Baadhi ya Lecturers wa Mzumbe wana degree Feki - VC wao naye FEKI

Unajua hili suala la academic qualification ni big deal sana katika nchi zinazoendelea kam Bongo lakini waajiri wengi katika nchi za ulaya wanajua kuwa wengi wenye academic qualifications wanamatatizo ya performance kazini

Kwa nini tuandikie mate wakati wino upo?

Tazama Tanzania ishakuwa na watawala walio na elimu za kubobea na mpaka leo baraza la mawaziri limejaa watu wenye postgratuate degrees lakini wanashindwa kuna na solution ya matatizo madogo madogo

sasa whats the point ya kuwa na Makaratasi ya kila namna halafu ufumbuzi wa matatizo ni ZERO?
 
kichuguu said:
Hiz paper ni za kibabaishaji tu, siyo concrete; they are too journalistic: ni kama "makala ya gazeti la habari". Hata hivyo inaonyesha kuwa Ngowi anayependa kujitahidi, ila labda alikosa usimamizi mzuri tu na tamaa ya udakitari wa mkatomkato.
-----------------
List ya vyuo feki iko hapa:

http://en.wikipedia.org/wiki/List_of_unaccredited_institutions_of_higher_learning

Kagueni Ph.D zote za Mzumbe inawezekana idadi ni kubwa kuliko inavyojulikana kwa vile tumezoea kuangalia PWU and COU tu. Angalia wale wanaolist Ph.D generically bila kuonyesha awarding institution. Kwa Mfano kuna watu wameandika Ph.D(USA), Ph.D(Norwegian School).

Vilevile kuna Ph.D zinazotokana na vyuo veye acredditation from unrecognized bodies kama ilivyo hapa chini:

http://en.wikipedia.org/wiki/List_of_unrecognized_accreditation_associations_of_higher_learning


Good Point bwana kichuguu lakini naomba kukuarifu kuwa hata hiyo wikipedia ambayo umepost link yake ina matatizo ya CREDIBILITY na IMPARTIALITY kwa sababu mtu yoyote anaweza kuandika akitakacho..

Actually hata mimi huwa naingiza mabo ambayo naona kuna mapungufu na mara ya mwisho nilifanya hivyo baada ya kukuta Michuzi (mpiga picha) kaingiza habari za JK amabo hazikuwa sahihi

-MZ
 
DrWHO said:
Good Point bwana kichuguu lakini naomba kukuarifu kuwa hata hiyo wikipedia ambayo umepost link yake ina matatizo ya CREDIBILITY na IMPARTIALITY kwa sababu mtu yoyote anaweza kuandika akitakacho..

Actually hata mimi huwa naingiza mabo ambayo naona kuna mapungufu na mara ya mwisho nilifanya hivyo baada ya kukuta Michuzi (mpiga picha) kaingiza habari za JK amabo hazikuwa sahihi

-MZ

OK, ninajua tatizo la wikipedia kuwa iko kama choo ambako kila mtu anaweza kwenda. Hata hivyo ripoti zake nyingi huwa ni sahihi kwa vile zile za uwong huwa zinachujwa na kama ulivyofanya.

Nina imani kuwa hiyo post nilyoweka hapa ni sahihi kwa zaidi ya asilimia 95 hasa kwa vile imekuapo kwa muda mrefu bila kufanyiwa mabadiliko makubwa. Kwa hiyo inaweza kuwa inaaminika.
 
Jamani hizi ndizo digrii feki....
Huyu Vice President amenambia inasikitisha sana kwamba kuna watu wamefikia kufyatua digrii zao kupitia njia zisizo halali na kuna kesi kibao Marekani ambazo zimewahusu wao jambo ambalo limefikia kiasi kwamba wamepoteza credibility hali washiriki hawakupata elimu hiyo. Ameendelea kunambia kuwa chuo hicho hakikushiriki kabisa kwa ufyatuaji wa hivi vyeti ambavyo vinauzwa mitaani ama kupitia mtandao. Na kila kesi zinavyozidi kuongezeka ndivyi wanavyozidi kupoteza biashara yao.
Yupo tayari kushirikiana nasi (viongozi wa elimu nchini) kuwaorodhesha wote wasiokuwa na elimu kwa kutumia jina la chuo hicho kwani inazidisha kuondoa nafasi yao ya usajili...
Kifupi, Phd hawatoi na yeyote anayedai kuwa amepata digrii hiyo toka chuo hicho ni mwongo!.
Sasa inabidi viongozi wetu walifungie kazi swala ambalo laonekana kuwa rahisi sana. Mtandao ama kupiga simu tu ktk shule husika utapata ukweli wote!
 
Mzee Mkandara kule bongo suala hilii liko wazi kabisa na PWU kinaeleweka kuwa ni chuo feki. Tatizo ni laisser faire culture tuliyokuwa nayo kwenye system yetu. I'm sorry to say, MU inatia aibu academia ndani ya Tz and I think somehow it even affects their decision making. Wakati IDM inabadilika kuwa MU wanafunzi ambao walisoma Adv Dipl. wote walishtukia wanakuwa upgraded na kuwa awarded degrees! To me this was a very controversial decision. But anyway hiyo ndio Tz yetu, wenyewe wanasema mwendo mdundo!
 
Mtz,

Nadhani hata Nungwi naye ni mmojawapo wa waliopata DEGREE baada ya kusomea ADVANCED DIPLOMA.
Inashangaza unapoomba kusoma diploma lakini mwishoni unapewa degree tena kwa syllabus ile ile ya diploma na ambayo aliyepita alisomea!!

MU kweli wanaaibisha!

FD
 
Fikraduni,
umeona gazeti la jana Udsm wanaomba msaada wa vitendea kazi hawana pesa, walimu n.k. shida hizi hazipo MU.
nimegundua chuki na taabu mlizonazo UDSM ndio zinapelekea kuionea wivu Mzumbe,
leo nilipita IFM basi staff yote imejazwa na MU kuna wataalam pale wameanza na Advanced Diploma hadi MBA toka mzumbe na wanamwaga vitu vya nguvu cha ajabu UDSM hawapo pale sijui wako wapi? ukienda Hazina huwakuti unamkuta mama Nyoni-Mhasibu mkuu product ya Mzumbe,
ukienda Ikulu, Utumishi n.k ni Mzumbe tu.
hao akina Dr.Assad vichwa vyao vigumu imewachukua miaka mitatu kupata Phd sasa wanapoona vipanga wa Mzumbe wanakamata Phd kama wamesimama, UDSM donge tayari.
Mara ooh MU wamechukua phd chuo kimoja tu PWU naomba utizame na IFM ambapo wamechukua masters toka chuo kimoja tu cha U.K ambacho wana mashirikiano nacho jee nao feki? pia kama MU wangekuwa feki basi wangekula sahani moja na wakali wa IFM.
KIFUPI UDSM hawaonekani kwenye maofisi makubwa nadhani wako busy kupika majungu tu.
Nani hajui wanafunzi wanavyoingia na vyeti feki Udsm kama kozi ya sheria ambapo kuna mwaka kulikuwa na wanafunzi feki 68 jee huo umakini wa kuwa chuo cha 13 uko wapi?
tukubali ndio ya 13 huenda hiyo league table ilifanyika mwaka 1947 wakati huo Mu isingeweza kuingia kushiriki haikuwa chuo kikuu na hata ingeshiriki isingeshindwa na UDSM(Mbagara charambe primary).
kuna mjumbe kasema wana kozi zote hadi kufuga njiwa ndugu yangu kula kwingi haina maana unakula diet au vitamini, mzumbe wanatoa kozi kutokana na mahitajio ya Taifa, kuna mijitu ilitoka UDSM baada ya kumaliza General Engineering na wakakosa kazi hatimaye wakaomba waje mzumbe wafanye ADCA, Mzee PROFESSOR,DR.Warioba akasema hatuchuwi makapi ya UDSM.
kuna mjumbe kasema ukiwa na division 11 hupati kitu UDSM, swali Michael Wambura na Mnyika John wameingia na DIVISION ONE point ngapi?
Hitimisho kama kuna watu wametumia miaka 6-7 kupata Phd na wakawa mbali na familia zao watu hawa wakiona mtu kapata Phd hapahapa TZ au katumia muda mfupi kupata PHD asiwafanyie chuki, kwani binadamu tunatofautiana uwezo wa kuelewa masomo nyie Wana Udsm uzito wenu wa kuelewa masomo msilazimishe kuwa hakuna wepesi wa kuelewa masomo.
pia kama umegundua sasa hivi hakuna mtu anaenda kufanya MBA Udsm watu wanajazana Mzumbe wakikosa nafasi ndio wanakwenda kwa wazushi(UDSM).
Maana MU wanatoa MBA makini na pia kuna MPA.
Firaduni acha uvivu wa kufikiri nenda IFM ukaone BAF za Mzumbe zinavyofanya kazi kuendeleza Taifa tena kuna dada tu anapiga chaki(mzumbe product).
WITO-mzazi peleka mwanao Mzumbe kwani in next 10 Mheshimiwa Dr.nchimbi atakuwa president wa TZ hapo akina FD wapanda juu kwenda kuziba wapi.
 
FD na wenzako.
nimesahau kuulizia ule mradi wa vitabu vya Finance ambapo DR.wenu Assad kakaa ndani akisaidiwa na FD, halafu wanawauzia wanafunzi eti mwl wetu katunga kitabu-msiba mkubwa huu.
FD mnawapa matango mwitu vijana nani atawaajiri kwa kufanya reference kijarida chenu(Author.Dr.Assad)? achenu uchoro UDSM
 
nungwi said:
Fikraduni,
umeona gazeti la jana Udsm wanaomba msaada wa vitendea kazi hawana pesa, walimu n.k. shida hizi hazipo MU.
nimegundua chuki na taabu mlizonazo UDSM ndio zinapelekea kuionea wivu Mzumbe,
leo nilipita IFM basi staff yote imejazwa na MU kuna wataalam pale wameanza na Advanced Diploma hadi MBA toka mzumbe na wanamwaga vitu vya nguvu cha ajabu UDSM hawapo pale sijui wako wapi? ukienda Hazina huwakuti unamkuta mama Nyoni-Mhasibu mkuu product ya Mzumbe,
ukienda Ikulu, Utumishi n.k ni Mzumbe tu.
hao akina Dr.Assad vichwa vyao vigumu imewachukua miaka mitatu kupata Phd sasa wanapoona vipanga wa Mzumbe wanakamata Phd kama wamesimama, UDSM donge tayari.
Mara ooh MU wamechukua phd chuo kimoja tu PWU naomba utizame na IFM ambapo wamechukua masters toka chuo kimoja tu cha U.K ambacho wana mashirikiano nacho jee nao feki? pia kama MU wangekuwa feki basi wangekula sahani moja na wakali wa IFM.
KIFUPI UDSM hawaonekani kwenye maofisi makubwa nadhani wako busy kupika majungu tu.
Nani hajui wanafunzi wanavyoingia na vyeti feki Udsm kama kozi ya sheria ambapo kuna mwaka kulikuwa na wanafunzi feki 68 jee huo umakini wa kuwa chuo cha 13 uko wapi?
tukubali ndio ya 13 huenda hiyo league table ilifanyika mwaka 1947 wakati huo Mu isingeweza kuingia kushiriki haikuwa chuo kikuu na hata ingeshiriki isingeshindwa na UDSM(Mbagara charambe primary).
kuna mjumbe kasema wana kozi zote hadi kufuga njiwa ndugu yangu kula kwingi haina maana unakula diet au vitamini, mzumbe wanatoa kozi kutokana na mahitajio ya Taifa, kuna mijitu ilitoka UDSM baada ya kumaliza General Engineering na wakakosa kazi hatimaye wakaomba waje mzumbe wafanye ADCA, Mzee PROFESSOR,DR.Warioba akasema hatuchuwi makapi ya UDSM.
kuna mjumbe kasema ukiwa na division 11 hupati kitu UDSM, swali Michael Wambura na Mnyika John wameingia na DIVISION ONE point ngapi?
Hitimisho kama kuna watu wametumia miaka 6-7 kupata Phd na wakawa mbali na familia zao watu hawa wakiona mtu kapata Phd hapahapa TZ au katumia muda mfupi kupata PHD asiwafanyie chuki, kwani binadamu tunatofautiana uwezo wa kuelewa masomo nyie Wana Udsm uzito wenu wa kuelewa masomo msilazimishe kuwa hakuna wepesi wa kuelewa masomo.
pia kama umegundua sasa hivi hakuna mtu anaenda kufanya MBA Udsm watu wanajazana Mzumbe wakikosa nafasi ndio wanakwenda kwa wazushi(UDSM).
Maana MU wanatoa MBA makini na pia kuna MPA.
Firaduni acha uvivu wa kufikiri nenda IFM ukaone BAF za Mzumbe zinavyofanya kazi kuendeleza Taifa tena kuna dada tu anapiga chaki(mzumbe product).
WITO-mzazi peleka mwanao Mzumbe kwani in next 10 Mheshimiwa Dr.nchimbi atakuwa president wa TZ hapo akina FD wapanda juu kwenda kuziba wapi.


Nungwi wacha uwongo wa kupata Ph.D bila kusomea au ksuomea nyumbani kwa miezi tisa tu; huo ni uwongo unaotoka mdomoni mwa mtu asiyejua maana ya digrii hiyo. Kwa madai yako ya waalimu wa mzumbe kupata digrii bila kuzisomea ukidai ni kwa sababu ya ukipanga wao umenikatisha tamaa kabisa kusoma posts zako. Niimegundua kabisa kuwa hujui kiti katika uwanja huu. Kuwa na wanafuinzi wengi wa Mzumbe serikalini siyo tatizo; Mzumbe kilikuwa chuo cha watumishi wa serikali na mlolongo wa uhusiano wa chuo na serikali umeendelea kuwapo. Kumbuka kuwa kuna alumni wengi sana wa UDSM ambao wanafanya kazi za kitaalamu na madaraka makubwa nchi za nje kama Marekani na Uingereza ambako wameajiliwa kutokana na uwezo wao na wala siyo kwa sababu ya historical link kati ya bosi wa serikali na chuo husika.

Watu wa busara walisema anayehishi kwenye nyumba ya vioo huwa hatupii wengine mawe. Kama kuna mtu hapo MU anapata Ph.D bila kusomea, atakuwa wa kwanza vile vile kutoa Ph.D kwa wengine bila kusomea na hilo ndilo tatizo kubwa ambalo watu wanaloliongelea. Angalia huyo Waryoba kutokana na yeye mwenyewe kujipachika Ph.D bila kuisomea amekuwa naye anaruhusu waalimu wake wajipachike Ph.D za namna hiyo hiyo hiyo. Kwa hiyo ni jambo la wazi kuwa kuna uwezekano kwa waalimu nao kutoa digrii kwa wanafunzi wao bila kuzisomea, hasa kwa vile siyo siri kuwa inajulikana ni waalimu gani walinunua Ph.D zao.


Mwisho, kama wewe Nungwi siyo mmoja wa waliokwapua hizo Piehidi za mkato, usizipigie kelele kuzitetea, unajipunguzia heshima.
 
Nchimbi kuwa President siyo hoja. After all Mwinyi alikuwa president bila kuwa product ya chuo chochote. Pamoja na kwamba Kikwete na Lowasa wana digrii za UDSM si vizuri kuwatumia kama vigezo vya mafanikio ya UDSM. Kuna wengi sana wa namna hiyo kutoka UDSM kama akina Museveni, marehemu John Garang na majaji wote wakuu hapo Tanzania, Kenya na Uganda. Hilo siyo tatizo, tunachoongelea na quality za Ph.D za waalimu
 
Ama Kweli Nungwi unachekesha! yaani unashangaa Assad kuchukua PhD kwa miaka 3! wakati ukienda continental europe ni miaka 4 na bila a minimum of 3 papers published kwenye well recognised journals huwezi kuwa eligible kudefend. US ndio kabisa si ajabu kupiga 5yrs maana watakuambia uingie darasani kabisa. Hizi PhD za miezi ndio zinadhihirisha wazi ufeki wake ambazo hata Bungeni zinapigiwa kelele cheki hapa nanukuu kutoka http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/HS-4-27-2006.pdf

"Mheshimiwa Spika, vile vile kumekuwa na tatizo la kuajiri walimu waliopitia katika vyuo visivyo na sifa na hata wengine wakiwa na Shahada za Uzamili na zile za uzamivu Ph.D. zinazopatikana kwa njia ya mawasiliano ya internet (online degrees). Shahada za aina hii inawezekana hazina tatizo kutumika kisiasa, lakini inapokuja suala la ufundishaji hasa katika Vyuo vyetu Vikuu linapaswa kudhibitiwa kwa nguvu zote.(Makofi)"

Hapa wabunge walikuwa wanadoubts ambazo tayari zinajitokeza hapo MU, nanukuu tena kutoka bungeni
"Hivi karibuni tumekishuhudia Chuo cha Mzumbe kimegeuzwa kuwa Chuo Kikuu
na tayari tumeshuhudia vile vile baadhi ya vyuo kama 5 vimepandishwa hadhi na kuwa Vyuo Vikuu Vishiriki. Mimi naogopa kwamba matatizo yale ambayo sasa hivi tunayakabili kutokana na mipango ya MMES na MMEM yasije yakajitokeza tena hapa katika kuendeleza Elimu ya Juu. Kwa sababu hapa itakuwa ni hatari sana. Sijui kama hii ni njia nzuri ya kuongeza idadi ya Vyuo Vikuu. Kupandisha tu hadhi vile Vyuo ama Sekondari ambazo zipo na kugeuza Vyuo Vikuu. Nafikiri ipo haja ya Wizara kutafakari zaidi ni njia gani bora ya kuongeza idadi hii ya Vyuo Vikuu. (Makofi)"

Tuache kupiga porojo Nungwi, MU haielekei pazuri hata kidogo.
 
mswahili said:
Kumbe University of Dar-es-salaam walikuwa wanatengeneza magaidi i.e Garang?

Usinichekeshe aisee,

Garang hakuwa Gaidi, alikuwa mpigania haki za watu weusi huko Sudan. Huyu jamaa alikwa na akili sana, alikuwa na Ph.D aliyopata University of Iowa. Kumbuka mara ya mwisho alikuwa vice president wa Sudan, kwa hiyo siyo kweli kuwa alikuwa Gaidi.

Hata hivyo ishu kubwa hapa ni kuhusu za Ph.D za maprofessor wa Mzumbe. Huyu Nungwi kutamnba kuwa Mzumbe products watakuwa mapresident na wananongoza ofisi zote za serikali na hazina msingi, lengo lake ni kudeflect objective ya mjadala huu.

Issue ya kucheka eti kwa vile gazeti limeandika UDSM kuomba vitendea kazi vile vile ni mtazamo finyu kwa vile hawezi kuprove kuwa Mzumbe ina kila kitu cha kufundishia. Chuo chochote ambacho ni progressive kila mara kinatafuta vifaa vipya ili kuweka mbinu mpya za kufundishia. Huenda wakasema wana kila kitu kwa vile wenyewe wana Ph.D za namna hiyo kwa hiyo hawajui mambo mapya ila yale waliyofundishwa enzi zao.

Kukimbilia kusema kuwa UDSM wanaona wivu wakati ameambiwa ukweli ni dalili ya Ukilaza wa hali ya juu: kila anayekukosoa ana wivu. PWU na COU zinajulikana kuwa ni degree mill-brief case institutions na kuna documents hata za serikali ya Marekani kuonyesha ukweli wa jambo hilo, halafu yeye anasema kuwa si hoja jamaa wa MU kupata degrees zao kutoka vyuo hivyo, watu wasiwaonee wivi, eti wao ni vipanga. Hiyo inanikera sana; hajui elimu ina maana gani, anachoangalia yeye na mbinu ya kupata ajira serikalini tu, basi. Swala la elimu halipo kabisa akilini mwake.

Kwa vile Nungwi analenga kupambanisha MU Vs UDSM angepigania kuhakikisha kuwa waalimu wa MU wana academic qualifications sawa na au zaidi ya wale wa UDSM na acedemic standards za MU zinapandishwa. Huo upuuzi wa kutoka vichochoroni wa kudai kuwa wanafunzi wanapata ajira serikalini kwa hiyo hicho ni kipimo tosha cha qaulity ya education ya mzumbe hauna maana yoyote kwa vile katika maswala haya mwalimu huwa anachangia sana katika quality ya elimu. Ndiyo maana kila digree lazima useme umeipata wapi, ili ijulikane kama ulikuwa na waalimu wazuri. Kutetea PHD uwozo eti kwa vile zinahuzu watu wa MU kutazidi kudidmiza maendeleo ya vyuo vyetu kwa jumla. Kushindwa kwake kukubali kuwa UDSM ni ya 13 Afrika ni jambo la ajabu kabisa, hajui standard za elimu. Amebobea sana katika kutetea MU kiasi kuwa asipoona MU kwenye list basi haridhiki. List hii ilikuwa published Mwaka jana tu, mwaka huu itatoka nyingine hivi karibuni tuangalie kama tutakuta MU.
 
Kichuguu, Mtz, FD na Mkandara,

Mnatumia nguvu nyingi sana kumuelimisha, mtu ambaye tunataraji atoke ktk ujinga lakini naona ndio hali inakuwa mbaya zaidi.

sometimes nafikiri huyu Nungwi analeta jokes hapa!! absolutely i can't imagine a balanced brain can be equated to Nungwi's one when reading his/her posts.

JKN alisema, moja ya kitu kibaya ktk jamii ni UJINGA, na inakuwa mbaya zaidi pale ambapo Mjinga hajijui/hajitambui.......Nungwi et al haitawezekana kuwatoa ktk kundi hilo.

Huyu Nungwi ananikumbusha kile kikatuni cha "ZERO" kwani hana tofauti.

Hivyo Wazee msipoteze muda wenu na huyu jamaa, hayo ni maoni yangu.
 
Ogah said:
Kichuguu, Mtz, FD na Mkandara,

Mnatumia nguvu nyingi sana kumuelimisha, mtu ambaye tunataraji atoke ktk ujinga lakini naona ndio hali inakuwa mbaya zaidi.

sometimes nafikiri huyu Nungwi analeta jokes hapa!! absolutely i can't imagine a balanced brain can be equated to Nungwi's one when reading his/her posts.

JKN alisema, moja ya kitu kibaya ktk jamii ni UJINGA, na inakuwa mbaya zaidi pale ambapo Mjinga hajijui/hajitambui.......Nungwi et al haitawezekana kuwatoa ktk kundi hilo.

Huyu Nungwi ananikumbusha kile kikatuni cha "ZERO" kwani hana tofauti.

Hivyo Wazee msipoteze muda wenu na huyu jamaa, hayo ni maoni yangu.


Asante, nafikiri sitamjibu tena huyu jamaa.
 
Mkuu Ogah,

Thanx. Kama mwalimu imenisikitisha sana kushindwa kumwelimisha mwanafunzi. Inawezekana mimi nikawa mwalimu feki au mwanafunzi wangu akawa ZERO.
Well, nitawaachia wasomaji wa judge. Nimejaribu kumuelimisha topic inahusu nini, yeye amei divert na kuipeleka kwenye Nchimbi na kulinganisha chuo kiachofundisha advanced diploma za aina nne na kinachofundisha Phd za aina kumi na ushee!!.

Sure, sometimes ukiwa unaoga mwizi akifungua mlango wa bafuni na kukuibia nguo, ukitoka kumfukuza watu watakuona wewe ni tahaira!. Inabidi ubakie bafuni.

Nabakia bafuni

FD
 
Msikimbie mmezoea kuzua uongo, sasa mnataka kukimbia wewe Ogah, Kichuguu na FD mmeona maji ya shingo, kwani ukweli umebainika nendeni IFM muone vijana wa Mzumbe kazi wanayoifanya.
nimeuliza kijarida cha Dr.Assad hamkuja na jibu lolote,
nimesema Dr.Nchimbi atakuwa rais wa kwanza ambaye ni Dr. nyie mnadai hata JK na EL ni product ya Udsm, mnashindwa kujua Nchimbi ni Dokta? ana degree 4.

Turudi kwenye mada Mzumbe imefanya wonders ndani ya utawala wa Professor Warioba kutoka kwenye Institute hadi University(London school of Economics ya TZ), ameweza kuzalisha MBA nyingi tu tena kwa muda mfupi maana UDSM unaweza kutumia hadi miaka mitano kupata Mba kisa roho ya korosho(graduate wawe wachache nchini ili tuwe tunatamba mitaani akina FD).

Mzee dr. Warioba kaliona hili na kalipatia ufumbuzi kwa kuweka MBA makini.
sawasawa na mtu kaenda gereji na katengenezewa gari yake vizuri sana halafu anaanza kuulizia hivi huyo dereva ana degree ngapi? kasoma Udsm? n.k mtu makini huhoji ubora au umakini wa matengenezo ya gari.
kadhalika ilitakiwa watu wahoji kama wanafunzi wanaotoka Mzumbe ni bomu? lakini imekuwa kinyume chake vijana wa Mzumbe ni vipusa kwenye soko la ajira, kuendelea kumpekua Dr.Warioba na timu yake huku vijana mtaani wanafanya miujiza ni ujinga na uvivu mkubwa, pia nimegundua UDSM wanadonge kubwa kuona DR.PROFESSOR Warioba hakupita UDSM(MAJUNGU HOUSE) na akaweza kufanya haya maajabu.

Swali kwa Fikiraduni huyo Baisi wako anafanya Phd toka 1994 na hadi sasa hajamaliza anaifanya hapo hapo Udsm, tizama ukiritimba wa Udsm? nae Bais kwa ujinga wake badala ya kuja Mzumbe afanye PHD yake ameng'ang'ana tu na wazushi,

Swali kwenu wana UDSM tunaomba Mwanafunzi mmoja tu ambaye ni bomu toka Mzumbe? jibu hakuna, sasa mnahoji nini? ndio maana serikali haina muda wa kusikiliza ujinga wenu ina mambo mengi ya muhimu kuyafanyia kazi i.e umeme.
pia hata ikisikia nyie mtapata nini? mosi serikali inatambua na kuenzi mchango wa Mzumbe kuzalisha vijana wengi wanaolisaidia taifa leo hii, zaidi ya hapo vijana wa Mzumbe ndio wako serikalini je mnategemea nini? kweli nyie mna akili? au mnafikiria? au ndio Fikira.....?

Hapo UDSM mwaka 1999 Chijoroga alichukua somo la Finance kuwafundisha mwaka wa Tatu cha ajabu kumbe somo hilo halijui(ana vyeti feki) akamuomba jamaa wa Ifm DR.abeid Gasper aje kumshikia darasa, basi DR.Gasper akafundisha na kutunga mtihani baadae wanafunzi wote wakafeli, wanafunzi hao wakaenda kwa Chijoriga ambaye ndiye dean wa faculty. wakamwambia Dr.Gasper katoa dozi nzito. basi wale wanafunzi wote wakapewa maksi nyingine(wakabebwa kwa kupasishwa) na Chijoriga huku hawajafanya mtihani mwingine. hiyo ndiyo UDSM ya 13.(msiba mkubwa) na hili ndio linalopelekea UDSM kushindwa hadi interview za kazi.
cha ajabu Dr. Chijoriga na utumbo huo amepewa UDEAN wa faculty na Professor Luhanga(mambo ya chupi tena).
wanaotaka kujua habari hii wamtafute Dr,Gasper yuko IFM au wanafunzi waliomaliza 1999 watakupa habari hii.

Dr. GASPER hakujua kuwa wale aliokuwa anawafundisha hawana misingi mizuri wanapita kwa kubebwa au kuuziwa mitihani au rushwa ya ngono ambayo ndio nyumbani kwake pale udsm hadi mtu kapewa UDEAN.haya hayapo MU kuna nidhamu ya kazi ya hali ya juu.
Akina FD naomba msikimbie kabla ya majibu ya hoja zangu.

Hitimisho kama MU wangekuwa wanafanya madudu hapo ndio mngekuwa na haki ya kuuliza PhD au Briefcase ya Mzee Warioba lakini mithali inafanya wonders bora tujadili jinsi ya kupata mawadati na vitabu Udsm maana mmetoa tangazo gazetini kueleza njaa yenu.
 
Bwana au Bibi Nungwi, Mimi ni mwalimu pia, nafundisha chuo kikuu kimoja hapa Marekani. Siwezi kukujibu kuhusu kitabu cha Assad kwa vile hakiko katika fani yangu pamoja na kuwa swali lako kuhus kitabu hiki pia silielewi. Ila najua kuwa Assad akishirkiana na watu wengine ameandika kitabu kimoja ambacho kiko listed kwenye Congress Library kwa jina la "Accounting and navigating legitimacy in NGO's." Nilijaribu kusearch kitabu cha Waryoba au Nchimbi sikupata hata kimoja wala Ph.D thesis zao hazionekani. Inawezekana nilikosea spelling za majina yao ingawa nilikuwa nin-cut and paste kutoka kwenye posting yako.


Mimi kama mwalimu niliyewahi kufundisha vyuo vingi sana hapa duniani kuanzia hapo UDSM na kendelea hadi South Africa, Australia, Japan, Canada na sasa hapa Marekani, nakuhakikishia kuwa hakuna chuo hata kimoja kinachotoa elimu nzuri ambacho utaingia asubuhi na kuondoka na digrii jioni; hicho kitakuwa ni kiwanda cha kupika titles tu siyo cha kutoa Elimu. Kulingana na maneno yako, kama ni kweli kuwa MBA hapo Mzumbe zinatoka kama njugu tu basi hali hiyo ndiyo inayotisha ambayo watu wanaipigia kelele. Ni mtiririko ule ule unatokana na waalimu kuwa na digrii feki, kwa hiyo nao wanaanza kutoa degrii feki bila uchungu : aliye kwenye nyumba ya vioo huwa hatupi mawe. Hapa Marekani kuna digree zinazoitwa executive MBA ambazo zinatolewa kwa muda wa kama miaka miwili au mitatu kwa njia ya correspondence na periodic oncampus stays. Hata hivyo digree za excutive MBAs ni targetted degrees zinazotegemea position na experience ya mtu, haziwekwi katika level ya MBA ya kawaida; normally holder anatakiwa aonyeshe kuwa ana MBA (Exec) au (Exec MBA).


Watu hawa wenye elimu ya kupaka mafuta ndio hao wanaoleta taabu sana katika undeshaji wa serikali kwa maamuzi mabovu na kuitia hasara serikali. Mara anyingi nimekuwa najiuliza inakuwaje serkili ya tanzania inafanya maamuzii ya kijhiga katika mikataba yake na nchio za nje kumbe inawezekana ni kutokana na wataalamu wake waliofundishwa na waalimu feki pale Mzumbe.
 
"DR" Nungwi,

Umesema Nchimbi ana digree nne. Nimecheki profile yake pale bungeni, huyu jamaa kumbe is a bogus material: ana ADA ya Mzumbe na MBA ya Mzumbe, zaidi ya hapo ana M.Sc na Ph.D za Commonewalth Open University, amefuata mkondo wa waalimu wake pale Mzumbe. Hilo ndilo jambo tunalosema kuwa waalimu wale wanachangia sana kujenga jamii isiyojua thamani ya elimu. Hata watoto wa shule za sekondari sasa wataanza kuplani jinsi ya kupata digrii zao kutoka COU na PWU bil kwenda chuo chochote. In fact nina imani kuwa baada ya muda mfupi kila mwanasiasa atakuwa DAKTA, na ikitokea kuwa anawakilisha nchi kujadiri mkataba na Dr. halali wa kutoka nje ya nchi tutaishia kupata pumba tu.
 
Back
Top Bottom