bado anawasiliana na ex...

Sio kawaida hiyo,kama anafanya hivyo ujue bado ana hisia na x wake ndio maana bado anamuamini katika mambo mbalimbali.
 
Si kosa ila mara nyingi huletea hao watu kuja kukumbushia enzi ambalo ni jambo la hatari kama mmojawapo tayari amepata mpenzi mwingine. Nafikiri si jambo jema sana kujenga ukaribu na ex (simaanishi msiwasiliane, ila kuwe na umbali fulani na hali ya kuheshimiana) na kwenye kushauriana pia si nzuri sana maana huwezi kujua kuwa huyo ex wako hata kama uliachana naye kwa wema yeye anakuwazia nini. Mara nyingi watu wakiachana huwa hawapendi ex wao wafanikiwe ktk maisha yao hususani ya mahusiano. Kwa mambo ya ushauri ni vyema utafuta mtu mwingine kabisa.
 
Hivi kwani watu wakiachana ndio kuwe na uadui? huo ndio unafiki wa mahusiano nisioupenda...
 
Simbaya kuwasiliana kama mmewachana kwa wema na amani hakuna tatizo na hata anapokuomba ushauri unaweza kumpa
kwani inawezekana kua anaamini au anaukubali mawazo yako au wezo ulojaliwa wa kumsaidia kimawazo kuliko huyo alokuanae,na as long as mnaheshimiana sioni tatizo au hamvuki mipaka......
 
kuna kale ka usemi ka mtalaka hatongozwi..............

nanusa harufu ya nimulikie mwiziiiiiiiiiiii hapo ingawa inaweza kuwa hisia tu.....
 
kwa nini Ex's wanaonekana kama laana??

Ina maana hakuna mtu anaweza wasialana na Ex bila ngono??

Kuna ajabu gani kuomba ushauri kwa Ex, kwani mtu akishakuwa Ex busara zinaondoka??

Maovu huanzia kichwani, kama ni kwa kuliwa ataliwa hata na bata mzinga.
 
Nimecheka balaaa! "Ukiona manyoya" ujue kesha liwa! Hahahaha kwa hiyo mahusiano na x inamaanisha kuwa wanaweza kukumbushia awali, wenyewe wanasema awali ni awali hakuna awali mbaya, mwingine nae akasema "mtalaka hatongozwi anakumbushwa tu"

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Avoid kuchukua walochukuliwa kwani.ni rahisi aliekuwa anamiliki kumchukua
 
Pole sana mkuu! huwa si vizuri. Ingawa mi sijui hata machungu ya ex maana tulianzana wote tukiwa wabichi.

Ila nikuambie ukweli kama mwanamke wewe ndo wa kwanza kwake hatokusahau....... Mi mpenzi wangu kuna siku nilimchokoza nikamwambia hivi siku tukiachana na umeshapata mpenzi halafu tukaja onana tena utafanyaje? Na nikikuambia Nimemic mambo yako utafanyaje?

Hehehe! Aibu zikamjaa mara oh usiseme hivyo mpenzi, mi sitaki bhana maneno yako ya kichokozi. Nikambana Akaniambia TUTA.....KUMB....SHI.... Full Aibu na kufunika Uso wake Kifuani kwangu
 
No offense , ila she sounds so cute aisee...
 
Back
Top Bottom