Babu wa loliondo amaliza watu Visiga

Ninaachoona hapa ni fitina tu kwani kumuita babau wa loliondo ndiye kawaua hao watu si kweli. Inawezekana hata wasingekwenda kwa babu wangekufa na si kwamba kwa babu walikunywa sumu ndio maana wamekufa. Kijijini kwangu watu wote waliokwenda wamepona na kama unavyojua ukienda kwa babu na imani mbili huponi kwani lazima uende ukiamini kwamba ukinywa kile kikombe mambo yako yatakuwa safi. We fikiria unampeleka mtu yuko mahututi na aelewi yuko wapi ni vigumu kupona kwa sababu mtu huyo hana fahamu za ku-exercise faith. Hafikiri wengi waliokufa ni watu ambao ufahamu wao ku-exercise faith ulikuwa umepotea au mtu aliekwenda tayari amekata tamaa na pale akaenda kama formality basi huyo ni vigumu kupona. Hivyo ndivyo ninavyo amini na correct me if I'm wrong.
Bado hujui kitu. Babu anadai anatibu kwa nguvu za Mungu! Utasemaje wanaokwenda wakiwa mahututi hawana uwezo wa kuexercise faith ivo hawawezi kupona? Lazaro aliyefufuliwa na Yesu alipataje imani? Na yule kichaa makaburini? Kubali tu babu sio tu ni agent wa shetani bali ni shetani!ushuhuda wa roho mtakatifu ni ,NYANYUKA NA JITWISHE GODORO LAKO! Yaan Rise&walk hayo mengine usemayo ni matakataka tu ndugu yangu.Mungu si wa mateso ivo kwamba wa2 wakapange foleni maili nyingi walale na kujisaidia vichakani ndo wapate uponyaji! Ikiwa ivo bac damu ya mwanakondoo ilimwagika bure! Yeye mwenyewe asema. NIRA YANGU NI LAINI NA MZIGO WANGU NI MWEPESI!
 
Wapo wengine wengi wamekunywa wapo fit majina tunayo mfano Mrema wa TLP.
Pole kwa wafiwa na mungu awapumzishe kwa amani waliotangulia.
Sote tusafari moja!

mkuu kuwa serious kwa mtazamo wako Mrema kapona?una uhakika?
 
tuseme nini kwa wale waliofariki baada ya kurudi kutoka kwa TB Joshua? Acha kila mja ajitafutie matumaini POPOTE anapoweza, hadi siku ya kuaga dunia itakapofika. Ni mambo ya kibinadamu tu.
Babu wa Loliondo ni sawa na hospitali ya India, TB Joshua, Sauzi na kwingine kokote kulingana na imani yako, nafasi yako, na uwezo wako. God bless.
 
Back
Top Bottom