Kwa anaefaham chochote kuhusu hiyo kozi inayotolewa na UDSM naomba anipe mawazo, kuhusu usomaji wake, field, na future.
Karibun wana JF wenzangu!
Soma zaidi: View attachment Prospectus 2012-2013 (SoED pg 199 - 209)].pdf
Karibun wana JF wenzangu!
Kimsingi hii ni shahada ya ualimu inayotolewa na Chuo Kikuu Dar es Salaam, pamoja na kufundisha stadi zingine za msingi za ualimu msisitizo wake upo katima michezo.
Wanafunzi wa shahada hii hutoka moja kwa moja Kidato cha Sita au kutoka vyuo vya ualimu na hufundishwa michezo karibu yote kiufundi, utawala, masoko, saikolojia na mambo mengine ambayo yanahusu michezo.
Mwanafunzi anayehitimu shahada hii huweza kuwa mwalimu wa michezo katika Sekondari au vyuo vya ngazi ya cheti na stashahada, huweza kuwa maafisa michezo wa wilaya, mkoa au mashirika mbalimbali na pia huweza kufanya kazi katika vyama, mashirikisho pamoja na vilabu vya michezo kote nchini.
Wanafuzu pia kuwa makocha, watawala au hata waamuzi wa michezo mbalimbali.
Karibu.
Soma zaidi: View attachment Prospectus 2012-2013 (SoED pg 199 - 209)].pdf