Babu wa loloindo anaendelea kugawa vikombe?

Stevemike

Senior Member
Mar 12, 2011
117
15
Muda sasa umepita mrefu kidogo bila kusikia habari za babu! Hivi, anaendelea kugawa vikombe? Na kwa nini hasikiki kwenye vyombo vya habari siku hizi kama zamani?
 
mmmh.....mrejesho ninaoupata kwa wale walioenda kunywa dawa.......wacha tuu
 
Muda sasa umepita mrefu kidogo bila kusikia habari za babu! Hivi, anaendelea kugawa vikombe? Na kwa nini hasikiki kwenye vyombo vya habari siku hizi kama zamani?
Wanahabari wote wameshapata kikombe kwahiyo hawahitaji kwenda huko tena-no one to report.
 
Vkombe mwana bado vinatembea ila wadau kwa sasa ni waganda,burundi na wakenya na huko ndo anasikika kweli mpaka washaadai yupo kusini mwa kenya
 
Mmh kweli ni muda mrefu hajasikika na wagonjwa hawaongei tena!
 
ivumayo haidumu, kwakasi iliyokuwepo ya watu kwenda kunywa kikombe, madhira na taabu zilizowapata watu kujaribu kukimbilia kwa babu imebaki kuwa kumbukumbu na simulizi. Hakika yaliyopita si ndwele.
 
uongo kamwe haudumu hasa unapo halalisha kutumwa na Mungu.
The good thing ni kwamba jinsi watu wengi walivyoenda kupata kikombe ndivyo ushuhuda wa uongo wa babu ulivyodhihirika.
Hta wale waliotoa povu kumtetea hapa jf wamepiga kimya maana kama sio wao ni ndugu zao au jirani amekwenda samunge na hakuna jipya zaidi ya kuendelea kuugua na matatizo yao
 
Wanahabari wote wameshapata kikombe kwahiyo hawahitaji kwenda huko tena-no one to report.
siyo waandishi hawaripot, wamesha ona dhambi waliyoiyengeneza kwa kusababisha vifo vya watanzania ambao wamekufa kwa sababu ya kalamu zao, kutangaza kuwa anatibu kisukari,na ukimwi kitu ambacho wamejikuta ni uongo sasa kutangaza ukweli wanaona aibu na kuendelea kutangaza uongo hawawezi kwani baada ya kuona waliokufa kwa sababu yao wanaogopa. Ivi leo ni miezi mingapi imepita toka wale watu 200 walio fanywa kama sample? mpaka leo kimya baada ya kujikuta hakuna dawa ila ni utapeli wa kimataifa unaendelea, mrema kamuulizeni kama anamabadiriko yoyote?
 
Back
Top Bottom