Baada ya Wema kumwaga, Diamond nae amwaga haya...

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
kweli Wasanii wa Bongo hamnazo:



KUFUATIA mafanikio alinayoyapata hivi sasa kwenye anga ya muziki wa kizazi kipya Bongo, staa wa muziki huo Naseeb Abdul ‘Diamond' ndiye mkali aneingiza mkwanja mrefu zaidi kuliko nyota wote wanaotamba hivi sasa hapa nchini.
Uchunguzi uliofanywa na Teentz.com umebaini kuwa Diamond anaingiza kiasi cha shilingi za kibongo Milioni 16 kwa kila shoo mbili anazofanya akiwa ndani na nje ya jiji la Bongo.


Katika kuhakikisha kuwa ukweli unapatikana Teentz ilimsaka Diamond na baada ya kufanikiwa kumpata alikiri kufikia kiwango hicho .
"Nashukuru Mungu kwa kufika hapa na ukweli ni kuwa nalipwa mkwanja huo na hii imekuja kufuatia kuweka nguvu zangu katika muziki na kufanya vitu vizuri kwa kuwa gemu ndiyo maisha yangu" alisema Diamond.


Akiendelea zaidi nyota huyo wa ‘Songi' la ‘Mawazo' alianika kuwa mafanikko haya yanakuja pia kutokana na sapoti anayoipata kutoka kwa watu wake wa karibu akiwemo Mama yake mzazi na wengine kibao.


Hapa chini ni mkataba ambao amelamba kutoka kampuni ya Emilates Hall kupiga shoo huko pande za Mtwara
attachment.php



http://kapingaz.blogspot.com/2012/06/hakuna-kama-diamond-cheki-na-moja-ya.html?spref=fb
 

Attachments

  • DIAMOND.jpg
    DIAMOND.jpg
    56 KB · Views: 2,595
Kwani kulikuwa na ulazima wa kumuandika WEMA katika habari yako au na wewe nawe ndio walewale gazeti haliwezi uzika mpaka liwe na kichwa cha kinoko noko??
 
Kama kuna mtu wa TRA humu na ni mzalendo afuatilie tupate chetu kwa njia ya kodi tafadhali.Si sahihi kuvuna pesa za wananchi bila kulipa kodi.Moja ya mambo yanayowasumbua TRA kwenye kukusanya kodi ni watu/taasisi/makampuni kuficha mapato yao halisi .Sasa huyu amekuwa muwazi kuweka kipato chake ,TRA mpo wapi ?ama mnasubiri mkusanye kodi kwenye beer na sigara!!!?
 
Jamani mimi naomba kuuliza tu, hivi na nchi nyingine kuna majitu majinga na mazembe kama hapa kwetu au ni sisi labda tumelaaniwa?
What is this!?....
 
We uliyeleta mada unaingiza shilingi ngapi kwa siku kwaajili ya familia yako na we binafsi.?

Kila mzalendo amwage humu anaingiza kiasi gani yeye na familia yake??

Diamond na Wema wamemwaga kwenye vyombo vya habari kuwajulisha watanzania wenzao kuwa wanaingiza/wameingiza ngapi..

A wise, grown-up and responsible person can not do that my friend!!!,

who cares kama si ulimbukeni!!?
 
mkataba mbovu ajabu, hivi tuhela take huto hanaga wanasheria wa kumsaidia kuingia mikataba, au anasubiri hadi apate tatizo kubwa ndo awe nao....manake mkataba huo umeeandikwa na mtu lay man mno....
 
Nauliza Wema anahusikaje na huu mkataba..........Hujanijibu swali langu bado..........

Mkataba aingie Almasi kumwagana na Wema kunatoka wapi sasa????
 
Back
Top Bottom