Baadhi ya Lecturers wa Mzumbe wana degree Feki - VC wao naye FEKI

Mkandara
Kwa maelezo yako sidhani kama kuna mjadala mrefu hapa, naungana na wewe cheti feki ni kile ambacho mtu amekipata bila kuhudhulia masomo yoyote kama alivyokuwa Kihiyo na elimu isiyo na kiwango ni ile iliyopatikana kwenye chuo kisicho na kiwango kama Phd ya my big friend Mh. Nchimbi on my opinion. Na lazima tutambue kuwa elimu ya njia ya matandao haimaanishi kuwa ni feki au haina kiwango. Mtu kuwa na cheti feki hilo halina mjadala ni kosa la jinai na mtu kuwa na elimu isiyo na kiwango siyo kosa ila ukitumia cheti chao kisicho na kiwango kupatia kazi au kuapatia cheo cha kisiasa tunaweza kukunyima kula kwa kuwa na elimu isyo na kiwango. Lakini tatizo lililopo toka kule bcs times nililipigania sana serikali lazima itoe list ya vyuo vyenye kiwango wanachokitambua baada ya hapo nitafikiria kuna na Nchimbi phase II au la. Mfano wa JK ameutumia kwa yule mbunge wa Bukoba ambaye inasadikika anatumia vyeti vya marehemu.
 
Sam,

Bado hujamuelewa mzee Mkandara. Yeye anasema hata elimu ya Nchimbi ya Phd SIO FEKI.

Mimi swali langu ni kuwa kweli tunaweza kumpa mtu Phd kwa wiki tatu?, somo litakuwa limeeleweka?. Kwanini basi wengine watumie miaka mpaka mitatu kuusaka huo u Phd?. Exceptions zinaeleweka Mkandara. Swali lingine ni kwa maslahi ya Taifa, kwanini wengi wa wenye hizo Phd za wiki tatu wapo Mzumbe tu? (nasikia na Moshi university pia nasikia wapo).
Mkandara are you comfortable supervised by a COU Phd graduate for your Phd?

FD
 
Namshauri Mkandara asome kwanza article ya Assad halafu ndio aijibu. Maelezo aliyoyatoa ni yale yale ya kule bcs na hayajazingatia maelezo aliyoyatoa Assad ambayo kwa kiasi kikubwa yalitoa mwanga wa kitaalamu katika hili jambo. Assad alianza kwa kueleza maana ya degree fake ambayo Mkandara hajazingatia katika maelezo yake.
 
Sam,
Hadi hapa tupo pamoja na nakubaliana na moja lakini hili la ELIMU isiyokuwa na kiwango. Nashindwa tafsiri yako kama ina maana neno Digri ya Falsafa - Phd, sio kiwango kinachozungumziwa. Nadhani kiwango cha elimu ni hayo majina yaliyopewa hizo elimu na sidhani kama usajili wa shule hizi ktk board mnazozitambua nyinyi ndizo zinazotoa elimu yenye kiwango.
Msomi wa UDSM mwenye masters na yule wa Tumaini wanapishana viwango lakini siwezi kuweka madai kwamba kuna elimu iliyokuwa feki hapa. Isipokuwa nakubali kwamba uangalifu lazima ufanyike ktk utoaji wa ajira kwa wasomi ambao wamechukua digrii zao ktk shule za mtini. Usinielewe vibaya kutumia jina la Tumaini kuwa ni chuo bomu - laah! huo ni mfano tu.

Fikiraduni,
Ndugu yangu mimi siwezi kabisa kusema digrii ya Nchimbi ni feki ikiwa hakuna ushahidi kwamba hakuweza kupata elimu hiyo. Lakini binafsi siwezi kumpa ajira wala kumpa nafasi ya kunifundisha... sijui umenipata. Nimejaribu sana kuepuka ubishi wa Mzumbe na UDSM kwa sababu sifahamu kitu.
Hilo la PWU kuwa chuo feki sijapata kabisa ushahidi wa kutosha kwa sababu ndugu yangu labda hamfahamu naposema Elimu ni biashara...Almasi za Mwadui zilikuwa zimeshuka bei tulipotaifisha na Nyerere alipata kipindi kighumu sana kuziuza kwani zikachukuliwa kama hazina standard inayotakiwa.. jamani hata chafu hazina standard gani?. Lakini leo hii baada ya kurudishwa kwa kaburu zimepanda bei mara kumi lakini hizo hizo Almasi bila mhuri wa Debeers zinaitwa feki!..
Huu ndio mfano unaonishinda mimi kuelewa hiyo feki inatokana na kitu gani?..
PWU kinajulikana kama chuo cha distance learning na kimekita hapo San Diego. Kina branch compuses huko Tokyo, Hong Kong, Taipei, Taiwan na Hanoi.

Mwanasiasa,
Naomba unipe hiyo makala ya Daktari Asaad niisome upya kama ulivyoagiza. Pia nadhani hukuelewa maelezo yangu hapo juu ambayo nilichukua jibu moja kwa maswala mengi yanayolingana ikiwa ni pamoja na hilo la Mh. Dr Asaad. Siamini kabisa kwamba kuna chuo ambacho kinaendesha utoaji wa elimu feki ktk dunia hii ikiwa hakuna mzani wa kimataifa kupima kiwango cha elimu hiyo. Kama kipo nakuombeni mkiweke hapa ili tupate kufahamu vyuo gani digrii zake hazitambuliki duniani kote!
Majuzi tu walikuja wanafunzi toka Finland wakachukua mtihani na wanafunzi wa Marekani wenye kiwango sawa cha elimu. Wa -Finland waligonga wastani wa 80 hali Marekani walikwenda chini ya 50. Ikazungumziwa sana lakini sikusikia mtu akisema kwamba elimu inayotolewa Marekani ni feki, isipokuwa madai yao ni kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.
Kwa hiyo ktk kujibu swali hili na hasa kwa ndugu Sam,
Sidhani kama kiwango cha elimu ni tafsiri nzuri ya neno digrii FEKI kwa sababu vyuo vilivyopimwa Marekani vyote vimesajiliwa na board mnayoitambua.
 
Naona hapa tuko kwenye suala zima la falsafa ya elimu, formal education na informal education... na elimu inapatikana vipi? na tunajua je mtu amesoma (upande mmoja) na ameelimika (upande mwingine)
 
Mzee Mkandara,

Kwanza huu mjadala sio wa UDSM v/s Mzumbe. Ni rafiki yangu Nungwi ndio alitaka kuufanya uwe hivyo. Kama kawaida tukamuweka sawa na sasa ni mmoja wetu.
Shukrani. Nina swali moja. Wewe hauna ushahidi wa COU au the like kuwa vyuo feki. Shukrani tena, ila kinachoshangaza saaaana kwenye maelezo yako, umesema HAUWEZI KUKUBALI NCHIMBI AKU SUPERVISE PHD (kama ungetaka kusomea Phd). Hii ina maana umeshaamua kuwa Nchimbi ana degree FEKI ya Phd.

NO???????????????????????????????????????????

If so why hitting around the bush??. Kama Nchimbi hana Phd feki kwanini usikubali akufundishe?

Nasubiri majibu hasa ukishasoma makala ya Dr Assad. Nimemtumia Dr Assad majibu yako. Akijibu nitaweka hapa akipiga simu nitakueleza anasemaje.

Ramadhan karim

FD
 
As a PhD candidate myself,nadhani kuna tatizo ambalo limeanza kujitokeza huko Bongo kwa academic qualifications kuwa equated with an elevated social status.Baadhi (I insist,baadhi) ya wanasiasa wamekuwa wakikimbilia kutafuta shahada za uzamivu (PhD) kwa manufaa ya kisiasa zaidi kuliko kitaaluma.Focus kubwa ya PhD iko kwenye research,its outcomes and,pengine cha muhimu zaidi,its contribution to a particular academic discipline.

Degree feki,whether ni katika level ya Bachelor,Masters au PhD,kama ilivyo kwa certificates na diplomas feki,hazina tofauti na conterfeit notes.In eyes of a deceived receiver a counterfeit Tshs 10,000 ni fedha halali kwa malipo kwenye transaction husika.Problems arise when he presents the note kwa wenye utaalam wa kubaini noti feki.Lakini kibaya zaidi,especially noti za namna hiyo zikiingia kwenye mzunguko wa fedha,ni athari zake kwa uchumi wa sehemu husika.Degree feki zinaliathiri zaidi Taifa kwa vile wanaozihold hawana uwezo wa kufanya yale yanayotarajiwa na genuine holders wa qualifications hizo.

Nadhani tatizo sio vyuo bali taasisi zetu zenye mamlaka ya ku-authenticate academic qualifications hususan zile zinazotolewa nje ya nchi.Vyeti feki vinavyotolewa na vyuo vya nje sio vingi kama vile vinavyouzwa pale jirani na Billicanas (Papaa Msoffe &co).Mushrooming of institutions offering fake degrees just complies with the laws of demand and supply.

Kwa upande mwingine,research degrees zinategemea sana jitihada za mwanafunzi binafsi when compared to taught degrees.However,that's not to say taught degrees ni "ubwete" kuliko research ones.Mjinga anayechukua PhD while yuko katika academic institution hana tofauti na bubu kwenye fani ya utangazaji.Nadhani ndio maana inakuwa rahisi kwa baadhi ya wanasiasa na wengineo "kuishi kwa amani" na degree hizo kuliko wanataaluma wenye degree feki,simply bcoz while the former do hardly apply their qualifications on day-to-day basis,the latter must.

Finally,while an accredition ya chuo ni muhimu katika authentication ya particular qualification,chuo kilicho accredited hakimaanishi kuwa ndio bora katika quality ya a particular qualification.Na ndio maana tuna wapuuzi kibao ambao wamegraduate Yale,Havard,Stanford,Oxford,Cambridge,LSE au Sorbonne lakini they dont deliver the goods.
 
Hapa tunachoongelea ni uwezo wa chuo kutowa kiwango cha elimu fulani na hivyo basi kutunuku wanafunzi wake shahada zinazokubalika na wala sio mwanafunzi huyo atatumiaje elimu hiyo aliyopata baadaye. Hili la kuonyesha matumizi ya elimu hiyo ni jingine na linastahili lijadiliwe peke yake. Likiongezwa hapa litavuruga mada tu. Watu wenye degree ya vyuo vya Cambridge, Oxford, Havard, Edinburgh, Glasgow, McGill, DSM, British Open University na vingine vingi kama hivyo vyeti vyao havitiliwi mashaka na ni tegemeo kuwa utendaji kazi wao utadhihirisha umahiri wa vyuo hivyo vilivyowasomesha. Na haiwezekani ukapewa PhD ya kusomea ya vyuo hivyo wakati husitahili PhD hiyo kwani checks and balances ni nyingi na za kuridhisha. Tunachoongelea hapa ni mtu au watu kuanzisha "vyuo" vyao binafsi na kumwaga PhD kama njugu vile bila ya kuona aibu ya kusema hivyo - lipa ada baada ya miezi kadhaa umekwisha kuwa PhD eti kwa sababu una uzoefu wa kazi. Hapa ndipo tunaposema kuwa jamaa waliopewa PhD hizo wazinduke na kuwacha kujinaki nazo.
 
Ogah,
Ahsante sana kwa msaada wako na sasa hivi nimeisoma yoteee! sijaona kipya isipokuwa yaleyale ya Utanganyika......KIKOROSHO!
Huyu Dr. Asaad anapofikia kusema kwamba BLA ni accreditor feki sijui ana maana gani?.. Kipimo kipi alichotumia. Na Hivi niulize mathlan tuachane na UDSM, chuo kama Tumaini na vyuo vinginevyo kibao vinavyoanzishwa kila siku wametumia kipimo gani na kuna hakika gani kwamba accreditor wetu nchini sio feki?...What makes a accreditor qouted as fake?
Hapa najaribu kumwelewa anachojaribu kusema pindi anapodai kwamba BLA yenyewe ni feki kwa hiyo lazima COU ni feki, na wapi kweli COU wamesema unaweza kupata degree bila kusoma!
Hiyo address imekuwa kichaa, wanashindwa kuelewa kwamba COU inajihusisha na distance learning tu sii kama PWU ambayo ina faculty na hata kama ingekuwa na majengo mbona PWU bado kaitoa nje?..

Ogah uliposema kuhusu Kabuntas, nakubaliana na wewe sana tu! na hii ndiyo sababu ya jibu langu kwa swali la Fikiraduni.
Fikiraduni,
Makabuntas kibao sana na wengine wamesoma Havard... kwa hiyo napomkataa Nchimbi sii kwa sababu ya COU bali nafahamu kuwa jamaa kainunua elimu toka Mzumbe na nafasi serikalini.
Kuhusu Dr. Asaad, huyu mtaalam kaingia mkenge tu. Kasoma e-mails bila kutafuna kayameza yote kwa jazba.
Kasema:- Commonwealth Open University is not an accredited degree awarding institution by any Commonwealth or US accrediting bodies.
Hapa namnukuu yeye mwenyewe, inaonyesha anashuku accreditation kutoka BLA!..wakati huohuo sidhani kama anaweza kutupa list ya accreditors wote ambao wanatambulika na board zote za distance learning, Uingereza. Naona katumia sana za Kimarekani ambazo pia sidhani kama amekwenda deep ktk kufanya utafiti.
Mfano kawaponda walimu wa Mzumbe kwa kusoma PWU na kuweka madai kama ya Nchimbi ya degree mills. Well, kuna maelezo haya hapa:-
1.The PWU University's degree programs are approved by the State of California's Bureau of Private Postsecondary and Vocational Education, in accordance with the provisions of California Education Code Section 94310 (d) (1) (A). The State of California lists PWU in its' list of Approved California Private Postsecondary Institutions.
2. PWU immediately joined the Association to Advance Collegiate Schools of Business (AACSB) as an Educational Member and it was determined that PWU should seek national accreditation.
Na kibaya zaidi kumshika Asaad accreditor wake anatambuliwa na CHEA ambayo kaiorodhesha yeye mwenyewe. nakuomba akupe jina la accreditor wa PWU kama kweli kafuatilia.
Mlalahoi,
Nadhani umefunga kazi... maelezo yako yameshika pande zote za shilingi na ndio sababu yangu kubwa kushindwa kulaani tu hali kila kona siku hizi ni mpango wa Kanyaboya. Hata JK kapewa yake ya ushikaji US kwa kitu gani basi?..tunu pia zina historia kidogo nyuma yake lakini siku hizi ndugu zangu siwezi kufahamu kabisa tofauti ya nyota na sayari.
Washikaji, Nitarudia tena usemi wangu wa hapo awali, Nilimtafutia sababu nchimbi kwa kila hali lakini nasema nilishindwa! Hizi accreditors ni board za binafsi ambazo zinashikwa na baadhi ya watu (Wayahudi) kama ilivyo board ya Uhasibu. Wanatengeneza fedha kishenzi isipokuwa nitakiri kwamba board za Uhasibu na professional nyingine kidogo zina utaratibu mzuri sana kuliko Academics.
Kuibiwa ndio tumeisha ibiwa! elimu haina hadhi tena zaidi ya fedheha na wala tusichambue COU na PWU kama mabomu, vyuo kibao vinatoa Makabuntas kila siku na vyeti vya nguvu. Kwa hiyo shule ikiwa na fedha ikajenga Mkataba mzuri inaweza sifika kishenzi, na mwanafunzi mwenye fedha leo hii anaweza kusoma Chuo kikuu chochote. kwani hao watoto wa Matajiri hakuna Makabuntas? mbona wote hawasomi vyuo vya akina mlalahoi ispokuwa vile vyenye majina makubwa!
Mshikaji inauma saaana hasa sisi tuliokaa mitihani hakuna cha calculator wala la mzungu kalala (Chagua kati ya ABCD -all of the above). nakumbuka darasa la saba ndio sisi tuliofunga mtihani wa eastafrika na mwisho wa darasa la nane! siku hizi tena na kuwepo mtandao aaaah! mnapeta tu. Ndio mabadiliko haya inabidi sisi tuyakubali laa sivyo ni KIKOROSHO tu.
 
ManjuMakuti said:
Hapa tunachoongelea ni uwezo wa chuo kutowa kiwango cha elimu fulani na hivyo basi kutunuku wanafunzi wake shahada zinazokubalika na wala sio mwanafunzi huyo atatumiaje elimu hiyo aliyopata baadaye. Hili la kuonyesha matumizi ya elimu hiyo ni jingine na linastahili lijadiliwe peke yake. Likiongezwa hapa litavuruga mada tu. Watu wenye degree ya vyuo vya Cambridge, Oxford, Havard, Edinburgh, Glasgow, McGill, DSM, British Open University na vingine vingi kama hivyo vyeti vyao havitiliwi mashaka na ni tegemeo kuwa utendaji kazi wao utadhihirisha umahiri wa vyuo hivyo vilivyowasomesha. Na haiwezekani ukapewa PhD ya kusomea ya vyuo hivyo wakati husitahili PhD hiyo kwani checks and balances ni nyingi na za kuridhisha. Tunachoongelea hapa ni mtu au watu kuanzisha "vyuo" vyao binafsi na kumwaga PhD kama njugu vile bila ya kuona aibu ya kusema hivyo - lipa ada baada ya miezi kadhaa umekwisha kuwa PhD eti kwa sababu una uzoefu wa kazi. Hapa ndipo tunaposema kuwa jamaa waliopewa PhD hizo wazinduke na kuwacha kujinaki nazo.

Mada si inasema "Baadhi ya Lecturers wa Mzumbe wana degree feki",sasa hao lecturers si walikuwa former students kabla ya kuwa lecturers?Na ili uwe mwanafunzi si unategemewa kuwa "mwanachuo"?Sikuelewi na siafikiani nawe unaposema kwamba kuzungumzia matumizi ya elimu waliyopata "kwenye vyuo feki" ni kupotosha mada.Mbona Mkandara amenielewa.Labda kukupa mwangaza zaidi,nimeichambua mada kwa on a theoretical (structure and agency) perspective,if you know what I mean.
 
Mkandara,

Nimekupata sana, na nashukuru mchango wako umeangalia pande mbili.
Maoni yangu ni kuwa na accredition body moja duniani inayo hakiki vyuo na dgree zinazotoa. Kwani hakuna kitu kama hicho?, najua umefanya utafiti kidogo, nisaidie katika hilo.

Ramadhani Karim

FD
 
Mtu anyetamka kwamba ana PhD na huku anajua kwamba "PhD yake" imetolewa na mojawapo wa vyuo vinavyotoa vyeti hivyo kwa fedha na sio kwa elimu ya kweli, ni mdanganyifu. PWU ni mojawapo wa vyuo vya aina hiyo.

Mwaka 2004, chombo cha uhakiki cha serikali ya Marekani (Governement Accountability Office, GAO) kilitoa ripoti, kwa baraza la Senate, iliyosema: "PWU is an unaccredited "diploma mill" for CV cheats"

Likizungumzia PWU, gazeti moja la Marekani, Pacific Business News limeandika "In the academic world it's just about as useless as it can be."

Unaweza kusoma zaidi hapa:
http://quackfiles.blogspot.com/2005/10/degree-of-doubt-for-berties-boffin.html

Kwetu sisi, inabidi kuchukua hatua zifuatazo:

(1) Wale ambao wametoa vyeti kutoka PWU na "diploma mills" nyingine, wafutiwe hizo digrii kwenye CV zao. NI CV CHEATS. Wasifukuzwe kazi, kwani waajiri nao wana udhaifu; walipashwa kuchunguza hivyo "vyuo" kabla ya kuzikubali hizo CV. Waendelee na kazi kwa kutegemea vyeti vyao vingine, mradi viwe vinaridhisha.

(2) Mwajiri ambaye hana uwezo wa kuhakiki usahihi wa digrii anazopewa kwenye CV, awe na uwezekano wa kuzituma kwenye Baraza la Vyuo Vikuu kuhakikiwa (at a fee). Hili baraza liwe na wasomi wa kufanya uchunguzi unaotakiwa, na kutoa ripoti ambayo inajadliwa na kikao rasmi cha baraza, ambacho ndicho kitatoa uamuzi wa mwisho.

(3) Ofisi ya bunge iwe na jukumu la kuhakiki digrii zinazoonyeshwa kwenye CV za wabunge wote. Hiyo ofisi inaweza kutuma hizo CV kwenye Baraza la Vyuo Vikuu ili zihakikiwe. Gharama za kuhakiki wasifu wa wabunge zitalipwa na Ofisi ya Bunge

Augustine Moshi
 
Augustine Moshi,

Mimi ninaafiki kabisa baadhi ya mapendekezo yako kwani shahada feki haswa doctorates ni tatizo lisilositahili uvumilivu wetu. Ni kweli baadhi ya hawa jamaa wana masters nzuri tu na kwa maana hiyo ni wasomi ambao tusingetegemea wadanganywe na "diploma mills" hizo. Kwa maana hiyo wanapotosha elimu kwa makhsudi. Wote hawasameheki kama unavyoshauri wewe kwani huwezi kumuacha VC wa chuo kikuu aendelee kuajiriwa hivyo wakati amejipachika PhD feki - huyu ni wa kufukuzwa kazi mara moja kwani athari za yeye kuendelea na madaraka hayo hasa pale chuo chake kinapojaribu kutunuku PhD za taaluma hiyo hiyo inayotajwa katika doctorate feki yake yeye akiwa ndio mtahini mkuu inakionea chuo hicho nacho kiwe feki. Tukiwalinda hawa jamaa tusije tukalalamika vyuo vyetu hivyo vikiorodheshwa katika list ya vyuo feki vya dunia. Mtoto wa nyani hawezi kuwa simba hata siku moja.
 
Fikiraduni,
Shukran kwamba tumefikia muafaka pia umeweza kuona kwamba nazungumzia pande zote.
Hoja yako ya kuwa na accredition body moja tu duniani nzuri sana, lakini mshikaji hilo haliwezekani kwa sababu elimu ni biashara na biashara yoyote ile wapo walanguzi, na kama nilivyosema huko nyuma uuzaji wa vitabu pamoja na vifaa vya elimu ndio almasi yenyewe sio Elimu kama wengi tunavyofikiri. Hata madawa yetu yanazo body za ajabu kiasi kwamba leo hii wewe ukivumbua dawa ya ukimwi mshikaji haiwezi kupita hata kama inaponyesha. Kwa upande wa pili wa shilingi hiyo hiyo ni kweli wapo matapeli wa madawa wengi sana. Body zinatakiwa kuwepo kuhakikisha madawa haya na bahati mbaya body hizhizi zinafanya biashara na njia za rushwa zinafunguka.
India leo hii inaongoza duniani na Tanzania ni moja kati ya nchi ZINAZOONGOZA kununua madawa feki ya India. Nambie basi kuna maduka mangapi Dar peke yake yanayouza madawa haya hali maduka hayo yana kibali toka kwa hawa wapitishaji. Je, hutuoni umuhimu wa kuzuia madawa hatari kwa maisha yetu maanake hapa hata msomi hana ujanja.
Nikirudi ktk swala la body moja tu, ebu chukulia Marekani wenyewe na tofauti ya hizi mbili kuu. CHEA na USDE ambayo Mh. Asaad hakuiorodhesha. Kuna accreditors ambao wanakubalika na CHEA lakini sii USDE vilevile vise verse. Kisha basi kibaya zaidi hao CHEA ni private company sii ya serikali lakini wamepewa jukumu la kupitisha chuo na gharama za kujiandikisha nao ni kubwa sana yaani mafia tu.
Tazama list zao uone wako wangapi hao accreditors hiyo Marekani tu achana na swala la dunia nzima.
Soma list zao:- http://www.chea.org/pdf/CHEA_USDE_AllAccred.pdf
Halafu tazama hii list ya USDE pekee utachanganyikiwa na biashara nzima kwani hizo hizo zimesajili na accredition body nyingine. kaliwa nani hapa? - sisi tunaotafuta elimu!
http://www.aju.edu/usdoe_accreditation.htm

Nd. Moshi heshima yako mkuu!..
Kuhusu PWU mshikaji nakuomba hiyo hutoba iliyotolewa na GAO kwa senate kuwa PWU ni bomu. Maanake nakumbuka mjadala ule ulikuwa ukizungumzia degree feki zinazotelowa na vyuo ambavyo havikusajiliwa na hawa wafanya biashara ya elimu - Accredition bodies.
Na Marekani inaongoza duniani kwa hao wenye degree feki, wengine wapo bungeni, ma lecturer, madaktari n.k. Bunge liliwekea mkazo kuzifungia shule zote za mazabe lakini bado inashindikana kwa sababu elimu kwao ni biashara na zipo shule ambazo hazitambuliwi kwa sababu tu sii wanachama wa body hizi.
Unajua katika Uhasibu ili uwe mwanachama wa ACCA huko Uingereza inabidi ulipe ada kama pound 1,000 kwa mwaka hata kama umehitimu vizuri masomo yako. Marekani kuna CPA nayo nadhani kitu kama elfu kwa mwaka ili utambulike ama kuruhusiwa kufanya corperate taxes za makampuni. Na ukiacha kulipa basi wanakuondoa ktk list yao na cheti chako hakina mdhamana yaani hawakujui tena na ukikamatwa unaendesha biashara ya kufnga mahesabu ya watu unaweza kufunguliwa mashtaka. Sasa jamani ebu nambieni hii sii biashara?
Mimi nadhani muhimu tuangalie yetu wenyewe na tuombe Mungu TZ iwe na sheria kali ktk shule na vyuo vyetu. Maswala ya Nchimbi ana digrii feki sidhani kama yanaweza kutupeleka mbele kwani Nchimbi ni Nchimbi! awe na digrii ama GDE bado angekuwa hapo alipo.
Kisha Augustine wewe shukuru Mungu hukupitia vichochoro hivyo. Miaka yetu hapakuwepo na imani hii chafu ya fedha!... Vita vyote Kongo, Afghanstan, Iraq, Ivory Coast, Sierra Lione.. U name it yote ni fedha tu. Hakuna cha kulilia ama kutetea haki za wanyonge. Na ndio maana leo hii watu wengi wanashindwa kuelewa Nyerere alikuwa akifanya nini kutuweka vitani bila malipo!.. Dunia imebadilika jamani na lazima tukubali mabadiliko kwani hakuna mtu anapigana vita kutafuta haki.
Kichekesho, majuzi JK alipokuwa NY alikuwa akiitwa Mkapa na viongozi wa Marekani tena basi nasikia kuna kiongozi mmoja alifikiri Tanzania ni visiwa fulani huko Asia.
 
Mzee Mkandara,

Heshima yako mkuu, hiii michango deep isiyokuwa na unafiki wala nia ya ku-WIN! ndiyo iliyokuwa inamiss humu, yes maana sas tumeingia era za kutafuta ku-WIN badala ya kukata issue,

Karibu mzee wangu, na heshima mbele!
 
Mkandara,

Umekata kiu yangu, nimekuelewa sana na nadhani sasa nina Phd kutoka kwenye "diploma mill" yako kwenye uelewa wa hili somo! ahahahah

Swali lingine, Tanzania ifanye nini? Mwalimu Moshi ame suggest na Jizalendo amerekebisha hatua moja wapo. Tunyamaze na kuacha nguvu za soko litawale au?

Asante sana

FD
 
Kwa mtizamo wangu,nadhani it is never too late to redress the situation.Pengine priority ya kwanza iwe kwa taasisi zetu zinazohusika na uhakiki wa qualifications hususan hizo za vyuo vya nje.Kikwazo kinaweza kuwa kwenye "who should lead such an initiative".Ntafafanua.Inafahamika kuwa baadhi ya wenye dhamana ya kusimamia zoezi kama hilo ni watuhumiwa pia.Sasa nani atakuwa tayari kujitia kitanzi yeye mwenyewe?Ukipelekwa mswaada bungeni kuhusu kuhakiki qualifications kuna uwezekano mkubwa hoja hiyo ikauwawa kwa vile baadhi ya lawmakers wetu ni wanufaika wa mfumo huo mufilisi wa qualifications feki.

Yaani ugumu wa suala hilo hauna tofauti na ule wa mapambano dhidi ya rishwa.Tunawezaje kumtegemea mla rushwa aendeshe mapambano dhidi ya rushwa?Tunaweza kuvisamehe vyuo vya nje kwa vile technically inaweza kuwa vigumu kuvibana.Serikali inafahamu sana kwamba ukienda pale Makunganya au Mkwepu unaweza kuondoka na cheti chenye first class ya Mlimani bila ya matatizo,na wahusika wanajulikana sana (hey,si watu wanajua syndicate ya Papaa Msofe na forgery ya documents).

Nadhani sote tunakumbuka ile sakata ya documents zenye muhuri wa Ikulu...imeishia wapi!!!Well,wahusika ni breed flani ya "untouchables" kwa vile wana mizizi kwenye kila kona,na wameshaiga ujanja wa matajiri wa nchi za magharibi wa ku-invest kwenye wanasiasa.Wanafanya hivyo kwa vile wanajua kuwa pindi watapowahitaji wanasiasa hao kwa ajili ya fadhila flani,watazipata.

Moja ya sura chafu ya utandawazi ni interaction between crooked suppliers (mfano vyuo vyenye kutoa degree feki) na crooked customers (mfano hao wanaotafuta na "kununua" shahada feki).Ni ile ile hadithi ya nani alaumiwe kati ya mtoa rushwa na mpokea rushwa.

Neglecting vikwazo hivyo (kama hilo linawezekana),serikali inapaswa kuiboresha ile bodi inayohusika na uhakiki wa qualifications (nadhani bado ipo),kwa mfano kuipatia nguvu za kisheria za kuwaadhibu wanaogundulika kuwa na qualifications feki.Kwa hali ilivyo sasa,mamlaka hiyo imeachwa kwa waajiri ambao kimsingi hawako well equiped kutekeleza jukumu hilo.

Again,uzalendo unahitajika sana ktk suala hili kwa vile mtu anayemwajiri mhitimu feki ilhali anajua anachokifanya,analihujumu Taifa hata kama madhara yake hayatoonekana mwaka huu.Quote my words,uchaguzi mkuu ujao utashuhudia ma-Dr kibao wenye qualifications tata,kwa vile,mosi,wapo wanaowaona ma-Dr feki wakipeta bila tatizo na pili nani mwenye kiu ya kupata u-Dokta ataachia fursa isiyo na kikwazo ya kuupata bila kuutolea jasho?[Na hapa "u-Dokta" as a qualification unatumika tu kama kiwakilishi cha qualifications nyingine including certificates,diploma,etc...Dr feki kwenye siasa is relatively less dangerous compared to nesi mchoma sindano aliye kihiyo na anabahatisha tu kubaini ni wapi kwenye veins]
 
Mlalahoi,

Na mimi nimetuma hela jana, baada ya wiki kama nne nitakuwa Dr.!
Kwasababu serikali yetu imeruhusu, basi na mimi nimeingia humo.

Tena naomba muache kutujadili, nikishaupata u dr basi narudi bongo, ajira serikalini. Upo hapo?

FD
If you cant beat them join them!
 
Fikiraduni,

Nadhani niliwahi kuandika kule Bsctimes kwamba ili Tanzania tuweze kuepuka fedheha hii ya elimu ni bora tuige nchi za wenzetu Unapotoka nje na digree yako. Tuwe na Body zetu wenyewe za kuhakiki vyeti kwa kuweka mitihani na muda wa kuhakiki cheti hicho usipungue mwaka mmoja. Hapo zamani Uhasibu walikuwa na NBAA peke yake, sijui siku hizi kama bado wana nguvu tena maana nchi yetu ipo sokoni kujiuza.
Na itakuwa kazi ngumu sana kuhakiki taasisi zote za elimu kwa muda mfupi, sababu nchi yetu maskini na inategemea sana elimu hata iwe ndogo kiasi gani tofauti na Ulaya ambao wanao muda wa kuwatihani watu na hata kuweka miaka isiyopungua mitatu kuchunguza cheti cha mhusika.
Kwa hiyo nchi kama Canada hata uwe umesoma Havard huwezi kuitumia elimu yako bila kutambuliwa na body husika na ktk miaka hiyo mitatu utabadilishiwa waangalizi mara kibao na kuitwa mitihani sii mara moja. Daktari aliyefuzu London ama Cuba bado sii daktari lazima apitie mitihani yao. Nurse vilevile ukitoka Mhimbili na kigrii chako mshikaji utabeba box kama hukufuatilia usajili - ambao ni miaka mingine darasani na mithani.
Tatizo kubwa nchi maskini body kama hizi hazina tafsiri nyingineyo isipokuwa KULA - Rushwa. Tumeyaona ktk Ubinafsishaji - Mwinyi na akina Ami Mpungwe; Uwekeshaji - Mkapa na akina Sumaye; sasa hivi JK - Uuzaji wa nchi yetu. yaani tunainadi nchi hadi ktk wallstreet mshikaji hapo kuna quality tena?...
Demand huendesha soko na sii quality tena kwa hiyo lazima twenda na wakati. Quality inahitajika lakini pale inapokosekana kabisa. Ule mpango wa sisi kudai kuvaa Armani tu haupo tena na tunapata taabu sana kuweza kukubalika ktk dunia hii ya akina Sean na Fubu. Siku hizi hata mitumba ndio poa, haya brand name zote zinatengenezwa China kwa mali ghafi hafifu na feki tupu. nimekataa kwa miaka kibao kutovaa nguo zilizotengenezwa China lakini waapi, nimekubali mwenyewe kushindwa na mabadiliko haya. Leo hii sitazami tena nguo inatengenezwa wapi..kama ulivyosema hapo juu - If U can't beat them, better join them.

Hadi itakapo fika serikali kuona kwamba Wakenya na wageni wengi wamejaa nchini hawana elimu ya kweli inabidi Mtanzania ushindane na wageni nchini mwako. Vyeti vyao feki wanachukua kazi zetu sasa wewe kama umeamuwa mshikaji kujipa digrii ya uongo poa kabisa (for now). ULIMBUKENI wetu wa kutofahamu kwamba lugha ya kiingereza sii kiwango cha ELIMU ya mtu umetuponza. Tumeifanya lugha ya kiingereza kuwa kitambulisho cha ELIMU, bila kuweka body za kuhakiki vyeti vya wahusika. Wageni wote hasa nchi za Nigeria, Kenya na Uganda kiingereza ni lugha ya kwanza ktk familia nyingi kwa hiyo rahisi kabisa kuweka madai ya kuwa wasomi.
Sidhani kama TZ watu wengi wanafahamu tofauti kati ya msomi aliyehitimu, aliyehudhulia na mwisho mtu anayezungumza kiingereza. Hii inabidi tufanyike kipindi maalum cha TV maanake Wageni wanatupiga sana mabao inapofikia ELIMU.
 
Back
Top Bottom