Baba Mzazi Wa Mwanamuziki Diamond Aibuka-Soma Mambo Mazito Aliyosema Hapo Chini

DIAMOND hebu mlee baba hata kama walileteana longolongo na mama check mzee wapo alivyojichokea khaaa
 
Yeah, Saa Nyingine ni Bora kwako wewe ambaye alikutoka Ukiwa mdogo, Mimi alimkimbia Mama yangu nikiwa na Miaka 4; Mama yangu alikuwa Masomoni Nje ya Nchi, akawa na mwanamke Mwingine... Sisi ikabidi tuhamie kwa ndugu wa Mama

Sikumuona tena baba yangu, hakututafuta, nilifaulu Darasa la saba yeye akafanya Party hakunialika akaalika Marafiki zake na Mama yangu Mkubwa

Baba yangu kafariki Simjui; Napewa Urithi wake Namshukuru Mungu lakini hatukujuana, Hakutaka kunijua...

Sasa hauwezi kujua ya DIAMOND yakoje, haujui DIAMOND mama yake yapi yalimkuta na Mwanaye yalimuuma sana

Kama mwanamke angeondoka nyumbani angekumbuka kuondoka na watoto. lakini father ameondoka saa tisa usiku peke yake watoto alimuachia nani? Baada ya hapo hajasema kama alikua anapeleka matunzo au vipi? Kama alitelekeza watoto na mama yao asitegemee radhi yake kumpata Diamond. Badala yake itampata yeye. Lakini naona wanafanana na baba yake. na Diamond akiwa mzee atakua hivi eti ee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom