendeleo, sasa tukirudi kwenye suala la Bagamoyo iwe mlingotini nk , tuanze na barabara ambazo zitaunganisha na sehemu zingine za nchi , kwani suala la kiuchumi ni la kutegemeana, jingine ni kuwa na usafiri wa reli mzuri, ambao baadae uta support hiyo processing zone hapo bagamoyo, maana usitegeme pamba itakuja kwa ndege/tumbaku nk nk, na jingine ni la umeme ambao litachoche elimu bora, uzalisha, na mazingira yote kwa ujumla, maana hata hiyo airport inategemeana na uwepo wa nyenzo kama umeme na watu wenye elimu bora.
kwa hiyo wote tuwekeze akili zetu na nguvu zetu kwenye vitu kama hivyo basi maendeleo mengine yatakuja kwa urahisi na speed inayotakikana bila kuathiri nguzo za kiuchumi ama sivyo tutajiwekea dhana ya kwamba mimi kwetu kumesahaulika nataka hichi nataka kile halafu kikiwekwa hakikusaidi kwa sababu umeacha vitu vya msingi.
kwa hiyo kwenye nia yako au plan naomba uanze na vitu vya msingi, na kama unaukaribu na viongozi/mbunge wako naomba uwaeleze kuwa usafiri bora (barabara, Reli) ambao utatuwezesha sisi wafanyakazi kutoka sehemu mbali mbali za tanzania kuja bagamoyo kufanya kazi au kuleta mali ghafi zetu kwa ajili ya epz na Nguvu za Umeme ndio utachochea maendeleo mengine, iwe bandari, airport nk na vitu hivi sio vinakuja overnight vinahitaji mipango ya muda mfupi , kati na muda mrefu
maelezo mengine naona Mkandara nae kaelezea vizuri suala hili.
 
Mkuu,

Umenikumbusha hii chemsha bongo:

"Ndege inasafiri kutoka Dar kwenda Mwanza inatumia saa moja na nusu na ikitoka Mwanza kuja Dar inatumia dakika 90. Swali ni kwa nini kuna tofauti ya muda?"

hahaaa

i just took a face value of it na nikaangalia roads zipi zinatoka mkuranga, kupitia mbagala ubungo hadi moro na upungufu wa roads tulio nao let alone ubora, halafu nikapiga quick hesabu ya kutoka bagamoyo, kupitia lugoba chalinze hadi moro... same same kama unaenda dom, tanga etc. nikagundua one is shorter hakuna cha saa moja na nusu au 90 minutes bali ni 4 hours vs. 60 minutes

Anyway i was just trying to take positive out of nothing!!! nothing indeed!!!! we need better roads hasa za kutoka Dar central kwenda peripheries na hiyo pesa ya airport wangepeleka lami dodoma arusha na dodoma iringa kukamilisha cape to cairo adventure

we also need proper facelifting and maintenance of the three bandaris we have na kuboresha Mwanza and Mbeya airport

we cant afford to spend billions wakati uwanja wa dar as we speak unafanyiwa ukarabati kwa pesa nyingi na tundege twenyewe tuchache tu tunatua!!!
 
uko serious ati dar vindege tuchache?
 
Back
Top Bottom