Badra Masuod PR Manager wa Tanesco bure kabisa hafai kushika Cheo alichonacho.........

mzee wa njaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
1,366
223
Jana katika taarifa ya habari TBC 1 alikuwa akihojiwa na Mtangazaji Asha Haji kuhusu suluhu ya tatizo la Umeme Mkoa wa Ruvuma hususani Songea.

Katika maswali MATANO aliyoulizwa kashindwa kujibu maswali yote na cha kushangaza yule mtangazaji alikuwa ana mlea badala ya kung'anganiza alijbu alichoulizwa akawa ana muacha yule bibie akitambaa na uongo wake.

Mfano: Mtu akuulize umezaliwa lini? Matokeo yake wewe ujibu JANA UMEKULA MATEMBELE. Ndicho alichokuwa anafanya bibie Badra Masoud.

Ushauri wa bure kwa Tanesco:
Tafuteni PR Manager ambaye ni Injinia wa Umeme na sio Badra tena yeye amesha prove Failure.

Kwa hali inavyoendelea watanzania tutakuja fanyiwa operesheni kwenye uwanja wa mpira kutokana na ukosefu wa umeme..................JK unatuua chimba makaburi tujizike wenyewe.
 
Kuna kitu sijaelewa jamani. Kwani Badra Masoud ni Meneja au Remote ya Meneja?
Sorry, I'm so confused!
 
Ukishakuwa na kiongozi nazi lazima wanaokusaidia ni makorona kabisa, tufanyeni review ya uongozi mzima wa nchi ndo mtajua kama Badra is right with the position. M4C will teach them the lesson
 
hana upeo mzuri wa matumizi ya umeme na semina amabzo kashatumikia ni zile za kijiweni kijiweni tuu. kakma hajui kuelezea matatitizo ya umemem kule songea ambayo hata kilaza anyajua , basi huyo tena ni mzigo kwa serikali ya kileo.
 
Hata mimi nilishtushwa sana,japo siku nyingi nilisha jiuliza nafasi ile anaitumikia vipi.
 
hata mimi nilimshangaa anaulizwa tanesco inadaiwa na wenye mitambo?yeye anasema habari za mtwara,vipuri,grid ya taifa

Mkuu hata mimi nilimsikia nikashangaa! Meneja wa TANESCO Songea alihojiwa kwanza akasema wana ukata wa fedha za kununulia mafuta lakini Badra anasema sijui mtambo wa ABC umahitaji vipuri mara mtambo utatoka Mtwara kabla sijasikia vizuri mara oooooh Songea inaunganishwa kwenye gridi ya taifa. Sijakaa sawa anasema tunajenga 132 KV toka makambako. Mara ooooo mtambo mmoja alioahidi Rais Jakaya Kikwete ndio unafanya kazi. Swali lilikuwa rahisi kwamba Wananchi wa Songea watapata lini umeme baada ya kutoupata hadi wakaandamana. Majibu yakawa hayo hapo juu.
 
Despite of all the incompetencies she might be having, I think we are wrong somewhere! Maana unapokuwa afisa uhusiano au habari kuna details ambazo huwezi kuzisema maana u r nt in the position to do so! Tujiulize, does she sit in the board? Is she one of management team? Maana kimsingi tumezidi kujadili watu humu
 
Lets be honest, yupi wakulaumiwa hapo, Masoud au huyo Meneja wa mkoa?
 
Mkuu nilichokisoma pale ni kwamba TANESCO wana ukata na tatizo lilikuwa ni mafuta. Badra pia alisema mafuta yamepatikana na yanapakuliwa.
 
Mkuu hata mimi nilimsikia nikashangaa! Meneja wa TANESCO Songea alihojiwa kwanza akasema wana ukata wa fedha za kununulia mafuta lakini Badra anasema sijui mtambo wa ABC umahitaji vipuri mara mtambo utatoka Mtwara kabla sijasikia vizuri mara oooooh Songea inaunganishwa kwenye gridi ya taifa. Sijakaa sawa anasema tunajenga 132 KV toka makambako. Mara ooooo mtambo mmoja alioahidi Rais Jakaya Kikwete ndio unafanya kazi. Swali lilikuwa rahisi kwamba Wananchi wa Songea watapata lini umeme baada ya kutoupata hadi wakaandamana. Majibu yakawa hayo hapo juu.

Absolutely right Mr. Kimbunga hao ndio ma PR wa shirika kubwa kama la Tanesco yaani rushwa pale aibu hata kwenye ajira.

Kwa hali inavyoendelea watanzania tutakuja fanyiwa operesheni kwenye uwanja wa mpira kutokana na ukosefu wa umeme..................JK unatuua chimba makaburi tujizike wenyewe.
 
Despite of all the incompetencies she might be having, I think we are wrong somewhere! Maana unapokuwa afisa uhusiano au habari kuna details ambazo huwezi kuzisema maana u r nt in the position to do so! Tujiulize, does she sit in the board? Is she one of management team? Maana kimsingi tumezidi kujadili watu humu

Kukusaidia tu ni kwamba interview ya aina ile si ya kushtukizwa, ni ambayo unafahamishwa well in advance, in fact zaidi hata ya wiki moja. Kwa maana hiyo una uwezo wa kuwasiliana na atakayekuhoji ili kujua nini kitajadiliwa na wewe pia unakuwa na muda wa kufanya utafiti.
Tatizo lake huyu ni lile lile linalotuumbua Watanzania siku zote ambalo ni uvivu wa kujituma badala yake tunataka mambo rahisi rahisi.
Kwa kifupi Badra is a hopeless public relations manager, huwezi kumtetea unless na wewe hujui PR inahitaji nini.
 
Despite of all the incompetencies she might be having, I think we are wrong somewhere! Maana unapokuwa afisa uhusiano au habari kuna details ambazo huwezi kuzisema maana u r nt in the position to do so! Tujiulize, does she sit in the board? Is she one of management team? Maana kimsingi tumezidi kujadili watu humu

FYI Badra ndiye msemaji wa Tanesco kwa nafasi yake. She should be knowlegable and dynamic! Nafasi za kupeana ndio tatizo lake. Hata hivyo zngeonyesha upeo wake pale anapoulizwa maswali technical kuwa asingeweza kujibu in details kwa vile yeyesi mtaalamu, kinyume chake anajibu tofauti na anavyoulizwa, hapo unaonyesha umbumbumbu! Yes, watu wakifanya ndio sio sio lazima wajadiliwe.
 
Kuna kitu sijaelewa jamani. Kwani Badra Masoud ni Meneja au Remote ya Meneja?
Sorry, I'm so confused!

kaka haya mashirika huwa watu wanapewa tu mashavu, utakuta mtu ni msemaji wa shirika lakini wao watamuita "Meneja msemaji" ili tu atafune mshahara wa ngazi ya umeneja
 
Huyu dada kawekwa pale anachojua yeye ni kuaandaa documentaries za "tanesco inaangaza maisha yako"wakati wanagawa giza,ila ameonyesha kuwa papokwapapo ni msumali wa moto kwake,anaulizwa songea watarajie lini kupata umeme anajibu mpango wa kujenga grid ya taifa kutoka makambako utakamilika punde!!!!! Na yule mtangazaji aliamua tu kukatisha mahojiano baada ya kuona kichefuchefu kinazidi....ajira za kupeana bar hizi!!!!!!!!!!!!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom