Baba Yangu Amebaka Housegirl-Mama Anataka Kuondoka!

babako ni mtu mzima,hayo naona kama ni mambo ya kumezea,kwanza hukutakiwa kulileta hapa,jifanye hayajatokea,kaa kimya endelea kumpa heshima dingi wako,watanzania mnapenda sana kushabikia mambo yasiyo na manufaa kama haya

O.M.G is this for real????Someone else's child was raped!!!!!!!!!!When will we as a society learn that "not everything can and/or is to be swept under the carpet"???Huku ni kujitafutia laana za bure..........................urgh!!!!!!!!
 
Pole sana kwa mkasa huo ulioikumba familia yako.....hapo inabidi mkae na mama yenu asichukue maamuzi yanayoweza kuisambaratisha familia yenu!
 
Huyo baba ukweli anaona aibu ndomaana anazua safari zisizoisha na nadhani anajuta kitendo alichokifanya,sasa chamuhimu kaeni na huyo binti mkiwa wapole na kumsikiliza kwanza anawaza nini na anataka nini alafu mshauriane naye chakufanya ila najua hawezi kurudi kufanya kazi hapo kwenu kwahiyo mpeni mtaji au mfungulie kibihashara aanze mambo yake na msimsahau kumpa company ili mkam save babayenu maana akijakukutana na tgnp tape basi mzee atakuwa ameumia na hatanyie itawasumbua sana na haibu juu
 
Wadau wa JF.
Hiki ni kisa cha ukweli kilichotokea wiki iliyopita. Ninakiandika kwa huzuni sana na aibu kubwa. Nilikuwa safarini na niliporudi nimekuta kesi hii inafukuta ikiwa imetokea kama siku 2 kabla ya mimi kuwasili.
Baba yangu ana umri wa miaka 70 plus. Mama yangu yupo Mid 60s. Ilitokea kwamba wana housegirl wa umri wa miaka 18 hivi toka maeneo ambayo hutoa wasichana wengi wa jinsi hii.
Bila kupamba jambo hili, baba yangu amembaka huyu msichana wakati mama hayupo. Msichana alitaka kwenda kushitaki polisi ila aliombwa sana na ndugu zangu asifanye hivyo.
Jambo hili limeleta vurugu kubwa sana nyumbani. Hakuna anayetaka kungea na mzee na mama amesema anafunga mizigo yake arudi kwao (at that age?). Watoto tumebaki tunashangaa hatujui la kufanya maana wale ni wazazi wetu na tunaona aibu hata ku-share na spouses wetu (tunaogopa kumbe nyiye ndivyo mlivyo). Pia watu wa dini unaanzaje kuwaelezea? Tunajiuliza kama huyo binti amepata ujauzito je? Kama akiamua kushitaki polisi je?
Yani sijawahi kupata fedheha kama hii. Hata sisi kwa sisi hatutaki kulizungumzia jambo hili.
Tumsaidieje mama?
Tuokoeje ndoa yao? Mzee hataki kukaa nyumbani safari za hapa na pale haziishi!
Tumsaidieje yule binti wa watu na trauma hiyo?
Naombeni msaada, bila matusi tafadhali. Mbakaji akiwa mbali rahisi kusema - afungwe, ila baba yako unasemaje?

Kajipange upya haiingii akilini mzee wa miaka 70 ambake mtoto wa miaka 18! ni uongo wa mchana kabisa njoo kivingine.
 
pole kwa matatizo ya mzee wenu.kitendo alichokifanya ni cha kinyama.kwa upande wangu mimi,simsamehe mbakaji hata awe na umri wa miaka 90,ningemshitaki ili iwe fundisho kwa wengine.na ningemuaibisha tu,jee hicho kitendo kama house girl angekuwa na umri mkubwa angembaka mtoto wa bosi,asingeshtakiwa?angeshtakiwa tu.kwa kuwa ni house girl.nao ni binaadamu ni vizuri haki itendeke
 
Chupaku, pole sana. Binafsi naona mumefanya haraka kumwondoa msichana huyo kisa mnataka kuokoa aibu ktk familia. Je huko aliko akawaambia wazazi na ndugu zake wakaamua kumchukulia baba yenu hatua?

La pili lilinisikitisha ni kitendo ya kumchukulia kama HG huku mkisahau kuwa naye ni binadamu na ana wazazi kama mlivyo nyie. Pia kumbuka ni binti wa watu. Fikiria angekuwa binti yako kabakwa na bosi wake ungefanya nini? Je mna uwezo wa kumwandolea trauma aliyonayo? Mnafikiri mnaweza mkamlipa kiasi gani cha fedha kuondoa unyama aliofanya mzazi wako?

Lingine ninaloliona hapa mumeshindwa kumkalisha baba yenu chini na ndio maana anakwepa machafu aliofanya na amewaachia uchafu huo mumwondoleeni. Ukweli unabaki pale amembaka binti wa watu. Mama ameumia sana. Je mumejaribu kuwakalisha wote watatu wahanga wa hili tukio mkajua mawazo yao wakilitazama kwa macho mengine yasiyojaa hasira? I mean an intervention.

Ungetuambia baba yako anasema nini hapo tungejua kama anastahili msamha au la. Je alimwomba binti wa watu msamaha? Je amemwomba mkewe msamaha? Tusijetukamsemea kuwa anajutia kosa lake kisa anatembe ana kuhangaika hakumwishi. Ninaona mahangaiko yake ni ktk kufikiria namna ambavyo anaweza kukwepa ukweli na siyo kujuta.

At the end of the day asipokaa chini mbele yenu na akaubeba msalaba wake akitumia kofia ya kwamba yeye ni binadamu na siyo mzazi wenu ndipo muafaka utapatikana. Msianze kumbembeleza mama huku mwenye kosa hajasema chochote. Mnamuongezea mama uzito.

Your family needs an intervention na ktk hilo msihi binti aje na mtu ambaye ameshamsimulia haya mambo ambaye ni ndugu yake.

I have seen my uncle akifanya decision ngumu kuhusiana na rape case kama hii na alienda jela kipindi kile abado sheria ya miaka 30 haijatolewa and I tell you his family has healed. The truth set him free.
 
Pole binti ulofikwa na mkasa huu...pole nawe kwa kuguswa sana na jambo hili pasi kujalialitefanya ni baba yenu mzazi...pole mama kwa fedheha mzee aliyokuletea uzeeni..Mpendeni huyo binti,mchunguzeni km hakupata maambukizi na hakikisheni anapata msaada wa kisaikolojia,na baba nae msimwache maana si bure naye akili aliyotumia yumkini si yake!
 
Pole sana ila waswahili wanasema heri fedheha kuliko lawama. Nawashauri hili jambo mliongelee wote kama familia bila kuoneana aibu. Wazee wanaoheshimika nikiwa na maana wenye influence kwa mzee wako wawepo mlijadili kama familia mfikie muafaka. Mkilifukia kwamba kila mtu anaona aibu au wengine wanahasira kutolizungumzia litaleta matatizo baadaye. Njia ya tatizo ni kulitatua na si kulikimbia.
 
Ndg poleni kwa yote yaliyo tokea ss tukiwa kama wana JF nafikiri umepata mawazo yetu mengi tu na kwa kuwa umeamua kupata ushauri wa kila mtu ningeomba ukaenda KITUO CHA POLISI PIA KUPATA USHAURI ZAIDI maana sio kweli kwamba wana JF pekee wanaweza kukusaidia.asante
 
Kuna kitu kinaitwa Post Expossure Prophylaxis (PEP) Hii ni muhim kwa mbakwaji na ifanywe ndan ya masaa 72 baada ya 2kio, hii huondoa/hupunguza HIV infection chanc huduma hii inaambatana kinga za magonjwa ya zinaa/maambukizi ktk via vya uzazi pia huduma ya kuzuia mimba isiyo tarajiwa inaunganishwa kwny PEP. In short hosptl ni muhim hata kama kunagharim baba yenu kukakamatwa!
 
babako ni mtu mzima,hayo naona kama ni mambo ya kumezea,kwanza hukutakiwa kulileta hapa,jifanye hayajatokea,kaa kimya endelea kumpa heshima dingi wako,watanzania mnapenda sana kushabikia mambo yasiyo na manufaa kama haya
maybe kwako wewe hayana manufaa.lakini likija kukutokezea ndio utajua uchungu wake
 
Wadau wa JF.
Hiki ni kisa cha ukweli kilichotokea wiki iliyopita. Ninakiandika kwa huzuni sana na aibu kubwa. Nilikuwa safarini na niliporudi nimekuta kesi hii inafukuta ikiwa imetokea kama siku 2 kabla ya mimi kuwasili.
Baba yangu ana umri wa miaka 70 plus. Mama yangu yupo Mid 60s. Ilitokea kwamba wana housegirl wa umri wa miaka 18 hivi toka maeneo ambayo hutoa wasichana wengi wa jinsi hii.
Bila kupamba jambo hili, baba yangu amembaka huyu msichana wakati mama hayupo. Msichana alitaka kwenda kushitaki polisi ila aliombwa sana na ndugu zangu asifanye hivyo.
Jambo hili limeleta vurugu kubwa sana nyumbani. Hakuna anayetaka kungea na mzee na mama amesema anafunga mizigo yake arudi kwao (at that age?). Watoto tumebaki tunashangaa hatujui la kufanya maana wale ni wazazi wetu na tunaona aibu hata ku-share na spouses wetu (tunaogopa kumbe nyiye ndivyo mlivyo). Pia watu wa dini unaanzaje kuwaelezea? Tunajiuliza kama huyo binti amepata ujauzito je? Kama akiamua kushitaki polisi je?
Yani sijawahi kupata fedheha kama hii. Hata sisi kwa sisi hatutaki kulizungumzia jambo hili.
Tumsaidieje mama?
Tuokoeje ndoa yao? Mzee hataki kukaa nyumbani safari za hapa na pale haziishi!
Tumsaidieje yule binti wa watu na trauma hiyo?
Naombeni msaada, bila matusi tafadhali. Mbakaji akiwa mbali rahisi kusema - afungwe, ila baba yako unasemaje?

Sasa huoni kana kwamba unamvua nguo babako kwenye jamvi hili? si unajua kuwa nick names za humu finale zinakutanisha wanajf physically na utaaibika kwa wanaokufahamu?

Pili sidhani kama mzee of 70ties ana nguvu za kubaka mtoto wa 18th hasa ukizingatia libido factors mzee kwenye purukushani hawezi ku maintain erection hapo kwa vyovyote kulikuwa na makubaliano kwanza labda wameitilafiana later.

Mwisho kama anakaa na mama yenu at that age ameingiwaje na tamaa hizo? kuna tatizo la kimahusiano hapo ebu tafuta watu wazima wakae kujadili ( I meana watu wazima wenye authority kwao kiukoo yaani ndugu wa karibu)
 
ingekuwa mimi ningeongeza ma HG wawe kama wa tatu hivi au wa 4. dinngi awe anajiponea bana!! ala
 
Wadau wa JF.
Hiki ni kisa cha ukweli kilichotokea wiki iliyopita. Ninakiandika kwa huzuni sana na aibu kubwa. Nilikuwa safarini na niliporudi nimekuta kesi hii inafukuta ikiwa imetokea kama siku 2 kabla ya mimi kuwasili.
Baba yangu ana umri wa miaka 70 plus. Mama yangu yupo Mid 60s. Ilitokea kwamba wana housegirl wa umri wa miaka 18 hivi toka maeneo ambayo hutoa wasichana wengi wa jinsi hii.
Bila kupamba jambo hili, baba yangu amembaka huyu msichana wakati mama hayupo. Msichana alitaka kwenda kushitaki polisi ila aliombwa sana na ndugu zangu asifanye hivyo.
Jambo hili limeleta vurugu kubwa sana nyumbani. Hakuna anayetaka kungea na mzee na mama amesema anafunga mizigo yake arudi kwao (at that age?). Watoto tumebaki tunashangaa hatujui la kufanya maana wale ni wazazi wetu na tunaona aibu hata ku-share na spouses wetu (tunaogopa kumbe nyiye ndivyo mlivyo). Pia watu wa dini unaanzaje kuwaelezea? Tunajiuliza kama huyo binti amepata ujauzito je? Kama akiamua kushitaki polisi je?
Yani sijawahi kupata fedheha kama hii. Hata sisi kwa sisi hatutaki kulizungumzia jambo hili.
Tumsaidieje mama?
Tuokoeje ndoa yao? Mzee hataki kukaa nyumbani safari za hapa na pale haziishi!
Tumsaidieje yule binti wa watu na trauma hiyo?
Naombeni msaada, bila matusi tafadhali. Mbakaji akiwa mbali rahisi kusema - afungwe, ila baba yako unasemaje?

Hakuna tusi wala nini DINGI yako ni muuaji na hafai kabisa kuwa baba hata siku moja, na ukimwachia wajukuu wake atawala huyo, mwacheni mama yetu aondokane na huyo mzee, mzee gani anabaka mjukuu wake? na huenda ana ngoma, mwacheni mtoto wa watu aende POLISI huyo FATAKI afungwe....kabaka nyumbani je nje si anafakamia lolote tu huyo? Umetaja MIMBA ukasahau UKIMWI na magonjwa mengine?Kampe pole Mama yako maana hata mimi imeniuma sana zee jinga sana hilo...
 
Duh! Hawa madingi wetu nao jamani.....khaa!
Mwacheni mama yenu arudi nyumbani ila msiruhusu aondoke na mizigo yake.
Inaweza ikasaidia kupunguza hasira kabla hamjazungumza hilo jambo.
Tafuteni mtu mzima mwenye busara kama zangu, mwelezeeni ishu nzima ili asaidie kutatua tatizo.
Huyo binti fanyeni mpango arudi na mtafutieni pa kukaa, atakapobaki kwao anaweza akashawishika kwenda kushtaki na pia anaweza kuzidi kuumia hasa kama hamtompa msaada wowote.
Halafu kama vipi mwacheni dingi akaonje jela kidogo maana nahofu ni mabinti wangapi wa nje ameshawaharibu.
 
naona wachangiaji wa hi thread wanachangia kwa hisia na kujiweka kwenye position ya mtoa mada.
Ni vigumu kuwa judge on your own couse or your relative. Its hard to decide a case when ur beloved one is a criminal. This is one side of the coin.
On the other side of the coin u may wish the criminal to be severed punished for the damage he/she couse to ur relative or other person.
But my advice on this case is that let the justice be served. That person is a criminal and you r deniying justice to that house girl. I know its pain to see ur daddy jailed bt think abt other raping case that have been already concluded? Is it fair to jailed them and leave this one? The answer is a big nooo!
We need justice to be served even if its hard to accept the reality. Am very sorry for what happened n may god be with u in this hard tough and challenged time to u n your family
 
Huyo binti fanyeni mpango arudi na mtafutieni pa kukaa, atakapobaki kwao anaweza akashawishika kwenda kushtaki

Halafu kama vipi mwacheni dingi akaonje jela kidogo maana nahofu ni mabinti wangapi wa nje ameshawaharibu.

husninyo hapo dingi ataendaje jela wakati housegirl amezuiliwa kushtaki.??
 
mtoa mada jiweke kwenye nafasi ya kaka wa huyo binti halafu ungetueleza ungemchukulia hatua gani huyo mbakaji,haijalishi kuwa ni babako huyo ni mbakaji kama wabakaji wengine,wasichana wa kazi wanateseka sana kwenye nyumba za watu jamani looo aibu!
 
Hayo mambo ni mazito Ndg zanguni! Ila ningependa yule H G apate vipimo vya kama ameadhiridha kwa namna yeyote ugonjwa na bila kusahau km amepata ujauzito na kama vipi akiwa okey atafutiwe fungu la CASH TZ SHILLING akapige nayo kimya kwao. Bila kuwasahau wazee wa ukoo ktk kila ha2a.

kweli tanzania rushwa haitaisha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom