Baba yangu anaichukia serikali ya ccm sana..haya ni machache niliyoongea nae leo..

Edson

JF-Expert Member
Mar 7, 2009
9,846
5,076
Edson: vipi mzee naona umekaa umetulia tuli ,gazeti gani hilo unasoma?


Baba: Aah! Leo si ni jumapili halafu kama haitoshi ni jumapili ya pasaka, kwa hiyo leo ni siku nzuri ya kupumzika na kutafakari ufufuko wa Yesu lakini pia maisha kwa ujumla...wewe ndio nadhani hii ni pasaka ya kwanza kuwa huku mara ya mwisho ilikuwa 2003.


Edson: ni kweli mzee , lakini mzee unaonaje hali ya nchi hii kwa ujumla?


Baba: kwa vipi?


Edson:katika nyanja zote za kisiasa, kiuchumi na hata kiutamaduni..unaonaje ukilinganisha na huko tulikotoka?


Baba: hakuna nyakati ngumu kama tulizopo katika nchi hii..hali ni mbaya sana hasa kiuchumi na kisiasa..hakuna kuthaminiana viongozi wamekuwa wabinasfi, walafi ,wachoyo, waongo na kila aina ya uovu wanafanya na nwanachi wameachwa wanajiongoza


Edson: yote haya yamesababishwa na nini ?


Baba: viongozi wabovu na mfumo mzima wa nchi unavyoendeshwa ni wa kibovu, nchi inaendeshwa vibaya sana..haki hakuna na uonevu kila mahali..sasa hivi kila mtu analia na kusikitika.watanzani wengi hawana nyuso za furaha kama zamani.ni manung’uniko kila mahali. Ila mi nasema udhalimu huu umekaribia kuisha maana mwamko nauona toka kwa wananchi.


Edson: hilo hata mi naliona..watu sasa hivi wamekuwa waelewa wanaelewa tofauti na zamani sasa sijui itachukua mda gani wote kuwa na uelewa na kuona kuwa sasa ni mwisho wa udhalimu.


Baba: zamani ilikuwa ni tatizo la elimu ya uraia..nashukuru sasa hivi kuna chama makini kinatoa elimu nzuri kwa raia na mwitikio ni mzuri kwa wananchi lakini pia teknolojia nachangia kuongeza ufahamu kwa watu.njia za kupashana habari zimekuwa nyingi sana.
.

Edson: chama gani, chadema?


Baba: sasa kuna kingine zaidi ya hicho!!


Edson: hata mimi nakikubali sana sasa hivi kila kona ni chadema na watu wameitikia vizuri..hivi mzee tatizo la ccm hasa ni ninj? Wapi wamekosea hadi watu wanakikataa?


Baba: wale ni wezi na wapenda fitina sana, kitu kingine ccm si chama cha wananchi wa kawaida wa hali ya chini, ni chama cha wafananyabiashara..


Edson: mzee wewe si umesomeshwa na serikali ya chama hiki enzi za mwalim? na wewe leo unawapinga?


Baba: mwanangu kipindi kile kulikuwa na haki na kuonyana na kuwajibisana kulikuwepo leo hii wezi wanatamba na ushenzi wa kila aina wanafanya na hakuna anayewanyooshea kidole..nyerere hakuwa kama hawa waliopo madarakani..siwezi kuunga mkono upuuzi wa ccm hata kidogo eti kisa nimesomeshwa na iliyokuwa na serikali ya ccm..hata mama yako sasa hivi amebadilika na anaichukia ccm sana.

Edson: mama aliniambia alipojitoa ccm...hivi mzee ngoja mi nikuulize, hivi tatizo la rais wa nchi hii ni nini hasa?


Baba:sijakuelewa unataka kusema nini hasa.


Edson:yaani namaanisha ana shida gani maana nchi hii imeyumba sana mikononi mwake.


Baba: hana uwezo wa kuongoza na hajui kuongoza , unajua edson ngoja nikwambie; kiongozi aliye na hekima atawafundisha watu wake yaliyo mema na siku zote atakuwa ni mfano kila apitapo na utawala wake utakuwa na utaratibu..sasa hivi vitu hana na hakuna Tanzania ndio maana kila mtu sasa hivi anajihisi anaweza kuwa rais maana wanaona aliyepo sasa hivi madarakani anavyofanya.ukiona mkuu wa nchi anarushiwa mawe na wakazi wa kijijini kabisa ujue hali ni mbaya


Edson: lakini mzee...!


Baba: ngoja nimalize kwanza, unajua watu wengi hawajui kuwa alivyo mkuu wa nchi ndivyo walivyo hata na mawaziri wake....kwa hiyo mnapowaona mawaziri wanaboronga, wanatembea na na AK 47 na mamilion ya dola na wanasema uongo ndivyo alivyo hata na rais..wanavyofanya kazi ndiyo reflection ya Yule aliyewaweka...ndio maana hakuna heshima tena


Edson: ni kweli mzee ila sasa nashindwa kuelewa ni kwa nini hana maamuzi magumu na mwepesi wa kupotoshwa.. nakumbuka kuna siku alisema kwa kimombo hivi ‘’ i have a smiling face but firm on issue!’’ sasa hili sijaliona hata kidogo.


Baba: hahaha..mi sikumbuki kama alisema hivyo ila ninachokumbuka ni kwamba aliwahi kukataa sura yake kwenye picha iliyopigwa ili iwe inawekwa maofisini na sehemu mbali mbali kwa kisingizio kuwa picha ile hajatoka vizuri na kuwa sura imejaa uchovu wa kampeni ..hata alipopiga nyingine ilikuwa na tofauti moja tu kuwa ile ya pili alikuwa amevaa miwani..


Edson: yaani nchi hii ilipofikia sasa hivi basi tu..


Baba: ngoja nikwambie mtoto, zamani nchi hii ilikuwa nzuri viongozi walikuwa waaminifu na wachapa kazi tofauti na sasa viongozi wamekukuwa wavivu wa akili hadi fikra, zamani nchi ilikuwa na haki na haki ilikaa ndani yake lakini sasa nchi imekuwa na viongozi wauwaji. Thamani ya pesa imekuwa taka taka, viongozi wamekuw waasi na rafiki wa wezi, kila mmoja wao amekuwa mpenda rushwa na posho..kwa hali hiyo usifikiri mtu wa chini na wa kawaida atasikilizwana kutimiziwa anayoyataka..hali ilipofikia ni pabaya sana..sasa hivi wafanya kazi ndio wanaendesha nchi hii kuwa kukatwa pesa kwenye PAYE.


Edson: sasa we unadhani ni cha kufanyika ili tuondokane na hali hii?



Baba: piganieni katiba mpya yenye kuleta usawa na tija kwa kila mtu.mi nakwambia wanao watalichapa kaburi lako na kulivuruga kwa mguu yao maana wataona kwa miaka yote uliyokuwa hapa duniani hujafanya kitu..ndio maana nakwambia hakikisheni nchi inapata katiba mpya yenye kuwafaa watoto wenu na wajukuu zenu, lakini mkicheza juu ya hili huko mbele mtalia sana.kataeni kila aina ya uovu mnaoona mnafanyiwa na serikali hii ...


Edson: hilo mzee nakuunga mkono katiba mpya ndio suluhisho la matatizo yote, ngoja tusubiri maana nimeona tume iliyoundwa sasa sijui hao wanakamati kama watajali maslahi ya wengi


Baba: hiyo tume wengi wao nawafahamu tena kwa ukaribu ila naona kama kuna kasoro flani..kuna mtu mmoja wamemwacha nje ya hiyo tume. Profesa Isa Shivji alifaa kuwa ndani ya iyo tume halafu warioba hakufaa kuwa mwenyeki wa tume..lakini ngoja tusubiri tuone walio nje ya hiyo tume inabidi wafanye kazi ya ziada ili mambo muhimu yenye tija kwa taifa yawe ndani ya katiba.


Edson: ila kwa kweli tuna safari ndefu ili kufikia ustawi wa taifa maana sasa hivi ni kama kuna wazawa na wahamiaji ndani ya nchi hii..


Baba: ukiwa mjini we waone watu wanavyohangaika, huyu anapita huku , huyu kule , mwingine anakimbia huku na kule..wao ukiwauliza wanakwambia wako kwenye mishe mishe kumbe mfumo wa nchi ni mbovu yaani mfumo ulivyo mbovu umewafanya watu waupokee uwe sehemu ya maisha yao, foleni barabarani, huduma mbovu za kijamii na mengine kibao..kwa hiyo inatakiw mabadiliko ya fikra miongoni mwa wananchi yanatakiwa ili udhalimu kama huu wanaofanyiwa uishe.


Edson: inabidi tufanye kila linalowezakana tuondokane na huu mzimu ccm maana vinginevyo ni maumivu.


Baba: hebu nimiminie maji kidogo...


Edson:sawa mze..


Baba: ccm ilikuwa nzuri zamani lakini kwa sasa hapana, hakifai kabisa..we ona wanavyogeukana halafu wengine wanasema eti ni wapiganaji wa ufisadi na wapinga uonevu..nakwambia edy ndani ya ccm hakuna mpiganaji huwezi kuwa mpigananji halafu ukawa ndani ya ccm .hata hao kina mwakyembe ni unafiki tu..na ni mnafiki sana..hivi hebu niambie mwakyembe amepinga ufisadi upi? Kusoma riport ya Richmond halafu akaficha baadhi ya mambo huko ndiko kupigana na ufisadi? Na mdomo wake ndio unamponza..aliingia ccm akaukuta mfumo huo wa uonevu na hata kuuwana. Na ndio maana sasa hivi fomula ya costra nostra inatumika kummaliza halafu akiguswa anarudi kwa wananchi na kuanza kulia..


Edson: tena kama sasa hivi kuna wengi wameshaanza mbio za urais chini kwa chini hadi mwakani watakuwa wamejitokeza ila sijui nani anakifaa chama hicho.


Baba: ccm hakuna kiongozi wa kulitoa taifa hapa lilipo,nimemsikia sitta anasema eti anaomba walau temu moja tu huyu nae hafai maana namfahamu nimesoma nae huyu.mbinafsi na ana majigambo sana..lowasa yeye alikuwa mchapa kazi kipindi cha uwaziri mkuu na lakini nae tatizo lake ni wizi na kiburi. Na lowasa namfananisha na utawala wa kisovieti miaka ile..wasovieti walikuwa na fomula tatu, ambazo ni materialism, myth of co-existance nay a tatu ilikuwa ni destroy with a kiss..lowasa always ana operate ndani ya hizi formula na ndio maana wengi wanaona anafaa lakini kwa formula hizo tatu hafai hata kidogo...ana tabia ya kuuma na kupuliza


Edson:yule hafai ila sasa tatizo wengi amewashika yaani sasa hivi ana wapambe hadi kwenye vilabu vya lubis na sasa hivi amejikita makanisani.


Baba:yule hafai kabisa..halafu wakati umeenda kanisani hukuzima computer yako niliikuta iko on na umefungua jamiiforums unasoma habari za..hivi yule ni mtoto wa mzee malecela?


Edson: willy ni mtoto wa malecela anataka kugombea ubunge wa afrika mashariki ndio hapo kama ulisoma alikuwa anaeleza nia yake ya kugombea.


Baba:nimeona ila naona wengi wanamchalenge sana halafu nimeona hana majibu mazuri na hajui kujieleza halafu kingine anaruka hoja ..nimesoma hadi page ya 8 nimeona ameshambuliwa kweli kuna vijana wamempa changamoto ila tatizo hajui kujibu na hata lugha ya kingereha haifahamu vizuri.


Edson: mwenyewe anadai kuwa amekaa marekani zaidi a miaka 20, labda cha kuongea anajua vizuri..


Baba: hakuna kitu kama hicho.


Edson: waache wapeane maana ni full nepotism ndani ya ccm.


Baba: hatima ya taifa hili iko mikononi mwenu ninyi vijana..kaeni mkijua hilo... sasa iasee ngoja mi nende kwa mzee Otto mara moja wewe utakuwepo hapa nyumbani?


Edson:mi nipo ila badae kidogo ntashuka kule chini kuangalia kama hawa jamaa wameleta madirisha maana nakataka kabla sijaondoka yawe yamewekwa.......
 
Mshua wako mwambie aelimishe mabolozi wa nyumba 10 wa ccm wanao tumiwa kama kondom na kutupwa!wanaboa ccm
 
Baba: hatima ya taifa hili iko mikononi mwenu ninyi vijana..kaeni mkijua hilo... sasa iasee ngoja mi nende kwa mzee Otto mara moja wewe utakuwepo hapa nyumbani?

i kawaida ya wazee waliodhurumiwa kugeuka wenzao!

Ila nimemkubali maana anapendekeza ZITTO agombee uprezdaaaa na inaonekana anajua mjadala wa umri huyo mzee
 
Wazee wetu wangekuwa kama huyo baba ukombozi ungepatikana haraka.
Mjomba wangu aliniudhi sana jana.
Mzee wangu japo alikuwa Mwenyekiti wa magamba wa wilaya lakini alituhimiza kupiga kura upinzani wakati ule mzee wa kiraracha
 
i kawaida ya wazee waliodhurumiwa kugeuka wenzao!

Ila nimemkubali maana anapendekeza ZITTO agombee uprezdaaaa na inaonekana anajua mjadala wa umri huyo mzee

Kubali tu kuwa mzee wa Edson ni noma na akipewa mike ni hatari kwa mafisadi kabisa CCM maana anawajua na anapiga pale pale kama Lusinde.
 
Edson asante sana kwa maelezo yako na mzee wako, Yanaelemisha kwa wale ambao bado wana roho ngumu na bado wankishabikia ccm. Ni kweli kabisa uwezi kupigana na mafisadi ukiwa nao pamoja watakumaliza. Hivyo akina Sitta, Mwakyembe na wengineo wengi wanawadanganya Watanganyika. Kwani utapingana vipi na mtu anaekulisha/kukuvalisha n.k ni uongo mkubwa. Mpinzani wa kweli watatoka ndani ya ccm lakini sio kwa kukaa ndani ya ccm ni UONGO. Watanganyika tuamke kama anavyosema baba yetu (baba Edson) ili tuikomboe nchi yetu Tanganyika. Mungu mlinde baba Edson ili apate afya njema ya kuweza kuwaelimisha wazee wenzie ili nao waweze kuwaelemisha vijana wao.
 
Mzee wako anasema manunguniko kila mahali kipindi hiki, hivi awamu ipi haikuwa na manunguniko?
 
Kama kweli ni baba huyo au wewe huyo ndo mtoto ndo baba, hakuna jipya wote WANAFIKI WAKUBWA hayo matatizo yeye ndo ameyaona leo baada ya kustaafu/kutemwa na system? Mwambie afe taratibu bila kelele.
 
edson muulizie mzee wetu kama alipewa lile deni lake la EAC?au yeye kaamua kulisamehe?
 
Asante kwa kutuwekea maoni ya Baba Edison hapa jamvini(ingawa naona kama umeandika maoni yako mwenyewe, sio mbaya ni namna nzuri ya kufikisha ujumbe kitofauti, safi umejipanga-ubunifu mzuri)

Kwa maoni yangu, swala si raisi kijana hilo nalikataa, swala ni raisi makini hilo ndio la muhimu.
Ndugu zangu labda tumesahau mwanzoni JK alipogombea na Mwalimu akamtosa wengi walilalamika kisa ni kijana ndio maana amekataliwa. Wazee bado wana umuhimu sana katika kutupa muongozo wa kuongoza nchi, wanaweza wasiwe maraisi lakini busara zao ni muhimu.

Kwa mfano ktk serikali tuliyonayo, wazee makini karibu wote wametengwa, wamebakia wazee wanafiki ambao hawathubutu kumueleza JK ukweli maana nao wanajipendekeza.

Kwa Zitto kuwa raisi mie napinga. Hajakomaa kiasi hicho, tena sasahivi nae kaisha changanyika tenga moja na samaki waliooza kwenye hiyo kamati yake anayoongoza, ingawa yeye bado hajaoza ila ameanza kuchina(vunda) wamekua kama askari, badala ya wachunguzi wa kumsaidia hakimu (bunge).

Kwa uwaziri sina tatizo nae ila urais hapana. Tena Mnyika na Mdee wako vizuri zaidi namuomba Mungu waendelee hivyo nao wasichanganyike na waliooza pindi umaarufu utakapo wazidia.

Vijana tuwepo kwenye uongozi, ila baadhi ya position kama urais na uwaziri Mkuu bado hatuna kijana kwasasa.

Hata hivyo busara za Mzee wetu Slaa na Mbowe na wengineo walioko nyuma ya pazia zinawafanya hao vijana wa Chadema wawe na maadili maana kuna wakubwa pale juu ambao watawakemea wakileta mambo yao ya dot.com.

Serikali ya JK haina wazee wa kukemea makosa na hata wachache waliotengwa, wanamuacha tu ili aumbuke ndio maana maadili hakuna maana hakuna mkubwa pale juu atakae wakemea.

Nyie waachieni hao vijana kama pale ikulu hapajagezwa ukumbi wa disco na basketball.

Ukishangaa ya Musa subiria ya Filauni!
 
Back
Top Bottom