Babu Mwasapile aungana na Rostam

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Hatimaye mch. mstaafu mzee Mwasapile ameungana na mbunge wa Igunga Bwana Rostam Aziz kwa kuwataka wagonjwa wanaopata tiba ya "kikombe" kuendeleana dawa za hospitali kama kawaida.

Hili limejitokeza wiki chache baada ya mbunge wa Igunga Rostam Aziz kuwataka wapiga kura wake wasibweteke na dawa za BABU na badala yake waendelee kutumia dozi ya hospitali, na kutoa ushuhuda kuwa ndugu zake watano wametumia "KIKOMBE" na bado wanaendelea kusumbuliwa na kisukari.

CHANZO: gazeti la Mwananchi
 
Hajauungana na huyu fisadi,

Babu anasema watu wanapona, fisadi anadai hawaponi.
wapi na wapi ?
 
Mpaka leo sijaona ushahidi wowote wa Daktari na mgonjwa wake, kuwa huyu nilikuwa na mtibu UKIMWI au Kisukari, kabla ya kwenda kwa babu vipimo vyake hivi hapa na baada ya kwenda kwa babu vipimo ni hivi hapa, Negative. Na baada ya miezi mitatu bila kutumia dawa za hospital bado negative, baada ya miezi sita bado negative, baada ya mwaka bado negative.

Nikipata hizo data, ndio ntamuamini na kumuunga mkono amteteae babu. Kwa sasa namuunga Mkono RA na mimi nasema ni kiini macho tu.
 
MAJIMSHINDO!,ni vema kama wewe utakaa na hiyo imani yako,na pia waache wenzio wamuaminio babu na tiba yake wawe huru na imani yao.HESHIMA kwa imani za wenzio ni msingi bora katika maisha ya dunia hii tupitayo.
Rostam naye tumuache na imani yake ya kifisadi na wote tusubiri hukumu yetu itakapofika kila mtu kwa yale aliyotenda.
 
Nawe ukae na imani yako, yangu kuhusu babu nimeiweka wazi hapo juu.

Na huo unaosema ufisadi wa RA sijauona ushahidi mpaka leo, naona porojo tu. Jee, unao ushahidi utujuze humu JF. Au kama unao wa ukweli kwa nini usimshitaki?
 
Nilichosikia ni kuwa babu amewaambia wagonjwa wakienda kwake wasiache kubeba dawa zao watakazokuwa wakitumia wakati wanasubiri tiba yake
 
Mpaka leo sijaona ushahidi wowote wa Daktari na mgonjwa wake, kuwa huyu nilikuwa na mtibu UKIMWI au Kisukari, kabla ya kwenda kwa babu vipimo vyake hivi hapa na baada ya kwenda kwa babu vipimo ni hivi hapa, Negative. Na baada ya miezi mitatu bila kutumia dawa za hospital bado negative, baada ya miezi sita bado negative, baada ya mwaka bado negative.

Nikipata hizo data, ndio ntamuamini na kumuunga mkono amteteae babu. Kwa sasa namuunga Mkono RA na mimi nasema ni kiini macho tu.

Husomi magazeti wewe ndo ungejua. Mgonjwa wake wa kwanza alitoa ushuhuda na daktari wake pale Wasso alielezea kushangazwa na kuongezeka kwa CD4 za mgonjwa wake ndo ikabidi wamuulize siri yake.
 
Nawe ukae na imani yako, yangu kuhusu babu nimeiweka wazi hapo juu.

Na huo unaosema ufisadi wa RA sijauona ushahidi mpaka leo, naona porojo tu. Jee, unao ushahidi utujuze humu JF. Au kama unao wa ukweli kwa nini usimshitaki?

Nachelea kupigwa ban ila hii nayo c**p!
 
Nawe ukae na imani yako, yangu kuhusu babu nimeiweka wazi hapo juu.

Na huo unaosema ufisadi wa RA sijauona ushahidi mpaka leo, naona porojo tu. Jee, unao ushahidi utujuze humu JF. Au kama unao wa ukweli kwa nini usimshitaki?

Yaelekea na wewe unatokea HABARI CORPORATION,ndio maana huelewi-elewi hivi.
 
Husomi magazeti wewe ndo ungejua. Mgonjwa wake wa kwanza alitoa ushuhuda na daktari wake pale Wasso alielezea kushangazwa na kuongezeka kwa CD4 za mgonjwa wake ndo ikabidi wamuulize siri yake.

Mkuu usiamini kila unachokisoma ,kwa sasa naombeni tuwe akina Thomaso wa kipindi cha yesu.

Yanayoandikwa kwenye magazeti sio yote ya ukweli,ni kuuza magazeti tu.bila shaka tunahitaji mtu aliyethibitishwa kuwa na magonjwa husika kabla na baada ya kupata kikombe tuifuatilie afya yake mpaka mwisho .

Lakini hii ya yule kasema hivi na mwingine vile.haitufikishi popote.Hlafu watu matapeli siku hizi wanakuja na kichaka cha dini,unakumbuka DECI.

Na je tuamini shuhuda zote zinazotolewa makanisani?Vipi kuhusu misukule kwanini siku hizi haifufuliwi?.Kila kitu kinafanywa kwa masilahi ya watu husika.Babu leo ni bilionea na bibi wa tabora keshokutwa atakuwa bilionea nhalafu wanapotea ghafla tu.

Turudi nyuma kipindi cha Tekero alivuma sana,akaja Mwandulami ,hao wote walikuwa wanasoma majira na nyakati na kuwaibia wananchi wa Tanzania wenye gonjwa kuu la ujinga
 
Ndio tabu ya kusikiliza radio mbao,babu aliongea vingine na wewe unatueleza vingine,achana na maneno ya kwenye kahawa.
 
MAJIMSHINDO!,ni vema kama wewe utakaa na hiyo imani yako,na pia waache wenzio wamuaminio babu na tiba yake wawe huru na imani yao.HESHIMA kwa imani za wenzio ni msingi bora katika maisha ya dunia hii tupitayo.
Rostam naye tumuache na imani yake ya kifisadi na wote tusubiri hukumu yetu itakapofika kila mtu kwa yale aliyotenda.

nawe uwaache wanaoamini kuwa babu ni tapeli SAWA?
Halafu tubandikie hapa ufisadi alofanya ROSTAM usilete longolongo.
 
Watu walio kwenye payroll ya Rostam utawajua tu kwa hoja zao!!!!

Shame on you Elungata!!!!

Tiba
 
Back
Top Bottom