Baadhi ya Wazanzibari Wapinga Muungano wadai kura ya maoni kuhusu Muungano

Tumekwisha kanyaga mavi!

Tulichotakiwa kujadili mwanzo ni kuwepo au kutokuwepo kwa muungano. Kama muungano unapendwa na wananchi basi ndiyo muundo wa muungano ujaliliwe na hatimaye katiba mpya.

Kitakachotokea kwa sasa ni Wazanzibari kuikataa katiba mpya wakiwa na maana ya kupinga kuendelea kuwa katika muungano. Endapo serikali itatumia nguvu kuulinda muungano kutazuka wanaharakati wengi ambao wataipotezea serikali muda mwingi wa kuwahudumia wananchi na badala yake kujibu hoja.

Ni vema serikali ikajiandaa mapema ili endapo Wanzanzibari watakataa katiba mpya, jambo ambalo ni dhahiri, mchakato wa kuvunja muungano uanze mara moja vinginevyo tutakuwa tunakaribisha Al Shabaab na Boko Harama na hivyo kuhatarisha amani na umoja wetu wa Watanganyika.
 
WAacheni WAzanzibari wajitenge, ni mzigo kwetu


Mi najishangaa sana na pia nawashangaa Watanganyika wote ambao tumo JF. Mbona hatuwaungi mkono Wazanzibari kuandamana kwenda Dodoma kuwashinikiza wabunge wetu kujadili kwanza uwepo wa kura ya maoni juu ya muungano kabla ya kuanza kujadili katiba mpya? Tunajadili vipi Katiba ya Muungano bila Tanganyika? Tunajadili katiba ya Muungano wa Zanzibar na nchi gani? Yaani sisi tunashabikia tu kuona Wanzanzibar wanaandamana kwenda baraza la wawakilishi na hatufanyi lolote kuwaunga mkono. Ina maana sisi tumeridhika na jinsi muungano unaendeshwa? Shame on us....Wanzibar kazeni buti mpate nchi yenu....kweli ukubwa wa PUA SIYO WINGI WA KAMASI....pamoja na idadi yetu kuw kubwa...approximately 44 millions, bado hatuna effect yoyote kwenye kuifanya serikali ifanye tunavyotaka...wazanzibar hata hawafiki 2 ml, but at least they do something....SIJUI TUMELOGWA???

TOGETHER WE CAN BRING THE CHANGES WE NEED....YES WE CAN....GOD BLESS TANZANIAN WHO WANTS CHANGES....
 
Watu wanapewa kiburi sijui na kitu gani ? Kuna visiwa kadhaa kama Comoro, nk ambavyo vinajiita nchi mbona sioni maendeleo ya maana humo? Mi nafikiri mtoto akililia wembe apewe umkate. Hao wanaoandamana nina uhakika hawajui watendalo na hata Zanzibar ikijitegemea kuwa nchi nachelea kusema hawataonja punje hata moja ya kile walichodanganywa kupigania. Wanatumika bila kujua wanaofaidi Muungano ni watu wa Zenji


Umesahau na Morisious, Japan,........etc
 
Tumekwisha kanyaga mavi!

Tulichotakiwa kujadili mwanzo ni kuwepo au kutokuwepo kwa muungano. Kama muungano unapendwa na wananchi basi ndiyo muundo wa muungano ujaliliwe na hatimaye katiba mpya.

Kitakachotokea kwa sasa ni Wazanzibari kuikataa katiba mpya wakiwa na maana ya kupinga kuendelea kuwa katika muungano. Endapo serikali itatumia nguvu kuulinda muungano kutazuka wanaharakati wengi ambao wataipotezea serikali muda mwingi wa kuwahudumia wananchi na badala yake kujibu hoja.

Ni vema serikali ikajiandaa mapema ili endapo Wanzanzibari watakataa katiba mpya, jambo ambalo ni dhahiri, mchakato wa kuvunja muungano uanze mara moja vinginevyo tutakuwa tunakaribisha Al Shabaab na Boko Harama na hivyo kuhatarisha amani na umoja wetu wa Watanganyika.

Duh!! hapo nimekupata Mkuu, wewe ni jembe la FORD.
 
Wenzetu wamesha jua uzur na ubaya wa muungano cc tulio weng kama mazuzu fata upepo
 
Breaking News:
Kuna taarifa ya Maandamano makubwa ya Vijana wanaojiita Wanaharakati wa Zanzibar kudai haki za wanzazibari, Polisi wako mbioni kuzuia maandamano hayo ili hali vijana hao wanadai kuwasilisha barua za maombi ya kufanya maandamano hayo.

Hakuna fujo yoyote mpaka sasa na kiasi cha watu watano wamekamatwa akiwemo kiongozi wa kundi hilo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, kikundi hicho ndicho kilichokwenda katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mwaka jana kudai haki za wazanzibar.

Madai yao makuu ni kutaka kabla ya mchakato wa katiba kuuanza kufanyike mjadala wa Muungano utakaohusisha kura za maoni.

Source: Arusha Mambo.

Hata mimi nawaunga mkono, huku bara pia tunataka mjadala wa Tanganyika yetu,kwani waasisi wa muungano hawakuwauliza watanganyika waliokuwa wengi ili watoe ridhaa ya muungano, huu muugano ulikuwa ni kwa maslahi ya kisiasa kwa zanzibar ambao walikuwa wakihofia mapinduzi kama ilivyokuwa shelisheli ya bob Bernad. Muugano wa serikali mbili ni kichekesho na yalikuwa ni maiigizo- ya kisiasa yaani "Political Comedy" haiwezekani wazanzibari wabaki na serikali yao ya Zanzibari na sisi eti tunaitwa Serikali ya Tanzania,Sisi tunataka Tanganyika yetu irudishwe na haki yetu ya kuamuamua mambo yetu kama Watanganyika irejeshwe, Hivi katika baraza la wawakilishi la Zanzibar kuna wabunge wa bara wamo????????????,
Lazima hata katika katiba mpya haaya yawekwe wazi.
Huu ni uhuni wa waziwazi na maamuzi ya kidikteta yaliyofanywa na waliojiita waasisi wa ualioitwa Muungano eti wa Tanganyika na Zanzibari.
Hata hati ya uhuru wetu toka kwa governor Edward Twining inasomeka kuwa uhuru wa Tanganyika ulikabidhiwa kwa Watanganyika na siyo kwa watanzania,huu ni uhaini ningekuwa na uwezo ningewafungulia mashitaka waliojiita eti waasisi wa muungano wa Tanganyika na Zanzibari.

"No thanks,We need back our Republic of Tanganyika"
 
.....kama ndio hivyo,ni bora hicho kikundi cha UAMSHO kiende kwa msajili wa vyama vya siasa kupata usajili tujue moja,kua ni chama cha siasa au ni moja kati ya taasisi za kidini?

Vyama vya siasa vinatumiwa kuimaliza Zanzibar, hilo tumeshalielewa muda mrefu .Kuibuka kwa vikundi vya kidini katika kudai haki za Zanzibar ni matokeo ya wanasiasa kushindwa kutetea matakwa ya Wazanzibari. Hatari inayofuata ni vijana wa kizanzibari kutumia dini yao kama njia pekee itakayawaletea ukombozi wa Zanzibar.
 
wakati muungano unaasisiwa wananchi hawakushirikishwa. Zilikuwa ni busara tu za viongozi wetu, labda kipindi kile ilionekana watu walikuwa na uelewa mdogo. Muda umepita sasa na watu wana uelewa mkubwa. Ni kwa nini isingepigwa kura ya maoni wananchi tuchague kama tunataka kuendelea na muungano au la?
 
wakati muungano unaasisiwa wananchi hawakushirikishwa. Zilikuwa ni busara tu za viongozi wetu, labda kipindi kile ilionekana watu walikuwa na uelewa mdogo. Muda umepita sasa na watu wana uelewa mkubwa. Ni kwa nini isingepigwa kura ya maoni wananchi tuchague kama tunataka kuendelea na muungano au la?

ulikuwa ni utashi wa viongozi, hakuna busara hapo!!!!
 
Kura ya maoni ni muhimu. Lakini sidhani kama viongozi wa ccm watakubaliana na hili. Maana wanaulinda muungano kwa polis na jeshi badala ya kutumia wananchi.
 
Muungano hauwezi kuvunjika bila kuchapana kwanza kama Sudan
 
Sasa wewe mwenyewe weka Poll hapo juu, ili uone japo kwa space ya JF tu, mambo yakoje!
 
Kura ya maoni ni muhimu. Lakini sidhani kama viongozi wa ccm watakubaliana na hili. Maana wanaulinda muungano kwa polis na jeshi badala ya kutumia wananchi.
Na kwa kufanya hivyo ndio wanazidi kuwafanya watu waauchukie Muungano kwa sababu wanaokama kama wanalazimishwa kuwemo ndani yake
 
Discussions on the union were conducted very secretively. From the archival materials and the statements of those who were in the ‘corridors of power' at the time, it would appear that not many people in the Tanganyika government or the Zanzibar Revolutionary Council knew what was happening. Apart from Nyerere and Karume, the only other people who might have been privy to those discussions were Rashidi Kawawa, Oscar Kambona, Job Lusinde, Abdallah Kassim Hanga, Abdul-Aziz Ali Twala and Salim Rashidi. (Haroub Othman)


Stuka!!!


The debates of 1983/84 resulted in major amendments to the 1977 union constitution and the formulation of a new Zanzibar constitution in 1984. But they also resulted in the forced resignation of Aboud Jumbe from all his state and party positions, the sacking of a Zanzibar chief minister and the serious warning given by the ruling party to a number of prominent Zanzibar figures. When these discussions were at an advanced stage, Nyerere is said to have called in his Attorney-General at the time, British expert Roland Brown, and asked him to draft a Union Agreement without anybody knowing. In the case of Zanzibar, the Attorney-General, Wolf Dourado, is said to have been sent on a one-week ‘leave' and instead a Ugandan lawyer, Dan Nabudere (accoridng to his own account which was corroborated by Babu), was brought in to advise Karume on the draft submitted by Tanganyika. Both Brown and Nabudere were present in the Karume-Nyerere discussions. One can speculate that one reason why Dourado was not involved was because he was ‘inherited' from the previous ZNP/ZPPP regime and the revolutionary government was hesitant to involve him in such a sensitive matter.
 
Dah ni hatari; ujue kule znz sa hizi kuna kundi moja linaitwa UAMSHO kundi hili linaongoza mchakato wa kudai Zanzibar huru sasa kama ni kazi basi huko Visiwani ipo haswaaa"

Ofcoz they deserve it, its their right ukizingatia utawala wa sasahivi hautoi matumaini kwa lolote, kama bara tunapigania uadilifu,maadili utawala wa sheria katika kuongoza nchi, nadhani Zanzibar ni zaidi thats is the only way kupata wanachokitaka. JK katumaliza!!! u wil come to knw ths clearly when u grw up, So sorry Tanzanians!!!!!!!!
 
Upele tu jipu, uwaziri wao, ubalozi wao tena mbaya kabisa uwaziri wa mambo ya ndani tanganyika ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom