Baada ya Posho Mbili kwa Kazi Moja, Sasa ni Pensheni Mbili!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Wakati vumbi la posho mbili kwa kazi moja halijatua sasa limeibuka tena suala la watumishi wa serikali kulipwa pensheni mbili Serikalini na kwenye Chama! Taarifa za uhakika zinataja orodha ndefu ya viongozi wa CCM ambao tayari wamepokea pensheni katika Chama na wanasubiri, au tayari wamepokea pensheni serikalini! Kwa mujibu wa taarifa, mbunge wa Mlalo Hassan Ngwilizi tayari amelipwa pensheni kwa "kukitumikia chama" chake katika kipindi hicho hicho ambacho alilipwa pensheni ya Bunge! Ngwilizi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM. Pia Mbunge wa Handeni Dkt Abdallah Kigoda ambaye amepokea Pensheni Bungeni na Serikalini! Mbali na Pensheni Dkt Kigoda na Ngwilizi walikuwa wakilipwa na CCM posho ya Tsh 40,000 kila siku ambazo walikuwa DSM kwa hoja kwamba kituo cha Ngwilizi na Kigoda kilikuwa ni Dodoma kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa CCM! Balozi wa TZ nchini Urusi Jaka Mwambi amelipwa TSh 16,320,000 zikiwa pensheni kwa kuitumikia CCM tr 28 Novemba 2007 kwa hundi # 062332 ya CRDB! Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Aggrey Mwanry alilipwa Tsh 3.7m/- kwa hundi #062333 ya CRDB ikiwa ni pensheni ya CCM huku akilipwa pensheni ya Bunge! Rostam Aziz amelipwa TSh 3,520,000 tr 10 Desemba 2007 kwa hundi #062331 ya CRDB ikiwa ni pensheni ya utumishi wa NEC, Fedha na Uchumi. Wengine waliolipwa pia pensheni na Bunge ni Salome Mbatia, Omar Ramadhan Mapuri! (Source: MwanaHALISI, Nov 4-10, 2009, uk. 2).
 
JK anaweza kuchukua muda akatolea ufafanuzi ama Hosea akasema ni lini atawahoji hawa watu ? Au pesa hizo hazihesabiki kama za wananchi?
 
Kama wanalipana kwa fedha za kwao CCM sioni ubaya, ila kama zinalipwa na serikali that's issue!
 
Kama wanalipana kwa fedha za kwao CCM sioni ubaya, ila kama zinalipwa na serikali that's issue!

Kwani hujui CCM wanapata pesa toka serikalini kama chama cha siasa, ukiachilia mbali zile zinazopika kwa makampunu kama Kagoda
 
Kwani hujui CCM wanapata pesa toka serikalini kama chama cha siasa, ukiachilia mbali zile zinazopika kwa makampunu kama Kagoda

Sure, kuna ruzuku kwa vyama vya siasa toka Serikalini ambapo CCM inapata "lion's share!" Sasa ruzuku hiyo haitokani na fedha za walipa kodi?
 
katika kuishi wakati wote kuna vipaumbele na mambo muhimu,unajua kuna watu wanatutega wanataka tusahau mambo ya muhimu zaidi yanayotusumbua.huu ni mkakati maalum wa akina lowasa rostam hosea wa kuhakikisha mambo nyeti hayajadiliwi kwa hiyo wanajaribu kupenyeza ishu katikati ya ishu nzito.wanataka tusahau richmond,meremeta,kagoda,deep green wanaamini watz tunaendelea kudanganyika....''HATUDANGANYIKI'' hatukatai kuwa wabunge hawalipwi posho zaidi ya inayostahili hilo lipo na wabunge kwa jinsi wanavyojitetea wanakili kwa shingo upande kuwa yapo .....sasa tunachotaka sisi sio kupeleka watu mahakamani tunataka waibaji hao wote wafilisiwe mali zao zikamatwe.....katika kipaumbele hawa kagoda,richmond na vikaragosi vingine ndio ishu yetu muhimu zaidi kwa sasa tukimaliza hawa na kwa kuwa document zipo hawa wa tuposho watashughulikiwa tu.....samahani sana akina lowasa na rostam tunajua nyie ni wasomaji sana wa jf lakini wenzenu tumechoka kwa nini mnatuzungusha sana vichwa vyetu? lakini aminini msiamini,mwisho wenu waja na sasa umeshakuwepo kaa chonjo...
 
Jile79: Ikitokea ishu ya ufisadi sasa hivi iwekwe pembeni ETI kwa kuwa kuna Richmond, Meremeta, Deep Green, etc? Au kwa sababu "wapiganaji" nao wameguswa pabaya ndio wanataka sympathy ya wananchi? Vita vipiganwe kotekote sio wengine wakiguswa inaonekana ndio "wateule" na hawagusiki wako juu ya sheria hata kugomea vyombo vya dola!
 
Wadau bado mnatafakari? Naona michango imepungua!
 
sheria za nchi inaruhusu...so angalieni kwanza laws to reform..
 
Hela za CCM sio pension, jaribu kutafuta maana ya pension and Retirement benefit.
 
Back
Top Bottom