Elections 2010 Baadhi ya wana-CCM Arusha wajiandaa kufanyakazi na utawala mpya wa Dr. Slaa!!!!

Jana jioni nilipata nafasi ya pekee ya kukutana na viongozi na wakereketwa wa chama tawala na kwa mbali walionyesha kukataa tamaa.

Waliniuma sikio kuhusu taarifa za siri za idara ya usalama wa taifa kuwa zinawakatisha tamaa kwa sababu vijana ambao ni asilimia sitini na tano ya wapiga kura wote wanamkubali Dr. Slaa kwa asilimia sabini na mikoa kumi na tano ambayo ndiyo yenye kura turufu ya Uraisi asilimia sitini ipo beneti na Dr. Slaa.

Hata hivyo jamaa zangu hawa wa karibu wanajivunia ya kuwa ushindi wa Dr. Slaa ni asilimia hamsini tu yaani bado ni kiduchu na atapaswa afanye kazi nao CCM kwani hatakuwa na kile walichokiita "overall mandate"

Yaani eti Dr. Slaa hatavuka asilimia hamsini na kuonyesha kukubalika nchi nzima. Wanasema watamdhibiti Bungeni kwani huko taarifa hizi zawapa matumani angalau ya kuongoza kwa idadi ya wabunge na hivyo kutoa Waziri Mkuu na kuunda sehemu kubwa ya baraza la mawaziri........Chadema wanapaswa kuwasaidia wagombea wao wa ubunge kama nia ni kuunda serikali nje ya CCM................

Mikoa ambayo inawapasua CCM bongo ni hii hapa Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora, Dar-Es-Salaam, Iringa, Morogoro, Iringa, Mbeya, Rukwa, Pwani, Singida na Dodoma kwa mbali.

Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma jamaa zangu hawa wa karibu walidai mambo ni swafi haswa yaani CCM ni 40%, CUF 30 na Chadema 20%.

Mikoa mingine jamaa zangu wanadai wapo salama. Hivyo umtegemee JK kuzuru hiyo mikoa 15 mara kwa mara kupunguza makali ya Dr. Slaa.

Yaani nilishtuka mno.

Ila kilichonisikitisha walinilaumu kuwa mimi na wana-CCM wengine wenzangu waliotubatiza jina bandia la wasomi eti tumekisaliti chama chetu.

Lakini jamani, ukweli si upo wazi? Sisi CCM kazi yetu ilikuwa ni kuleta uhuru kazi ya kuujenga uchumi historia yabainisha upinzani wataifanya shughuli hiyo vyema.........

Dr. Slaa kwenye hotuba yake ya kuapishwa Uraisi ninamwomba sana awe muungwana na atupungeze CCM kwa kuleta uhuru hata kama kazi ya uhuru wa kiuchumu tumeboronga.

Ni hayo, tu wanajamvi wenzangu..........


Nchi ni yetu wote. Kwa nini watu wengine wafikirie kwamba wao wana HAKI ZAIDI ya kuitawala kuliko wengine? Wametawala miaka 50, wameshindwa kuiendesha. Sasa udereva apewe mwingine mwenye uwezo. Dk. Slaa ameonesha anaweza. Hata Hayati Mwalimu angekuwapo ANGEMKABIDHI NCHI na hawa wachachuaji wa kura wasingekuwa na la kusema!
 
Back
Top Bottom