Ndugu wanaJF salamu
Kutokana na mchakato tulionao hivi sasa kuhusu mabadiliko ya katiba yetu, leo nimependa nitoe maoni yangu kuhusu baadhi ya mambo ambayo ningipenda yaingizwe kwenye katiba mpya tunayoitaka.
Fuatana nami na utoe na yako ili tuweze kuboresha katiba ijayo.
1. katika katiba ijayo ningependa idadi ya wizara zipungue mpaka 10 to15 tu, zitajwe na ziwe "fixed". Sio leo anakuja Raisi huyu na wizara zake kulingana na anavyoona yeye. Mara Wizara ya Uwezeshaji, mahusiano nk, ilimradi tu kupeana ulaji. Hii siyo sawa hata kidogo, lazima kuwe na utaratibu unaoeleweka wa kufuatwa na kila mtawala.
2. katiba ijayo izungumzie sera za nchi kwa kila wizara, idara na mashirika ya umma. siyo leo anakuja mkubwa huyu anakuja na mipango yake. Sote ni mashahidi ktk haya; Mungai alikuja na sera ya kufuta michezo mashuleni na kuunganisha masomo mashuleni, leo tunashuhudia mabadiliko mengine tena. yaana hakuna la kueleweka.
3. Katiba mpya iwaondoe wabunge kuwa mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya. Raisi ateue mawaziri kutoka uraiani.
4. Wakuu wa idara na tasisi za umma wateuliwe na raisi na kuthibitishwa na bunge ama mabaraza ya madiwani katika ngazi husika.
5. katiba mpya itamke wazi kuwa kila kiongozi wa kisiasa aweke maslahi kwanza kwa nchi na si kwa chama. kwa maana hiyo lazima kuwa na wagombea uongozi huru.
6.Katiba mpya itamke uwepo wa serikali ya Tanganyika
7. katiba mpya itamke adhabu ya kifo kwa mafisadi wa mali ya umma.
8. katiba mpya itamke mali zote zilizohodhiwa na CCM ambazo zilipatikana wakati wa chama kimoja zirudi serikalini na ziwe za umma wote wa waTZ na si ilivyo sasa kw CCM kumiliki mali zote km viwanja vya mpira, majengo, viwanja nk
Ndgu wanaJF hayo ni baadhi tu ya mambo mengi ninavyoona mie yawemo kwenye katiba mpya ijayo. Wewe je, unayoya kwako?
Tujadili!