Baadhi ya Wazanzibari wapinga Tanzania kudai eneo zaidi la mpaka wa bahari kuu

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu amesema ombi la serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Umoja wa Mataifa kuomba nyongeza ya mpaka katika Bahari ya Hindi ni kuipokonya Zanzibar haki yake. Jussa amekusudia kuwasilisha hoja ya binafsi katika Baraza la Wawakilishi Jumatatu, akitaka lazima kuwepo na mazungumzo ya kuamua nani anamiliki nini kati ya Tanzania na Zanzibar kabla ya ombi hilo kuwasilishwa katika Umoja huo.

Ombi hilo tayari limeshawasilishwa katika Umoja wa Mataifa, New York, na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi wa Tanzania, Professa Anna Tibaijuka, akitaka kilomita 150 zaidi za bahari. Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa aliyeliibua suala hilo kwenye Baraza la Wawakilishi hapo juzi, Amina Abubakar amezungumza na Ismail Jussa kuhusiana na msimamo huo kwa kusikiliza mahojiano hayo.

 
Sasa wanapinga nini wakati nyaraka zimewasilishwa UN? Halafu nijuavyo mimi, kwa mujibu wa International Law, Bahari Kuu (High Seas) ni eneo lisilomilikiwa na nchi yoyote, ndio maana Tanzania inaliomba, sasa hapa Zanzibar imepokonywaje madaraka ya eneo isilomiliki?
 
Wazanzibari ni vilaza sana tena sana, hasa huyu Jussa!!!!

Wanasahau kuwa mambo ya nje ni ya muungano!!

Tanzania ina waziri wa mammbo ya nje mmoja tu, ambaye ni wa muungano. Zanzibar haina waziri wa mambo ya nje. sasa nani angepeleka hilo ombi??
 
waache unafiki, wanapinga wakati eneo lenyewe si lao? Wapinge na kupokea 4.5% basi!
 
Who is Jussa? au ndio cheap politics kama kawa. I fail to understand what he really wants to achieve?
 
Kumbe Zanzibar siyo sehemu ya Tanzania? Anyway, out of curiosity, hilo eneo litakuwa mkoa gani? Dar au Lindi au Tanga? Maana usikute meck sadiq anataka kujiongezea eneo maana Dar imeshajaa
 
Mesej ambayo nimeletewa sasa hivi na inaelekea inasambazwa inasema hivi:

TWENDENI kwa wingi kike kwa kiume kesho Jumatatu na saa mbili asubuhi tuwe tumeshakaa nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Chukwani ili kuonyesha Ulimwengu kuwa Wazanzbari hatukubaliani na azma ya Tanganyika na Shamhuna kuiondoa nchi yetu Zanzibar kwenye ramani ya dunia. Shime tufike kwa wingi na utulivu. " Sisi sote tuna uchungu kwa ndugu zetu walopotea kwa kugombania nchi yetu…."

Source: Ally Saleh Facebook
 
tanganyika nayo mmeiua ili muifanye mnavotaka znz bt muda unazungumza .tanganyika yenu inarudi soon mungu atupe uzima
 
tatizo wamejawa na chuki na ufahamu ni zero. Usishangae kukuta Hata hizi sheria hawazijui, si ajabu wamejazwa maneno na watu wachache wanaowatumia kama madaraja kisiasa!
Acha waandamane dunia iwaacheke.

Sasa wanapinga nini wakati nyaraka zimewasilishwa UN? Halafu nijuavyo mimi, kwa mujibu wa International Law, Bahari Kuu (High Seas) ni eneo lisilomilikiwa na nchi yoyote, ndio maana Tanzania inaliomba, sasa hapa Zanzibar imepokonywaje madaraka ya eneo isilomiliki?
 
hivi sheria za kimataifa za bahari wanazijua? Au wanadanganywa na wanasiasa,na wao bila kuchanganya na za kwao wanakurupuka.
Acha waende dunia iwacheke.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom