Baada ya umeme, mafuta nayo juu

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
WAKATI gharama za umeme zikiwa zimepanda wa asilimia 18.5 kuanzia Januari Mosi, mwaka huu, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), pia imetangaza rasmi kupanda kwa bei za mafuta ya Petroli vituo vyote nchini.

Katika taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari jana na kusainiwa na mkurugenzi wake, Haruna Masebu, inasema bei hiyo mpya ilianza kutumika rasmi jana kwenye vituo vya mafuta.

Inasema bei ya jumla na rejareja zimepanda ikilinganishwa na toleo lililopita la Desemba 22, mwaka jana ambapo bei ya rejareja kwa petroli imepanda kwa asilimia 3.41, dizeli imepanda kati ya asilimia 4 na 5.07, na mafuta ya taa asilimia 6.33.

Bei ya jumla ya petroli imepanda kwa asilimia 3.54, dizeli asilimia 5.13 na mafuta ya taa 6.68.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, kupanda kwa bei hiyo kunatokana na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo soko la dunia, na kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania.
http://www.mwananchi.co.tz/biashara/-/8099-baada-ya-umeme-mafuta-nayo-juu

"Kwa mujibu wa sheria ya mafuta ya mwaka 2008, bei ya bidhaa za mafuta na petroli zitaendelea kupangwa na soko, Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei elekezi za bidhaa za mafuta na bei kikomo," inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kutokana na kuwepo kwa ushindani katika uuzaji mafuta nchini, taarifa hiyo imetoa tahadhari kwa kampuni za mafuta kwamba, zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani, lakini ziwe chini ya bei kikomo.

"Wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo, ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika," inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo bei kikomo na elekezi ya petroli jijini Dar es Salaam ni Sh1,722 na 1852, Arusha Sh1,806 na 1,942, huku dizeli ikiwa Sh1,730 na 1,860 jijini Dar es Salaam na Sh1,814 na 1,950 kwa Arusha.

Dodoma bei ya petroli itakuwaSh1,781 na 1,915, dizeli ikiwa Sh1,789 na 1,923, Kigoma petroli Sh1,953 na 2,100, huku dizeli ikiwa Sh1,961 na 2,109, Mwanza dizeli ni Sh1,880 na 2021.

source:http://www.mwananchi.co.tz/biashara/-/8099-baada-ya-umeme-mafuta-nayo-juu
 
source:Baada ya umeme, mafuta nayo juu

Asante kwa taarifa, lakini nina kaswali kadogo tu! Wadau naomba mnisaidie, kwa kuwa bei ya umeme na mafuta vimepanda, Obvious kilakitu kitapanda zikiwemo nauli za kusafili hapa na pale, JE, UWURA ya Wafanyakazi itatangaza lini nyongeza ya mishahara ili kuendana na hali halisi ya maisha?.

Au ndo imetoka? NAomba msaada wadau.
 
Back
Top Bottom