Baba yake Dk Ulimboka atoa ya moyoni

ukiona hivyo ujue MWANAE DK ULIMBOKA KAMNYIMA MGAO WA SERIKALI...YEYE AHUSIKI AMUULIZE MWANAE KWA NINI KAKAA KIMYA AMA WALIMALIZA YALE MENO NA KAMA DAMU IKIISHA WANAONGEZA KWA NINI MENO KAMA YAMEISHA WASITUAMBIE TUMTOLEE AONGEEEE CHEZA NA CHAPAAAAAAAA WEWE@RAHIM.NAPITA
 
"Nilimkanya kabisa kuhusu mambo ya migomo hasa baada ya kuniambia kuwa amechaguliwa kuwa msemaji mkuu wa madaktari wenzake na kwa bahati mbaya ndiyo yakatokea hayo yaliyotokea,"

Chanzo: www.mwananchi.co.tz
Hayo ni maneno ya baba wa Ulimboka. Hivyo, ukimya wake inaonesha kuwa amekanywa tena asilizungumzie suala hili. Inawezekana kwa vitisho walivyopata toka serikalini au wamepokea ahadi nzuri toka serikalini. Lakini pia inawezekana mapenzi tu ya baba kwa mtoto hivyo asingependa kuona mwanawe anadhurika tena. Kwahiyo hapo imebakia sisi watanzania kila mtu kusema lake juu ya ukimya huu. Wengine watasema mbona hamjafanya kitu kwa wale waliotajwa? Je, na ya Mwangosi tumefanya nini? Je, mafisadi tumewafanya nini? Mishahara ya wabunge ukilinganisha na sekta nyingine tumefanya nini? Ndipo baba wa Uli inawezekana akamwambia mwanawe hatapata faida yeyote kwa hili zaidi ya kumgharimu yeye na familia yake.
 
... Alisema alimkanya mtoto wake huyo aachane na masuala ya migomo na siku chache baada ya onyo lake ndipo akatekwa na kujeruhiwa vibaya.

"Nilimkanya kabisa kuhusu mambo ya migomo hasa baada ya kuniambia kuwa amechaguliwa kuwa msemaji mkuu wa madaktari wenzake na kwa bahati mbaya ndiyo yakatokea hayo yaliyotoke
The mzee is not media savvy, badala ya kulaani kipigo alichopata mtoto wake yeye anasema alimkanya hakusikia! Basi mwanae ni mkaidi aliye deserve kipigo cha mbwa, maana hasikii la babae na babae ana mind openly. Kama hau support your son's struggles kaa kimya, sio ku undermine his cause kwa kwenda kumshitaki kwenye magazeti kwamba hasikii!
 
Huyu dada ulimboka kadata kweli.......
Waandishi mmeanza kuzodolewa sasa,,,,,ENDELEEN KUJADILI SUALA LA MWANGOS

wale wadada vichwa ngumu wale!! Wee! Waulize jamaa wa tiss waliokuwa wanajidai ndugu ili waingie moi.
 
Hivi ni lini ataweka mambo bayana kama alivyoahidi mara alipotua nchini au ndo kishawekwa mfukoni maana kila mtu ana bei yake

nyie ndo wambea, wavivu msiotaka kushughulisha vichwa vyenu. Kitu gani unachotaka aweke bayana ambacho hakipo? Ingia you tube utapata kila kitu. Labda kama mnataka aelezee ubora wa ndege alizopanda na hosp za sauz.
 
Ashapewa mgao wake na kaambiwa ssssshhhhhhh!!!!! Ole wako ufungue tena bakuli,tutakuweka kibla
 
Ni sawa mnahitaji habari, but be patient hivi unafikiri tatizo lililompata ni dogo? Unahisi familia yake ilijisikiaje kwa yaliyompata japo ameshapona? Hebu mpuzisheni kwanza.

Lakini waandishi walikuwa mstari wa mbele kutetetea na kuutayarisha umma kusimamama pamoja na Uli. Ilisaidia sana kujenga uzio fulani wa kiuslama toka kwa nguvu ya umma. Leo sasa wamekuwa wambeya wa kushadadia ya watu?? Huu ni usaliti!!
 
Florence Majani
BAADA ya kimya cha muda mrefu, baba mzazi wa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Stephen Ulimboka, amekubali kuzungumzia sakata la mwanaye kutekwa, kuteswa, kutibiwa na hatimaye kurejea nchini akisema kwamba kupona kwake ni neema za Mungu, huku akiishutumu Serikali kuwa imewatelekeza Watanzania.


Hii ni mara ya kwanza kwa baba huyo, Ulimboka Mwaitenda kuzungumza tangu mwanaye alipotekwa, kuteswa na baadaye kutupwa katika Msitu wa Pande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.


“Naishangaa Serikali hii ambayo wananchi wanapigwa na kuuawa bila makosa. Nakumbuka kiongozi aliyeipenda Tanzania ni mmoja na ameshatangulia mbele za haki,” alisema akimaanisha Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Mwaitenda alitoa kauli hiyo jana baada gazeti hili kumtafuta ili azungumzie habari zilizoenea nchini kwamba mwanaye, amepata kazi nje ya nchi.

Kuhusu madai hayo, Mwaitenda alikanusha akisema kuwa mtoto wake hawezi kwenda nje ya nchi bila yeye kufahamu... “Pengine ana mipango hiyo, lakini mimi sijui wala sijasikia, lakini atakwenda nje ya nchi kufanya nini? Hizi habari hizo ndiyo nazisikia kwako kwa

mara ya kwanza eti Ulimboka anataka kwenda nje ya nchi? Akafanye nini alichokosa hapa Tanzania!”

Wakati mwandishi akiingia nyumbani kwa Mwaitenda, Ubungo Kibangu, Dar es Salaam, alipishana na Dk Ulimboka akiwa kwenye gari na wenzake, wanne. Hata hivyo, hakufanikiwa kuzungumza naye.

Kuhusu tukio la kutekwa, kuteswa na kutupwa katika Msitu wa Pande, Mwaitenda alisema: “Mpaka sasa, tumeiona kazi ya Mungu, ile ni neema ya Mungu kwa sababu wewe uliona wapi mtu akapigwa namna ile halafu akapona kama si kwa neema tu.”


Alisema alimkanya mtoto wake huyo aachane na masuala ya migomo na siku chache baada ya onyo lake ndipo akatekwa na kujeruhiwa vibaya.


“Nilimkanya kabisa kuhusu mambo ya migomo hasa baada ya kuniambia kuwa amechaguliwa kuwa msemaji mkuu wa madaktari wenzake na kwa bahati mbaya ndiyo yakatokea hayo yaliyotokea,” alisema.


Alielezea kushangazwa kwake na watu waliompiga mtoto wake akisema, hajui walikuwa wanataka nini. Alisema hakuwa na uhasama na mtu yeyote kuanzia kazini kwake hata kwa marafiki zake.


“Mpaka sasa nashindwa kuelewa kwa nini waliamua kumpiga, kwa sababu kwa ninavyomjua Steven, hajawahi kuwa na ugomvi na mtu tangu anasoma shule ya msingi mpaka anamaliza chuo kikuu. Sijawahi kupata mashtaka kuwa amegombana na mtu. Nashangaa haya yanayotokea leo.”


Akitoa wasifu wa mwanaye huyo alisema tangu utoto wake, daktari huyo alikuwa mtulivu na mwenye upeo wa hali ya juu. Alisema anasikitishwa mno na yaliyompata akisema kwamba siku moja ukweli utawekwa wazi kwani siku zote kazi za Mungu na kazi za shetani haziwezi kuchangamana.


“Kama mafuta na maji, ukiyachanganya... mafuta yatakuwa juu na maji yatabaki chini. Najua siku moja Mungu ataweka wazi ukweli,” alisema.


Kuhusu afya ya Dk Ulimboka, Mwaitenda alisema ingawa yeye si daktari, lakini anamwona mtoto wake kuwa yu mwenye afya na kuongeza kuwa hata mwanaye huyo amekuwa akisema kwamba sasa ana afya njema.

Hali nyumbani kwa Mwaitenda

Baada ya kufika nyumbani kwa mzazi huyo wa Dk Ulimboka, mwandishi alikaribishwa vyema na mzazi huyo ingawa alimtahadharisha kwamba endapo angekutana na daktari huyo hapo au ndugu zake, wangemfukuza.


“Una bahati ungewakuta hapa watoto wangu tusingezungumza. Hata hawa mabinti zangu wakikukuta, hatutaendelea na mazungumzo....”


Hivyo ndivyo ilivyotokea kwani baada ya kuelezea hayo, mabinti wake wawili walitokea na mmoja akaanza kwa kusema... “Shikamoo Baba, umesharudi? Huyu nani?”


Mzee Mwaitenda, kwa bashasha aliwatambulisha mabinti hao... “ Huyu ni Florence... mwandishi wa Mwananchi...” Hata kabla hajaendelea binti huyo na mwenzake walimshika mkono na kumwamuru atoke nyumbani hapo mara moja.


“Haya dada toka, toka, mmeshindwa kuandika kuhusu mwandishi mwenzenu aliyekufa (Daudi Mwangosi), mnakuja kutufuata mpaka huku Kibangu.... mtazame miguu ilivyomchafuka kwa vumbi kwa kushadadia ya watu, toka kabla sijakupiga makofi,” alisema mmoja wa mabinti hao.

Madai Dk Ulimboka kutoweka


Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi ambaye alikuwa karibu na Dk Ulimboka wakati wa mgomo wa

madaktari nchini, alisema tangu waonane aliporejea nchini kutoka Afrika Kusini, hajawasiliana tena.

“Hatujawasiliana naye,” alisema Dk Mkopi na kusema kulingana na ukubwa wa tatizo lililompata, hakuwa na mpango wa kumsumbua, bali kumwacha apumzike hadi atakapokuwa amejisikia mwenyewe kurejea kazini.

Aliyekuwa kiongozi wa jopo la madaktari waliomhudumia, Profesa Joseph Kahamba alisema, hajawahi kuonana wala kuwasiliana na Dk Ulimboka tangu alipopelekwa Afrika Kusini, Juni mwaka huu.
Baba yake Dk Ulimboka atoa ya moyoni
 
Dr. SU anajipanga vema, he is bright!!! Alitupa 40 days kuwa zikimalizika atasema kitu!!! Hataki kukurupuka!! Jipange comrade ili umalize kabisa kila kitu!!! Chinjia baharini!!
 


"Haya dada toka, toka, mmeshindwa kuandika kuhusu mwandishi mwenzenu aliyekufa (Daudi Mwangosi), mnakuja kutufuata mpaka huku Kibangu.... mtazame miguu ilivyomchafuka kwa vumbi kwa kushadadia ya watu, toka kabla sijakupiga makofi," alisema mmoja wa mabinti hao.
 
Acheni ushabiki kwenye maisha ya watu, habari ngapi mmepewa hakuna mlichofanya, mbona unyama liofanyika Iringa ni mkubwa kuliko wa Ulimboka na wafanyaji wamefanya mchana kweupeee na picha wamepigwa hakuna hatua mliyochukua zaid ya kujaza comments kwenye mitandao, hakuna lolote la maana mtalofanya akishasema hicho mnachotaka ndo maana kawapuuza Ulimboka,Madaktari wanachapa mzigo kama,nyie mnapiga kazi zenu kama kawa, mnataka wenzenu wapambane nyie mpambane kwa njia ya mtandao, Ulimboka hongera kwa kuwapuuza !
 
Wa kulaumiwa ni nani kama sio Serikali ya Mzee JK.? Wakati wa Mwalimu Baba wa Taifa Mzee Julius Nyerere hakukuwepo mambo ya ya mtu kutekwa kisha kupigwa kwenye Misitu ya Pande. Haya mambo Serikali yetu inayaiga toka

Serikali ya Kenya. Serikali ya Kenya Ukiipinga tu unauwawa kinyama tu Viongozi wa Wapinzani ya Serikali ya Kenya wanauwawa kama Nzi tu. Tanzania yetu haina haki ya Binadamu imebaki nchi yetu jina tu lakini hakuna amani Polisi

wanauwa watu ovyo tu pasipo na sababu Viongozi wetu wa Serikali hili Tatitzo wamelifumbia macho kweli Viongozi wa Serikali yetu sina imani nao kabisa.
 
Ukweli ni haki na Haki always ni lazima. Bado tunamtaka Dr.Ulimboka atueleze ukweli
Hata kama Dr Ulimboka akisema Fulani ndie aliyenipiga Serikali ya Mzee Jk itafanya kitu gani? Serikali imesha sema awali kuwa Mkenya ndie aliyemteka Dr Ulimboka hebu angalia hii Video




sasa hapa huo ndio ushahidi wa Serikali wakulaumiwa nani kama sio Serikali?
 
Last edited by a moderator:
Hata kama Dr Ulimboka akisema Fulani ndie aliyenipiga Serikali ya Mzee Jk itafanya kitu gani? Serikali imesha sema awali kuwa Mkenya ndie aliyemteka Dr Ulimboka hebu angalia hii Video




sasa hapa huo ndio ushahidi wa Serikali wakulaumiwa nani kama sio Serikali?


Wote tunahisi serikali imehusika, tunachotaka ni Ukweli toka kwa Dr.Ulimboka. We careless or not at all about JK na serikali yake. Siku moja watakuwa hawana madaraka wala kinga, Sheria na Haki itachukua mkondo wake
 
Last edited by a moderator:
Tumuacheni DR Uli, kwani hata tulipoujua ukweli wote kupitia mwanahalisi tulifanya nini? hatua gani tulichukua? mimi naona ni bora DR Uli ajikalie kimya tu. sababu hata akisema ukweli wote watz kwa jinsi tulivyo hakuna tutakacho fanya zaidi
 
Back
Top Bottom