Baadhi ya Wabunge Ugiriki walishinikiza kuvamiwa ofisi za umoja wa Watanzania?

Ni kweli hali ya uchumi nchini Ugiriki inasemekana imefanya hicho chama cha kifashiti kijizolee sifa. Mfano sasa kinatetea wazawa kwa kukandamiza haki za wahamiaji

Na kwamba chama hicho cha Chrysi Avgi kinachukua sheria mkononi . Ubabe unafanyika mbele ya polisi

Ni jukumu la wabongo kufahamu kwa kiasi fulani hali hii ni natural reaction kwa wazawa wanapojikuta katk halia ya kujiona kuwa wamenyang`anywa kila kitu na kuhisi kundi fulani linahusika.Wabongo wanatakiwa wawe na makundi yenye kusoma wakati kama zilivyo jamii za kiyahudi na wengine ambao mara zote hupima mazingira yao na kuona jinsi gani watu wanakuwa "anti- Semitic". Wabongo kwa nini wasijue wakati upepo unawaendea watu weusi vibaya na kutafuta mbinu za kujenga Taswira ya kukbalika?

Nasema haya yote ili wabongo wajue ni jinsi gani wapo hovyo kiulewa na wakiwa nje ya nchi ndio kabisa wanakuwa kama nyumbu.Wkaijenga taasisi zinazoenda mbali zaidi ya kufa na kuzikana, zaidi ya Bongo flavour na ujinga miwngine kama mitandao ya wizi na unga.Pia wajue kuwa wanaweza saidia nchi ktk upelelezi wa kiuchumi ,kisiasa, kiutamaduni na hata kujenga paltform ya kuwachunguza majirani zetu kupitia mitandao yao iliyopo nje kama inteligensia yetu haiwezi chunguzo hizo nchi mojakwa moja.Na hizo taarifa kuja nyumbani ili nchi ijue nafsi yake kimataifa na mengine.

Lazima wakusanye brilliant minds za watu waliopo Greece kwa taaluma zao, wanaofanya kazi zinazotambulika,wapelekwe mbele ili waweze fanya lobbying mbalimbali za kuwasaidia huko, na hata kuisadia nchi yao hali inapokuwa si njema sana.Israeli inawatumia wayahudi wao kufanya lobbying bila kuchoka ili taifa lao lissulubiwe na mataifa katika UN.Kuna mataifa mengi tuu yapo ktk hali ya kushawishika vibaya juu ya israel na hel aya waarabu imeshafanya hali ye hewa kuwa si shwari sana.Sasa wabongo kama hawana hizi akili na malengo ya kujenga Civilization kama walivyo wenzetu wa kihindi basi watabaki mmoja mmoja kama lonely dog na kupotea kimyakimya.Mkijenga taasisi imara popote muendapo mtafikia mahalia pa kuwa na sauti nyumbani, na mazingira kama haya mnaweza wataka wawaletee balozi huko.

Imagine wakati wagiriki wakipunguzwa kazi halafu jamii ya kitanzania ikajikusanya na unagalia kati yao walio na vitega uchumi halali na kutangaza kutoa ajira kadhaa(wakataja idadi ya nafasi ) kwa wagiriki.N tukio hilo wakalitazama kama shemu ya kushiriki kipindi kigumu na ndugu zao wa ugiriki, ambao wana historia ndefu sana tangu Nyumbani ambapo kuna wagiriki wengi tuu waliolowea.Wagiriki ambao ni racist wengine hawajui kuwa kuna wenzao wanatengeneza pesa huku kwa faida ya wao huko.Kwa hiyo hapa wangekuwa neutralized na wengine kujengewa positive views.
 
Back
Top Bottom