Baada ya polisi kuzima maandamano ya waislamu "sporadic violence" is now imminent

Kitabu kitakatifu kwa aliyekikojolea au kwa aliyekileta kikojolewe? Ni sahihi kuchukua kitu unachoamini kuwa ni kitakatifu nyumbani kwenu ukampelekea mtu asiyeamini katika utakatifu wa hicho kitabu akikojolee? Mimi naona mngeanza na huyu aliyetoa nyumbani kwao kitabu kinachoitwa kikatatifu kikakojolewe.

Nimejiuliza sana kwenye hii point yako, lakini naona hamna aliyetilia maanani kabla. Sijui naye wamemuonya au ameachwa kama hero! Manake hachelewi kumpelekea mtoto mwingine tena!
 
Nikukipiga marufuku kikundi cha kikristo kinachoitwa SIMBA ULANGA kinachokashifu uislam na mtume wake

Mkuu kuleta amani pande zote, nafikiri vingepigwa marufuku vyote hata vile vya uislam vinavyokashifu ukristo. Ingawa huwa nasikia vikundi hivi vinajuana na malengo huwa ni source ya sadaka, sijui kuna ukweli?
 
Sasa tunaelekea ktk kutunga katiba mpya,cha msingi kiwekwe kipengele kinachozuia dini moja kuzungumzia dini nyingine.
Pili,wale waislamu walioenda shule kama mimi uwez kutukuta tunafanya ujinga kama huu hao ni wale ambao hawahujui ata uislamu wenyewe.wanajazwa maneno bila kuyapima kujua ukweli wake wao wanakurupuka,tujue baadhj ya viongozi wana ajenda zao na wanatafuta umaarufu. WAISLAMU TUJICHUNGE.
 
Viongozi wa nchii hii wanapaswa kutafuta suluhu ya matatizo haya yanayosababisha maandamano na machafuko kwa kutafuta kiini hasa cha tatizo hili vinginevyo amani ya nchi yetu itakuwa tumeiweka rehani.

Kama kuna watu wanatumika na mataifa ya nje kuvuruga amani ni bora hatua za kuwadhibiti zichukuliwe mapema vinginevyo nchi yetu itageuka iran,afghanistan,iraq na kwingineko.

Usalama wa taifa hapa ndio wanajukumu kubwa na kama hili litakuwa gumu basi tutarajie muendelezo wa matukio kama haya siku za usoni.

Sectarian violence could cause civil war if it goes unchecked.

Mkuu me naamini matatizo haya viongozi wetu waliyajua lakini yalikuwa na faida kwao kisiasa kujihalalishia kutawala bila kujali kuwa mbinu hii ni ya hatari sana, si kwetu tu bali hata kwao pia! Harakati zilizoendesha misikitini kwamba dk. Slaa ni mkatoliki na kwamba angechaguliwa ingekuwa sawa na kuuchagua ukatoliki wakati wa kampeni za 2010, pia kutuaminisha kwamba CUF ni chama cha waislamu na ambaye angekichagua angekuwa amechagua uislamu zilikuwa ni mbegu mbaya sana za udini kuwahi kupandwa! Mbegu zile ziliota, zikapaliliwa na vyombo vyao kama redio Imaan, gazeti la alnoor na mihadhara ya dini iliyolenga kukashifu dini za wengine, zikakua na sasa haya ni matunda yake! Sasa watawala wanashughulika na matokeo! Nafikiri sasa wanaona kuwa madhara ya mbegu zile yanatugusa wote, si waislamu wala wakristu, wala wasiokuwa na dini!
 
Kitabu kitakatifu kwa aliyekikojolea au kwa aliyekileta kikojolewe? Ni sahihi kuchukua kitu unachoamini kuwa ni kitakatifu nyumbani kwenu ukampelekea mtu asiyeamini katika utakatifu wa hicho kitabu akikojolee? Mimi naona mngeanza na huyu aliyetoa nyumbani kwao kitabu kinachoitwa kikatatifu kikakojolewe.

Taarifa... yule mtoto kitabu hakukitoa nyumabni kwao, alikuwa anatoka madrasa kusoma na njiani akawakuta wenzie wanacheza mpira wa miguu nae akaanza kucheza kitabu ameweka pembeni, yule kijana aliyekojolea kitabu ni rafiki mkubwa wa kijana ambaye kitabu chake kimekojolewa. So katika utani wao wa kawaida tu ndipo yakazuka mabishano juu ya athari mtu anazoweza pata akikojolea kile kitabu, ili kuthibitisha hayo yule mwingine ndio akakikojolea na yakatokea yaliyotokea!
 
Viongozi wa nchii hii wanapaswa kutafuta suluhu ya matatizo haya yanayosababisha maandamano na machafuko kwa kutafuta kiini hasa cha tatizo hili vinginevyo amani ya nchi yetu itakuwa tumeiweka rehani.

Kama kuna watu wanatumika na mataifa ya nje kuvuruga amani ni bora hatua za kuwadhibiti zichukuliwe mapema vinginevyo nchi yetu itageuka iran,afghanistan,iraq na kwingineko.

Usalama wa taifa hapa ndio wanajukumu kubwa na kama hili litakuwa gumu basi tutarajie muendelezo wa matukio kama haya siku za usoni.

Sectarian violence could cause civil war if it goes unchecked.
Unataraji hii hali itawezekana wakati ni serikali nzima inatumiwa na mataifa makubwa kuwadhibiti raia wake waislamu.Na si Tanzania tu.Angalia Kenya,Mali na mbali zaidi.
Kwa vile hizi serikali zina nguvu kubwa za kijeshi wanazopewa kutoka huko sisi hatutoyaweza,tutajikaza tu lakini tusubiri ghadhabu za Mwenyezi Mungu ndiye atakayeyazima na hao akina Kikwete,Kova,Pinda na Mussa watahizika wawe dhaifu kuliko alivyokuwa Abraha.
 
SULUHU NI KUWAUWA VIKOJOZI wanaokojolea vitabu vitakatifu....no more kuchokozana
na zanzibar vinakojolewa vitabu,ni heri umfundishe mtu juu ya ubora wa imani yako kwa maisha unayoishi,lakini si kumtisha na nguvu za kitabu chako,amka ndugu yangu risasi,panga,jambia,kiwembe havichagui dini bali vinakula nyama yoyote.
 
Nimejiuliza sana kwenye hii point yako, lakini naona hamna aliyetilia maanani kabla. Sijui naye wamemuonya au ameachwa kama hero! Manake hachelewi kumpelekea mtoto mwingine tena!

Ni kweli Dina. Sitarajii hoja hii itiliwe maanani kwa sababu waumini wa hicho kitabu tayari wameshaingia kwenye "blame mode" bila kwanza kutafakari suala zima kwa mapana yake. Sasa hivi wako bize kutafuta mchawi na wanasahau ule msemo wa waswahili kuwa "kikulacho ki nguoni mwako". Kimsingi huyo mtoto aliyepeleka kitabu kikojolewe na yeye alitakiwa aunganishwe kwenye kesi pamoja na huyo aliyekikojolea kwa kosa la kupanga, kuwezesha na kushuhudia kosa likifanyika bila kuchukua hatua.

Hebu tafakari hii "scenario". Unamtambia mwizi kuwa hawezi kuiba ndani ya nyumba yako hata ukimpa ufunguo wa nyumba yako. Yeye anakwambia kuwa ukimpa ufunguo wako atakuibia bila kukamatwa. Baada ya mabishano unaamua kuchukua ufunguo wa nyumba yako unamkabidhi huyo mwizi ili kuthibitisha kama ataiba au la. Mwizi anafanya kweli na kukuibia bila kukamatwa. Je utamlaumu huyu mwizi peke yake au wote hapa mmeshiriki kwenye wizi? Kwa mtazamo wangu muumini wa dini yoyote ile ana wajibu wa msingi wa kutetea, kulinda na kutunza kitabu anachokiamini kuwa ni kitakatifu kwake. Just thinking aloud!!
 
Taarifa... yule mtoto kitabu hakukitoa nyumabni kwao, alikuwa anatoka madrasa kusoma na njiani akawakuta wenzie wanacheza mpira wa miguu nae akaanza kucheza kitabu ameweka pembeni, yule kijana aliyekojolea kitabu ni rafiki mkubwa wa kijana ambaye kitabu chake kimekojolewa. So katika utani wao wa kawaida tu ndipo yakazuka mabishano juu ya athari mtu anazoweza pata akikojolea kile kitabu, ili kuthibitisha hayo yule mwingine ndio akakikojolea na yakatokea yaliyotokea!

Tunarudi palepale ndugu yangu. Muumini wa dini yoyote ana wajibu wa msingi wa kulinda, kutetea na kutunza kitabu anachokiamini kuwa ni kitakatifu kwake. Kitabu kitakatifu kwako kwa mwenzako ni kitabu cha kawaida tu. Huyu mtoto aliyekuwa anatokea madrassa alitakiwa aunganishwe kwenye kesi ya rafiki yake kwani walishirikiana kuvunja sheria.
 
SULUHU NI KUWAUWA VIKOJOZI wanaokojolea vitabu vitakatifu....no more kuchokozana
mkuu labda niongeze tu msisitizo kwa ulichoandika "SULUHU NI KUWAONDOLEA MBALI WANAOKOJOLEA KITABU KITAKATIFU.......no more kuchokozana"
 
Back
Top Bottom