Baba Diamond Ashinda Njaa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
MSIKIE BABA DIAMOND AKIFUNGUKA

NA

WAANDISHI WETU, Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Wakati mwanaye staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na mwanaye Tiffah wakiteketeza kiasi cha fedha kinachokadiriwa kufikia shilingi Mil.100 barani Ulaya walikokwenda kula bata, baba mzazi wa msanii huyo, Abdul Juma anadaiwa kushinda njaa kutokana na ugumu wa maisha, twende na Risasi Jumamosi.

IMG_3230.jpg

Baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mzee Abdul Juma.

Diamond na familia yake hiyo sambamba na madansa wake, waliondoka nchini mwishoni mwa wiki iliyopita kwenda Frankfurt, Ujerumani ambapo pamoja na kufanya ziara ya kimuziki katika nchi tofauti balani Ulaya, staa huyo aliitumia ziara hiyo kuponda raha.

diamond1.jpg
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ pamoja na mtoto wao Tiffah wakila ‘bata’ Ulaya.

TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kililiambia gazeti hili mapema wiki hii kuwa, baba Diamond kwa sasa ana maisha magumu na mara nyingi amekuwa akishinda njaa huku baadhi ya majirani wakimpa msaada hali inayowasababisha kushangaa baada ya kusoma kwenye magazeti kwamba mwanaye huyo anatumbua fedha kibao na familia yake, ndugu na marafiki huku mzazi wake huyo akiteseka.

mama-d-ulaya1.jpg

Familia ya Diamond Platnumz ‘wakitumbua’ Ulaya.

“Jamani baba Diamond anateseka! Muoneeni huruma. Alikuja kwangu kuniomba elfu moja lakini bahati mbaya na mimi sikuwa nayo. Mara nyingi amekuwa akishinda njaa. Mbaya zaidi anasumbuliwa na ugonjwa wa miguu na hana mtu wa kumpeleka hospitali. Njooni mumuone yupo hapa kwake anatia huruma,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Kiukweli baba Diamond anasikitisha sana. Tunashindwa kujua tatizo liko wapi kati yake na mwanaye, maana kuna wakati huwa anamsaidia lakini wakati mwingine anampotezea.”

MAPAPARAZI WAMUIBUKIA
Baada ya kuzipata habari hizo, mapaparazi wetu walifika nyumbani kwa baba Diamond, Magomeni ya Kagera jijini Dar na kumkuta nje ya nyumba yake akiwa ameshika tamaa huku akionesha hali ya kunyong’onyea kama mtu aliyekata tamaa ya maisha.

IMG_3235-001.jpg
Mzee Abdul Juma.

HALI YAKE NI MBAYA
Akizungumza na gazeti hili baada ya salamu, baba Diamond alieleza kwamba bado hali yake ya miguu ni mbaya kwani anatembea kwa kuburuza laiti angekuwa kama zamani angeweza kufanya shughuli ndogondogo za kujipatia kipato angalau apate fedha kwa ajili ya kula hasa katika kipindi hiki ambacho hana msaada.

3-1-1.jpg

“Niko hapa bado mambo siyo mazuri, miguu inanisumbua kama unavyoona. Nasikia mwanangu (Diamond) ana ziara nje ya nchi na juzi niliona mmeandika ameteketeza milioni 100 na familia yake, namsubiri akirudi huko naamini atanisaidia angalau fedha hata ya kwenda kwenye matibabu na kula kama ataamua maana alishawahi kuniahidi, hali yangu siyo shwari nabangaiza tu hapa,” alisema baba Diamond.

diam.jpg

DIAMOND ASEMAJE?
Alipotafutwa Diamond aliyeko Ujerumani kwa sasa ili aweze kuzungumzia suala hilo alisema hana cha kuzungumza kwa sasa.
“No comment kwa sasa, subirini nikirudi tutaliongea hilo kwa kirefu,” alisema Diamond.

ALIOKWENDA NAO ULAYA
Katika gazeti lenye udugu wa damu na hili, Ijumaa Wikienda la Jumatatu iliyopita, ukurasa wake wa mbele lilikuwa na kichwa kisemacho; DIAMOND
ATEKETEZA SH. MIL 100 ULAYA.
Katika habari hiyo, Diamond aliandikwa kusafiri na ‘ujumbe’ mrefu wa idadi ya watu 14 ambao wote walikuwa chini yake kwa malazi na chakula. Watu hao ni Zari, mama yake mzazi, Tiffah (mwanaye), Romy Jons (DJ wake), Kifesi (mpigapicha), Salam (meneja), mke wa meneja wake mwingine Batu Tale, madansa wanne na dada mmoja ambaye ni ndugu wa Zari. Hao walikwea pipa na kufikia Frankfurt, Ujerumani.

BABA DIAMOND AMEFIKAJE HAPA?
Baba Diamond anadaiwa akiwa angali kijana, alitengana na mama Diamond akiwa na mtoto huyo mdogo kwa miaka mingi bila kumpa huduma zozote kitu ambacho kimemsukuma Diamond kuwa na chuki na ashindwe kumpa matunzo mzazi wake huyo baada ya kupata mafanikio.
Hata hivyo, mara kadhaa Diamond amekuwa akimsaidia fedha baba yake huyo lakini si kwa asilimia mia moja kama anavyomtunza mama yake ambaye anaonekana kula raha hususan kipindi hiki ambacho bwana mdogo huyo kutoka Tandale, maisha yamemnyookea.

Gladness Mallya, Erick Evarist na Richard Bukos. Chanzo.GBP
 
Attachments

  • Diamond 1.jpg
    Diamond 1.jpg
    48.6 KB · Views: 280
  • Diamond 3.jpg
    Diamond 3.jpg
    31.8 KB · Views: 327
  • Diamond 4.jpg
    Diamond 4.jpg
    50.4 KB · Views: 179
  • mama-d-ulaya1.jpg
    mama-d-ulaya1.jpg
    30.9 KB · Views: 418
  • baba.jpg
    baba.jpg
    57.6 KB · Views: 228
  • baba diamond.jpg
    baba diamond.jpg
    36.5 KB · Views: 244

kwani huyu mzee ana mtoto mmoja tu (diamond) ?
 
Kama kuna mzazi juha huyu jamaa anashika namba moja...mzazi mwenye kujitambua hawezi kukubali huu upuuzi wa kuhojiwa kwenye gazeti la udaku mambo binafsi yanayohusu familia yake
Huu ni upuuzi na upumbavu wa kiwango cha juu mno
Hivi kalipwa bei gani?
Hivi anajua jamaa wametengeneza bei gani kupitia hiyo habari
Huyu hajitambui na atafakari alipokosea kuliko kuja kulialia kwenye vyombo hovyo vya habari...huku ni kujidhalilisha
 
Diamond kama mtoto Wa kiume sahau jikaze unaweza ukakuta ata wewe uliacha mbegu sehemu msaidie baba yako shoo moja tu inamtosha matumizi kama utaki kumpa,ela mweke bili hotel karibu awe anakula Milo mitatu mpeleke hospital umwache Fanya kama MTU aliyechangia mbegu zako ukaja duniani kama mwanaume Fanya ivyo jua mama yako bila huyo mzee kuchangia mbegu zake usingekuwa diamond ata ulaya wachangia mbegu wanalipwa gari achakusikiliza kila kitu anachosema mwanamke ata Mungu alisema tuishi nao kwa akili
 
Nadhani wazazi na magazette ifike hatua waheshimu maisha ya mtu binafsi!
Labda sielewi jambo, wakati Diamond akilalia maji na kushindia ubuyu utotoni, huku baba mtu akitumbua hivyo vyombo vya habari vilienda kumhoji baba diamond au diamond mwenyewe!
iweje hata iwe gumzo kwa diamond tu na si wazee wengine! kuna wazee kibao wanaishi bila kufuatilia magazette na vyombo vya habari kuwachafua watoto na wanaishi.
Ushauri wangu, Vijana tusiwe wepesi kukamua ndimu mboga ikiwa chachu tunalalamika kuomba misaada na huruma.
huyu jamaa haumwi na ni utoz unamsumbua tu. Jinz aliyovaa na aina ya mnyoo vinasadifu uhalisia wa maisha yake.. anaonekana full kunywa gongo. tujiulize hela anapata wapi! namshauri akaanze maisha kijijini ya kilimo na diamond atakuja mtafuta. maana tunapotelekeza watoto huwa tunasema watatutafuta. sasa asubiri watamtafuta
 
Huyu mzee Lofa kweli!Hana tofauti na Baba yangu!Baba yangu yupo,ila hakuwahi nilipia hata thumni ktk elimu yangu zaidi ya mjomba angu upande wa mama,halafu kesho niwe mbunge wa iramba kupitia chadema,ndio aje ajifanye ananijua?hatopata hata dala langu kudadadeki!
Mkuu unaongea from experience, ila nimecheka sana, hahahaha, kiukweli mzazi asiyekusaidia hata wewe utaona hana thamani.
 
Hili fundisho tunalipata wazazi ambao watoto wetu bado wadogo.
Sio tunadinya halafu tule kona, tudinye na tuwe tayari na majukumu ya matokeo ya Kudinya.
Vinginevyo ndio haya ya mzee Diamond.
Mzee anadhalilika tu ilihali mwanzo alikimbia majukumu.
Mama Diamond alifuata mfumo wa wanawake wa Kijapan....
Mfumo wa wanawake wa kijapan ukoje?
 
Back
Top Bottom