Baada ya tamko la polisi majambazi wapora Sh40m kweupe Dar

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,003
Date::3/17/2009
Baada ya tamko la polisi majambazi wapora Sh40m kweupe Dar

Festo Polea na Hidaya Kivatwa
Mwananchi

Siku moja baada ya Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar es salaam, Suleiman Kova kutangaza kuunda kikosi cha kupambana na uhalifu wa aina zote, watu watatu, wakiwa na silaha, jana walipora zaidi ya Sh40 milioni kwenye duka maarufu la Kariakoo Barzaar na kutoweka nazo.

Kova alikuwa ametangaza kuunda kikosi maalum cha askari ambao wamepewa mafunzo maalum ya kupambana na uhalifu, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliyetaka wahalifu katika soko la Kariakoo, stendi ya Ubungo na sehemu nyingine washughulikiwe na jana majambazi hao walifanya uporaji huo kwenye maeneo hayo ya Kariakoo.

Majira ya saa 3:45, majambazi hayo manne yalimvamia mhasibu wa duka hilo la Kariakoo Barzaar Ltd, Kishori Sheti na kufanikiwa kupora fedha taslimu karibu Sh 40 milioni na kusababisha kizaazaa kwenye Mtaa wa Swahili na Narung'ombe, eneo lenye watu wengi.

Mara baada ya kupora, wamiliki wa duka hilo walijaribu kulifukuza gari lililowabeba majambazi hao wakati wakitimka, tukio lililoonekana kama maigizo.

Watu walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa, majambazi hao waliokuwa wakitumia gari aina ya Toyota Corolla iliyokuwa na namba T429 AAT walimshambulia mhasibu huyo mara baada ya kushuka kwenye gari akitokea katika duka lao jingine lililo Mtaa wa Livingstone na Maina akiwa amebeba begi lililokuwa na fedha zilizoporwa.

Kwa mujibu wa mashuhuda, kabla mhasibu huyo mwenye asili ya Kiasia hajafika dukani, alivamiwa na watu watatu. Watu wawili kati yao, walijaribu kuvuta begi hilo, huku mwingine aliyesalia akimtishia kwa bastola.

Tukio hilo mfano wa sinema liliendelea kwa dakika kadhaa ndipo mlinzi wa mhasibu huyo aliyefahamika kwa jina la Joseph Hassan, aliyekuwa amebaki ndani ya gari ambalo 'bosi' wake alishuka, alitoka na kupiga risasi hewani.

Baada ya kusikia mlio wa risasi majambazi hao nao walijibu mashambulizi kwa kupiga risasi mbili hewani kwa lengo la kumtisha mlinzi huyo na kufanikiwa kupora begi hilo na kuingia kwenye gari lao na baadaye kutoweka, wakimuacha mlinzi huyo akipiga risasi kuelekea kwenye gari la majambazi hao na kupasua kioo cha nyuma cha gari hilo.

Hata hivyo, juhudi za mlinzi huyo kuokoa fedha hizo ziligonga mwamba na majambazi hao kufanikiwa kutoroka huku wakifyatua risasi hewani wakati wakifuatwa na wafanyabiashara hao waliokuwa na gari aina ya Toyota Double Cabin.

Mkurugenzi wa Kariakoo Barzaar, Nurdin Abdallah alisema gari hilo lilifanikiwa kutoroka, lakini wakiwa katika juhudi za kulisaka ghafla walisimamishwa na gari la polisi ambao walihofia kuwa ni majambazi.

“Tulishangaa kusimamishwa ghafla na polisi wakitushuku sisi ndio majambazi na baada ya kutoa maelezo walituachia, lakini wakati huo wezi wale walishatuacha mbali hivyo hatukuweza kuwaona tena,” alisema mkurugenzi huyo akionekana kushtushwa na tabia hiyo ya polisi kutojiunga nao kwenye msako.


Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alikiri kutokea kwa uporaji huo na kuongeza kuwa gari lililotumiwa na majambazi hao pamoja na watu wawili wanaoshukiwa kuwa walihusika kwenye uporaji huo, wameshakamatwa.

“Ni mapema mno kutaja majina ya watuhumiwa hao kwa kuwa ndiyo kwanza tumeanza kuwahoji ili kufanikisha kuwapata watuhumiwa wengine waliohusika,” alisema Kamanda Shilogile.

Kamanda Shilogile alisema inasadikiwa kuwa risasi iliyopasua kioo cha gari la majambazi hao, ilimjeruhi mtu mmoja aliyekuwa ndani.

Alisema licha ya kukamatwa kwa watu hao wawili wanaoendelea kuhojiwa na polisi, watu wengine watatu waliokuwepo katika duka hilo ambao wanahisiwa kuhusika katika kupanga tukio hilo la uporaji, wanashikiliwa na polisi.

“Tunawashikilia pia watu watatu kutoka katika duka hilo ambao nao huenda wamehusika kwa namna moja au nyingine kufanya mipango iliyofanikisha uporaji huo, kwa kuwa hakuna mtu anayejua kuwa wakati huo jamaa hao walikuwa na fedha isipokuwa watu wa ndani humo. Hivyo nao tunawahoji,” alisema Kamanda Shilogile.

Matukio ya ujambazi yalishamiri mwanzoni mwa mwaka 2006 kiasi cha serikali kuamua kuchukua hatua madhubuti za kuukomesha, ikiwa ni pamoja na kuwaweka chini ya ulinzi maalum baadhi ya watu waliohisiwa kuwa wanafadhili wahalifu hao.

Hatua hizo zilisaidia kupunguza kwa ujambazi, lakini kuanzia mwishoni mwa mwaka jana vitendo vya uhalifu huo vilianza kurejea na wakati fulani majambazi walidiriki kupora mchana kwenye masoko ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Katika hatua nyingine, Kamanda Shilogile aliwataka wafanyabiashara na wananchi kutumia jeshi la polisi wakati wanapotaka kusafirisha fedha zao na kuachana na kujiamini kupita kiasi.

“Msijiamini... tumieni polisi wetu kwani tulishatoa wito huo wa kutumia polisi wetu katika harakati za kusafirisha fedha, lakini hadi leo watu wengine hawatumii. Wanajiamini wakati majambazi wana silaha za moto ambazo zinawafanikishia uhalifu kama huo wakati wowote,” alisema.
 
Pamoja na tamko hilo la polisi la kutoa huduma ya ulinzi watu wanaposafirisha pesa nyingi, pia ni jukumu la wale wenye kubeba pesa hizo kujiwekea ulinzi kamili wenyewe ili kupunguza au kuzuia kabisa matukio hayo ya kuporwa pesa. Siku hizi kuna vifaa mbali mbali ambavyo, ukivinunua kwa pesa kidogo tu, unaweza kuokoa mamilioni ya pesa. Vifaa hivi ni kama kuweka security cameras ndani na nje ya jengo lako ili kunasa matukio, na pia kuwa na vyombo maalumu vya kubebea pesa ambavyo vitawazuia majambazi kukimbia na pesa zako. Kifaa kimojawapo ni 'Security Briefcase' ambayo mtu akikupora, mwizi yule atapata sawia mshtuko wa umeme mkubwa ambao utamfanya asijiweze tena. Hebu soma maelezo yake:

[B]Function [/B]
It can emit high-voltage pulse electric shock from all direction of the surface for protection, The high-voltage pulse output power voltage exceeds 30 kV. It has the function of remote radio control. You can turn on or off the switch at random by radio control remotely.
It has the functions of "anti-loss-proof", "theft-proof" and "anti-robbery":


Anti-loss " is a unique special function of the super safety suitcase. When traveling, In order to avoid being stolen or forgotten, you can set the suitcase on "loss-proof" function, and bring the remote controller with you. Once the distance between you and the suitcase exceeds 3-15m, an alarm will go off automatically to remind you. If you find your suitcase has been stolen, set "robbery-proof" function to force the thief to leave it.

Theft proof function
On "Theft proof" mode, both the sound alarm and whole surface high-voltage pulse electric shock will simultaneously be effective. The sound level exceeds 85db; electric shock power voltage exceeds 30 kV.

When you need to go far from your suitcase for settling other businesses, you shall just set it on "stealing-proof" model, bring the remote controller with you . In case the robber or thief touches any place of the suitcase, alarm will ring and trigger electric shock. Even when the owner is absent, the robber and thief can steal the briefcase.

Anti-Robbery function
On " Anti-Robbery" mode, one being robbed, both the functions of sound alarm and whole surface high-voltage pulse electric shock will become effective at the same time. The sound volume exceeds 85db and electric shock power voltage exceeds 30kV. Remote control distance exceeds 50m.

If you are threatened by the robber, for protection, you shall give it up first, Once the distance between you and the robbery within 50m, you can set the "anti-robbery" mode by the remote controller. The alarm will ring and high-voltage electric shock will take effect, which can force the robber to leave it and run away.

Technical Specifications
Anti-losing ("loss-proof") effect distance 3~15M
Anti-robbing ("robbery-proof") longest effective distance: 50m
Electric shock high voltage pulse power supply>30KV
Alarm sound level>85dB
Power supply:
Transmitting remote box:1 type 23A/27A battery with 12V voltage
Alarm electric shock device: 6 size-2(type C) super alkaline batteries with 7.2-9V voltage, or 6 size-2(type C) chargeable batteries.

Case Body
The case body is a special code file-case, covered with PVC or leather material and equipped with double code locks.


Kama una maswali zaidi kuhusu kifaa hiki au vifaa vingine vya usalama, nitumie PM.
 
Back
Top Bottom