Baadhi ya muvi za bongo zinachefua

The Planner

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
357
118
Kila kitu katika dunia hii kina hatua zake toka kuzaliwa (kuanzishwa) mpaka kufa kwake, Katika kila hatua kuna changamoto zake lukuki, lakini changamoto ndo zinafanya hatua inayofuata iwe bora zaidi, lakini mmh si katika muvi za Bongo. Leo nataka japo kwa ufupi kujadili suala la "Bongo Movies" jamani maproduza wetu hata kama tupo katika hatua za awali katika tasnia hii hebu basi jaribuni kuweka uhalisia kidogo, kuna baadhi ya movie zinachefua kwa kweli, yaani unakuta watu wako makaburini ndugu wa marehemu anakunywa bia na kucheka pembeni yake kitu ambacho katika utamaduni wetu wa kitanzania hakipo. Halafu tusiponunua mnalalamika hatuna uzalendo wala hatuwasapoti, jamani mnachefuaaaaaaa.................jirekebisheni!
 
Yaani ni bora ukae uangalie cartoon kuliko kuangalia yale matakataka jamani yanachefua sana.leo nimeangallia maigizo fulani ya kanumba THE BLACK SUNDAY yaani inasikitisha watu wazima w ale kuigiza madudu kama yale..lkn sishangai sana hili kila mtu anajifanyia anachoona sawa machoni pake na hii ni zao la utawala mbovu manake hakuna usimamizi maigizo pumba hayana viwango halafu yaanachiwa sokoni...MUNGU INUSURU TANZANIA
 
Back
Top Bottom