Babu atoa kikombe cha 300,000

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MCHUNGAJI Ambilikile Masapila 'Babu' wa Samunge wilayani Ngorongoro, Arusha amefikishwa vikombe laki tatu wiki hii tangu kuanza kwa tiba hiyo Oktoba mwaka jana, imefahamika.Habari
zilizopatikana na kuthibitishwa na Msaidizi wa Babu, Bw. Jackson
Dudui zimeeleza kuwa takwimu hizo zilizopatikana kutokana na idadi ya watu wanaokunywa dawa hiyo na fedha zinazokusanywa, sh 500 kwa kila kikombe (sh milioni 150), zinaleta faraja kwao kwani kama dawa hiyo hiyo inayodaiwa kutibu magonjwa sugu kama kisukari, saratani, shinikizo la damu, pumu na ukimwi isingekuwa na manufaa kwa jamii huenda idadi hiyo isingefikia.

Bw. Dudui alisema wanaamini hali hiyo ndiyo inayosababisha kuendelea
kumiminika kwa wagonjwa kijijini hapo kufuata kikombe hicho
kinachotibu magonjwa hayo, ambapo kwa juzi jumla ya wagonjwa
17, 065 walipata huduma hiyo.

Alisema jana walitaraji kutoka tiba kwa magari zaidi ya 400 yenye wagonjwa
zaidi ya 3,000 yalikuwa yakimgonja mchungaji huyo atoke kanisani na
kwamba idadi kubwa ya wagonjwa hao kwa sasa inatoka nchini Kenya
tofauti na hapo awali.

“Hivi tunavyozungumza yapo magari zaidi ya 400 yakimsubiri Babu atoke
kanisani na kuanza kuwahudumia kuanzia saa 8 mchana na hakika babu
atawamaliza leo hii,” alisema.

Aliongeza kuwa bado wageni wakiingia ambapo katikati ya wiki iliyopita walipata wachungaji zaidi ya 10 kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati waliokuwa kijijini hapo
ambapo pamoja na mambo mengine walisaidiana na Mchungaji Masapila kutoa tiba hiyo.

Akizungumzia maendeleo ya tiba hiyo na mtafaruku kuhusu ukusanyaji wa ushuru kati ya Halmashauri ya Wilaya hiyo na Serikali ya Kijiji cha Samunge, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Elias Wawa Lali alieleza utoaji tiba
unaendelea vizuri kijiji hapo.

Kuhusu mtafaruku huo Mkuu huyo alisema mtafaruku huo wa ushuru wa magari na helkopta umekaa kisiasa zaidi na kuomba mwandishi kusubiria hadi leo
maamuzi halisi yatakapotolewa baada ya kukaa kikao
kitakachofanyika kijijini hapo.

Alisema bado maamuzi hayajafikiwa kujua ni mamlaka ipi
itakayokuwa ikikusanya ushuru huo kati ya Halmashauri ya Wilaya ya
Ngoromngoro na Serikali ya Kijiji cha Samunge. Hadi kikao hicho
kitakapokaa.

“Siwezi kuingia kwa undani zaidi kuzungumzia suala hilo naomba usubiri kikao cha kesho (leo) kutakuwa na kikao kitakachozungumzia suala hilo na
tutawapeni taarifa na kuomba leo usiandike chochote kuhusu suala
hilo,” alisisitiza.

Kumekuwepo na mvutano kwa muda sasa kugombea ushuru wa magari na helkopta kati ya pande hizo na wakati fulani polisi wamekuwa wakiingilia kati ili
kupunguza jazba miongoni mwao na kuhakikisha Babu anaendelea na
tiba.
 
Kuna sredi nyingine humu inayodai kuwa ni cha 3,000,000 au macho yangu? Ipi ni ipi? Na ni nani huyu very independent counter ambaye tunaweza kuamini takwimu zake bila shaka?
 
Kuna sredi nyingine humu inayodai kuwa ni cha 3,000,000 au macho yangu? Ipi ni ipi? Na ni nani huyu very independent counter ambaye tunaweza kuamini takwimu zake bila shaka?
Ni Miss Judith huyo!
Yeye huwa anasikiliza redio mbao zinazoishia Magomeni!
 
ametoa jumla ya vikombe 300,000 (vikombe LAKI TATU), ambayo times Tshs. 500 equal = Tshs. 150,000,000 bila VAT.

TRA wapo tu wamekaa wanahangaika kutukata kodi sisi tunaoingiza sh. elfu thelathini kwa siku au wiki kabisa.

Hii ni Tanganyika zaidi ya uijuavyo, yani akili kumkicha tu wala hulali njaa..........
 
ametoa jumla ya vikombe 300,000 (vikombe LAKI TATU), ambayo times Tshs. 500 equal = Tshs. 150,000,000 bila VAT.

TRA wapo tu wamekaa wanahangaika kutukata kodi sisi tunaoingiza sh. elfu thelathini kwa siku au wiki kabisa.

Hii ni Tanganyika zaidi ya uijuavyo, yani akili kumkicha tu wala hulali njaa..........

Naombeni Ufafanuzi wa Hii kitu jamani. kwani Babu abastahili kulipa Value Added Tax?
Kama ni hivyo nikienda nimdai Invoice yangu ya Kikombe kabisa.
 
Naombeni Ufafanuzi wa Hii kitu jamani. kwani Babu abastahili kulipa Value Added Tax?
Kama ni hivyo nikienda nimdai Invoice yangu ya Kikombe kabisa.

Kwanini asilipe VAT? sisi tunalipa VAT hata kwa mazao yetu tuliyopanda na kutaka kuuza sokoni sembuse yeye ambaye ameikuta hiyo miti imeota porini ikiwa ni rasilimali ya taifa?
 
Mi nafikiri tusiende mbali sana kuhusu VAT kulipa ama kutolipa maana hatoi hata invoice/proforma cha msingi ni kwamba anatakiwa kulipa income Tax as per Income tax act 2006 Sec 6 (1, a).
 
Safi sana babu! Huo ndo uwajibikaji, kwa kutoa Ripoti Isiyo Rasmi ya Mapato!
 
Back
Top Bottom