Baadhi ya makalani wanahujumu zoezi la Sensa

The Planner

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
357
118
Kaya yangu ni moja kati ambazo zilikuwa hazijahesabiwa katika siku saba za mwanzo. Nilikuwa na maswali mengi kichwani, mojawapo likiwa kama mimi nipo mjini ambapo kuna miundombinu ya kutosha sijafikiwa, itakuwaje kwa mtu aliyepo kijijini. Lakini leo asubuhi alikuja karani wa sensa nyumbani kwangu lol, ni bora hata asingefika tu maana kwa upeo wangu mdogo najua kuna dodoso refu lenye maswali 62 na fupi lenye maswali 32. Bahati nzuri nimefanikiwa kuyaona yote na maswali yake jinsi yalivyo. Sasa huyo karani amefika na kuniuliza maswali juu ya watu waliolala nyumbani kwangu usiku wa kuamkia hy trh 25, nikamtajia.,nikitarajia follow-up questions kwa kila mwanakaya but that was not the case, akaniuliza maswali ya kizushi kama manne, then akanishukuru kwa ushirikiano. Nikamuuliza vp mbona kama kuna maswali umeskip juu ya kaya yangu nani atayajibu.,akasisitiza kuwa amemaliza maswali yake.,nikakmtajia kipengele kidogo tu mbona hujaniuliza juu ya household assets, akaniambia amemaliza! Kwa ujumla ni kwamba anakwenda kupika data zake jinsi anavyojua yy na kusubmitt hayo madodoso yake. Kwa jinsi zoezi zima lilivyokuwa nikapata picha mbili
i) Mgomo baridi: Either kwa sababu ya malipo kiduchu, makarani wameamua kufanya kazi kwa thamani ya pesa wanayolipwa
ii)Uvivu na uzembe wa karani: Maswali yamekuwa mengi na karani ni mvivu na mzembe(But hili silipi sana kipaumbele)

Implication yake ni kwamba kama data zinapikwa maana yake ni kuwa hakuna development planning yeyote ya maana kwa kuwa data sio halisi, then zoezi zima ni kupotezeana muda tu unless kama wht is needed ni idadi ya watu tu.
 
ahhh .......
ulikuwa ujui kwamba ni buruza twende. taarifa hizi za sensa utakuja kusikia zinatofautia na idadi ya waliopata vitambulisho vya mkazi..
 
Back
Top Bottom