Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,301
Wote tumeshuhudia media inavyotupasha habari kila uchao kuhusu yanayojiri kule kijiji cha Semunge wilaya ya Loliondo. Babu amekuwa kwenye kurasa za mbele za magazeti yetu kila uchao na kutufanya kusahau mambo muhimu ya nchi. Hii ni faraja kwa baadhi ya watu kwani kwa kiasi fulani wamepumua na ni hasara kwa wale wengine kwani sasa hivi hakuna asikiae malalamiko yao watu wako bize na "babu".
Babu kazungumziwa sana na yeye kuzungumza nimeanzisha thread hii ili kila alichosema babu tuki quote then tu read between the lines.
Babu kazungumziwa sana na yeye kuzungumza nimeanzisha thread hii ili kila alichosema babu tuki quote then tu read between the lines.
Dawa hii ni lazima unywee hapa hapa na si mahala pengine na mtu anayetakiwa akunyweshe ni mimi tu
Mchungaji Masapila pia alisema kazi ambayo amekuwa akifanya kwa saa zaidi za 13 kila siku, haimsumbui akidai kwamba tayari alikwishamuuliza Mungu kwamba atawezaje kutoa tiba kwa watu wengi ilihali ni mzee na akaelezwa kuwa ataongezewa nguvu.
Naishukuru Serikali maana naona wananiunga mkono, hii ni dawa kutoka kwa Mungu na wala sio mti pekee na nilijua wakipima hawatakuta madhara yoyote kwani Mungu alikwishanieleza kuwa watapima wataalamu wa ndani na nje ya nchi dawa hii na watakuta haina madhara
Hakuna madhara kwa mgonjwa kuendelea na dawa zake za awali hata baada ya kunywa dawa yake na kwamba si vyema kuacha ghafla kutumia dawa hizo