Baba wa Ubatizo Kafanya Kweli!!!

DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
Ndoa ngumu jamani!!

Kuna mjamaa baada ya kuwa baba wa ubatizo, akawa anatumia sana hiyo kofia kwenda nyumbani alipo mtoto kwa nia ya kumsalimia. Kumbe Jamaa alikuwa anakula yule mama wa yule mtoto. Baba wa mtoto ni rafiki sana wa baba wa ubatizo. Huo mchezo wao wameendelea, na huyo mama alikuwa anatumia njia za uzazi wa mpango. Lakini bahati mbaya au kama ndio laana za Mungu huyo mama kashika mimba, na mumewe ameshajua kwamba mkewe ni mjamzito. Sasa baadae huyu mama akagundua kwamba ile mimba sio ya mumewe ni ya baba wa ubatizo. Alipomshirikisha baba wa ubatizo kwamba hiyo mimba itakuwa ni ya kwake, Jamaa sasa anahaha itakuaje!, Jamaa naye ni mme wa mtu, mume wa huyo mama (Jamaa ni Captain wa Jeshi) ameshajua kuwa mkewe ni mjamzito!, na ni marafiki na wanaheshimiana na jamaa. Mimba inaendelea kukua, Jamaa hajui atatoka vipi.

Huyu Jamaa sijui utamshauri vipi. Mi nadhani ajinyonge mapema.
 
Ndoa ngumu jamani!!

Kuna mjamaa baada ya kuwa baba wa ubatizo, akawa anatumia sana hiyo kofia kwenda nyumbani alipo mtoto kwa nia ya kumsalimia. Kumbe Jamaa alikuwa anakula yule mama wa yule mtoto. Baba wa mtoto ni rafiki sana wa baba wa ubatizo. Huo mchezo wao wameendelea, na huyo mama alikuwa anatumia njia za uzazi wa mpango. Lakini bahati mbaya au kama ndio laana za Mungu huyo mama kashika mimba, na mumewe ameshajua kwamba mkewe ni mjamzito. Sasa baadae huyu mama akagundua kwamba ile mimba sio ya mumewe ni ya baba wa ubatizo. Alipomshirikisha baba wa ubatizo kwamba hiyo mimba itakuwa ni ya kwake, Jamaa sasa anahaha itakuaje!, Jamaa naye ni mme wa mtu, mume wa huyo mama (Jamaa ni Captain wa Jeshi) ameshajua kuwa mkewe ji mjamzito!, na ni marafiki na wanaheshimiana na jamaa. Mimba inaendelea kukua, Jamaa hajui atatoka vipi.

Huyu Jamaa sijui utamshauri vipi. Mi nadhani ajinyonge mapema.

Mkuu we ni kabila gani la pale Iringa, nahitaji kujua please!
 
kitanda hakizai haramu bwana!

weeeeeeeeeeeeeee, mitazamo yako ya kizamani hiyo peleka kuleeeee! ushindwe na urgeee. Ukifumania unamkata naniiiiiii mgoni wako, halafu mimba unaona sawa, acha hizo mkuu!
 
Hiyo poa tu. Mke ana uwezo na haki ya kuamua akipendacho kama mwanadamu mwenye haki mbele ya sheria na Mbele ya Mungu kwa wale waamini
 
mume atajuaje kama mto si wake? Au huyo baba wa ubatizo ni mchina au mzungu? Kama ni mswahili mbele kwa mbele mumele atalea mtoto huyo.
 
Mi sielewi unaongea nini!!, kwani kitanda ndio kimeshika mimba!!. salamu
Sio kitanda mkuu_kalikoroga inabidi alinywe,.....haki haitafutwi ukiwa umelala kitandani.
 
mume atajuaje kama mto si wake? Au huyo baba wa ubatizo ni mchina au mzungu? Kama wote ni waswahili mbele kwa mbele kwa mbele mume atalea mtoto huyo.
 
Mkuu we ni kabila gani la pale Iringa, nahitaji kujua please!

Sijui mi ni wa wapi. We amua. Lakini Babu yangu wa mababu alitokea huko, Babu aliyefuata mkewe anatokea Arusha, Aliyefuata mkewe anatokea manyara, aliyefuata mkewe anatokea Singida, Aliyefuata mkewe anatokea Songea, Aliyefuata mkewe n mkurya, aliyefuata mkewe ni mmasai, aliyefuata mkewe ni mpare, aliyefuata mkewe ni mkurya tena, halafu ndio mimi ambaye mke wangu ni msukuma.
 
Sasa hapa tunatakiwa tutoe ushauri kwa nani?

Kwa Wazinzi au kwa aliyeibiwa?

Kwa wazinzi nawashauri wakanywe sumu wafe.
Kwa aliyeibiwa namshauri awe mvumilivu na mwenye moyo wa subira ili awazike wezi wake.
 
Back
Top Bottom