Babu Seya, Papii Kocha wafungwa maisha - Soma hukumu

Bibie, tuna uhakika kwamba babu seya na papii wamebaka, na tunaweza kuwaita wabakaji bila shaka yeyote, mahakama ya juu kabisa ishathibitisha.

tatizo watanzania mtu akishakua maarufu tunamfia kabisa, au ndio dawa wanazoendea kwa waganga walikoambia wabake, ndio zinatupumbaza?

ushahidi umethibitisha bila shaka kwamba wawili walibaka, sasa mnang'ang'ania mbona wengine wameachiwa, kama hamna ushahidi wa kutosha wafungwe tu?
hapo unakosea mkuu,
mzee Nguza alisema roho yake chukueni ila watoto wake waachieni (if and only if you want to destroy him).

As long as the government has decided to punish him, its well and good. The government of CCM will never be in power forever. I know someday, though not so soon but it will come to pass.

Tanzanians will be free in deed. Now we are just living under the shadow of a so called 'fake democracy'

sorry guys, thats my opinion!
 
Wataomba case yao kupitiwa tena!
Kwani sheria inasemaje hapo? Ingekuwa vyema kabla mheshimiwa hajatoka madarakani basi apitishe 'msamaha'
kutokana na necha ya kesi yao, ITAKUA NGUMU kupata msamaha wa rais.
 
hapo unakosea mkuu,
mzee Nguza alisema roho yake chukueni ila watoto wake waachieni (if and only if you want to destroy him).

As long as the government has decided to punish him, its well and good. The government of CCM will never be in power forever. I know someday, though not so soon but it will come to pass.

Tanzanians will be free in deed. Now we are just living under the shadow of a so called 'fake democracy'

sorry guys, thats my opinion!

CCJ itawatoa jela, I HOPE SO.
 
Tanzanians will be free in deed. Now we are just living under the shadow of a so called 'fake democracy'

This was not the question of democracy in Tanzania but rather the 'rule of law'!
 
HUKUMU HIYOOO! Papii Kocha na Baba yake, Babu Seya wameonekana na hatia hivyo wataendelea kukaa jela For The Rest of Their Lives!!....kwa video na mengineyo nimeyafuma hapa click here DARHOTWIRE
 
Hivi what is the real story behind this case jamani? Mi huyo mdogo kanitoa machozi anavyolia hivyo. Ni out of guilt au innocence? Au analilia kakake na babake wanaobaki jela?
 
Jamani mimi sio mtaalam wa sheria naomba niulize, kama hawa wote walihukumia kwa makosa yanayofanana na urgement ya wakili Marando ilikuwa ile hukum ya kwanza na ile ya hakimu Lyamuya zilikuwa na makosa, iweje hawa wawili tu ndio waonekane bado na hatia na hao wengine ni innocent?
 
paparazi wa bongo nao mmmh ni noma kweli kweli


i1769_untitled.JPG

 
Hivi what is the real story behind this case jamani? Mi huyo mdogo kanitoa machozi anavyolia hivyo. Ni out of guilt au innocence? Au analilia kakake na babake wanaobaki jela?
wenye data watujuze jamani
 
umesikitika nn? kuachiwa au kufungwa maisha?
unaujua undani wa issue yenyewe?
Tuhuma za kulawiti watoto bana......kama kweli mm naona wapewe maisha, na viboko 10 kila siku!

Mi naona bora wangekata hizo dudu zao, pambafffffffffffff
 
wanaweza kukata rufaaa tena, ngoja tuone...ila nina amini watatoka tu ni vile serikali inajishaua tu na inaona noma kuwaachia huru wote kwa pamoja!

Kwanini unataka watoke ikiwa mahakama imethibitisha kuwa wana hatia.
Hivi jaribu kujiweka katika nafasi ya mzazi ambaye mtoto wake amebakwa, au hao watoto waliobakwa.

Kama kweli imethibitika beyond reasobale doubt, WAFUNGWE Milele.
 
Kisutu baada ya kupatika na makosa ya ubakaji na kulawiti.

Katika rufaa ya kesi hiyo, baba yao, Babu Seya na kaka wa ndugu hao, Papii Nguza ‘Papii Kocha’ wameeendelea kusota gerezani katika kifungo cha maisha.






Familia ya Nguza ikiwa chumba cha Mahakama kabla ya kusomwa kwa rufaa yao, mapema leo

Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, wakiongozwa na Jaji Natalia Kimaro, Salum Massati baada ya kupitia upya makabrasha ya rufaa hiyo, iliyosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Neema Chusi, wamewachia huru vijana hao baada ya kuridhika na hoja za upande wa utetezi kuwa hawakuhusika katika tukio hilo lililohusisha familia hiyo mwaka 2003.

Pengine maamuzi ya leo ya Mahakama ya Rufaa yanakuwa yameacha maswali mengi miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatilia kwa karibu shauri hilo nje na ndani ya nchi ambapo awali Jarida moja maarufu la ‘Le Mans’ la Ufarasa liliwahi kutoa chapisho la makala ndefu likihoji iweje mwanamuziki huyo afungwe kifungo cha maisha ugenini badala ya kurudishwa nchini kwao.





Francis (kulia) akiwa na kaka yake Mbangu muda mfupi kabla ya kuingia chumba cha mahakama

Hakika ilikuwa ni safari ya kiza totoro kwa familia hii ya mwanamuziki huyu mkongwe ambaye kabla ya kukutwa na masaibu hayo alikuwa kwenye mikakati ya kuitangaza albamu ya mwanae Papii Kocha iliyojulikana kwa jina la Salima ambayo ndani yake kulikuwa na nyimbo kama fanta , Seya na Salima wenyewe zilizokuwa zinatamba kwa kiasi kikubwa wakati huo.

Mwanzo wa kesi hiyo iliyokuwa imegubikwa na utata uliripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti moja maarufu la Burudani na michezo kuwa mwanamuziki huyo ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kubaka watoto wa kike wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huo.

Ulikuwa ni mshituko mkubwa kwa mashabiki wa muziki wa dansi hasa wale ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa na mapenzi ya kweli na mwanamuziki huyu na kiasi kikubwa jambo hilo liliibua minong’ono mingi ya hapa na pale juu ya kukamatwa kwao

Lakini baada ya upelelezi na taratibu kukamilishwa kesi hiyo ilitinga mahakami na ili kuona haki inatendeka upande wa mashitaka uliita mashahidi 24, huku upande wa utetezi ulikanusha vikali kutenda makosa hayo na kuita mashahidi wanane.

Baada ya kesi kuunguruma kwa takribani mwaka mzima hatimaye hakimu mkazi wa mahakama ya kisutu Addy Lyamuya aliwakumu kifungo cha maisha jela, Katika hukumu yake, Hakimu Lyamuya alitupilia mbali utetezi wa Babu Seya na wanawe na kuwatia hatiani wote katika makosa yao yaliyokuwa yanawakabili baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashitaka.

Hata hivyo Babu Seya na wanawe hawakuridhishwa na hukumu hiyo na kuamua kukata rufaa kwenye Mahakama Kuu na kwa bahati mbaya Januari 27, 2005, aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo, ambaye kwa sasa amestaafu alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.





Francis Nguza akitoka nje ya Mahakama huku akilia kwa uchungu

Baada ya maamuzi hayo Babu Seya aliamua kupiga hatua zaidi kwa kukata rufaa nyingine safarii hii katika mahakama kuu ya rufani na Januari 3, mwaka huu, jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani wakiongozwa na Jaji Nataria Kimaro, Salum Massati, na Mbarouk Mbarouk walisikiliza rufaa hiyo kwa siku moja.

Wakati wa utetezi wao, mawakili wa warufani hao, waliomba mahakama iwaachirie huru wanamuziki hao kwa madai kuwa hukumu iliyowatia hatiani, ilikuwa na dosari nyingi za kisheria.

Mawakili hao walidai kuwa kesi hiyo ilikuwa ya kupangwa na kwamba hawajawahi kuona hukumu ya hovyo ya kama hiyo tangu waanze kufanya kazi ya uwakili kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Mawakili hao waliwasilisha sababu nne za kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa na Jaji mstaafu, Thomas Mihayo, na hukumu iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Addy Lyamuya, ambao wote waliwatia hatiani washtakiwa kwa makosa ya kuwalawiti watoto wadogo, hivyo kuwafunga kifungo cha maisha jela.

Miongoni mwa sababu hizo ni kwamba jaji na hakimu huyo walikosea kisheria kutoa hukumu hiyo kwani sheria inaitaka mahakama kabla haijaanza kuchukua ushahidi wa mtoto ni lazima ijiridhishe kwamba mtoto huyo ana akili timamu na anaelewa maana ya kiapo na kisha irekodi hayo kwenye jarada la kesi lakini Hakimu Lyamuya hakufanya hivyo wala kuandika rekodi,” alidai Marando.

Marando akiwasilisha sababu hizo kwa kujiamini, alidai kuwa kwa makosa hayo ya kisheria, yaliyofanywa na hakimu Lyamuya na jaji huyo hadi wakafikia uamuzi wa kuwafunga kifungo cha maisha warufani, ni wazi kwamba walikuwa wanapingana na sheria za nchi na maamuzi yaliyotolewa na majaji wa mahakama za hapa nchini kwenye kesi mbalimbali, ambazo alizitumia kutetea hoja zake.

“Lakini majaji katika rufaa ya Mahakama Kuu hakuna ushahidi uliotolewa unaoonyesha warufani walibaka...hayo yalikuwa ni mawazo ya hakimu kwamba lazima Babu Seya na watoto wake waende gerezani,....narudia tena sijawahi kuona hakimu wa aina hii na hukumu ya aina hii ambayo hakimu aliamua kuweka maoni yake binafsi kwani kinachowatia hatiani washtakiwa katika kesi zote ni ushahidi na siyo maoni ya hakimu.

“Ni wajibu wa mahakama kutafakari ushahidi wa utetezi hata kama hauna uzito; sasa huyu Lyamuya katika hukumu yake amewataja mashahidi wa utetezi waliokuja kutoa ushahidi bila kueleza mashahidi kwa mapana walieleza nini!

“Kwa mkanganyiko huu uliofanywa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Lyamuya, siyo tu alikosea kisheria; nasema alifanya makusudi na alikuwa ameshaamua kuwapeleka jela warufani!” alidai Marando.





Baba na Mwana, wakikumbatiana kwa huzuni....safari yao ya maisha ndo imeishia hapa...


Alihoji sababu zilizosababisha upande wa mashtaka kuficha ripoti ya daktari aliyewafanyia uchunguzi watoto hao wanaodaiwa kubakwa na warufani na kushindwa kuleta mashahidi ambao ni wanamuziki wa bendi ya Achigo, mama wa Babu Seya na mke wa Babu Seya, kwa sababu waliona mashahidi hao wangewaumbua.

“Kesi hii ni ngumu kwetu sote na kama mahakama na sisi tunaona warufani walifanya haya makosa tuwalaani ila mimi Marando nasema nimejiridhisha hawajafanya hayo makosa.

“Hivi tujiulize kibaiolojia kweli inawezekana mtoto wa miaka sita abakwe na wanaume hawa (warufani) nyuma na mbele halafu aweze kutembea? Haingii akilini hata kidogo; nasema kesi hii ni ya kutunga kwani hata mwanamke mwenye umri wa utu uzima akifanyiwa unyama huu hawezi kutembea!” alidai Marando na kusababisha umati uliofurika kuendelea kuacha vinywa wazi kwa mshangao.

Akijibu hoja za mrufani, Wakili Mkuu wa Serikali, Justus Mulokozi, ambaye alitumia nusu saa kujibu hoja hizo alidai kuwa kitendo cha shahidi kushindwa kumtambua mshtakiwa mahakamani siyo sababu inayopelekea ushahidi wa shahidi huyo kuonekana hauna thamani.

Pia alidai mahakama ikiamini upande mmoja, hailazimiki kuangalia upande mwingine lakini hata hivyo hoja hiyo ilipingwa vikali na Marando ambaye alidai kuwa hoja hiyo haikupaswa kutolewa na wakili mwandamizi kama Mulokozi kwani hoja hiyo inatofautiana na sheria za nchi na kauli hiyo ya wakili wa serikali imedhihirisha sasa ni kweli Lyamuya aliegemea ushahidi wa upande wa mashtaka tu.

Kwa babu Seya maamuzi ya leo yanaweza kuwa ya faraja kwake kwani mara nyingi amekuwa akililia kuachiwa kwa watoto wake hao.
 
Wanaweza kuwa na makosa lakini slogan ya wanasheria si inasema haki sio tu itendeke lakini ni lazima pia ionekane kutendeka, kwa hili la Seya nadhani hata kama hukumu hii ni ya haki, lakini haki haionekani kutendeka!
 
Natumaini kwa wema wa rais wetu, akama alivyofanya kwa wafiwa baada ya Ditopile kutumia bunduki yake, mara hii pia tunamuomba aitembelee familia ya Nguza.
 
Wanaweza kuwa na makosa lakini slogan ya wanasheria si inasema haki sio tu itendeke lakini ni lazima pia ionekane kutendeka, kwa hili la Seya nadhani hata kama hukumu hii ni ya haki, lakini haki haionekani kutendeka!

Inategemea ni nani anaangalia. Kama ni kweli hawa kina Nguza wote walifanya vitendo hivyo, kitendo cha hao wawili kuachiwa huru kinaweza kisiwaridhishe wazazi pamoja na watoto waliofanyiwa 'unyama' huo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom