BABU WA LOLIONDO: nimeoteshwa, muujiza mpya unakuja kaeni mkao wa kula.

Leonard Robert

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
11,064
7,196
amefunguka leo ndani ya supermix ya e.africa radio
amedai ameoteshwa na mungu na ameambiwa ataanza kutenda muujiza mpya soon, tena utakua wenye nguvu kuliko kile kikombe maarufu kama kikombe cha babu.
Amesema anashangazwa na watu wanaosema amejenga nyumba ya m.200,wakati yeye amenunu gari dogo moja na ka-lori kakubebea dawa,na nyumba ndngo isiyofika thamani m.10
amedai watu bado wanamiminika toka msumbiji,malawi,mombasa na kenya.
Kuhusu bei ya tiba amesema ni ileile sh.500 au sh100 kwa wakenya.
Mwisho kamalizia kwa kusema ameoteshwa muujiza mpya unakuja.zimbwela na baluti walipomuuliza kuhusu list ya vigogo..ameng'aka na kudai ni siri.
 
Amesema anashangazwa na watu wanaosema amejenga nyumba ya m.200,wakati yeye amenunu gari dogo moja na ka-lori kakubebea dawa,na nyumba ndngo isiyofika thamani m.10

Babu bwana..
 
Kwa hiyo babu naomba utupe na bei ya huo muujiza mpya ili tuanze kuzichangachanga duh yaani sasa hivi natafuta kiwanja huko. Nahamia loliondo jamanii. Huko ni full ma miujiza
 
Huyo mzee ana matatizo, kaona mia tano tano hazikumtosha sasa anataka aanzishe mzigo wa buku buku , na sisi watanzania tusiwe wajinga kiasi hicho kila mtu akiamka na idea zake basi tuwe kama milimbukeni.Wake up tanzania
 
ushirikina una sura nyingi sana, masikitiko ni kuwa hata serikali inaendeshwa kishirikina shirikina tu! watu wanaikabidhi nchi kwa washirikina na wachawi kisha wao wanaruka kwenda kula maisha nje!
 
ni habar njema kwa wale wanaojua umuhimu wa zile safari za loliondo, babu aendelee kubarikiwa na aje na miujiza mingi.
 
Babu ni mbabaishaji na mimi naona kama ni ishara ya shetani kuangalia kama akiibua kitu ni vipi anaweza kuwateka wanadamu kupitia miujiza feki.
 
ushirikina una sura nyingi sana, masikitiko ni kuwa hata serikali inaendeshwa kishirikina shirikina tu! watu wanaikabidhi nchi kwa washirikina na wachawi kisha wao wanaruka kwenda kula maisha nje!

Mimi nahisi ni bora tukachukua mfano wa Babu kama mbunifu wa miradi tofauti, lakini kumshutumu nahisi kama tunakosea kwani kila mtu ana akili ya kufikiri kwahiyo mtu anayepeleka 500 yake kwa babu ni kutokana na uamuzi wake mwenyewe ambao tunauita ni uamuzi uliofanywa na mtu mwenye akili timamu, sasa vipi lawama tumtupie Babu, ni watu wangapi ambao wanatumia hela kwa kwenda kwenye burudani au kuhonga bila ya sababu ya msingi, kwahiyo matumizi yoyote mtu anayoyafanya kwa babu naamini ni halali tu, yeye kama mbunifu wa mawazo ya kutafuta hela kulingana na uwezo wa baadhi ya waTanzania wanaekubaliana naye, basi hatuna ila zaidi wengine kubaki kuwa waangaliaji. Ni kama mtu ukinunua kanda ya muziki wa rap za kimarekani ambayo hata huelewi kinachosemwa, mwisho wa yote ni burudani tu, Basi naombeni wenzangu tumuweke Babu katika kundi la watoa Burudani, kama unahisi hukubaliani naye kuwa hana miujiza wala dawa inayotibu.
 
Babu ni mbabaishaji na mimi naona kama ni ishara ya shetani kuangalia kama akiibua kitu ni vipi anaweza kuwateka wanadamu kupitia miujiza feki.

hapo ndipo nashindwa kupata tafsiri halisi ya shetani,..........maake kwa wale wanaoamini wamepona wanasema ni Mungu na wale wasioamini wanasema ni shetani,.....anyway_hata mimi siamini ila siwezi kutamka for sure kuwa ni shetani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom