Babu Wa Loliondo Alikuwa Mgonjwa Wa Akili

sasa kama tabibu alikuwa na matatizo ya kiakili je wagonjwa wake walikuwa na matatizo yapi?Nalog off
 
title ya hii thread na contents tofauti,nilitegemea mngetupa maelezo ya kitaalam,ugonjwa wa akili wa babu,unaitwaje na diagnosis ikoje badala yake kumejaaa lawama tu,babu hakuita mtu mlienda wenyewe kwa hiari yenu.
 
Mobhare Matinyi: " Huenda Babu Wa Loliondo Alikuwa Mgonjwa Wa Akili"

Uko sahihi kabisa.

Huyu Babu alikuwa janga kwa taifa letu na anapaswa kulaaniwa vikali na watu wote wenye akili timamu. Uwezekano mkubwa ni kwa Babu wa Loliondo kuwa na tatizo la akili ambalo halikujitokeza kwa namna tuliyozoea - ile kupiga kelele na kuvua nguo. Huyu babu labda ni mgonjwa akili aliyejikita katika imani za kimiungu.

Watanzania, kutokana na ujinga wetu, umaskini wetu, na maradhi yetu, tulimpa fursa ambayo hakustahili. Taifa lenye watu zaidi ya 60% wanaoamini ushirikina, asilimia 40% wasiojua kusoma na kuandika, 35% wanaoishi katika umaskini uliokithiri, na viongozi wengi wanaoshinda kwa waganga, watu wanaofikiri kuwa unene tipwatipwa na ulevi ni afya, ni lazima mtu kama Babu angeonekana shujaa kwetu.

Dawa za Babu zilielezwa na wazee wa Kisonjo kwamba ni za kawaida, na zinatibu magonjwa kadhaa likiwemo kisukari, lakini kwa ujinga wetu watu wakawa wanakunywa kikombe kimoja kwa kudhani imani za kimiujiza zitawasaidia. Wale mababu hawakunywa vikombe vya Babu na bado wanaendelea kuzitumia bila shida kila wakiumwa. Mababu wasiojua kusoma na kuandika wanatushinda akili watu tuliokwenda shule. Dawa zile zimefanyiwa utafiti duniani na zikaonekana kuwa na uwezo wa kufanya kazi fulani, hivyo, ukinywa kikombe kimoja unaweza kupata nafuu lakini hutapona kwa sababu hukunywa kitaalam. Unafuu huu ndio uliowapa wajinga imani kwa Babu anaponya.

Babu hakuwa na utumishi wa uungu wowote wala utabibu wowote. Huenda ni mgonjwa wa akili na ni kweli amekuwa janga la kitaifa. Aibu na fedheha kwa taifa letu.

Mobhare Matinyi.


The whole thing was a stratagem - a scheme propagated by the government to avert public "esprit de corps" that was present towards the anticipated social revolution "thought" to be prompted by CHADEMA.
 
hahahaha kama huyu babu ana matatizo ya akili waliopanga foleni kupata kikombe je?

Waliotoa magari ya kusomba dawa?

Waliokodi helicopta? Kwenda kupata kikombe?

Waliopanga foleni kungojea kikombe?
 
Viliibuka vikombe Tabora, Mbeya, Mtwara, singida, na Rombo kwa Mramba..sijui ila na mimi nilienda japo nilipeleka tim ya watu...it was Nite mare...
 
Babu wa Loliondo ni muhuni na tapeli, kawatapeli watu wengi sana, eti anatibu magonjwa yote huu si uhuni..

Sasa hivi anakula bata tu
Muhuni hufuata watu na kuwatapeli Babu hakuwahi fuata mtu pengine watu ndio walijihunisha wenyewe.. na Kwa Taarifa yako Bado anaendelea na Tiba... Nabii hakubaliki Nyumbani Kwake..

Ngoja uje kuugua ndio Utajua kama ni Muhuni au Lah.... Siombei Ugonjwa... My Nephew amepona Asthma
 
13th March 2011 22:30

Tupo tunakusanya nauli tukufuate. Mganga hajigangi, nyimbo za mzee wa upako vipi? Mi hata ningesikia sauti ya babu kwenye radio najua ndo nimepona kabisa. Mungu awabariki wote mnaoamini.

Imani imeishia wapi? ulipona?
 
Back
Top Bottom