Badilisha mtazamo wako upate ajira

sensa

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
397
22
Habari wandugu,

Wengi wetu tumepata ujuzi mzuri tu na hatujabahatika kuajiriwa au tumeajiriwa lakini kipato ni kidogo mno kiasi kwamba tunaishi kwa taabu sana na malalamiko katika maisha yetu yametawala.

Tujiulize huko kwenye kuajiriwa tunaenda kufanya kazi gani?Na inakujenga vipi kimaisha achilia mbali kukutosheleza kimahitaji?Je fani uliyosomea ndiyo uliyoipenda au ulifanya tu kwa vile ndio njia nafasi pekee uliyoipata?

Kwa tathmini yangu wengi tumekuwa tkiajiriwa kwa ujira mdogo sana ambao hauendani na ujuzi pia tunatumikishwa sana kwa faida ya wachache.Mara nyingi tnawafanyia watu biashara huku sisi wenyewe hatujifanyii kwa visingizio vingi tu ambavyo siwezi kuvitaja,maanake sisi wengi tunafanya biashara lakini si kwa faida yetu.

Hivyo basi kuliko kuhangaika na ajira ambayo ni ngumu kuipata kwa sasa,au ajira ambazo hazikidhi mahitaji ya maisha,kufanya kazi tusizozipenda,kubanwa kwa muda,kupangiwa mapato,sheria na na ukandamizaji mwingi kutoka kwa waajiri naona ni vyema mtu ukajifanyia biashara binafsi,ukawa bosi wa biashara yako,ukajipatia muda wa kutosha kukaa na familia,ukapata kipato cha kutosha kwani nguvu na muda utakaowekeza kwenye shughuli yako utakula matunda yake kwa uwiano huo huo.

Ambaye amenielewa kwa hili anitumie email sensa28@gmail.com niweze kumwonyesha fursa niliyonayo aweze kujiajiri aachane na utumwa wa ajira.Kwani kipindi cha utumwa watu walikuwa wakifanya kazi bure huku wakipatiwa mlo kujikimu na maisha yao,na ajira za leo unalipwa lakini ni ziada gani unayobaki nayo?Ni kosa kusema ajira ni utummwa?Acha kuwafanyia wenzio kazi jifanyie mwenyewe upate kufurahia maisha.

Shukrani zangu za dhati kwenu wote.
 
Kusema ajira ni utumwa ni fikra potofu. Mara zote maisha hutegemeana inaweza ikawa mwajiri au mwajiriwa au kwa namna nyingine yeyote ile. Sikatai kwamba kujiajiri au kufanya shughuli zako mwenyewe kunakupa uhuru mkubwa sana. Ila sizani katika karne ya sasa unaweza kufanya kazi zote peke yako ni lazima utajiri mtu. Hivyo basi kutokana na fikra zako zitamnyima mtu fursa ya kufikilia ajira kwa mtu yeyote yule. Sasa je kama kila mtu akiamua hivyo tutafika wapi? Katika jamii ya sasa kila mtu ni mtumwa wa mwezake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom