Baba yangu Mchawi... Anatuangamiza, nifanyeje?!

ushauri wangu ni huu...unafahamu makanisa wayojihita ya kilokole?yoyote yale uyoyajua wewe,nenda siku moja mtafute mchungaji mweleze hari halisi then atakusaidia kwenye maombi usikae na mzigo mwenyewe kwenye moyo wako itakusumbua.mimi nahamini hizo nguvu za giza zipo washikaji wangu kibao walikuwa na story kama hizo.usiwaone watu wako balabarani kila mtu anamapito yake..kamwe usiende kwa waganaga wa kienyeji watakula pesa yako bure na nafuhuu hautapata.nenda kwa ombewe kwanza ni bure na uhakika utapona.amin tu.
 
Mpwa unakosea kusema MUNGU yuko kimya wakati yeye ndie amekuoigani hadi leo hii umepata uwezo wa kutupasha haya unayotupasha, usijaribu hata siku moja kumpangia MUNGU jibu, muache tu yeye hafanyi maamuzi kwa pressure ya Mwanadamu, ila mkumbushe kuwa yeye ndiye aliyekutoa huko alikokutoa muombe uendelee kuiona na kesho nyingine ili mzazi wako huyo kabla hajafa aione nuru ya MUNGU na wokovu wa familia yako.
 
Tafuta kanisa la kilokole.mweleze mchungaji, atakuombea wewe na kuvunja hizo nguvu za giza zinazowasumbua ndugu zako na ukoo mzima.
Mwamini Yesu na ishi maisha ya kumtegemea yeye pekee. hakuna nguvu ya uchawi itakayokuweza wewe wala familia yako ikiwa utampokea Yesu.
Barikiwa sana.
 
Tobaaa huyo ni baba mzazi?
Kwa mtazamo wangu mchawi hatakiwi kuishi na dawa ya mchawi mkabizi mwanao, sasa nachokushauri
mchanie laivu, mwambie dingi wewe mchawi na umeshamfanyia fulani na flani usiogope, na wewe umsogelee mungu kwa karibu zaidi, ila usiogepe maana shetani hamuwezi mwenyezi mungu cha msingi wewe uweke imani yako kwa
mungu, usiende kwa waganga utapoteza muda hapo piga goti kwa sana utashinda mkuu
 
Ngugu Kifront naamini uko njema kaka!! Ila mimi nakuomba kitu kimoja ili uwee kupata ulinsi wa Mungu ni lasima umpokee bwana Yesu na maanisha umpe yeye maisha yako akupe ondoleo la dhambi na kukusafisha kwa damu yake ya thamani na uishi sawasawa na neno la Mungu. Nasikitika kukwambia kuwa unawesa enda kwa waganga ukisani utapata dawa/ suluhisho ya hayo sana sana unabaki kuwa mtumwa wa shetani tu maana uningiswa kwenye mikataba naye kupitia maajenti wake. Hatuwesi kusishinda ngufu sa gisa/ ulosi/ uchawi huku sisi maisha yetu hayako nuruni. Tambua kuwa kuna pande mbili tu kuwa upande wa nuru au gisa...... na yeyote asiyeishi sawaswa na neno la mungu ambaye hajaokoka huyo hawesi kumshind ibilisi..... nilasima tumpokee mwana wake Mungu ndipo tunawekwa huru, maana kwake adui hawesi kumgusa aweye yeyote yule. UPO ULINSI WA KUTOSHA WA MUNGU KWA WALE WAMWAMINIO MWANA WAKE. i
@Gaijin;
Umechangia kiasi kwa mie ku-post hii thread baada ya kuona ulivyo-comment kwa mtu mmoja aliyesema kaka yake karogwa. Nikaona na mie nipost hiki kisa changu maana naona imani inaanza kutiswa na ibilisi. Jamani If I could give you details of my story, mtashngaa tunayofanyiwa na huyu mtu. Any way thanks for your comments, will help me to stand still and let God move katika kipindi hiki kigumu. So sad to see the people you grew up together happily going mud for no reason.
Imagine the position of our mom, I cant tell.
 
Asee

Kifront...mtu wa kwanza nayehitaji uokozi ni wewe mwenyewe na familia yako....uokolewe kutoka hiyo IMANI ya uchawi uliyo nayo...huwezi kutumikia mabwana wawili, kama unamwamini Mungu ni Yeye peke yake anayeweza kujua ni lini akupe nini ...usiseme kuwa anachelewa kujibu maombi! maana hujamwomba hasa unachokitaka.

Rudi kwenye imani yako, funga/sali sana naye atatenda tu Miujiza yake...atakukinga na mabaya yote, atakuelekeza njia gani upitie ili usidhurike kwa neno au tendo lolote la hao wachawi. hapa IMANI yako ndo mwokozi wako...usijidanganye kwenda kwa waganga hakuna mganga wa kweli hata mmoja nao ni wachawi vile vile,

Good luck
 
nenda sumbawangana au kigoma wewe umkate dingi makali ila usimuue.....dawa ya moto ni moto!!!!
 
mkuu pole sana.. Hii ni mitihani ya hapa duniani na kawaida mungu humpa mtu mtihani anaoweza kuukabili. Jambo la msingi ni kuendelea kumuomba mungu na kuwa na subira, na kutambua kuwa ipo siku shida zote hizi zitaisha maana hakuna atakayeishi milele. Kwa waganga usiende mkuu nao wanashida zao kama wewe na zimewashinda kutatua..mfano shida za umaskini na kipato kidogo mpaka wakaamua kufanya uganga. Mkabidhi mungu shida zako kwa imani nae atakutasaidia.
 
Nataka nimchane Laivu, ila sijui ndo makombora yote atayaelekeza kwangu?

Huwezi kushindana na mchawi kwa njia za kibinadamu. kumchana ni kazi bure tena anaweza kukudhuru zaidi.
Jina la Yesu pekee ndio liwezalo kukusaidia. Mpokee Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako ndugu, matatizo hayo yote yatakuwa historia kwako na hutakaa ujute.
 
uchawi uko na hata kwenye vitabu vitakatifu vimeandika, Ushauri wangu kwako ni kumtumaini MUNGU kumwomba bila kukata tamaa kwani yeye pekee ndo anaweza kukulinda wewe na familia yako,

Sure.Uchawi upo maana hata kwenye vitabu vitakatifu imeandikwa.Kama unaamini existence of god basi lazima pia uamini uchawi kwamba upo maana kwenye vitabu hivyo hivyo vya mungu umeelezwa!Ukisema eti huamini uchawi kama upo na hapo hapo unajifanya kuamini mungu una jicontradict mwenyewe!Chamsingi ni kuamini kwamba MUNGU ANA NGUVU ZISIZOWEZWA NA UCHAWI!
 
Nataka nimchane Laivu, ila sijui ndo makombora yote atayaelekeza kwangu?
..

Pole sana Kifront...nakupa kwa sababu as you said you are only 26yrs old; ni kweli ni ngumu sana kisaikolojia kuyakabili matatizo makubwa kama hayo. Kuhusu uchawi; upo au haupo ni tunawza kubishana mwaka mzima tusifikie muafaka. Kwangu mimi la muhimu ni wewe binafsi unaamini nini; ukiamini unaweza kulogwa/kuloga then uchawi utauona ukifanya kazi yake. wanasaikolojia wanaeleza vizuri dhana ya uchawi, na jinsi gani inavyo develop. Tazama jinsi mtoto mdogo anavyo ogopa giza...theory ya uchawi nayo inadevelop hivyo hivyo; inajengwa na experience yetu ya nyuma (toka wadogo tunakua) ambayo inaathiri namna tunavyotafsiri matukio mbalimbali katika maisha yetu. Mfano kama umekua ukisikia jinsi uchawi unavyofanya kazi, ukapata masimulizi ya watu waliorogwa; pengine ukawaona mf. vichaa, wagonjwa nk unafika mahali unaanza kuhusisha matukio fulani na uchawi (mfano; Mr. Y kakosana na baba yako, kafukuzwa kazi, kawa mlevi, kawa mwehu). Kwa mtu ambaye hajakulia katika mazingira/makuzi ya kuamini uchawi anaweza ku reason hivi; Mr Y hakuwa mtendaji mzuri, watu wengi walikuwa wanalamika including dingi yako, bosi kapata taarifa, uchunguzi ukathibitisha , kafukuzwa kazi, out of stress kaamua kunywa pombe apoteze mawazo (he has a poor coping mechanism), pombe ,stress vinamfanya kuchanganyikiwa). Nadhani nimejitahidi kuonyesha kuwa uchawi ukiuamini utauona (actually, wakati mwingine utautafuta na kulazimisha kuwa umeuona).
 
1. Mwambie baba yako bila kumuogopa na mwambie kwa ukali na kujiamini, kamwe hatasogelea.
2. Zidi kumuomba Mungu zaidi na zaidi usichoke! Ukichoka tu, shetani atakumaliza.
 
kwa Mungu hakuna neno lolote lililo gumu lisilowezekana. Kumbuka ombeni mtapewa, tafuteni mtapata, gongeni mtafunguliwa. Imani yako i atakuponya
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom