Baada ya Ulimboka, Je Mnyika atasalimika?

Status
Not open for further replies.

Head teacher

JF-Expert Member
Mar 10, 2012
1,796
411
Nimeanza kuingiwa na hofu juu ya usalama wa wananchi wazalendo wanao pigania haki na rasilimali za watanzania dhidi ya watawala wa CCM walioinyonya nchi yetu kuliko wakoloni weupe walivyotuibia.
Madai ya madaktari ni ya msingi kabisa, kwa mfano kwa zaidi ya miezi 7 hospitali ya muhimbili haina CT scan, gharama ya kununua CT scan ni kama shilingi milion 250 tu. Serikali, kama isingekuwa dhaifu ingeweza kuahirisha safari moja tu ya Rais, badala yake aende waziri, fedha za safari zingetumika kununua vifaa vya hospitali. Mpango wa kumuangamiza Ulimboka unatia shaka zaidi kwamba Serikali yetu si tu dhaifu bali na ni goigoi, na iliyoishiwa fikra. Mhe. Mnyika aliposema rais DHAIFU, CCM puuzi, nilikuwa napingana naye. Lakini sasa si tu kwamba nakubaliana na Mnyika bali namtahadharisha Mhe Mnyika kuishi kwa uangalifu mkubwa. Tena ikibidi atafute walinzi wasiopungua SITA wenye weledi mkubwa wa ulinzi
 
How long shall they kill our prophets while we stand aside and look! GAMBA LINATEKETEA NA SERIUALI. CCM inaponwa na huyu aliyepata uraisi kupitia kwake!
 
Wako wengi hao, ukitoa mmoja, wanakuja kumi, ukitoa kumi wanakuja mia NK. Muulize gadafi huko alikokimbilia.
 
mungu ni mwema,ndiyo maana hata gr hajafa ili waweze kuelezea uma kilichomtoke.so mazalendo tuendeleze jitihada za ukombozi wa nchi yetu,wale waombaji nawaombe dua na sala kwa taifa hili.maana utashina vyote lakini mungu akisimama hakuna wa kumpinga.
 
Usiwe na hofu mkuu serikali haiwezi.

Yan sitaki kufikiria kama wanaweza kujaribu, sasa wataua wangapi?

Yan hawawezi kugusa huo moto.
 
wamguse Mnyika waona kama kutakalika magogoni ....yaani kama wao wanaume kweli wampige hata na manati waone mtiti wake
 
Hitasaidia?Kumbuka ujumbe wa Osama kwa wamarekani kuwa hata wakimuua yeye marekani watabaki salama.....coz osama2 wameshazaliwa wengi tu
 
How long shall they kill our prophets while we stand aside and look! GAMBA LINATEKETEA NA SERIUALI. CCM inaponwa na huyu aliyepata uraisi kupitia kwake!

Haiingii akilini kwa binaadam yeyote mwenye fikra japo kidogo, eti Serikali wakuchukuwe, wakupige, wakutupe Mabwepande halafu waje haki za binaadam kukuota.
 
Mkwawa walimua wakaamua kubeba na kichwa chake.Lakini walibuka akina Nyerere,Kwame Nkuruma,salmola machela
Some history kama hamjalewa madaraka na utajiri wa kifisadi.
Nasema mnaamini ngiza
 
Yaani mnasubiri mpaka wamguse Mnyika ndipo pasikalike, hili tu la Dr Ulimboka linatosha kuanzisha tiff la kuwachomoa watu kwenye vyeo vyao.
 
Wajaribu waone,huo upuuzi wao tutauondoa hata kwa mbinde. Hata kama raia walioko dsm watakaa kimya sisi wengine toka Mbeya,Mwanza,Arusha,Iringa,n.k tutajua la kufanya.Ulimboka ni ndugu yangu and I am stressed enough to participate in a movement against the government,Those who dead during the strike are my friends,relatives,e.t.c This is all because of poor governance under ccm.I am tired!
 
Ina maana mbaya wa dk.ulimboka rais? Jamani tusifike huko ya mnyika ni ya mnyika na ya ulimboka ni ya ulimboka.katika hili si vema kumumhusisha president ni hatari sana.kwani alivyosema mnyika ile ni siasa na kuhusu dk. Ulimboka huyu ni mtaaramu,hivyo tusitengeneza mazingira ya uhadui ndani ya nchi kupitia viongozi wetu hawa.yawezekana waliomteka dk. Ni wahuni tu ambao wametaka kudhihirisha kauli za wanasiasa juu ya kile wanachokisema udhaifu wa serikari ili ionekane kwamba kweli serikari hii ni ya kidhalimu.
 
kabla ya kusubili wamguse mnyika tunatakiwa kutake action nau, kwa ksema inatosha.
 
acheni uchochezi. mwenye ubavu aende ikulu akaandamani kesho. atakiona chamtemakuni. waislamu wakilalamika kila siku na kuandamana wanaitwa wajinga. sasa maandamani ya nini!? tulieni. huu ni upepo utapita
 
Watanzania msilalamike mliyataka wenyewe! Hiyo serikali mnayoilalamikia haikuingia msituni na kutwaa madaraka! Ni ninyi wenyewe kwa ushabiki wenu wa Yanga na Simba katika siasa mlipiga kura kama vipofu. Tulieni mkamuliwe vizuri hadi hapo mtakapopata mang'amuzi mwaka 2015.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom