Bachelors Club: Tuzungumze

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,366
11,154
Nazungumzia wanaume ambao hawajaoa na ambao wanataraji kuoa na au wanaotaraji kuoa lakini wanakatishwa tamaa na story nyingi hasi kuhusu ndoa.

Nimeandika haya kufuatia mazungumzo na baadhi yao kama mimi ambao wameshakata tamaa kuoa kutokana na changamoto kadhaa za wazi wanazoziona kutoka kwa waliooa.

Najua kwamba kila jumamosi ama jumapili au Ijumaa kuna ndoa zinafungwa lakini nafahamu pia kuna Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi wanandoa wengi wanalia juu ya mahusiano mabaya ndani ya ndoa zao na mengine yanavunjika kabisa. Hili si tu linakatisha tama mabachala kama sisi lakini pia linatengeneza sintofahamu kubwa kuhusu hii taasisi muhimu katika maisha.

La kuzingatia:

1. Kwa nini watu wanaoa/kwa nini tuoe
2. Changamoto za kuzingatia kwenye ndoa
3. Sababu zipi za zitakufanya uvunje ndoa

Kwenye hii semina nawakariibsha watoa mada na ushauri hawa hapa kwenye mjadala: Mtambuzi, HorsePower, mito, Babu D.c , Ngongoseke na wengineo watakaojisikia kutoa neno kwenye Bachelor club yetu.

Lakini pia kwenye side comments nawakaribisha kinadada walioko kwenye ndoa (angalau kwa mujibu wa maelezo yao) nyumba kubwa, gfsonwin, The secretary, Nakshi, cacico n.k watoe neno.

Lakini pia niwatambue mabachala hawa: Obe, Eiyer na wengineo.

Seriosly ni mjadala muhimu na wa w
azi

Update
Mtambuzi kapost mada nzuri kuhusu ishu inayofanana na hii fuata hii link https://www.jamiiforums.com/mahusia...ata-mchumba-mwenye-tabia-uzitakazo%85%85.html
 
Last edited by a moderator:
Ahsante platozoom, labda kwa kuanza ningependa kuzungumzia migogoro ya ndoa............

110.jpg

Wanandoa wanatakiwa kujua kwamba lengo la ndoa siyo kuepuka kukorofishana , hapana . Ukweli ni kwamba kukorofishana kunapotumiwa vema huweza kujenga uhusiano mzuri na imara sana. Kwa sababu kukorofishana hakuwezi kuepukika kwenye ndoa kunatakiwa kutumika kama shule na dawa ya kuimarisha ndoa.

Bila kukwaruzana kwenye ndoa zetu inaweza ikawa vigumu sana kwetu kubandua tabaka la uongo lililotufunika ambalo humfanya kila mmoja kati yetu kushindwa kuona na kumfahamu mwenzake katika tabia yake halisi. Bila kukwaruzana, kila mmoja wetu atajidanganya kwamba anamfahamu mwenzake kama alivyo wakati siyo kweli.

Tunapokwaruzana tunapata nafasi ya kufahamiana vizuri katika hali halisi.
Inabidi tujue kwamba hakuna binadamu aliyekamili, yaani asiyekosea, kama ilivyo dunia yenyewe. Kwa hali hiyo hakuna ndoa ambayo haina makosa, kwa sababu ndoa ni binadamu hao ambao siyo kamili. Kwa hiyo, mtu anapotarajia kuwa au kuishi kwenye ndoa isiyo na kukwaruzana, ni sawa na mtu huyo kutarajia kukutana na binadamu ambaye ni kamili, yaani asiyekosea.Kutarajia kuwa na ndoa ambayo haina kukwaruzana kunaelezwa kuwa ni chanzo kizuri sana kwa ndoa nyingi kulegelege au kuanguka kabisa.

Mtu anapoingia kwenye ndoa akitarajia kwamba huko hatapambana na maudhi au kero za aina fulani, ni lazima ajue kwamba, hatadumu kwenye ndoa yake kwa sababu ndoa hiyo anayoitarajia haipo.
Mtu ambaye hakubali au angalau hataki kuelewa kwamba, ndoa ni lazima iwe na mikwaruzo anaweza kukabiliwa na tatizo lingine baya zaidi kwenye ndoa yake. Kwa kutokujua au kuepuka kukwaruzana, hawezi kuwa tayari kukubali kujadili migogoro ya kindoa ili kupata ufumbuzi.

Hawezi kulikubali hilo kwa sababu haamini kwamba ndoa yenye kukwaruzana ni ndoa.
Wakati mwingine rafiki, ndugu au jamaa zetu hutusimulia jinsi ndoa zao zisivyo na kukwaruzana kama kwamba ni za malaika watupu. Bila kujua, huwa tunajikuta tumewaamini. Tunapowaamini huwa tunachukulia kukwaruzana kuliko kwenye ndoa zetu kama jambo au kitu ambacho hakikutakiwa kuwepo.

Hapo hujikuta tukitamani kuondoka kwenye ndoa hizo kwa matarajio kwamba tunaweza kukutana na "malaika" ambao tutajenga nao ndoa zisizo na doa.
Hata pale ambapo tunasema wanandoa wanapendana sana, bado ndoa yao ni lazima itakuwa na kukwaruzana.

Lakini wanachofanya hawa na ambacho huenda wengine hawafanyi ni kujadili tofauti hizo sawia na kuamua kuzisahau na hapo wote kukubali kujifunza kutokana na tofauti hizo.
Wale walio tayari kujadili tofauti zao sawia ndiyo ambao ndoa zao huwa na afya sana hadi wengine kushangaa kama siyo pamoja na kuona wivu.

Wale wanaodhani ndoa ni mahali pa kila jambo kwenda kama mtu atakavyo, ndoa zao hupogoka vibaya na kufa kwa kishindo........
11.jpg
 
Nimekusoma Mtambuzi....kwa hiyo in summary umejikita kwenye mikwaruzano kama njia bora ya kujenga ndoa. Lakini swali la nyongeza: Unazungumzia kukorofishana kwa viwango vipi, kwa mfano umemfumania mke wako (sikupenda kuliweka hili mwanzo) hii nayo itaitwa mikwaruzano au kuna yale yanayopaswa kuwekwa kwenye viwango vya kukwaruzana ama kuna yale yamepitwa kwenye viwango hivyo?
 
Last edited by a moderator:
Kweli kabisa!

Hapo hujikuta tukitamani kuondoka kwenye ndoa hizo kwa matarajio kwamba tunaweza kukutana na “malaika” ambao tutajenga nao ndoa zisizo na doa.
Hata pale ambapo tunasema wanandoa wanapendana sana, bado ndoa yao ni lazima itakuwa na kukwaruzana.

Lakini wanachofanya hawa na ambacho huenda wengine hawafanyi ni kujadili tofauti hizo sawia na kuamua kuzisahau na hapo wote kukubali kujifunza kutokana na tofauti hizo.
Wale walio tayari kujadili tofauti zao sawia ndiyo ambao ndoa zao huwa na afya sana hadi wengine kushangaa kama siyo pamoja na kuona wivu.

Wale wanaodhani ndoa ni mahali pa kila jambo kwenda kama mtu atakavyo, ndoa zao hupogoka vibaya na kufa kwa kishindo........
11.jpg
 
Nimekusoma Mtambuzi....kwa hiyo in summary umejikita kwenye mikwaruzano kama njia bora ya kujenga ndoa. Lakini swali la nyongeza: Unazungumzia kukorofishana kwa viwango vipi, kwa mfano umemfumania mke wako (sikupenda kuliweka hili mwanzo) hii nayo itaitwa mikwaruzano au kuna yale yanayopaswa kuwekwa kwenye viwango vya kukwaruzana ama kuna yale yamepitwa kwenye viwango hivyo?
platozoom mama Ngina kaniita chumbani, naomba nijibu swali hili kesho.....................LOL
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru kwa nafasi hii platozoom, na mimi kwa kuanza ngoja niongozee kile alichosema Mtambuzi, ila nitajikita zaidi kwenye chanzo cha migogoro ya ndoa. Nitaongea kwa kifupi sana, ila kwa ambaye atakuwa hajaelewa asisite kuuliza ili nifafanue zaidi.

Kwa ujumla kuna vyanzo vikuu viwili vya migogoro ya ndoa, navyo ni cheating na kudharauliana. Ukichunguza matatizo mengi ya ndoa utakuta chanzo chake ni cheating au kinahusiana na cheating, vilevile unaweza kukuta chanzo chake ni dharau au kinatokana na dharau za mhusika. Naamini cheating inajulikana kwa kila mmoja wetu hivyo sitaizungumzia zaidi. Ngoja nizungumzie zaidi kuhusu dharau ktk ndoa.

Ukishaoa (au kuolewa), yaani mkaanza maisha ya pamoja kama mke na mume, hapa sasa ndo mnaanza kufahamiana in and out. Kasoro au mapungufu ya kila mmoja yatajulikana kwa mwenzio. Matarajio uliyokuja nayo yote ndo sasa yatadhihirika au yatapotea kabisa. Kifupi strengths and weaknesses za kila mmoja zitakuwa wazi kwavile sasa mnaishi pamoja na mnafahamiana vilivyo, kila kitu kilichokuwa feki ktk mahusiano yenu ya uchumba sasa kitajulikana. Hapa sasa ndo utakuta maswali kama "hivi kumbe huyu yuko hivi? yanaanza kujitokeza. Matokeo yake unaanza kumshusha thamani siku hadi siku, heshima kwake nayo inaanza kuporomoka, upendo unatoweka taratibu, na dharau inaingia. Unaanza kumuona si mali tena kwako, hana tena nafasi moyoni kwako kivile. Akikukosea hata kidogo tu, kwako ni kosa kubwa sana hata huwezi kumsamehe (si unamdharau!), uvumilivu unatoweka, unaanza kujiuliza 'hivi bila yeye kuishi?. Taratibu unaanza kuona substitute mitaani, kitakachotokea nadhani unakijua.......

Mnapopendana hadi kufikia hadi kufunga ndoa na kuishi pamoja, inatakiwa kuzingatia alichoeleza Mtambuzi hapo juu kwamba migogoro ni sehemu ya maisha. Ujenge upendo halisi kwa mwenzio (kwa kumjali, kumheshimu, kumthamini). Ifikie mahali ujione uwezi kuishi bila huyo mwenzio! Na yeye pia aone hivyo hivyo. Mkijenga upendo wa namna hii, migogoro ya ndoa mtaisikia kwa kwa jirani tu.
 
Platozoom naomba pia nichangie kuhusu sababu zipi zitakufanya uvunje ndoa

Hapa kusema kweli inategemea na mtu mwenyewe. Kwangu mimi cheating tu ndo inaweza kusababisha nikavunja ndoa yangu. Na hii ni kwa sababu hata nikijifanya kumsamehe kwa kweli nitakuwa na-pretend tu. Ukweli ni kwamba sitaweza kumwamini wala kumpenda tena kama ilivyokuwa mwanzo. Kiukweli nitamboa tu hadi mwenyewe atagundua.

Sababu zingine zote kwangu zinazungumzika na zinasameheka ndani ya moyo wangu.
 
Nitazungumza niyajuayo tu.Kwanza napenda nikubali kuwa,kwa mtu anaetaka mke/mume makini(siyo asiekosea)ana kibarua kigumu sana siku hizi.Niliamua kutokuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu sana,nikawa mtazamaji,lakini sasa nimeamua kusaka mke,kazi ipo,tena kubwa.Wanawake wa leo hawapo wa kuoa. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .Nasema hayo kwa sababu,leo kwa mfano,ukimkuta mwanamke anataka kuolewa,kinachomfanya aolewe sio ndoa ni mambo mengine tu na hii ni kwa wanawake wengi.Nimewazungumzia wanawake kwa sababu nawajua kwa kiasi fulani na ndo nakabiliana nao kwenye eneo hili. . . . . . . . . . . . . . . . Sasa basi,ni jambo gumu sana ukaelewana na mtu anaetaka kuolewa kwa sababu ya shinikizo fulani pengine la kikazi,kufuata mkumbo,kutimiza wajibu,kufuata pesa n.k,mtu huyu mtashindwana tu kama wewe ukiwa unataka mke kwa sababu unahitaji kuoa kwa sababu unahitaji ndoa.Katika mambo nadhani yanasababisha nisiwe kwenye ndoa ni pamoja na hayo japokuwa ni mengi sana. . . . . . . . . , . . . . , . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
. .Kuhusu ndoa kuvunjika hapo kuna mambo mengi sana,ila lililokubwa ni kutokujua upendo ni nini.Watu wamekua wakianzisha ndoa kwa sababu za hovyo sana,wanadhani ndoa ni jambo la kukurupuka tu.Hautaweza kuvumilia kutofautiana maamuzi,mtazamo pia baadhi ya maudhi kama hamuujui upendo.Kama mmeanzisha ndoa kwa sababu ya mwili,pesa na mambo kama niliyoeleza hapo juu,lazima yataibuka mambo mengi kama aliyosema Mtambuzi hapo juu. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .All an all hakuna ndoa isiyokua na tofauti kwenye baadhi ya mambo yanayopelekea maudhi ya hapa na pale!
 
Last edited by a moderator:
Utafiti unasema chanzo #1 cha mmigogoro ndani ya ndoa
ni suala la upatikanaji na matumizi ya pesa ndani ya nyumba:
nani anatafuta, anatafuta kwa njia gani? nani anatumia,
anatumia kwa kupata vitu gani? nani anaset priorities?
Kuna mengine pia, ngoja niwapishe wana ndoa wataje,
mi nimeleta hili ambalo limesha fanyiwa utafiti (source)
 
Kuna ukweli hapa ila mimi nadhani hizi monetary problems hutumiwa kama ngao ya kuhalalisha tu hizo divorce lakini underneath huwa kuna sababu halisi imejificha.
Ohh!!!Let me declare interest kwanza kabla ya kusema mengi Super-Bachelor..
 
mmh! mimi sijui ninzie wapi ila ngoja nianze kwa maswali haya ka hawa bachelor's kama wewe platozoom na Eiyer.

Nawaona Mtambuzi na mito pia Mwali wakiongelea migogoro miye n sawa na wamepatia kabisa. Lakini hapa tumeulizwa maswali haya:-
1. Kwa nini watu wanaoa/kwa nini tuoe
2. Changamoto za kuzingatia kwenye ndoa
3. Sababu zipi za zitakufanya uvunje ndoa

majibu kwa mtazamo wangu;
1) Binafsi naomba niwaambie sababu kubwa ya kwanini watu wanaoa ni ili kupata wenza maisha yao. Ujue kwamba bibadam huwez kuwa kama kisiwa upo muda ambao unahitaj mweza ambaye atakuwa ni sehem yako ya maisha ambaye utakuwa tayari kushare nae amani, furaha na upendo wako ambaye utakuwa huru kujieleza kwake na ambaye pia atakuwa huru kukusikiliza, kukusaidia na hata kukushauri. Unategemea mtu huyu awepo wakati wa raha na tabu ambaye wewe utajitoa kwake kwa halia na mamali na yeye ajitoe kwako kwa hali na mali. hapa silaha kubwa ni uaminifu

2)changamoto za kuzingatia kwenye ndoa kwangu mimi ni nyingi sana, kwani ikumbukwe kwamba sisi sote tu bnadamu na tunamapungufu hivyo basi mapungufu yote ama udhaifu wa aina yeyote ambao tunao basi ni changamoto kwa wenzi wetu.. Hapa silaha kubwa ni uvumilivu.

3) sababu kubwa za kukufanya uvunje ndoa binafsi mimi kama mimi sijaiona lakin kwa kua hapa dunian tunatofautiana basi hizi zaweza kuvary mfano mito kasema cheating, Mwali kasema kipato na matumuzi yake , mwingine atasema kudharauliwa na kunyanyaswa, mwingine atasema ulevi nk. Kwahiyo ni swala la mtu binafsi. silaha ya hapa ni upendo na msamaha.

Ngoja ni kwambie platozoom, mimi huwa nina kanuni yangu ya 50% and that is our motto in ma house hata mgeni akija unaweza ukakutana na hili neno "nusu nusu" utashangaa sana ila liko established kwamba katika chochote kile ili upate furaha nacho lazima ucontribute by 50% na pia katika kosa lolote lazima wewe umecontrribute by 50% so to me before hujanza kumlaumu na kutupia lawama mwenzi just look at yourself and assess your nusu umeitimiza kweli?
kumbuka hata leo nikikukaribisha nyumbani kwangu ili ufurahie ugeni wako kwangu u have to play your 50% honestly and be reassured kwamba you will enjoy. sasa hapo na mimi nikiplay zile nusu yangu lazima utapata furaha tu na hutoboreka . sasa huo ni mdfano tu wa maisha ya kawaida waweza pia kuurelate kwenye maisha ya ndoa.
All in all lazima Mungu akutangulie ili akuwekee silaha zote hizo kwa wepesi na si vinginevyo.

Hope hii BEGY PARTY nimeifanya vyema ma kungwi wenzangu watanisaidia tena zaid. Jumapili njema maswali yenu yawekeni nitayajibu nikitoka kanisani saa tano.
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru kwa nafasi hii platozoom, na mimi kwa kuanza ngoja niongozee kile alichosema Mtambuzi, ila nitajikita zaidi kwenye chanzo cha migogoro ya ndoa. Nitaongea kwa kifupi sana, ila kwa ambaye atakuwa hajaelewa asisite kuuliza ili nifafanue zaidi.

Kwa ujumla kuna vyanzo vikuu viwili vya migogoro ya ndoa, navyo ni cheating na kudharauliana. Ukichunguza matatizo mengi ya ndoa utakuta chanzo chake ni cheating au kinahusiana na cheating, vilevile unaweza kukuta chanzo chake ni dharau au kinatokana na dharau za mhusika. Naamini cheating inajulikana kwa kila mmoja wetu hivyo sitaizungumzia zaidi. Ngoja nizungumzie zaidi kuhusu dharau ktk ndoa.

Ukishaoa (au kuolewa), yaani mkaanza maisha ya pamoja kama mke na mume, hapa sasa ndo mnaanza kufahamiana in and out. Kasoro au mapungufu ya kila mmoja yatajulikana kwa mwenzio. Matarajio uliyokuja nayo yote ndo sasa yatadhihirika au yatapotea kabisa. Kifupi strengths and weaknesses za kila mmoja zitakuwa wazi kwavile sasa mnaishi pamoja na mnafahamiana vilivyo, kila kitu kilichokuwa feki ktk mahusiano yenu ya uchumba sasa kitajulikana. Hapa sasa ndo utakuta maswali kama "hivi kumbe huyu yuko hivi? yanaanza kujitokeza. Matokeo yake unaanza kumshusha thamani siku hadi siku, heshima kwake nayo inaanza kuporomoka, upendo unatoweka taratibu, na dharau inaingia. Unaanza kumuona si mali tena kwako, hana tena nafasi moyoni kwako kivile. Akikukosea hata kidogo tu, kwako ni kosa kubwa sana hata huwezi kumsamehe (si unamdharau!), uvumilivu unatoweka, unaanza kujiuliza 'hivi bila yeye kuishi?. Taratibu unaanza kuona substitute mitaani, kitakachotokea nadhani unakijua.......

Mnapopendana hadi kufikia hadi kufunga ndoa na kuishi pamoja, inatakiwa kuzingatia alichoeleza Mtambuzi hapo juu kwamba migogoro ni sehemu ya maisha. Ujenge upendo halisi kwa mwenzio (kwa kumjali, kumheshimu, kumthamini). Ifikie mahali ujione uwezi kuishi bila huyo mwenzio! Na yeye pia aone hivyo hivyo. Mkijenga upendo wa namna hii, migogoro ya ndoa mtaisikia kwa kwa jirani tu.

NIimekupata mito....sasa tuseme ndio hivyo umegundua mapungufu ya mwenzi wako mechanism gani inayotumika ku-solve tatizo ama inategemea utakalofikiria wakati huo?
 
Last edited by a moderator:
Platozoom naomba pia nichangie kuhusu sababu zipi zitakufanya uvunje ndoa

Hapa kusema kweli inategemea na mtu mwenyewe. Kwangu mimi cheating tu ndo inaweza kusababisha nikavunja ndoa yangu. Na hii ni kwa sababu hata nikijifanya kumsamehe kwa kweli nitakuwa na-pretend tu. Ukweli ni kwamba sitaweza kumwamini wala kumpenda tena kama ilivyokuwa mwanzo. Kiukweli nitamboa tu hadi mwenyewe atagundua.

Sababu zingine zote kwangu zinazungumzika na zinasameheka ndani ya moyo wangu.

Evidence ya cheating ni ngumu sana.........ni rahisi kwa mfano wewe mke wako kupata ushahidi wa cheating kuliko wewe ambavyo unaweza kumkamata.............Unaweza kutumia ushahidi wa mazingira kumwacha mkeo? Au utasubiri kwa maumivu makali ushahidi wa papo kwa papo?

Hebu tuseme ndio imetokea huta-consider factors nyingine kabla ya kuamua? (kama watoto, namna wewe na mkeo mlivyoanza maisha mkiwa hamna na senti na leo baada ya miaka 10 au 20 kosa moja linafuta historia yote nzuri?)
 
madame gfsonwin, mzee Mtambuzi na mito naomba niwashukuru kwa niaba ya mabachelor na mabachelorette wote wa humu jf. mnatutia moyo sana ili tuwe waangalifu na makini kuingia ktk chama kubwa la TAMU (TAnzania Marriage Union). naomba kuongezea point ndogo sana. wanandoa wanapaswa kuchuliana madhaifu yao na sio kuyafanya yale madhaifu kuwa kigezo cha kumnyanyasa / kumdharau mwenzi wako. bali kumrekebisha kwa upendo kwan hakuna binadamu mkamilifu. . .
 
Last edited by a moderator:
Nitazungumza niyajuayo tu.Kwanza napenda nikubali kuwa,kwa mtu anaetaka mke/mume makini(siyo asiekosea)ana kibarua kigumu sana siku hizi.Niliamua kutokuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu sana,nikawa mtazamaji,lakini sasa nimeamua kusaka mke,kazi ipo,tena kubwa.Wanawake wa leo hawapo wa kuoa. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .Nasema hayo kwa sababu,leo kwa mfano,ukimkuta mwanamke anataka kuolewa,kinachomfanya aolewe sio ndoa ni mambo mengine tu na hii ni kwa wanawake wengi.Nimewazungumzia wanawake kwa sababu nawajua kwa kiasi fulani na ndo nakabiliana nao kwenye eneo hili. . . . . . . . . . . . . . . . Sasa basi,ni jambo gumu sana ukaelewana na mtu anaetaka kuolewa kwa sababu ya shinikizo fulani pengine la kikazi,kufuata mkumbo,kutimiza wajibu,kufuata pesa n.k,mtu huyu mtashindwana tu kama wewe ukiwa unataka mke kwa sababu unahitaji kuoa kwa sababu unahitaji ndoa.Katika mambo nadhani yanasababisha nisiwe kwenye ndoa ni pamoja na hayo japokuwa ni mengi sana. . . . . . . . . , . . . . , . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
. .Kuhusu ndoa kuvunjika hapo kuna mambo mengi sana,ila lililokubwa ni kutokujua upendo ni nini.Watu wamekua wakianzisha ndoa kwa sababu za hovyo sana,wanadhani ndoa ni jambo la kukurupuka tu.Hautaweza kuvumilia kutofautiana maamuzi,mtazamo pia baadhi ya maudhi kama hamuujui upendo.Kama mmeanzisha ndoa kwa sababu ya mwili,pesa na mambo kama niliyoeleza hapo juu,lazima yataibuka mambo mengi kama aliyosema Mtambuzi hapo juu. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .All an all hakuna ndoa isiyokua na tofauti kwenye baadhi ya mambo yanayopelekea maudhi ya hapa na pale!

Sawa ndio umeingia kwenye ndoa halafu unagundua huo udhaifu (kwamba mwenzako ameingia kwenye ndoa kwa sababu ya pressure ya familia yake) what should you do......Unamwacha? kama si hivyo mbinu ipi inatumika kuhakikisha mnakuwa kwenye mstari mmoja
 
mmh! mimi sijui ninzie wapi ila ngoja nianze kwa maswali haya ka hawa bachelor's kama wewe platozoom na Eiyer.

Nawaona Mtambuzi na mito pia Mwali wakiongelea migogoro miye n sawa na wamepatia kabisa. Lakini hapa tumeulizwa maswali haya:-
1. Kwa nini watu wanaoa/kwa nini tuoe
2. Changamoto za kuzingatia kwenye ndoa
3. Sababu zipi za zitakufanya uvunje ndoa

majibu kwa mtazamo wangu;
1) Binafsi naomba niwaambie sababu kubwa ya kwanini watu wanaoa ni ili kupata wenza maisha yao. Ujue kwamba bibadam huwez kuwa kama kisiwa upo muda ambao unahitaj mweza ambaye atakuwa ni sehem yako ya maisha ambaye utakuwa tayari kushare nae amani, furaha na upendo wako ambaye utakuwa huru kujieleza kwake na ambaye pia atakuwa huru kukusikiliza, kukusaidia na hata kukushauri. Unategemea mtu huyu awepo wakati wa raha na tabu ambaye wewe utajitoa kwake kwa halia na mamali na yeye ajitoe kwako kwa hali na mali. hapa silaha kubwa ni uaminifu

2)changamoto za kuzingatia kwenye ndoa kwangu mimi ni nyingi sana, kwani ikumbukwe kwamba sisi sote tu bnadamu na tunamapungufu hivyo basi mapungufu yote ama udhaifu wa aina yeyote ambao tunao basi ni changamoto kwa wenzi wetu.. Hapa silaha kubwa ni uvumilivu.

3) sababu kubwa za kukufanya uvunje ndoa binafsi mimi kama mimi sijaiona lakin kwa kua hapa dunian tunatofautiana basi hizi zaweza kuvary mfano mito kasema cheating, Mwali kasema kipato na matumuzi yake , mwingine atasema kudharauliwa na kunyanyaswa, mwingine atasema ulevi nk. Kwahiyo ni swala la mtu binafsi. silaha ya hapa ni upendo na msamaha.

Ngoja ni kwambie platozoom, mimi huwa nina kanuni yangu ya 50% and that is our motto in ma house hata mgeni akija unaweza ukakutana na hili neno "nusu nusu" utashangaa sana ila liko established kwamba katika chochote kile ili upate furaha nacho lazima ucontribute by 50% na pia katika kosa lolote lazima wewe umecontrribute by 50% so to me before hujanza kumlaumu na kutupia lawama mwenzi just look at yourself and assess your nusu umeitimiza kweli?
kumbuka hata leo nikikukaribisha nyumbani kwangu ili ufurahie ugeni wako kwangu u have to play your 50% honestly and be reassured kwamba you will enjoy. sasa hapo na mimi nikiplay zile nusu yangu lazima utapata furaha tu na hutoboreka . sasa huo ni mdfano tu wa maisha ya kawaida waweza pia kuurelate kwenye maisha ya ndoa.
All in all lazima Mungu akutangulie ili akuwekee silaha zote hizo kwa wepesi na si vinginevyo.

Hope hii BEGY PARTY nimeifanya vyema ma kungwi wenzangu watanisaidia tena zaid. Jumapili njema maswali yenu yawekeni nitayajibu nikitoka kanisani saa tano.

Nimekupata gfsonwin.........Kwa hiyo hutakiwi kuingia kwenye ndoa ukiwa na kanuni zako:

1. Kwamba nataka ndoa yangu iwe kwenye mfumo fulani?

2. Kwamba kuna kanuni maalum zinazoniongoza..kwamba mwenzi akizivunja hizo ndoa imefikia tamati yake au sitavumilia

3.Lakini hapo umezungumzia falsafa ya fifty fifty.............lakini huo unakuwa mtazamo wa upande mmoja......Je kama mwenzi wako hawezi kubeba nusu yake? umlazimisha............kwamba ni lazima ajue kwenye kila tatzizo ndani kuna mchango wako pia.......Au kama haelewi unambebea na ile nusu yake?
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom