Baba-mama-mume-mke

Mimtamu

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
368
105
Kwa mwanamke, ni nani aliye na mamlaka ya juu kwako kati ya Mume au Baba yako mzazi?

Kwa mwanaume, ni nani mwenye kipaumbele kwako kati ya Mke au Mama mzazi?

Toa sababu ambazo mmoja anamzidi mwenzake
Nb: Usihukumu kwa tabia au uthaifu wa mlengwa
 
Jiulize swali vilevile wakati upo kwa Baba yako na Mama yako nani alikuwa juu yao kimamlaka?
 
Excuse me!! Yaani mwanamke ameolewa alafu baba yake ndio awe na mamalaka kwake?
Aliyesema hivyo nadhani hayupo kwenye ndoa.
 
miezi tisa tumboni,miaka sita kumyonyesha!!!!!!na mengine,usiku nikumwa utasikia baba anauliza tu anaendeleaje huyo!!mama yeye halali!!acha bwana!!!

Lakini mkuu, wajibu wake huo ati kwani hukuomba akuzae but yeye ndiye aliyeamua so lazima hali kama hiyo iwe. zaidi ya yote kazi yake ishakwisha.

Hebu nipe na matamu ya mke tuone uwiano
 
mamlaka kwa baba juu yako yametoka wapi tena wakati alishakukabidhi kwa mume mbele ya Mungu na binadamu?

Lakini utaona pale binti anapopata tatizo baba huwa muwajibikaji na mwenye sauti kuliko mume, hapo vp?
 
miezi tisa tumboni,miaka sita kumyonyesha!!!!!!na mengine,usiku nikumwa utasikia baba anauliza tu anaendeleaje huyo!!mama yeye halali!!acha bwana!!!

Hapo kwenye miaka sita umepitiwa ama?
 
Jiulize swali vilevile wakati upo kwa Baba yako na Mama yako nani alikuwa juu yao kimamlaka?

Ukumbuke hapo ulikuwa kama mtoto katika familia-a, na katika familia-b utakuwa mama/baba hapo ndipo kwa mke anapomilikiwa na mume
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom