Baba wa Taifa na sifa za kiongozi

Mtumiabusara

JF-Expert Member
Nov 18, 2009
473
40
Katika kupitia speech za Baba wa Taifa, hii niliipenda, nitanukuu point chache alizozungumzia kuhusu sifa kiongozi wa Taifa letu wakati akihutubia mkutano mkuu wa CCM:

  1. Watanzania wanahitaji mabadiliko. Wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM
  2. Watanzania wanahitaji kiongozi anayetambua matatizo yetu, na matatizo hayo yanamkera. Alitaja baadhi ya matatizo ni

  • Rushwa
  • Umaskini (aliwakemea kuwa CCM siyo chama cha matajiri)
  • Udini
  • Ukabila
Je tunashughulikia vipi matatizo haya?
 
Yeye mwenyewe hakuweza kuyarekebisha hayo wakati wa utawala wake, vipi kwenye hotuba zake alaumu uongozi wa chama alicho kianzisha yeye mwenyewe?

Yaani ni sawa na kukemea kivuli chake mwenyewe.
 
Hapa alikemea wakati mwinyi anataka kumwachia mkapa. Hivyo kwa mtazamo wake matatizo haya yaliongezeka wakati wa awamu ya pili
 
Yeye mwenyewe hakuweza kuyarekebisha hayo wakati wa utawala wake, vipi kwenye hotuba zake alaumu uongozi wa chama alicho kianzisha yeye mwenyewe?

Yaani ni sawa na kukemea kivuli chake mwenyewe.

Nyerere alishindwa kuyafanya hayo ila alijua watanzania wakiamka watampa tabu sana kuongoza ndio maana akawaficha taarifa. Angelikuwa ameona mbali katika muda kama huu ambapo watanzania huna cha kuwadanganya.
 
Yeye mwenyewe hakuweza kuyarekebisha hayo wakati wa utawala wake, vipi kwenye hotuba zake alaumu uongozi wa chama alicho kianzisha yeye mwenyewe?

Yaani ni sawa na kukemea kivuli chake mwenyewe.

Inaelekea wewe hukuwepo wakati wa utawala wa Nyerere, bali unasikiliza hizo propaganda zinazotolewa leo na ma-opportunists mbalimbali wakijua kuwa yeye mwenyewe hayupo. Wengi ni wale wanaotaka ku-discredit efforts zake katika kujenga Taifa hili ili kuhalalisha ajenda zao za kubomoa Taifa hili kwa kutumia zaidi udini. Hayo ya udini na ukabila sitayaongelea kwa sasa; mtafute Salim Ahmed Salim umuulize kuhusu udini na ukabila wa Nyerere. Yeye atakuwa katika nafasi nzuri sana kukujibu vizuri.

Mimi nitakukumbusha jinsi gani Nyerere alivyokuwa mkali kuhusu rushwa. Wakati wa Nyerere hakukuwa na rushwa katika kiwango tulichonacho leo; ilikuwa ni aibu sana kwa kiongozi kujihusisha na rushwa. Ingawa wizi wa mali za umma ulianza kipindi hicho kwenye mashirika ya umma, serikali ilikuwa iko macho sana na wote waliokuwa wakinaswa walikuwa wanatumikia vifungo virefu sana kwenye gereza la Kingorwira. Yule mwandishi mashuhuri Marehemu A. E. Musiba aliyekuwa mhasibu wa TAZARA naye alikumbwa na adhabu hiyo, na kuna wahasibu na mameneja wengi sana wa mashirika ya umma waliofungwa. Kipindi cha Mikingamo kilikuwa ni njia mojawapo ya ya kuongeza transaparency ya kuwanasa wala rushwa na kweli kilifanya kazi sana. Kwa hiyo siyo kweli kuwa Nyerere alishindwa, tatizo la rushwa katika jamii yoyote ni persistent, na hivyo serikali nayo inatakiwa iwe persistent kulishughulikiwa. Tofauti ya Nyerere na serikali zizilomfuatia ni kuwa zenyewe zililea rushwa na kuifanya ishamiri.
 
ccm kilianzsishwa na waswahl wa pwani wakishkiliana na waarab wa zanzidaer na oman ndio maana rangi za bendera ya ccm zinafanana nma rangi za bendemra za sikukuu ya maulid.
 
Nani alifuta adhabu ya viboko kwa wala Rushwa? Kuna Speech Nyerere anasema mtu akila Rushwa ilikuwa lazima aende jela miezi si chini ya 6, achapwe viboko 6 siku anaingia na viboko 6 siku ya kutoka
 
Katika kupitia speech za Baba wa Taifa, hii niliipenda, nitanukuu point chache alizozungumzia kuhusu sifa kiongozi wa Taifa letu wakati akihutubia mkutano mkuu wa CCM:

  1. Watanzania wanahitaji mabadiliko. Wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM
  2. Watanzania wanahitaji kiongozi anayetambua matatizo yetu, na matatizo hayo yanamkera. Alitaja baadhi ya matatizo ni

  • Rushwa
  • Umaskini (aliwakemea kuwa CCM siyo chama cha matajiri)
  • Udini
  • Ukabila
Je tunashughulikia vipi matatizo haya?

alitawala nchi hii kwa miaka zaidi ya 20 kwa katiba kandamizi leo hii bado anachukuliwa kama role model! kweli wajinga bado wengi nchi hii
 
Nani alifuta adhabu ya viboko kwa wala Rushwa? Kuna Speech Nyerere anasema mtu akila Rushwa ilikuwa lazima aende jela miezi si chini ya 6, achapwe viboko 6 siku anaingia na viboko 6 siku ya kutoka

hotuna za nyerere ni kama sinema tuu ambazo zinavutia kuzitazama lakini hazina uhalisia wowote! kipindi chake walikuwepo kina amir jamal waliiba huku wakiwa na uraia wa nchi mbili na hakufanya chochote!
 
ccm kilianzsishwa na waswahl wa pwani wakishkiliana na waarab wa zanzidaer na oman ndio maana rangi za bendera ya ccm zinafanana nma rangi za bendemra za sikukuu ya maulid.

na bado! muda wenu wa kutawaliwa umefika na mtatawaliwa sana.thank god nyerere kafa!
 
Inaelekea wewe hukuwepo wakati wa utawala wa Nyerere, bali unasikiliza hizo propaganda zinazotolewa leo na ma-opportunists mbalimbali wakijua kuwa yeye mwenyewe hayupo. Wengi ni wale wanaotaka ku-discredit efforts zake katika kujenga Taifa hili ili kuhalalisha ajenda zao za kubomoa Taifa hili kwa kutumia zaidi udini. Hayo ya udini na ukabila sitayaongelea kwa sasa; mtafute Salim Ahmed Salim umuulize kuhusu udini na ukabila wa Nyerere. Yeye atakuwa katika nafasi nzuri sana kukujibu vizuri.

Mimi nitakukumbusha jinsi gani Nyerere alivyokuwa mkali kuhusu rushwa. Wakati wa Nyerere hakukuwa na rushwa katika kiwango tulichonacho leo; ilikuwa ni aibu sana kwa kiongozi kujihusisha na rushwa. Ingawa wizi wa mali za umma ulianza kipindi hicho kwenye mashirika ya umma, serikali ilikuwa iko macho sana na wote waliokuwa wakinaswa walikuwa wanatumikia vifungo virefu sana kwenye gereza la Kingorwira. Yule mwandishi mashuhuri Marehemu A. E. Musiba aliyekuwa mhasibu wa TAZARA naye alikumbwa na adhabu hiyo, na kuna wahasibu na mameneja wengi sana wa mashirika ya umma waliofungwa. Kipindi cha Mikingamo kilikuwa ni njia mojawapo ya ya kuongeza transaparency ya kuwanasa wala rushwa na kweli kilifanya kazi sana. Kwa hiyo siyo kweli kuwa Nyerere alishindwa, tatizo la rushwa katika jamii yoyote ni persistent, na hivyo serikali nayo inatakiwa iwe persistent kulishughulikiwa. Tofauti ya Nyerere na serikali zizilomfuatia ni kuwa zenyewe zililea rushwa na kuifanya ishamiri.

pumba!
 
hotuna za nyerere ni kama sinema tuu ambazo zinavutia kuzitazama lakini hazina uhalisia wowote! kipindi chake walikuwepo kina amir jamal waliiba huku wakiwa na uraia wa nchi mbili na hakufanya chochote!

Hujajibu hoja mkuu. Kwanini wala rushwa hawachapwi viboko? Kwa mtazamo wangu watu wanaogopa viboko kuliko kufungwa au kulipa faini
 
Nakumbuka alivyopambana na EL baada ya kugundua amepangishia majumba ubalozi wa Afrika kusini, analipwa kwa $ lakini hakuwa akilipa kodi ya mapato.
 
Kwa umri wa wengi wenu humu itoshe tu kuwaambia kuwa enzi za Mwalimu hakukuwa na mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Hakukuwa na watu wa aina ya RA, Mengi, Manji, Jiitu Patel, Chenge, Mama Mkapa, Mama Kikwete,.......
Tulikuwa na akina Rashid, Sokoine, Prof MMari, Jenerali,.......
 
Inaelekea wewe hukuwepo wakati wa utawala wa Nyerere, bali unasikiliza hizo propaganda zinazotolewa leo na ma-opportunists mbalimbali wakijua kuwa yeye mwenyewe hayupo. Wengi ni wale wanaotaka ku-discredit efforts zake katika kujenga Taifa hili ili kuhalalisha ajenda zao za kubomoa Taifa hili kwa kutumia zaidi udini. Hayo ya udini na ukabila sitayaongelea kwa sasa; mtafute Salim Ahmed Salim umuulize kuhusu udini na ukabila wa Nyerere. Yeye atakuwa katika nafasi nzuri sana kukujibu vizuri.

Mimi nitakukumbusha jinsi gani Nyerere alivyokuwa mkali kuhusu rushwa. Wakati wa Nyerere hakukuwa na rushwa katika kiwango tulichonacho leo; ilikuwa ni aibu sana kwa kiongozi kujihusisha na rushwa. Ingawa wizi wa mali za umma ulianza kipindi hicho kwenye mashirika ya umma, serikali ilikuwa iko macho sana na wote waliokuwa wakinaswa walikuwa wanatumikia vifungo virefu sana kwenye gereza la Kingorwira. Yule mwandishi mashuhuri Marehemu A. E. Musiba aliyekuwa mhasibu wa TAZARA naye alikumbwa na adhabu hiyo, na kuna wahasibu na mameneja wengi sana wa mashirika ya umma waliofungwa. Kipindi cha Mikingamo kilikuwa ni njia mojawapo ya ya kuongeza transaparency ya kuwanasa wala rushwa na kweli kilifanya kazi sana. Kwa hiyo siyo kweli kuwa Nyerere alishindwa, tatizo la rushwa katika jamii yoyote ni persistent, na hivyo serikali nayo inatakiwa iwe persistent kulishughulikiwa. Tofauti ya Nyerere na serikali zizilomfuatia ni kuwa zenyewe zililea rushwa na kuifanya ishamiri.
Mkuu hapa suhala la udini na ukabila, sijalizungumzia, labda ndio unataka kunifahamisha kuwa Nyerere alikuwa mdini na mkabila, ilo ni lako.

Kuhusu uwajibikaji wa viongozi wa mashirika ya umma si kweli kuwa kulikuwa na ufanisi mzuri.

Nani akumbuki enzi za Nyerere wakurugenzi na mameneja walikuwa wakiharibu shirika moja wanaamishwa shirika lingine?

Enzi za Nyerere si ndio kulikuwa na shida ya vyakula mpaka tukaingizwa kwenye maduka ya kaya?

Kwani hatukushuhudia JKT wakisaidiana na polisi kukamata wale walioitwa wahujumu uchumi, kiasi ikapelekea nchi kuwa na shida ya vyakula na mavazi...! Wangapi walikamatwa kwa kukutwa tu na dawa ya meno pakiti moja, au kipande cha sabuni ya kodrai.

Huyo Salim Ahmed Salim, kuna wakati alikwenda Mtwara, na kwenye mkutano wake wananchi waliudhuria walikuwa wanaume watupu kwa kuwa wanawake waliwaazima wanaume zao kaniki na magunia ili waende kumsikiliza, au hili nalo lilikuwa jambo jema?

Nyerere nchi ilimshinda, ndio maana akaamua kung'atuka kwa sababu alinusurika kupinduliwa zaidi ya mara ishirini...!
 
Angalia swali liloulizwa

Katika kupitia speech za Baba wa Taifa, hii niliipenda, nitanukuu point chache alizozungumzia kuhusu sifa kiongozi wa Taifa letu wakati akihutubia mkutano mkuu wa CCM:

  1. Watanzania wanahitaji mabadiliko. Wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM
  2. Watanzania wanahitaji kiongozi anayetambua matatizo yetu, na matatizo hayo yanamkera. Alitaja baadhi ya matatizo ni

  • Rushwa
  • Umaskini (aliwakemea kuwa CCM siyo chama cha matajiri)
  • Udini
  • Ukabila

Je tunashughulikia vipi matatizo haya?

na jibu lako hapa:

Yeye mwenyewe hakuweza kuyarekebisha hayo wakati wa utawala wake, vipi kwenye hotuba zake alaumu uongozi wa chama alicho kianzisha yeye mwenyewe?

Yaani ni sawa na kukemea kivuli chake mwenyewe.
 
Yeye mwenyewe hakuweza kuyarekebisha hayo wakati wa utawala wake, vipi kwenye hotuba zake alaumu uongozi wa chama alicho kianzisha yeye mwenyewe?

Yaani ni sawa na kukemea kivuli chake mwenyewe.

....alijitahidi ukilinganisha na mkwere! Bear in mind we can NEVER get a leader who will take us to the sun,,,,,but at least he/she should help us land on the clouds!! Natamani siasa za "ujamaa wa kisasa" kama ule wa China zirudi leo kwetu!!
sasa mkwere instead of taking us atleast to the clouds, he is taking us to a bottomless pit!
 
Inaelekea wewe hukuwepo wakati wa utawala wa Nyerere, bali unasikiliza hizo propaganda zinazotolewa leo na ma-opportunists mbalimbali wakijua kuwa yeye mwenyewe hayupo. Wengi ni wale wanaotaka ku-discredit efforts zake katika kujenga Taifa hili ili kuhalalisha ajenda zao za kubomoa Taifa hili kwa kutumia zaidi udini. Hayo ya udini na ukabila sitayaongelea kwa sasa; mtafute Salim Ahmed Salim umuulize kuhusu udini na ukabila wa Nyerere. Yeye atakuwa katika nafasi nzuri sana kukujibu vizuri.

Mimi nitakukumbusha jinsi gani Nyerere alivyokuwa mkali kuhusu rushwa. Wakati wa Nyerere hakukuwa na rushwa katika kiwango tulichonacho leo; ilikuwa ni aibu sana kwa kiongozi kujihusisha na rushwa. Ingawa wizi wa mali za umma ulianza kipindi hicho kwenye mashirika ya umma, serikali ilikuwa iko macho sana na wote waliokuwa wakinaswa walikuwa wanatumikia vifungo virefu sana kwenye gereza la Kingorwira. Yule mwandishi mashuhuri Marehemu A. E. Musiba aliyekuwa mhasibu wa TAZARA naye alikumbwa na adhabu hiyo, na kuna wahasibu na mameneja wengi sana wa mashirika ya umma waliofungwa. Kipindi cha Mikingamo kilikuwa ni njia mojawapo ya ya kuongeza transaparency ya kuwanasa wala rushwa na kweli kilifanya kazi sana. Kwa hiyo siyo kweli kuwa Nyerere alishindwa, tatizo la rushwa katika jamii yoyote ni persistent, na hivyo serikali nayo inatakiwa iwe persistent kulishughulikiwa. Tofauti ya Nyerere na serikali zizilomfuatia ni kuwa zenyewe zililea rushwa na kuifanya ishamiri.

viva mkuu,,,hata mie nimeona post yake hapo kunavitu ninavitilia mashaka! tutasema mengi lakini the footprints of JK Nyerere in Tanganyika and Tanzania shall always remain in the heart of any true patriot of this country!!!
 
WanaJF,
Kupitia jamvi hili la JF kumekuwa na threads kadhaa zinazolenga kubeza mchango wa Mwalimu Nyerere katika ustawi wa nchi yetu kijamii, kisiasa na kiuchumi. Baadhi ya wachangiaji wa threads hizo wanamshambulia Mwl. Nyerere kwamba alishindwa kujenga uchumi imara kwa sababu za siasa yake ya ujamaa na kujitegemea. Wengine wamefikia hatua ya kusema kwamba aliwapendelea wakristo katika mambo muhimu na kuwabagua waislamu. Bahati mbaya sana, mifano inayotolewa kuhusu upendeleo huo ni ya kijinga na isiyo na mantiki kwa mtu mwenye akili na ufahamu wa kuchambua mambo.

Jambo moja ambalo linasahaulika katika hoja za wanaompinga Mwl. Nyerere ni je, huo uchumi unaoonekana sasa umeimarika tofauti na ilivyokuwa wakati wa Nyerere, unamnufaisha nani? Ni watanzania wangapi wanaofaidika na uchumi wa sasa? Je, uchumi wa sasa (kama kweli upo) tumeujenga kwa misaada yenye masharti yanayovuruga hata uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu wenyewe au tumeujenga kwa kujitegemea kirasilimali na kimawazo?

Kimsingi, Mwl. Nyerere alilenga kujenga uchumi ambao hata kama haukuwa mkubwa lakini ulinufaisha jamii pana ya watanzania. Alijitahidi kujenga nchi yenye uhuru kamili wa kujiamulia mambo yake kadri inavyoonekana inafaa. Hakuwa 'A YES SIR/MADAM PRESIDENT', kama ilivyokuwa kwa marais waliofuata na hususan rais wa sasa. Leo hii kila sekta nchini inaendeshwa kwa sera zilizojengwa chini ya misingi ya World Bank na IMF. Ndiyo maana ukisoma sera ya biashara, maji, elimu, n.k. ya Tanzania huwezi kuona tofauti ya sera za sekta hizo kwa nchi za Uganda, Kenya, Msumbiji, n.k. Na sababu kubwa ndiyo hiyo kwamba sera zote zinatokana na matakwa ya wakubwa hao wa dunia, jambo ambalo Mwl. Nyerere alikataa maishani mwake.

Mwl. Nyerere ataendelea na anastahili kuenziwa kama BABA WA TAIFA LA TANZANIA. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani wakati huo Bi. Maldelin Albright alipokuja nchini kwenye msiba wa Mwl. Nyerere alisema jambo moja kuhusu Mwl ambalo sitakuja nilisahau maishani mwangu. Bi. Albright alisema 'katika maisha yangu sijawahi na sitarajii kushuhudia kiongozi wa kiafrika mwenye msimamo thabiti na anayewatetea wananchi wake mbele ya mataifa makubwa, kama Mwl. Nyerere. Nitaendelea kumkumbuka Mwl. Nyerere kama mmoja wa viongozi maarufu wa karne hii'. Hivyo ndivyo alivyosema Bi. Albright uwanja wa Taifa (sasa uwanja wa uhuru) wakati wa hafla ya kuaga mwili wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Nyerere.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom