BAE systems ni wezi na wameshathibitishwa na mahakama wasipewe pesa zetu wazigawe

kade030

Member
May 4, 2010
25
4
BAE nao pia ni wezi tuu kama our tainted tz gov.

Mi nadhani kama wanataka kuwapa NGO then fedha wapewe serikali ya uingereza halafu wao ndio waratibu huo ugawaji.
La sivyo kwa hiyo E-mail BAE systems wanaenda Bar kunywa vodka kazi ishaisha.. mkono huu unatoa halafu unapokea na mwingine.

Basi
 
Hata kuwapa Waingereza wazigawe bado si sahihi. Kwa mamlaka gani hao waingereza wanapaswa kuingilia mgao wa fedha zetu. Sisi tumeshasema zitatumika kuimarisha suala la elimu na tayari matumizi na mchanganuo umetolewa, sasa hatujiamini nini mpaka tuombe msaada wa mtu kuziratibu?
 
mmmmh! hivi jamani tukiachana na chenchi, waliotufikisha hapa wapo wapi?
 
Watoe scholarship kwa watanzania 1450 za pound 20, 000 kwa degree za miaka mitatu hukohuko uingereza itakuwa jumla ya pound 29M. Ni bora tuwape kizazi kijacho cha Tanzania hivyo pesa haita potea.
 
Hata kuwapa Waingereza wazigawe bado si sahihi. Kwa mamlaka gani hao waingereza wanapaswa kuingilia mgao wa fedha zetu. Sisi tumeshasema zitatumika kuimarisha suala la elimu na tayari matumizi na mchanganuo umetolewa, sasa hatujiamini nini mpaka tuombe msaada wa mtu kuziratibu?
Achaneni na mambo ya chenji shughulikieni kwanza waliowafikisha hapo hata waingereza wanawashangaa.
 
Hata kuwapa Waingereza wazigawe bado si sahihi. Kwa mamlaka gani hao waingereza wanapaswa kuingilia mgao wa fedha zetu. Sisi tumeshasema zitatumika kuimarisha suala la elimu na tayari matumizi na mchanganuo umetolewa, sasa hatujiamini nini mpaka tuombe msaada wa mtu kuziratibu?

Hamkujua kuwa kuna hela imeibiwa, serikali yenu mpaka leo inakataa kuwa kuna huo wizi ulifanyika, iweje leo udenda unatoka kufuatilia hizo hela!! ?? Yaani hili li serikali la kidwanzi kweli aibu tupu....
 
Mbona hao wabunge hawafuatilii fedha za Meremeta, Deep Green, KAGODA, Kiwira n.k na hili suala la nani asimamie ugawaji wa fedha hizo Bae System kwa kujua kwamba wao pamoja na serikali ya Tanzania ni wahusika wakubwa waliamua kujihengua na kuomba iundwe bodi huria ya kusimamia urejeshwaji wa fedha husika.
 
Sishangai hao Waingereza wanataka kuratibu hizo pesa.Mzee wa vijisenti bado anatanua.Wapo watu kibao wamehusika na si ajabu hata JK anajua na ilimpitia kwenye anga zake alipokuwa Waziri,sasa unashangaa au utawalaumu Waingereza kwa kuzuia kuwapa Serikali ya Tanzania hizo pesa?Mpango wa Elimu,wapi?Hiyo ni propaganda tu.Udanganyifu umezidi kwenye Serikali yetu!Hizi danganya toto kuna wakati zinagonga ukuta.Kuliko kumpa mwizi mwenzio ni bora wewe mwizi usimamie labda zitafika kwa wananchi wetu.HASIRA KWELI!
 
Hazina maana hizo pesa. Kama tunazitaka tuwatupe segerea kwanza wahusika then twende kuomba chenchi yetu jamaa wakikataa hapo hata mimi nitasema, kwa sasa hatuna hoja ya msingi ya kuwaambia watu makini huko london
 
BAE nao pia ni wezi tuu kama our tainted tz gov.

Mi nadhani kama wanataka kuwapa NGO then fedha wapewe serikali ya uingereza halafu wao ndio waratibu huo ugawaji.
La sivyo kwa hiyo E-mail BAE systems wanaenda Bar kunywa vodka kazi ishaisha.. mkono huu unatoa halafu unapokea na mwingine.

Basi

Wewe unadhania serikali yako inavyoweza kuingilia makampuni ya biashara yanayofanya kazi nchini, basi inakuwa applied na kwenye nchi nyingine. Serikali ya uingereza haiwezi na haina mamlaka ya kuwaambia BAE wafanye nini na hizo pesa ni amri ya mahakama tu. Sasa kama serikali yako ilikuwa inafuatilia kesi na kusikiliza basi waiombe mahakama iwaamrishe BAE wawalipe.
 
Kwa hili BAE wamepewa rungu, na most likely watalitumia kuwalinda wale wabaya wetu maana tangia mwanzo ndio walikuwa watupige za usoni bila haya. Pressure inayowekwa kwamba serikali isilipwe ni njema hakuna tunachoweza kufanya zaidi labda sisi tunaoipinga serikali tufungue kesi ili mahakama i-rule kivingine. Hakuna options zaidi maana hatukuepo kwene parities ya hukumu ya mwanzo.
 
Back
Top Bottom